Kilichonikuta baada ya kupalilia makaburi

Kilichonikuta baada ya kupalilia makaburi

Aiseee..pole mkuu sasa uhusiano wa mtoto kulia, wewe kupata ajali na kufilisika ni upi?
Yani hakuna uhusiano kabisa...ameungaunga matukio ya yeye kupata ajali na kufilisika akaunganisha na kusafisha makaburi ili apate sympathy ya matatizo yake....

Yani badala ya kutafuta suluhu ya matatizo yake, yeye anatafuta nchawi...
 
Sasa unaposema tusiyazoee makaburi kuna mapepo huko na wachawi. je.? sisi ambao nyumba zetu zipo upande wa pili ambapo njia lazima ukatize makaburini unatuambuaje.. mbona tushazoea kila siku tunapita usiku na mchana hayo mambo hayatupati..huwenda ulikuwa na mapepo yako tu binafsi..muulize mchungaji vizuri asikudanganye..

Achanaye huyo....ana maruwenge
 
Aiseee..pole mkuu sasa uhusiano wa mtoto kulia, wewe kupata ajali na kufilisika ni upi?
Hapo alikuwa anawajulisha wanawake humu JF ya kwamba mwaka 2011 alikuwa na milioni 60 Benki na alinunua gari ya milioni 15 mkuu. Bila kusahau biashara yake ya dhahabu.
Sipati picha alivyopata usumbufu huko PM.
 
Hapo alikuwa anawajulisha wanawake humu JF ya kwamba mwaka 2011 alikuwa na milioni 60 Benki na alinunua gari ya milioni 15 mkuu. Bila kusahau biashara yake ya dhahabu.
Sipati picha alivyopata usumbufu huko PM.
Mhh mtafanya watu wasiwe wanaweka thread zao humu kama kweli ndivyo ilivyokua kuna ubaya kuongea?? Acheni wivu
 
Huyo mchungaji anataka kukupiga pesa tu,na sisi tulio na makaburi majumbani kwetu mbona kila siku tuna mandinga mapyaaa,yoooh!!
Mkuu baadhi yetu sisi Wafrika tunasafari ndefu sana ya kukombolewa kifikra.....

Jamaa badala ya kutafuta suluhu ya ajali na kufilisika anatafuta mchawi wa matatizo yake..

Na haya matapeli ya kilokole, yanajua mahali pa ku-hit kabisa..mwisho wa siku watamwambia hao waliokufa walikuwa wachawi hivyo atoe sadaka ya kufunguliwa mti wa ukoo na laana....Jamaa alivyo zuzu atatoa bila kujua anazidi kufilisika huku mchunguji akizidi kunufaika...
 
Hata wewe una element za kishirikina mkuu, kwa nini uende kusafisha makaburi saa kumi na mbili jioni na si asubuhi? Sisi tunasafisha makaburi kila mara na hakuna tabu tunayopata.
Kweli alienda jioni mnoo asubui ni nzuri zaidi
 
Mhh mtafanya watu wasiwe wanaweka thread zao humu kama kweli ndivyo ilivyokua kuna ubaya kuongea?? Acheni wivu
Utakuwa ni mmoja wa wasumbufu wa PM wewe. Pole sana binti.
Wivu kwa porojo za JF? Tehe tehe...... Just Tehe tehe.
 
Huyo n mchungaji uchwara, siwez acha kupariria kaburi la mama yangu kamwe, uniambie sijui biashara ya mapepo sijui upepo. Na ndo kwanza nikiendaga kijijini nikirud mjini ndo natusua. Wewe kuna jambo uliwauzi wenye makaburi yao sio siri, kaa utafakari.
Na kupalilia ni kufanya usafi kama usafi mwingine...

Hapo Mchungaji ameshajipatia mgodi wa kuvuna mapesa....maana jamaa ameshatekwa akili yake kuwa matatizo yake yamesababishwa na kupalilia makaburi..hivyo tegemea aambiwe yafuatayo

Atoe sadaka ya ukombozi kwa familia..
Atoe Sadaka ya kuvunja laana...
Atoe sadaka ya kung'o mti wa Ukoo
Atoe Sadaka ya kusafisha nyota yake...

Atatoa sadaka mpaka siku anaingia kaburini....
 
