Kilichonikuta baada ya kupalilia makaburi

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Posts
1,583
Reaction score
2,702
Sitasahau maishani mwangu, ilikuwa ni mwaka 2011 niliposafiri na mke wangu pamoja na mwanangu kwenda nyumbani kijijini kusalimia.

Wakati huo mwanangu alikuwa na umri wa mwaka mmoja tu,baada ya kufika nyumbani tulipumzika na kisha kesho yake mida ya saa 12 jioni tulielekea makaburini mimi na mke wangu na mtoto wetu alibebwa mgongoni ,na mimi nilibeba jembe.

Baada ya kufika tu makaburini ,mwanangu aliyekuwa amelala mgongoni aliamka na kisha akaanza kupepesa macho huku na kule,akishangaa mandhari ya makaburini,mimi nilianza kupalilia makaburi na dk 5 baadaye mtoto akaanza kulia,mama yake alimshusha mgongoni ili amnyonyeshe lakini ndo alizidi kulia kana kwamba anachomwa moto.
Tulijaribu kumbembeleza mtoto lakini ndo alizidi kulia kwa kasi ya kutisha,sijawahi kuona mtoto akilia kama mwanangu siku hiyo .

Mtoto alilia hadi tukarudi nyumbani,kufika nyumbani ndo alilia zaidi huku akitutazama kwa jicho la huruma,hakuwa ktk hali ya kawaida hata uso wake ulibadilika kabisa.
Nakumbuka siku hiyo tulishindwa hata kula,mida ya saa 4 usiku mtoto alitulia akalala,tukabaki tunajiuliza ni kitu gani kilitokea,kesho yake nilipanga kuanza safari ya kwenda Dar kununua gari,nilikuwa na pesa za kutosha Benk zaidi ya sh mil 60 nilizokuwa nimezipata kwa biashara ya Dhahabu .

Siku nyingine iliyofuata nilianza safari ya kwenda Dar,nilifika salama na kufanikiwa kununua gari zuri la kutembelea,kutokana na uzoefu wangu mdogo wa kuendesha magari ilinibidi nikodi dereva,tulipokaribia kufika Manyoni Singida saa moja usiku,gari iliacha njia ikapinduka tukiwa na mwendo kasi,ajabu tulipona wote ila gari ikaharibika vibaya mno,kama ungeiona usingeamini kama watu walisalimika.

Gari ya sh mil 15 haikutamanika hata kidogo,usiku wa manane tukiwa pale msituni baada ya gari letu kupinduka,tulivamiwa na kundi la watu wasiojulikana,wakatupora kila kitu na jambo la kushangaza walikuwa na vifaa vya kufungua na kuchukua spea za gari,walichukua hadi tairi.

Alfajiri ikapita patrol ya police na kutupeleka hadi Manyoni mjini.
Nilirudi nyumbani nikilia kwa huzuni,mke wangu akanipa moyo,baada ya hapo niliendelea na bishara zangu nikaanza kufirisika tu,kila nalofanya haliendi,nikauza kila kitu hadi nyumba na kwenda kupanga,nilirudi nyuma na kuwa maskini wa kutupwa.
Hadi chakula na sabuni ya kuogea ama kufulia tu ikawa shida kuipata.

Nilimfuata mchungaji wa kanisa moja moja nikamwelezea mkasa wote,akaniambia ni hatari sana kuweka mazoea na makaburi,mtu anapokufa na kuzikwa,yeye halisi huondoka kabisa duniani na pale kaburini hubaki mwili tu ambao hauna uhai kama jiwe.
Kwa hiyo,mapepo ya uharibifu hukaa makaburini yakijua kuwa mwanadamu ni lazima ataenda makaburini kwa sababu hana maarifa ya kujua hatari za makaburi,wachawi nao hutega mikosi yao huko wakijua kuwa watu wengi hawajui undani wa makaburi na hivyo ni lazima waende huko,Na ndo maana mwanangu alikuwa akiyaona yote hayo ila kusema hawezi.

Wakuu, hiki ni kisa cha kweli kabisa.
 
Sasa unaposema tusiyazoee makaburi kuna mapepo huko na wachawi. je.? sisi ambao nyumba zetu zipo upande wa pili ambapo njia lazima ukatize makaburini unatuambuaje.. mbona tushazoea kila siku tunapita usiku na mchana hayo mambo hayatupati..huwenda ulikuwa na mapepo yako tu binafsi..muulize mchungaji vizuri asikudanganye..
 
Vijijini watu wanazika karibu na makazi yao. ni yepi yalikuwa maoni ya mchungaji wako juu ya hilo? au hukuuliza?
Na kwa mjini panapoitwa makaburini kila siku watu waenda kuzika, mapepo yanakuwa hayapo au yana muda maalum? au tusizikne?
 
Sasa unaposema tusiyazoee makaburi kuna mapepo huko na wachawi. je.? sisi ambao nyumba zetu zipo upande wa pili ambapo njia lazima ukatize makaburini unatuambuaje.. mbona tushazoea kila siku tunapita usiku na mchana hayo mambo hayatupati..huwenda ulikuwa na mapepo yako tu binafsi..muulize mchungaji vizuri asikudanganye..

Adhabu ya nyumba unayoishi jirani na makaburi
Siafu hawaishi ndani...cha ajabu wanazuka ghafla tu hao siafu.
Kingine Nyoka Yaani utasingizia mashimo mara nyumba ina vichiguu pembeni
Lkn habari ndio hio,,
Kama utabisha au kupinga hili swala labda ulipinge tu humu JF lkn ukwrli ndio huo
Hayo maswala ya mapepo sijui uchawi hata mm nayaskiaga tu
 
NIMECHEAA MPAA BASII
NAMI NILITAKA KUMUULIZA ZILE.NYUMBA ZILIZO KARIBU NAMAKABURI KINONDONI WAZIAMISHIE MBWENI AMA
 
Huyo mchungaji anataka kukupiga pesa tu,na sisi tulio na makaburi majumbani kwetu mbona kila siku tuna mandinga mapyaaa,yoooh!!
Hahahaaaaaa kwahioo ukiweka makaburu nyumbanu jamaa anamaanisha unakatibisha wachawi na mapepo fyyuuuuuu pepo analimwenyewe ajikague
 
Adhabu ya nyumba unayoishi jirani na makaburi
Siafu hawaishi ndani...cha ajabu wanazuka ghafla tu hao siafu.
Kingine Nyoka Yaani utasingizia mashimo mara nyumba ina vichiguu pembeni
Lkn habari ndio hio,,
Kama utabisha au kupinga hili swala labda ulipinge tu humu JF lkn ukwrli ndio huo
Hayo maswala ya mapepo sijui uchawi hata mm nayaskiaga tu

MBONA WALE MALAYA WANAOFANYA MAPENZI MAKABURI YA KINONDONI KILANSIKU WATEJA WANAJAZANAAA.....NAO UANWASHAURIJE
 
Sitasahau maishani mwangu, ilikuwa ni mwaka 2011 niliposafiri na mke wangu pamoja na mwanangu kwenda nyumbani kijijini kusalimia.
Wakati huo mwanangu alikuwa na umri wa mwaka mmoja tu,baada ya kufika nyumbani tulipumzika na kisha kesho yake mida ya saa 12 jioni tulielekea makaburini mimi na mke wangu na mtoto wetu alibebwa mgongoni ,na mimi nilibeba jembe.
Baada ya kufika tu makaburini ,mwanangu aliyekuwa amelala mgongoni aliamka na kisha akaanza kupepesa macho huku na kule,akishangaa mandhari ya makaburini,mimi nilianza kupalilia makaburi na dk 5 baadaye mtoto akaanza kulia,mama yake alimshusha mgongoni ili amnyonyeshe lakini ndo alizidi kulia kana kwamba anachomwa moto.
Tulijaribu kumbembeleza mtoto lakini ndo alizidi kulia kwa kasi ya kutisha,sijawahi kuona mtoto akilia kama mwanangu siku hiyo .
Mtoto alilia hadi tukarudi nyumbani,kufika nyumbani ndo alilia zaidi huku akitutazama kwa jicho la huruma,hakuwa ktk hali ya kawaida hata uso wake ulibadilika kabisa.
Nakumbuka siku hiyo tulishindwa hata kula,mida ya saa 4 usiku mtoto alitulia akalala,tukabaki tunajiuliza ni kitu gani kilitokea,kesho yake nilipanga kuanza safari ya kwenda Dar kununua gari,nilikuwa na pesa za kutosha Benk zaidi ya sh mil 60 nilizokuwa nimezipata kwa biashara ya Dhahabu .
Siku nyingine iliyofuata nilianza safari ya kwenda Dar,nilifika salama na kufanikiwa kununua gari zuri la kutembelea,kutokana na uzoefu wangu mdogo wa kuendesha magari ilinibidi nikodi dereva,tulipokaribia kufika Manyoni Singida saa moja usiku,gari iliacha njia ikapinduka tukiwa na mwendo kasi,ajabu tulipona wote ila gari ikaharibika vibaya mno,kama ungeiona usingeamini kama watu walisalimika.
Gari ya sh mil 15 haikutamanika hata kidogo,usiku wa manane tukiwa pale msituni baada ya gari letu kupinduka,tulivamiwa na kundi la watu wasiojulikana,wakatupora kila kitu na jambo la kushangaza walikuwa na vifaa vya kufungua na kuchukua spea za gari,walichukua hadi tairi.
Alfajiri ikapita patrol ya police na kutupeleka hadi Manyoni mjini.
Nilirudi nyumbani nikilia kwa huzuni,mke wangu akanipa moyo,baada ya hapo niliendelea na bishara zangu nikaanza kufirisika tu,kila nalofanya haliendi,nikauza kila kitu hadi nyumba na kwenda kupanga,nilirudi nyuma na kuwa maskini wa kutupwa.
Hadi chakula na sabuni ya kuogea ama kufulia tu ikawa shida kuipata.
Nilimfuata mchungaji wa kanisa moja moja nikamwelezea mkasa wote,akaniambia ni hatari sana kuweka mazoea na makaburi,mtu anapokufa na kuzikwa,yeye halisi huondoka kabisa duniani na pale kaburini hubaki mwili tu ambao hauna uhai kama jiwe.
Kwa hiyo,mapepo ya uharibifu hukaa makaburini yakijua kuwa mwanadamu ni lazima ataenda makaburini kwa sababu hana maarifa ya kujua hatari za makaburi,wachawi nao hutega mikosi yao huko wakijua kuwa watu wengi hawajui undani wa makaburi na hivyo ni lazima waende huko,Na ndo maana mwanangu alikuwa akiyaona yote hayo ila kusema hawezi.
Wakuu, hiki ni kisa cha kweli kabisa.

NDUGU YANGU MPENDWA.
BWANA YESU ASIFIWE.KWA MDA HUU WAWEZA NIITA PAST DIDY KWA MDA....

NI HABARI NZURI NA YA KUFUNDISHA INGAWAWENGINE WANAFANYA. N YA MASIHARA..KAMA UTAKUWA NA SIMU YA SMARTPHONE TAFUTA SOMO LA MALANGO LA MTUMISHI WA MUNGU MWAKASEGE JIBU UTALIPATA......

SHETANI AWEZI KUKUINGIA KIRAHISI KAMA LANGO LAKO LIKO NA NGUVU..NN MAANA YA MALANGO YOOTE UTAPATA HUKO.WANAPOSEMA WENYE NGUVU NDIO WATAUONA UFALME WA MUNGU SIO WABEBACHUMA...WENYE NGUVU KWELIKWELI.CHA MUHIMU ANGALIA WAPI UMELIACHIA LANGO LAKO WAZI HILO SHETANI LA UFILISI NA AJALI LIKAKUINGIA...LANGO LAWEZA KUWA N DHAMBI .A DHAMBI YAWEZA KUWA YAKO AMA KWA NIABA YAUKOO ILE DHAMBI INAKUNYEMELEA UNAISHIA KUWAZA YAMAKABURINI..

ANGALIA MAPN YA FAMILIA YAKO HAKUNAWALIOKUFA KWA AJALI??KAMA WAPO ANGALIA HILO NALO N LANGO LIKOWAZI.....TUBU KWA AJILI YA UKOO FANYA MAOMBI YAUKWELI KEMEA KABISAAA......MENGINE NTAKUJA ASBH KUKUFUMBUA MACHO
 
Back
Top Bottom