Kilichonikuta baada ya kupalilia makaburi

Kilichonikuta baada ya kupalilia makaburi

Hakufanya sala huyo yakuwaombea .
Sasa mkuu kova kama ilitakiwa awaombee ili asipatwe na yalompata basi ubora si kuwaombea wao kwanza, bali yeye amwombe yule ambaye alitaka kuwaombea wale ili amlinde yeye na familia yake katika hilo jambo.
Lakini pia makusudio yake ni nini kwenda kupalilia makaburi? je ni usafi kama kawaida ya kusafisha baada majani kuota kwa wingi au na yeye ana imani fulani kuhusiana na hayo makaburi, kama nafsi yake ina imani fulani ya kuamini hayo makaburi yana nguvu flani au uwezo wa kunufaisha au kudhuru basi kwa yeye kupatwa na yalompata hili ni jambo tegemewa.
 
Mtoto ambaye hajaanza kuongea huwa anaona vitu vingi sana ,ila hawezi kukueleza.Akianza kuongea na uwezo wake wa kuona vitu unapotea kabisa.
 
Na wasiwasi na hayo madini ukumpiga mtu?ongea ukweli mkuu maana biasahara za madini imejaa utapeli sana.
 
Mchungaji alipata mteja wajinga ndio waliwao.Mtu akizikwa ni end of story mtu akiwa maiti hana tofauti na nyau au ng'ombe aliyekufa binadamu tunawapa heshima tu vile tuna akili.Je wanaochomwa nao tusemeje.Kuna baadhi ya madhehebu wana amini kufanya hivi ni makafara.Hebu kampime mwanao malaria na polisi wapime chanzo cha ajali.Wewe mwenyewe umerahisa jibu ulikuwa speed kali.Ungekuwa 50km/hr au 80km/hr isingetokea tuache kila baya tunamsingizia shetani siku ya mwisho anaweza muambia mungu mengine wananisingizia.Migodini hasa binafsi wanakufa sana mtasema shetani wakati mtatumia majembe?Akili kichwani jiongezeni
 
naomba ni pm please naweza kuwa msaada wako mkubwa na ukarud kwenye hali yako
 
Huyo mchungaji anataka kukupiga pesa tu,na sisi tulio na makaburi majumbani kwetu mbona kila siku tuna mandinga mapyaaa,yoooh!!
Ya nyumbani hayana shida ila yale ya jumuiya ndo marubani(wachawi) huwa wanafanya yao, mara ngapi ushasikia stori za watu kuoga makaburin, sijui nini na nn waganga wanakutuma ukazindike makaburini nk.
 
Mleta mada naomba utujuze kwa haya.....hivi huyo mchungaji wako ni Gwajima au Mama Rwakatare?
 
Mkuu baadhi yetu sisi Wafrika tunasafari ndefu sana ya kukombolewa kifikra.....

Jamaa badala ya kutafuta suluhu ya ajali na kufilisika anatafuta mchawi wa matatizo yake..

Na haya matapeli ya kilokole, yanajua mahali pa ku-hit kabisa..mwisho wa siku watamwambia hao waliokufa walikuwa wachawi hivyo atoe sadaka ya kufunguliwa mti wa ukoo na laana....Jamaa alivyo zuzu atatoa bila kujua anazidi kufilisika huku mchunguji akizidi kunufaika...

Bwahahahaaaaaa,kweli kabisa mkuu
 
Yani hakuna uhusiano kabisa...ameungaunga matukio ya yeye kupata ajali na kufilisika akaunganisha na kusafisha makaburi ili apate sympathy ya matatizo yake....

Yani badala ya kutafuta suluhu ya matatizo yake, yeye anatafuta nchawi...
Hatari aisee kama ndio mwendo huu
 
Hapo alikuwa anawajulisha wanawake humu JF ya kwamba mwaka 2011 alikuwa na milioni 60 Benki na alinunua gari ya milioni 15 mkuu. Bila kusahau biashara yake ya dhahabu.
Sipati picha alivyopata usumbufu huko PM.
Aiseeh
 
Back
Top Bottom