Kwa ekari moja kwa hesabu za hapo juu inaonyesha unaweza kupata sio chini ya 5M ukiwa na ekari 10 unapata 50M
Duuuuu,sidhani kama hizi hesabu zipo realistic but all in all nisikukatishe tamaa just try but I'm sure kinalipa tu hicho kilimo
Mkuu tena hiyo hesabu iko chini. Nimesoma article moja yeye anasema unaweza kupanda miche Hadi 25,200 Kwa ekari which means ni mara mbili ya mahesabu ya huyu. Inaonyesha kilimo cha nanasi kinalipa. Nami naenda kulima aiseee.
KILIMO BORA CHA MANANASI
Zao la mananasi hulimwa sana hapa nchini maeneo ya
Bagamoyo, Kibaha, Geita, Mwanza, Tanga, Mtwara,
Lindi na maeneo mengine. Zao hili lina kiasi kikubwa cha vitamini
A na
B na kiasi kidogo cha vitamini
C, pia kuna madini kama potasiam, kalsiam, chuma na magnesiam
HALI YA HEWA
Manansi hustawi sana ukanda wa pwani usawa usiozini mita
900 toka usawa wa bahari ambapo kuna mvua nyingi kiasi cha milimita
1500 na unyevu wa kutosha, pia unaweza kupanda kwenye maeneo yenye mvua chache lakini kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, Hali ya joto ni kuanzia sentigredi
15 - 32, huwa haya stahimili baridi
UDONGO
Udongo wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji ndi unaofaa kwa ajili ya kilimo cha mananasi, unaweza kutumia samadi au mbole vunde ili kuongezea rutuba ya udongo wako.
MSIMU
Kwa ukanda wa pwani wenye mvua mbili kwa mwaka upandaji wa mananasi huanza mara baada ya mvua za kwanza kuanza, ni vizuri kupanda kwa muda mfupi ili uzaaji usipishane sana na pia kusaidia kupata mvua za kutosha kabla ya msimu kuisha.
UPANDAJI
Tumia miche ya aina moja na yenye umri sawa ili huduma zifanane na pia uzaaji uwe wa mpangilio, umbali toka mmea hadi mmea ni sentimeta
30 na mstari hadi mstari ni sentimeta
60, na umbali kila baada ya mistari miwili miwili ni sentimeta
90
Kwa ekari moja unaweza kupanda miche
25,200 na kwa hekta moja unaweza kupanda miche
44,000. ili mananasi yako yastawi vizuri basi tengeneza kama mtaro mdogo na kwenye mitaro ndio upande mananasi yako, hii husaidia kupata unyevu zaidi
MBOLEA
Kwa wale wanaotumia mbolea za viwandani, ni vizuri kutumia
NPK na DAP ambazo utaweka miezi miwili baada ya kupanda na miezi
12 baada ya kupanda baada ya hapo hautahitaji mbolea tena, lakini ni vizuri zaidi kama utatumia mbolea za asili
WADUDU
Wadudu wanaoshambulia mananasi ni aina ya mealybug ambao huondolewa kwa kupulizia dawa kama dume na karate.
Ugonjwa wa kuoza moyo wa miche unaweza kuzuiwa kwa kupiga dawa za copper oxychloride au kwa kuzamisha miche kwenye dawa za fungasi
(fungicides)kabla ya kupandwa shambani
UVUNAJI
Mananasi huwa tayari kuvunwa miezi
18 mpaka 24 baada ya kupandwa kutegemeana na mbegu na matunzo ikiwemo kiasi cha mvua, mbolea na unyevu shambani, Uvunaji hufanyika kwa kutumia visu na vibebeo maalum kuhakikisha ubora wa zao hili