Kilimanjaro: Waendesha bodaboda wamwaga chakula msibani, wadai marehemu alikuwa ananyimwa msosi

Waendesha bodaboda wa kituo cha Kisangiro kata ya Kilema Kaskazini wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wamevamia msiba wa Lenard Abel (20) na kumwaga chakula na pombe kwa madai kuwa marehemu alikuwa hapewi chakula alipokuwa hai.

Walifika katika msiba huo saa 9 alasiri jana Jumatatu Mei 3, 2021 baada ya mazishi wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula na kumwaga chakula hicho kitendo kilichozua tafrani na waombolezaji kulazimika kutimua mbio.

Shuhuda wa tukio hilo, Lucy Lyimo amesema kundi hilo la vijana lilifika msibani na kuvamia jikoni na kuanza kumwaga chakula na pombe aina ya mbege sambamba na kuvunja viti.

“Wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula kulitokea kundi la vijana zaidi ya ishirini wakipiga ukunga na kusema huyu marehemu kipindi akiwa hai alikuwa hapewi chakula iweje leo amekufa chakula kipo na pombe, " amesema Lucy akibainisha wakati wakisema hayo walikuwa wakielekea ilipohifadhiwa pombe na chakula

Amesema walipomwaga chakula na pombe waliwasha mishumaa na kuelekea makaburi yalikofanyika mazishi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kyou, Paul Lyimo amesema wakati vijana wakifanya vurugu za kumwaga chakula na vinywaji Padri wa Parokia ya Kilema aliyeendesha ibada ya mazishi aliwafuata kuwaomba wasifanye vurugu ila hawakusikia.

"Padri aliwapigia hadi magoti kuwaomba wasifanye hivyo lakini waliendelea kumwaga chakula huku wakipiga ukunga na baada ya hapo walienda kuwasha mishumaa kwenye kaburi na kutawanyika," amesema
Duu, hiyo kali
 
Duh, washkaji wa marehemu wana msimamo kwelikweli.

Ila kwa upande mwingine inakera sana, unakuta mlishindwa kumnunulia marehemu dawa alipokuwa hai ila wakati wa mazishi mnaweka mpaka makamera na kamati za vyakula na vinywaji.
Ni kweli. Kama walikuwa hawampi chakula halafu alipofariki wakapika hilo ni kosa. BTW kichwa cha habari kilinipiga chenga nikadhani bodaboda wamepeleka chakula msibani kwa wingi (eg kama wanavyosema kumwaga fedha)
 
Huyo mmojawapo
FB_IMG_1613816640987.jpg
 
Moshi. Waendesha bodaboda wa kituo cha Kisangiro kata ya Kilema Kaskazini wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wamevamia msiba wa Lenard Abel (20) na kumwaga chakula na pombe kwa madai kuwa marehemu alikuwa hapewi chakula alipokuwa hai.

Walifika katika msiba huo saa 9 alasiri jana Jumatatu Mei 3, 2021 baada ya mazishi wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula na kumwaga chakula hicho kitendo kilichozua tafrani na waombolezaji kulazimika kutimua mbio.

Shuhuda wa tukio hilo, Lucy Lyimo amesema kundi hilo la vijana lilifika msibani na kuvamia jikoni na kuanza kumwaga chakula na pombe aina ya mbege sambamba na kuvunja viti.

“Wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula kulitokea kundi la vijana zaidi ya ishirini wakipiga ukunga na kusema huyu marehemu kipindi akiwa hai alikuwa hapewi chakula iweje leo amekufa chakula kipo na pombe, " amesema Lucy akibainisha wakati wakisema hayo walikuwa wakielekea ilipohifadhiwa pombe na chakula

Amesema walipomwaga chakula na pombe waliwasha mishumaa na kuelekea makaburi yalikofanyika mazishi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kyou, Paul Lyimo amesema wakati vijana wakifanya vurugu za kumwaga chakula na vinywaji Padri wa Parokia ya Kilema aliyeendesha ibada ya mazishi aliwafuata kuwaomba wasifanye vurugu ila hawakusikia.

"Padri aliwapigia hadi magoti kuwaomba wasifanye hivyo lakini waliendelea kumwaga chakula huku wakipiga ukunga na baada ya hapo walienda kuwasha mishumaa kwenye kaburi na kutawanyika," amesema.
 
Back
Top Bottom