Kilichonikuta baada ya kupalilia makaburi

Kilichonikuta baada ya kupalilia makaburi

Na kupalilia ni kufanya usafi kama usafi mwingine...

Hapo Mchungaji ameshajipatia mgodi wa kuvuna mapesa....maana jamaa ameshatekwa akili yake kuwa matatizo yake yamesababishwa na kupalilia makaburi..hivyo tegemea aambiwe yafuatayo

Atoe sadaka ya ukombozi kwa familia..
Atoe Sadaka ya kuvunja laana...
Atoe sadaka ya kung'o mti wa Ukoo
Atoe Sadaka ya kusafisha nyota yake...

Atatoa sadaka mpaka siku anaingia kaburini....
Hahaaaa hio ndo Tafsiri halisi ya jinii limekula mganga
 
Mkuu Pole sana na mapito yaliyokukuta...

Kabla ya kuanza kulaumu makaburi na maeneo yake kwanza jitafakari mwenyewe kwenye mizunguko yako, kila kitu huwa na chanzo chake.. Huko kwenye biashara zako na maisha yako na mke wako mjichunguze kwanza muangalie kama hakuna matendo mabaya mmeshawahi wafanyia watu, dhulma, uchawi na kitu chochote kibaya...
Pili mkuu angalia historia yako na ukoo wako huko nyuma na uhusiano wa hilo kaburi na wewe, Marehemu aliyelala kwenye hilo ana historia gani kwenye ukoo wenu?...
Kama ni mkristo au muislamu fanya misa au dua ya familia kumuomba MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA ARDHI AWAEPUSHE NA LAANA YEYOTE NDANI YA FAMILIA... WAKUMUOMBA HAPO NI MUNGU TU..
katika woote humu..wewe ndo umetoa ushauri!
 
Pale kibaha kwa mfipa zinapopita hizi nyaya za umeme mkubwa,
siku ya kusafisha malalo wakaenda wenye ndugu zao waliolala mahali pale.
kitendo cha kuanza kupalilia tu, waya ukaachia ukawashukia,
mmoja alikatwakatwa vipande wengine wawili walienda kupona au kufia hospitalini.

Waangalieni wazazi.
 
It's not a loughing matter my dear!!! Inasikitisha sana.....Wachungaji siku hizi ndio wamekuwa wachonganishi na kuleta chuki na visasi kwa jamii

Nimeshuhudia mtu akimuita mama yake mchawi kisa mchungaji amefunuliwa na roho kuwa mama yake ni mchawi...sasa hapo kuna tifauti gani na waganga wa kienyeji
Hatari sana majibu yao ni ya kubahatisha usipokuwa makini unapptea au kugombana na watu ila yote ni sababu watu tunaangaika na maisha ya duniani tule nn tuvae nn baada ya kuutafta ufalme wa mungu
 
Sitasahau maishani mwangu, ilikuwa ni mwaka 2011 niliposafiri na mke wangu pamoja na mwanangu kwenda nyumbani kijijini kusalimia.

Wakati huo mwanangu alikuwa na umri wa mwaka mmoja tu,baada ya kufika nyumbani tulipumzika na kisha kesho yake mida ya saa 12 jioni tulielekea makaburini mimi na mke wangu na mtoto wetu alibebwa mgongoni ,na mimi nilibeba jembe.

Baada ya kufika tu makaburini ,mwanangu aliyekuwa amelala mgongoni aliamka na kisha akaanza kupepesa macho huku na kule,akishangaa mandhari ya makaburini,mimi nilianza kupalilia makaburi na dk 5 baadaye mtoto akaanza kulia,mama yake alimshusha mgongoni ili amnyonyeshe lakini ndo alizidi kulia kana kwamba anachomwa moto.
Tulijaribu kumbembeleza mtoto lakini ndo alizidi kulia kwa kasi ya kutisha,sijawahi kuona mtoto akilia kama mwanangu siku hiyo .

Mtoto alilia hadi tukarudi nyumbani,kufika nyumbani ndo alilia zaidi huku akitutazama kwa jicho la huruma,hakuwa ktk hali ya kawaida hata uso wake ulibadilika kabisa.
Nakumbuka siku hiyo tulishindwa hata kula,mida ya saa 4 usiku mtoto alitulia akalala,tukabaki tunajiuliza ni kitu gani kilitokea,kesho yake nilipanga kuanza safari ya kwenda Dar kununua gari,nilikuwa na pesa za kutosha Benk zaidi ya sh mil 60 nilizokuwa nimezipata kwa biashara ya Dhahabu .

