Kilimanjaro: Waendesha bodaboda wamwaga chakula msibani, wadai marehemu alikuwa ananyimwa msosi

Waendesha bodaboda wa kituo cha Kisangiro kata ya Kilema Kaskazini wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wamevamia msiba wa Lenard Abel (20) na kumwaga chakula na pombe kwa madai kuwa marehemu alikuwa hapewi chakula alipokuwa hai.

Walifika katika msiba huo saa 9 alasiri jana Jumatatu Mei 3, 2021 baada ya mazishi wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula na kumwaga chakula hicho kitendo kilichozua tafrani na waombolezaji kulazimika kutimua mbio.

Shuhuda wa tukio hilo, Lucy Lyimo amesema kundi hilo la vijana lilifika msibani na kuvamia jikoni na kuanza kumwaga chakula na pombe aina ya mbege sambamba na kuvunja viti.

“Wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula kulitokea kundi la vijana zaidi ya ishirini wakipiga ukunga na kusema huyu marehemu kipindi akiwa hai alikuwa hapewi chakula iweje leo amekufa chakula kipo na pombe, " amesema Lucy akibainisha wakati wakisema hayo walikuwa wakielekea ilipohifadhiwa pombe na chakula.

Amesema walipomwaga chakula na pombe waliwasha mishumaa na kuelekea makaburi yalikofanyika mazishi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kyou, Paul Lyimo amesema wakati vijana wakifanya vurugu za kumwaga chakula na vinywaji Padri wa Parokia ya Kilema aliyeendesha ibada ya mazishi aliwafuata kuwaomba wasifanye vurugu ila hawakusikia.

"Padri aliwapigia hadi magoti kuwaomba wasifanye hivyo lakini waliendelea kumwaga chakula huku wakipiga ukunga na baada ya hapo walienda kuwasha mishumaa kwenye kaburi na kutawanyika," amesema.
Safi sana!
 
Wao bodaboda walimpa au walimsaidia Nini huyo marehemu mpaka wajione wana haki zote za kufanya hivyo
 
Wachagga wanapita Kimiaaaaaa kama hili la aibu kubwa haliwahusu, naona UTV wamerusha hili tukio ni aibu sana Wachagga kumbe mu wachoyo.
 
Waendesha bodaboda wa kituo cha Kisangiro kata ya Kilema Kaskazini wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wamevamia msiba wa Lenard Abel (20) na kumwaga chakula na pombe kwa madai kuwa marehemu alikuwa hapewi chakula alipokuwa hai.

Walifika katika msiba huo saa 9 alasiri jana Jumatatu Mei 3, 2021 baada ya mazishi wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula na kumwaga chakula hicho kitendo kilichozua tafrani na waombolezaji kulazimika kutimua mbio.

Shuhuda wa tukio hilo, Lucy Lyimo amesema kundi hilo la vijana lilifika msibani na kuvamia jikoni na kuanza kumwaga chakula na pombe aina ya mbege sambamba na kuvunja viti.

“Wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula kulitokea kundi la vijana zaidi ya ishirini wakipiga ukunga na kusema huyu marehemu kipindi akiwa hai alikuwa hapewi chakula iweje leo amekufa chakula kipo na pombe, " amesema Lucy akibainisha wakati wakisema hayo walikuwa wakielekea ilipohifadhiwa pombe na chakula.

Amesema walipomwaga chakula na pombe waliwasha mishumaa na kuelekea makaburi yalikofanyika mazishi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kyou, Paul Lyimo amesema wakati vijana wakifanya vurugu za kumwaga chakula na vinywaji Padri wa Parokia ya Kilema aliyeendesha ibada ya mazishi aliwafuata kuwaomba wasifanye vurugu ila hawakusikia.

"Padri aliwapigia hadi magoti kuwaomba wasifanye hivyo lakini waliendelea kumwaga chakula huku wakipiga ukunga na baada ya hapo walienda kuwasha mishumaa kwenye kaburi na kutawanyika," amesema.
Sio mbaya walifanya la maana sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Kwa hiyo Waombolezaji woote wakashindwa kuthibiti vijana wasiozidi 20 na kukubali kumwagiwa chakula cha Msiba?
 
Pia na mambo ya ulevi kwenye misiba ni ya kawaida.
Yaani siyo kawaida tu, bali kama msibani watu hawajalewa lazima mtasemwa sana, misiba ya huko usione kila mtu kavaa koti, jamaa wanaonunua konyagi ndogo ndogo na kuzificha humo.

Chooni kila dakika kumbe mtu anaenda kupiga fundo 😁!.
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom