Makamanda wenzangu
min -me ,
secretarybird ,
Castle_Lite ,
dosho12 ,
Mshana Jr ,
MENEMENE TEKERI NA PERESI na makamanda woteeeeeee ambao ni wadau wa VINYWAJI CHANGAMSHI kwa Ujumla bila kumsahau mdogo angu
Monetary doctor..
Ilikua siku tulivu sana miaka mitano iliyo pita nikiwa maeneo ya Mbagala nionane na rafiki yangu mmoja..
Nilikua na pesaa nyingi mfukoni nikakaa maeneo ya uwanjani Kuna meza zinawekwaga pale nikanywa flying fish kama mbili mida ya jioni jioni kagiza ka USONI rafiki yangu hakutokea ile nimeagiza flying fish ya tatu nilikua natumia glass kunywa
Jamaa kama watatu wakaja mmoja akiwa ana yumba akagonga chupa na glass niliyo kua nakunywa vitu vikadondoka nikawai chupa ikawa imebakia nusu.. yule jamaa akasema aninunulie ingine nikakataa..muhudumu akaleta glass ingine ikiwa imeloa loa..
Nikamimina ile flying fish ilio bakia kwenye glass...akili ikanambia kunywa yotee nyanyuka ondoka sepa ili eneo
Kweli nikanyanyuka nikapanda bajaji nikawa nimeondoka nikafika maeneo ya center moja Huwa wananiita Brother white nikatafuta Kuna ki restaurant nikaingia Nika agiza nyama choma na chips nikiwa nasubilia nikawa nakula mishikaki kidogo nikatafuta Kona nikakaa ilikua kama saa tatu ivii usiku..
Nikazinduka pale saa nane na nusu usiku..nilipo sinzia ni kama dakika kadhaa kumbe nazinduka saa nane nikiwa nashangaa missed call kama zoteee yaani acha TU
Pesa mfukoni zipo zotee...wale jamaa nikawashukulu pale wakasema brother white sio kawaida Yako..sisi tulikua tunajua umechoka sana uka amua upumzike haaahaa ndio nikawapa mkasa wa mbagala wale jamaa wa mbagala uwanjani sijui waliniwekea nini kwenye glass yangu
Wale jamaa wa mbagala mtego ungetiki ningefanywa nini pale ugenini pona yangu nilivyo nyanyuka ni kunyanyuka pale na kusepa
Huwa napaogopa sana Mbagala tangu siku iyo NIMEKUA mtu makini sana kwenye mwenendo napo kutana na ma stranger nipo makini mno mno