Siku nyingine iliyofuata nilianza safari ya kwenda Dar,nilifika salama na kufanikiwa kununua gari zuri la kutembelea,kutokana na uzoefu wangu mdogo wa kuendesha magari ilinibidi nikodi dereva,tulipokaribia kufika Manyoni Singida saa moja usiku,gari iliacha njia ikapinduka tukiwa na mwendo kasi,ajabu tulipona wote ila gari ikaharibika vibaya mno,kama ungeiona usingeamini kama watu walisalimika.

Gari ya sh mil 15 haikutamanika hata kidogo,usiku wa manane tukiwa pale msituni baada ya gari letu kupinduka,tulivamiwa na kundi la watu wasiojulikana,wakatupora kila kitu na jambo la kushangaza walikuwa na vifaa vya kufungua na kuchukua spea za gari,walichukua hadi tairi.

Alfajiri ikapita patrol ya police na kutupeleka hadi Manyoni mjini.
Nilirudi nyumbani nikilia kwa huzuni,mke wangu akanipa moyo,baada ya hapo niliendelea na bishara zangu nikaanza kufirisika tu,kila nalofanya haliendi,nikauza kila kitu hadi nyumba na kwenda kupanga,nilirudi nyuma na kuwa maskini wa kutupwa.
Hadi chakula na sabuni ya kuogea ama kufulia tu ikawa shida kuipata.

Nilimfuata mchungaji wa kanisa moja moja nikamwelezea mkasa wote,akaniambia ni hatari sana kuweka mazoea na makaburi,mtu anapokufa na kuzikwa,yeye halisi huondoka kabisa duniani na pale kaburini hubaki mwili tu ambao hauna uhai kama jiwe.
Kwa hiyo,mapepo ya uharibifu hukaa makaburini yakijua kuwa mwanadamu ni lazima ataenda makaburini kwa sababu hana maarifa ya kujua hatari za makaburi,wachawi nao hutega mikosi yao huko wakijua kuwa watu wengi hawajui undani wa makaburi na hivyo ni lazima waende huko,Na ndo maana mwanangu alikuwa akiyaona yote hayo ila kusema hawezi.

Wakuu, hiki ni kisa cha kweli kabisa.
Duu pole sana mkuu ,kuna mda maalum wa kusafisha makaburi ni asubuhi mapema kabla watu hawajaamka ...kuna vitu vya ajabu ,mim niliwah kwenda kusafisha kwenye makabur ya babu zangu asubuhi ilipofika usiku nkapandisha mapepo hatari yakadai nirud tena nkasalimie usiku huohuo usiku SAA sita, wanafamilia wakayabembeleza yakawa yamekubar kuwa nirud kesho asubuhi ila sio usiku huohuo ,pole xana hii huwa inatokea kama una direction flan ya maisha
 
Mkuu Pole sana na mapito yaliyokukuta...

Kabla ya kuanza kulaumu makaburi na maeneo yake kwanza jitafakari mwenyewe kwenye mizunguko yako, kila kitu huwa na chanzo chake.. Huko kwenye biashara zako na maisha yako na mke wako mjichunguze kwanza muangalie kama hakuna matendo mabaya mmeshawahi wafanyia watu, dhulma, uchawi na kitu chochote kibaya...
Pili mkuu angalia historia yako na ukoo wako huko nyuma na uhusiano wa hilo kaburi na wewe, Marehemu aliyelala kwenye hilo ana historia gani kwenye ukoo wenu?...
Kama ni mkristo au muislamu fanya misa au dua ya familia kumuomba MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA ARDHI AWAEPUSHE NA LAANA YEYOTE NDANI YA FAMILIA... WAKUMUOMBA HAPO NI MUNGU TU..

Wanaowajaza mafundisho ya namna hii watapokea thawabu yao siku ya mwisho. Wanaangamiza mamia kwa maelfu ya watu. Ikiwa matendo ya ndugu zetu huko nyuma yanaweza kutuathiri sisi, iweje iwe kwa mambo mabaya tu? Mbona hatuwi matajiri kwa sababu Babu,bibi,mjomba au shangazi alikuwa tajiri? Inakuwaje familia au koo zinakumbwa na njamaa wakati Baba au mama walikuwa wanasaza chakula? Inakuwaje Babu,Baba au mama walikuwa walevi lakini mtoto au mjukuu hawi mlevi? Kwa nini lakini tumeruhusu akili zetu zichezewe kiasi hiki?
 
