Ayaaaaaa....kwa hiyo siku zingine siongeagi pointi?
Nilidhani umetoroka kwa kaka btw
Mimi hata sijasoma.....ka gazeti...!
Umeona Elli tena ni unafiki mkubwa unaweza kukuta huyo anaejifanya hataki kuoa msichana aliezaa nae ana wtt kama 6 hivi aliowakataa kama si umburula ni nini?Yeyek akimuoa anatarajia kupata nini kama sio watoto! Tuache unafiki wa kujifanya wasafi
Amesoma sema hataki kuelewa tu!Mmmmmh Ngoja @ Muuza ubuyu aje!
Damaged goods....
Kinachomuuma rafiki yangu ni kuwa,
Binti alimdanganya awali,
Ukweli kaupata kwa watu wengine,
hivyo alitegemea mahari ishuke kwa sababu tayari binti ni used na c fresh.
Asimuoe!
Atampata atakayemthamini pamoja na kuwa amezaa!!
Eti hadhi ya bint,yeye kijana ana hadhi gani?
Kisa siyo kuzaa! Tatizo mwanamke mwenzenu ameficha issue ya kuwa na mtoto kwa jamaa kila anapoulizwa kuhusu hilo kwa zaidi ya mwaka mzima mpaka jamaa akaja kugundua kivyake vyake ndipo binti kukiri! We hapo huoni shida? Msitetee upuuzi wa huyo binti! Kama anaweza kukana mtoto wake huoni kwamba anaweza fanya mambo mengine na yakaleta madhara ndani ya ndoa yake? That lady is stupid indeed!Amwache asimuoe, atakuja kumsumbua tu huyo binti kisa mtoto, hapo alipo upendo umeshapungua sana kisa kagundua ana mtoto, hadi kuagiza mahari isizidi 1m inamaana akimapata sawa asipompata pia ni sawa tu kwake, mshauri atafute bunti mwingine asiye na mtoto ila mwambie na dadake nae akizaa kabla ya ndoa atanyanyapaliwa hivyo hivyo
Kongosho, hivi Mahari uwa yanatoa taswira ya "thamani" ya mwanamke? Ufafanuzi tafadhali...!
Hata humu mpo mliozaa bila kuolewa wanawake kwa wanaume! Wote tunatenda makosa, ila usiongeze kosa juu ya kosa! Ukipata mtu mkapendana MUELEZE WAZI si kumficha, utaharibu msikabali wa mahusiano/ndoa yenu!
Maskini....tunathaminishwa kama bidhaa dukani
Kisa siyo kuzaa! Tatizo mwanamke mwenzenu ameficha issue ya kuwa na mtoto kwa jamaa kila anapoulizwa kuhusu hilo kwa zaidi ya mwaka mzima mpaka jamaa akaja kugundua kivyake vyake ndipo binti kukiri! We hapo huoni shida? Msitetee upuuzi wa huyo binti! Kama anaweza kukana mtoto wake huoni kwamba anaweza fanya mambo mengine na yakaleta madhara ndani ya ndoa yake? That lady is stupid indeed!
Mimi kuoa mwanamke aliyezaa kabla ya kuolewa ninaweza kumwoa, ila awe muwazi tangia mwanzo hata bila ya mimi kumuuliza! Nitakachoangalia tu ni mazingira aliyompatia huyo mtoto kama hayatakuwa na negative impacts kwenye ndoa yetu na tabia yake ikawa nimeridhika nayo basi, naweka ndani mara moja bila simile!