Kilichomtokea rafiki yangu ni funzo kwangu

Kilichomtokea rafiki yangu ni funzo kwangu

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
496
Reaction score
379
Tunafanya naye kazi hapa, alimchumbia binti, alipomuuliza kama ana mtoto binti akakataa kuwa hana, alimuuliza kama mara tatu binti akasema hapana sina.

Wiki iliyopita acha ya juzi tulienda kwao kupajua na kujitambulisha rasmi tulikaribishwa vzr tukakaa na kula then mazungumzo na binti pamoja na rafiki yakaanza baadae wazazi wake waliitwa.

Baada ya kujitambulisha pale na kuzungumza nao ukafika muda tukaaga kuondoka ili tukalale guest then kesho yake tuondoke, tukiwa njiani kuelekea guest baba yake akampigia simu na kumwambia asiende kulala hadi afanye uchunguzi kuhusu binti huyo, tulishirikiana pale kufanya uchunguzi ndipo watu watatu tuliowahoji kwa muda tofauti wakisema kuwa huyo binti ana mtoto wa kiume alimpata akiwa shuleni.

Tuliishiwa nguvu lakini nikampa moyo rafiki yangu sasa akaamua kumpigia tena simu binti huyo akamuuliza tena kama ana mtoto yaaan ndipo akakili kuwa ni kweli na mtoto ni wa kiume.

Du! alipomwambia baba yake akasema haina shida hata kama ana mtoto cha msingi anachojua ni kuwa mtoto wa kiume kwa kabila la wanyantuzu huwa anakuwa upande wa ujombani.

Rafiki yangu akatafakari sana kisha akamwambia baba yake kuwa sawa wajiande waende kupanga mahari ila akatoa conditions kuwa mahari isizidi milioni moja ikiwa watashindana basi warudi tu. Baba mtu wakaenda juzi Jumamosi na wakaambiwa ngo'mbe 13 mbuzi 2 na kitenge wax moja, mzee akakubali na ktk pesa ngo'mbe 13 ni sawa na T.shs. milioni 1 laki 7 hadi 8 sasa baba mtu kumwambia kijana wake kijana amekataa kata kata kuwa hiyo mahari ni kubwa ukilinganisha na hadhi ya huyo binti.

Kasema nimshauri jamani ushauri wenu hapa ni muhimu, je amuache? Kijana ana 28 yrs old na binti ana 21 yrs.
 
Hadithi nyingine tamu, huyu binti kwa miaka 21 leo,alizaa lini na kumlea lini huyo mtoto na shule ya msingi alimaliza na umri gani ?
 
Mambo ya kukutana na binti mwenye mtoto..mimi sisemi hapa ni majanga..
 
Hadhi ya binti ipi? Kisa ana mtoto?
hivi nyie mnaowachukulia negative mabinti wenye watoto huwa mnawaza nini?
mtoto/watoto si kitu kwenu?kuna watu wanakunywa dawa za miti shamba, wengine kutwa kukimbiza majogoo kwa waganga
ili wapate mtoto.....!!!
mtoto ni majaaliwa ya mungu sio mpango wa binadamu, hamtaki binti asepe zake
 
Kama anaona thamani ya mchumba wake imeshuka si amuache tu, akatafute wenye thamani wenzake. Kwa hiyo yeye kaona huyo binti ana thamani ya 1 M?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hadithi nyingine tamu, huyu binti kwa miaka 21 leo,alizaa lini na kumlea lini huyo mtoto na shule ya msingi alimaliza na umri gani ?

mkuu amini nachokwambia mm binti ana mtoto na kwa maelezo yake ana 21 yrs unless awe amemdanganya tena rafiki yangu kwa mara nyingine! cha ajabu binti ni mwalimu wa primary kaajiriwa mwaka huu alisoma katoke TC.
 
Hadithi nyingine tamu, huyu binti kwa miaka 21 leo,alizaa lini na kumlea lini huyo mtoto na shule ya msingi alimaliza na umri gani ?

Amini nachokueleza mm, yawezekana binti kamdanganya jamaa tena!!!!! but hayo ndo maelezo yake.
 
Hadhi ya binti ipi? Kisa ana mtoto?
hivi nyie mnaowachukulia negative mabinti wenye watoto huwa mnawaza nini?
mtoto/watoto si kitu kwenu?kuna watu wanakunywa dawa za miti shamba, wengine kutwa kukimbiza majogoo kwa waganga
ili wapate mtoto.....!!!
mtoto ni majaaliwa ya mungu sio mpango wa binadamu, hamtaki binti asepe zake
Eve bwana, unajifanya huelewi kinachoendelea hapa!!!
 
Mahali kubwa mno ukilinganisha na HADHI ya binti...mmmhhhh
 
Hivi wanaolewa bure bila mahari hawana thamani?
Tatizo kwa waafrika wengi na hususani kama ni wanyantuzu, bride price is what it is "bride price", ni bei. Kwa upande mwingine hao wanaoolewa bure inawezekana hilo neno "bure" linatumika kimakosa kwa sababu muktadha wa ndoa kwao ni tofauti kidogo kwa maana ni muungano wa binadamu wawili zaidi wapate kuishi pamoja kuliko kuwa biashara ya mwanamke.
 
Hivi wanaolewa bure bila mahari hawana thamani?

Kinachomuuma rafiki yangu ni kuwa,

Binti alimdanganya awali,

Ukweli kaupata kwa watu wengine,

hivyo alitegemea mahari ishuke kwa sababu tayari binti ni used na c fresh.
 
Back
Top Bottom