Hatari sana majibu yao ni ya kubahatisha usipokuwa makini unapptea au kugombana na watu ila yote ni sababu watu tunaangaika na maisha ya duniani tule nn tuvae nn baada ya kuutafta ufalme wa mungu

Hao washenzi wanaiangamiza Afrika na Waafrika. Nina mjomba wangu huko kijijini. Nilipigiwa simu Wiki iliyopita kuwa anaumwa sana na kwamba amehama nyumbani yuko kwa Mganga wa kienyeji. Nilichofanya mimi nikampigia simu huyo mgonjwa mwenyewe. Hakupokea; baadaye akaja kunipigia na kuniambia alikuwa kwenye maombi na washirika wenzake juu ya hilo tatizo lake. Nikamsaili juu ya kinachomsibu. Nika-suspect mambo kadhaa. Nikatuma pesa aende hospitalini akafanyiwe check up. Vipimo vimetoka yuko na UTI ya muda mrefu sana. Yuko na Syphilis na Amoeba kibao. Sasa unaweza kuona ujinga unavyoweza kuchukua maisha ya watu hivi hivi.

Nikiona hawa wanajiita wachungaji,manabii na maaskofu uchwara wanavyodanganya waumini wao nachukia sana.
 
Hivyo Mungu aliumba hii dunia, kisha baadhi ya maeneo akamwachia Shetani ajivinjari na maeneo mengine akayapa ulinzi...?? Huyo mungu wako atakuwa mpumbavu kupita kuasi...

Mungu wangu ni muweza wa vyote, na kila kitu kiliumbwa na yeye na Mungu wangu yupo mahali pote(Kila mahali)

Au ungemuuliza kama mapepo,"majini" na "wachawi" hao wote wana uwezo wa kujipenyeza kwenye makaburi na kujitawala huko na kupafanya himaya yao je,ina maana hata kule alikozikwa Yesu Kristu nako mapepo na "mijini" ilitia mguu? Na kama hiyo mipepo inakuwa na nguvu huko ilikuwaje Yesu akafufuka?

Loh! Acha wajinga na wasiofikiri kwa mantiki watunguliwe pesa na matapeli. Madhali,Magufuli kakaba kila sehemu na chochoro za kujipatia pesa kiujaujanja zimezibwa sasa wengi watahamia huko kwenye ulaji laini ambako hakuna investment kubwa zaidi ya Biblia na koti na tai tena vyote vya kutoka Kariakoo.
 
Sasa unaposema tusiyazoee makaburi kuna mapepo huko na wachawi. je.? sisi ambao nyumba zetu zipo upande wa pili ambapo njia lazima ukatize makaburini unatuambuaje.. mbona tushazoea kila siku tunapita usiku na mchana hayo mambo hayatupati..huwenda ulikuwa na mapepo yako tu binafsi..muulize mchungaji vizuri asikudanganye..
😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😱😱
 
Pale kibaha kwa mfipa zinapopita hizi nyaya za umeme mkubwa,
siku ya kusafisha malalo wakaenda wenye ndugu zao waliolala mahali pale.
kitendo cha kuanza kupalilia tu, waya ukaachia ukawashukia,
mmoja alikatwakatwa vipande wengine wawili walienda kupona au kufia hospitalini.

Waangalieni wazazi.

Hakuna uthibitisho pasipo shaka kwamba kuanguka kwa nyaya hizo kuna uhusiano na kutaka kusafishwa hayo makaburi. Nyaya za umeme au simu kila mara tunazishuhudia mitaani zinadondoka. Sio jambo la pekee kama unavyolieleza hapa. Kama kuna upekee kihivyo kwa nini haikunyesha mvua kali sana tena kwenye boundaries za makaburi tu? Au kikavuma Kimbunga kikali kabisa kama Maria kilichochukua maisha ya watu huko juzi Marekani? Na Kimbunga chenyewe kianzie pale pale makaburini na kuishia hapo hapo. Muujiza sharti ubebe mambo ambayo hayaelezeki kirahisi. Lazima kuwe na scenarios zinazovuka senses zetu.
 
Hata hivyo hulazimishwi kuamini;

Walikufa auntwa mie oooh..wapone wajigambe
 
Back
Top Bottom