Utakuwa ni mmoja wa wasumbufu wa PM wewe. Pole sana binti.
Wivu kwa porojo za JF? Tehe tehe...... Just Tehe tehe.
Hahahha naanzaje kumfata mtu pm kwa kipi labda. Nimekushangaa wewe the way umecoment. Katika kitu ambacho sitakuja kufanya humu JF ni kumfata mwanaume ambae simjui PM
 
Adhabu ya nyumba unayoishi jirani na makaburi
Siafu hawaishi ndani...cha ajabu wanazuka ghafla tu hao siafu.
Kingine Nyoka Yaani utasingizia mashimo mara nyumba ina vichiguu pembeni
Lkn habari ndio hio,,
Kama utabisha au kupinga hili swala labda ulipinge tu humu JF lkn ukwrli ndio huo
Hayo maswala ya mapepo sijui uchawi hata mm nayaskiaga tu
Ni kweli Karisa. Hilo la siafu. Na nyoka
 
Huyo mch alikushauri vizuri. Mtu anapokufa Mungu huondoa ulinzi wake kwasababu imeandikwa Mungu si Mungu wa wafu... Hivo baada ya mtu kufa malaika huondoka na shetani huleta wa kwake na kufanya maskani tulivu kwao. Ndo maana wachawi, washirikina maeneo ya makaburi ni sehem muhimu sana kwao kwasababu ni maskani ya mashetani, ni maeneo ambayo hakuna roho wa Mungu wala malaika watakatifu, ni maeneo huru kwa shetani.
Hivyo Mungu aliumba hii dunia, kisha baadhi ya maeneo akamwachia Shetani ajivinjari na maeneo mengine akayapa ulinzi...?? Huyo mungu wako atakuwa mpumbavu kupita kuasi...

Mungu wangu ni muweza wa vyote, na kila kitu kiliumbwa na yeye na Mungu wangu yupo mahali pote(Kila mahali)
 
Tatizo sio makaburi. Tatizo ni nini ulichoenda kufanya makaburini. Wengi huenda makaburini kufanya ibada ya wafu bila kujua. Na inawezekana wakati unapalia makaburini uliingia katika hisia na kujikuta ukiabudu na kutambikia kwa mawazobi mwako. Sijui wewe ni wa imani gani, Lakini kwa wakristo, hawapaswi kufanya matambiko kama vile kumwaga maji, au pombe, juu ya kaburi. Hilo ni tambiko ambalo moja kwa moja unaamsha mzimu wa mfu . Jambo hilo MUNGU amelikaza ni sawa na kuabudu wafu. Vile vile yawezekana tatizo lako likatokana na kazi yako ya machimbo. Tumeona wengi waliotajirika kwa njia ya machimbo hasa ya dhahabu, wameishia katika kufilisika. Wengi kati ya wachimba dhahabu huwa wanaaguliwa na waganga ili kupata utajiri( ndagulwa au ndagu kwa kisukuma).
Wanapokiuka masharti, hupatwa na kama yaliyokupata wewe. Je, wewe halo makaburini ulipoenda kupalilia makaburini, ulikuwa na lengo gani, kupalilia au kufanya ibada ya mizimu( wafu)?.
 
Nenda kanisa la eagt city centre kwa pastor katunzi liko mtoni mtongani ,baada ya kuvuka reli inayopita juu,huyo pastor atakusaidia kwa maombezi umefungwa na mapepo,nimeona kwa macho mtu mwenye tatizo kma hilo lako likiisha bure kabisa ibada pale ni kila siku,mwamini Mungu ukifka pale utapona unaweza omba onana na pastor mwenyewe pastor katunzi.
Naona unamuunganisha kwa mganga mwingine wa kienyeji(mchungaji)....Vipi mtoa mada alisema alishamuona mchungaji ndo akamwambia kilichokuwa nyuma ya pazia..

Au unataka kutuambia yule mchungaji wake hana nguvu..?? Na nguvu zipo kwa huyo katunzi.. ??

Huu si Uganga wa kienyeji huuu...?? Maana atakuja mwingine atamwambia aende kwa mwingira ndio kiboko, kakobe, transformer....Yani hakuna tofauti na waganga wa kinyeji...

Maana mimi nilizoea kusikia, njoo kwa mganga huyu au yule, au mganga wa Sumbawanga, ni koboko, wa Tanga ni mwisho wa Mambo, wa bagamoyo ni komeshs.
Ila leo mambo yamebadilika . waganga wa kienyeji wamekimbilia makanisani..


Walokole na Wapentekoste mnatuharibia Ukristo
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
It's not a loughing matter my dear!!! Inasikitisha sana.....Wachungaji siku hizi ndio wamekuwa wachonganishi na kuleta chuki na visasi kwa jamii

Nimeshuhudia mtu akimuita mama yake mchawi kisa mchungaji amefunuliwa na roho kuwa mama yake ni mchawi...sasa hapo kuna tifauti gani na waganga wa kienyeji
 
Back
Top Bottom