Mkuu
Malafyale nikuambie kitu? Dada zako wana thamani kubwa sana ndiyo maana wakapata waume wa kuwaoa! Thamani ya mtu huwa ipo pale anapojijengea tabia ya kujiheshimu na kuheshimu wenzake akiambatanisha na sifa ya kuwa mkweli! Mtu kuzalia nyumbani bila kuolewa/kubakwa na akajiongezea tabia ya kusema UONGO tayari huyo heshima yake ipo chini na vivyo hivyo thamani yake ya kuwa mke inakuwa imeporomoka! WANAWAKE WOTE WANGEKUWA NA THAMANI SAWA YA KUWA MKE basi pasingekuwepo na kuhangaika kuchagua mtu anayefaa kuolewa/kuwa mke tena aliye mwema, tungekuwa tunaoa yeyote tu! Na vivyo hivyo hata kwa wanaume! Na hapa tunazungumzia THAMANI YA KUWA MKE/MME ANAYEFAA, siyo bora mke/mme!
Ila kwa thamani ya kuwa ni 'binadamu' ipo pale pale tu kwa wote bila kujalisha alizaa kabla hajaolewa au ndani ya ndoa!
Baba yako nampa hongera kwa kuwalea vyema dada zako mpaka wakapata waume wa calibre waipendayo ambao najua walikuwa willing kulipa mahari ifaayo lakini mzee kwa mtazamo wake akaona ni vyema watoto niwape familia/jiko na la mahari halina thamani kwangu!! Hata mie nimeipenda!!