Kilichonikuta baada ya kupalilia makaburi

Kilichonikuta baada ya kupalilia makaburi

Naomba uniunganishie scenarios zote nipate kukuelewa
 
Sema mkuu hizo dhaabu ulizokwenda uza dar ulizipata kihalali au kuna mkono wa dhulma ndani yake?

Hata kama kuna dhuluma hiyo haitoshi kumfanya apate ajali ya gari au afisilike. Kwenye gari ilitosha tu achukue tahadhari kabla ya kuliingiza barabarani: aikatie comprehensive Insurance na awe dreva mweledi. Hakuna uonevu wala dhuluma inayoweza kumupotezea mtu mali zake.Malipo ya mwenendo mbaya wa mwanadamu ni mpaka siku ya mwisho na sio wakati mwingine wowote.Kuna watu huwa wanapoteza muda wao kuwaombea watesi wao mabaya;sala kama hizo hazina nafasi.
 
Hivyo Mungu aliumba hii dunia, kisha baadhi ya maeneo akamwachia Shetani ajivinjari na maeneo mengine akayapa ulinzi...?? Huyo mungu wako atakuwa mpumbavu kupita kuasi...

Mungu wangu ni muweza wa vyote, na kila kitu kiliumbwa na yeye na Mungu wangu yupo mahali pote(Kila mahali)
Endelea kupiga ishara ya msalaba makaburini omba kwa wafu watakuombea kwa mungu wako
 
Endelea kupiga ishara ya msalaba makaburini omba kwa wafu watakuombea kwa mungu wako
Kama unadhani Roho ya mtu inapotea ni bora ukayapitia hapa

Mhubiri 12:7
Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa,
Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
 
huyo mwenye kaburi alikuwa na kinyongo na wewe hivyo hakutaka umzike wala ufike kaburini kwake wewe na kimbelembele chako ukaenda ukajifanya unampaenda ilhali wakati yupo mzima hukumsaidia chochote hata muda wa kuumwa kwake. funzo .mkikaa mjini msiwasahau wa nyumbani hasa mama, mamaakikununia na hatari sana akisema nukifa usije nizika pliz usiende otherwise solve mapema b4 her death. kilio cha mama ni hatari
 
Sitasahau maishani mwangu, ilikuwa ni mwaka 2011 niliposafiri na mke wangu pamoja na mwanangu kwenda nyumbani kijijini kusalimia.

Wakati huo mwanangu alikuwa na umri wa mwaka mmoja tu,baada ya kufika nyumbani tulipumzika na kisha kesho yake mida ya saa 12 jioni tulielekea makaburini mimi na mke wangu na mtoto wetu alibebwa mgongoni ,na mimi nilibeba jembe.

Baada ya kufika tu makaburini ,mwanangu aliyekuwa amelala mgongoni aliamka na kisha akaanza kupepesa macho huku na kule,akishangaa mandhari ya makaburini,mimi nilianza kupalilia makaburi na dk 5 baadaye mtoto akaanza kulia,mama yake alimshusha mgongoni ili amnyonyeshe lakini ndo alizidi kulia kana kwamba anachomwa moto.
Tulijaribu kumbembeleza mtoto lakini ndo alizidi kulia kwa kasi ya kutisha,sijawahi kuona mtoto akilia kama mwanangu siku hiyo .

Mtoto alilia hadi tukarudi nyumbani,kufika nyumbani ndo alilia zaidi huku akitutazama kwa jicho la huruma,hakuwa ktk hali ya kawaida hata uso wake ulibadilika kabisa.
Nakumbuka siku hiyo tulishindwa hata kula,mida ya saa 4 usiku mtoto alitulia akalala,tukabaki tunajiuliza ni kitu gani kilitokea,kesho yake nilipanga kuanza safari ya kwenda Dar kununua gari,nilikuwa na pesa za kutosha Benk zaidi ya sh mil 60 nilizokuwa nimezipata kwa biashara ya Dhahabu .

Siku nyingine iliyofuata nilianza safari ya kwenda Dar,nilifika salama na kufanikiwa kununua gari zuri la kutembelea,kutokana na uzoefu wangu mdogo wa kuendesha magari ilinibidi nikodi dereva,tulipokaribia kufika Manyoni Singida saa moja usiku,gari iliacha njia ikapinduka tukiwa na mwendo kasi,ajabu tulipona wote ila gari ikaharibika vibaya mno,kama ungeiona usingeamini kama watu walisalimika.

Gari ya sh mil 15 haikutamanika hata kidogo,usiku wa manane tukiwa pale msituni baada ya gari letu kupinduka,tulivamiwa na kundi la watu wasiojulikana,wakatupora kila kitu na jambo la kushangaza walikuwa na vifaa vya kufungua na kuchukua spea za gari,walichukua hadi tairi.

Alfajiri ikapita patrol ya police na kutupeleka hadi Manyoni mjini.
Nilirudi nyumbani nikilia kwa huzuni,mke wangu akanipa moyo,baada ya hapo niliendelea na bishara zangu nikaanza kufirisika tu,kila nalofanya haliendi,nikauza kila kitu hadi nyumba na kwenda kupanga,nilirudi nyuma na kuwa maskini wa kutupwa.
Hadi chakula na sabuni ya kuogea ama kufulia tu ikawa shida kuipata.

Nilimfuata mchungaji wa kanisa moja moja nikamwelezea mkasa wote,akaniambia ni hatari sana kuweka mazoea na makaburi,mtu anapokufa na kuzikwa,yeye halisi huondoka kabisa duniani na pale kaburini hubaki mwili tu ambao hauna uhai kama jiwe.
Kwa hiyo,mapepo ya uharibifu hukaa makaburini yakijua kuwa mwanadamu ni lazima ataenda makaburini kwa sababu hana maarifa ya kujua hatari za makaburi,wachawi nao hutega mikosi yao huko wakijua kuwa watu wengi hawajui undani wa makaburi na hivyo ni lazima waende huko,Na ndo maana mwanangu alikuwa akiyaona yote hayo ila kusema hawezi.

Wakuu, hiki ni kisa cha kweli kabisa.
Unaposema mtu akifa yeye halisi hutoweka na mwili ndo unabaki unamaanisha kusema halisi .
 
Kuna vitu jamaa ameskip kwa manufaa yake na kuilinda famili yake isijulikane humu. Kiufupi watoto baadhi huwa na uwezo wa kuona vitu ktk ulimwengu wa kiroho(hii ninauhakika nayo imeshayoke ktk falimia).

Kikubwa hapa si kuwa karibu na makaburi bali ni kujiungamanisha na kaburi ktk ulimwengu was kiroho ndiyo tatizo la huyo jamaa lilivyokuwa. Huwezi kufunga safari hadi mkoani just kwenda kufagia makaburi tuu bila kuamini utendaji wake kiroho. Jamaa ameskip vitu lakini nimemuelewa.
 
Back
Top Bottom