Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Kwa maneno haya machache ya kiushabiki bado hujamsafisha na tuhuma zake!yeye ni mwanadamu.....je anatuhumiwa kwa makosa gani?mbona hujayaandika hapa na kuchambua moja baada ya jingine ili udhibitishe usafi wake?mahakama ni chombo cha haki. ....tusubiri!
Nani kaandika kumsafisha?
 
Wanamuonea!
Mungu atakusimamia usife moyo Mhando
Ni mapito tu!
 
Kwani mtu hawezi kuwa mwanahabari huru halafu akawa fisadi?
 
Hivi una uhakika na uliloliandika hapo" mkurugenzi wa BBC wa kwanza mweusi??? Hebu acha kulisha watu matango pori hajawahi kushika hio post na haitatokea kamwe mweusi kua mkurugenzi wa BBC. Kama una maana BBC swahili services nitakuelewa maana hako ni ka dept kadogo ka BBC Africa.naomba kuwakilisha hoja.
Kwahiyo hajawa Mkurugenzi BBC?
 
Kinyongo cha CCM dhidi ya Tido ni pale aliporusha midahalo ya wagombea ubunge majimboni la ajabu CCM waligoma kushiriki wakidai siyo sera yao kuwajuza wananchi juu ya wasifu na malengo ya kugombea ya wateule wao.

Baada ya hapo, JK kwa ghadhabu kubwa alitengua uteuzi wa mwathirika huyu wa umangimeza wa CCM!

Leo azushiwa jinai za manunuzi huku haohao leo wananunua from single source mifano mfukoni lakini.

Hata kandarasi kubwa kubwa waheshimiwa hawa hudai..."waachiwe wao" kwani mkandarasi tayari wanaye mfukoni.

Sijui wako juu ya sheria au kuna nini hapo.

Sheria ya manunuzi inaruhusu single sourcing sasa uhujumu uchumi unachipukia wapi?

Viwanda vya kusulubiana kwa sababu za chuki na vinyongo vya kisiasa ni tishio kwa usalama wa taifa!

Acheni uhasama tujenge nchi, pliiiiiiiiiiz

SAHIHISHO CHA KICHWA CHA HABARI

Siyo uwaziri bali uwazi

Tido akili yake ni zaidi ya ccm wote ndo maana wanamhofia huko azam atawachana bila kupapasa macho
 
Mzee Tido kwa ujasiri wako katika fani ya utangazaji mwenyezi mungu atakulinda kwenye mtihani huu.
 
Mkuu unamung'unya maneno ya nini? Nani alishiriki tenda ya Bombadier? Nani alishiriki kwenye tenda ya ujenzi wa uwanja wa ndege Chattle? Je, wao hawatumii madaraka vibaya?
Hawawezi.kudili na Bakhresa mmiliki wa kityo imebidi waanza na Tido.
 
Tulikubaliana kutokufukua makaburi. Inakuwaje sasa tunafukua makaburi kwa visasi?
 
Namuonea huruma mzee Tido mhando kufanya kazi nchi hii shida angebakihukohuko mbele
 
Tunachukia watu smart kwa ajili ya ujanja ujanja tu.
Siku tukifanikiwa kuacha "personal sentiments",tutapiga hatua sana.
 
kilichomponza ni ufisadi wake ameiba kodi za watanzania wanyonge CHADEMA acheni kutetea wahalifu
Waweza kuwa na hoja nzuri sana Mkuu,na hii inanifanya nijiulize maswali mengi sana!!
Tido amefikishwa mahakamani kwa sababu ya ufisadi,(kwa madai yako)
Mbona Lowasa mpaka sasa hapelekwi Mahakamani??
Au yeye ufisadi wake ni was aina gani tofauti na wa Tido?
 
Ufisadi gani

Vp kuhusu chenge aliyekiri kupokea kabisa pesa za rada lakin had Leo kapewa nafasi ya uenyekiti bungeni
Kuna wezi wengine wa escrow walitaka kurudisha hela walizoiba,lkn zilikataliwa,na mpaka Leo wanapeta mjengoni.
Hii n chuki ya dhahiri na double standard.
Ufisadi wa 2008,ndio unakumbukwa lkn wa juzi tu haukumbukwi?
 
Kinyongo cha CCM dhidi ya Tido ni pale aliporusha midahalo ya wagombea ubunge majimboni la ajabu CCM waligoma kushiriki wakidai siyo sera yao kuwajuza wananchi juu ya wasifu na malengo ya kugombea ya wateule wao.

Baada ya hapo, JK kwa ghadhabu kubwa alitengua uteuzi wa mwathirika huyu wa umangimeza wa CCM!

Leo azushiwa jinai za manunuzi huku haohao leo wananunua from single source mifano mfukoni lakini.

Hata kandarasi kubwa kubwa waheshimiwa hawa hudai..."waachiwe wao" kwani mkandarasi tayari wanaye mfukoni.

Sijui wako juu ya sheria au kuna nini hapo.

Sheria ya manunuzi inaruhusu single sourcing sasa uhujumu uchumi unachipukia wapi?

Viwanda vya kusulubiana kwa sababu za chuki na vinyongo vya kisiasa ni tishio kwa usalama wa taifa!

Acheni uhasama tujenge nchi, pliiiiiiiiiiz

SAHIHISHO CHA KICHWA CHA HABARI

Siyo uwaziri bali uwazi
c1fd90915e6d207add4b230fd8ee389f.jpg
 
Kuna Uzi Upo humu unaonesha investigation ilianza 2011 . tuache siasa za kuzusha mambo.
 
Tido ni mtu muhimu kwa ustawi wa media.He is confident and creative journalist and a real passionate leader.
Kawaida yetu ni kuchukia watu wetu hasa wenye weledi wa mambo.
Anyway tutafika tu.
Nashukuru kama umelitambua hilooo.... kwakweli tz kunashida kubwa sana Mr. Ukiwa mzalendo ndio unaonekana mchochezi wa mambo, hufai wala huna maana.
 
Kuna wezi wengine wa escrow walitaka kurudisha hela walizoiba,lkn zilikataliwa,na mpaka Leo wanapeta mjengoni.
Hii n chuki ya dhahiri na double standard.
Ufisadi wa 2008,ndio unakumbukwa lkn wa juzi tu haukumbukwi?
Na je, hivi yoka kipindi hicho hakuna aliyekuwa akijua kuwa TIDO MUHANDO alikuwa amefanya ubadhirifu wa fedha hizo?
Watanzania tujiulize kabla ya Tido kupewa ukurugenzi wa TBC, je ipi ilikuwa nafasi ya TBC kama chombo cha utangazaji cha taifa, na pia wapi ameifikisha?.
Nijuavyo TBC imetambulika sna wakat bwana mkubwa TIDO anashikilia uongozi pale.

Sijui sasa Tanzania tunahitaji wazalendo wa aina ipi ambao kwa hao tutakili kuwa wamelitumikia taifa letu vyema.
 
Back
Top Bottom