Beka Mpole
JF-Expert Member
- Feb 4, 2017
- 490
- 375
Tulikua tunafanya uchunguziHuo ufusadi ndo wanauona Leo auditors walikua likizo? Ukurupukaji. com. Watashindwa except Kama no maagizo kutoka juu.
Tulikua tunafanya uchunguziHuo ufusadi ndo wanauona Leo auditors walikua likizo? Ukurupukaji. com. Watashindwa except Kama no maagizo kutoka juu.
Wewe lazima ni juha la kutupwa, zilizopo ni tuhuma ndio maana amepelekwa mahakamani. Mahakama ndio itatoa ukweli kama tuhuma ni za kweli ama la. Vipi sasa wewe huo unauita ufisadi wake unaushahidi wowote. Acha ushabiki wa ki pimbi na kipumbavu.kilichomponza ni ufisadi wake ameiba kodi za watanzania wanyonge CHADEMA acheni kutetea wahalifu
Muosha huoshwaTulikua tunafanya uchunguzi
Well said mkuuTIDO MHANDO!
Aliombwa na Rais JK kuja kuifufua na kuiokoa TBC, Tido akaifanya kazi hiyo kufa na kupona na TBC ikaimarika, ikawa Shirika halisi la Utangazaji la Taifa. Tangu Tido aondoke TBC shirika hilo limegeuka kuwa tawi la CCM na Serikali na si chombo cha wananchi.
Malipo anayopewa Tido ni hili la kuisababishia hasara serikali ya Shilingi Milioni 800. Sawa, sote tunajua kuwa mahakama itaamua, tuiwache iamue na ukweli utajulikana mbeleni.
Lakini wakati Tido akipandishwa kizimbani kwa kutuhumiwa kufanya ubadhirifu wa Shs. Milioni 800, wako magwiji wazito wa rushwa na ufisadi wenye ushahidi wa wazi ambao hawaguswi.
Mmoja wa magwiji hao ni Andrew Chenge, Chenge wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) alihusika kwenye mikataba mibovu ya ununuzi wa rada, kisha akapewa mgao (rushwa) ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1 za Kitanzania. Ufisadi mkubwa!
Benki iliyowekewa fedha hizo ilihakikisha kupokea fedha hizo. Chenge mwenyewe alikiri kuwa amewekewa fedha hizo, tena akiziita vijisenti - hadi leo Chenge yuko huru, tena CCM na Bunge wamemchagua kuwa Mwenyekiti mmojawapo wa bunge letu tukufu.
Chenge, aliyekiri mwenyewe kuhongwa fedha za rada na kuliletea taifa hasara za mabilioni ya fedha leo anapandishwa vyeo na yuko huru. Tido ambaye aliinua TBC kitaifa na kimataifa yuko kizimbani kwa tuhuma nzito.
By the way, tangu Azam TV warushe mahojiano ya Tundulissu kwa kirefu na kwa uwazi, nilijua Tido na wenzake wanapaswa kujichunga. Serikali za Ki-Afrika huongoza kwa kutumia madaraka yake vibaya, zikiona mtu fulani anazivua nguo kwa mabaya yake, humwandama mtu huyo hadi anyooshe mikono.
Ni visasi juu ya visasi, ni kuwaumiza watu wasio na hatia kwa sababu ya misimamo yao. Tuliyaona kwa Yusuph Manji (japo yanatofautiana kidogo) lakini ajenda za maovu hayo ya dola dhidi ya watu wenye misimamo fulani, hufanana! Tumeona maaskofu wenye misimamo ya kuionya serikali wakihojiwa juu ya uraia wao, bila sababu - tumeona wabunge wanaoikosoa serikali kwa nguvu wakifunguliwa mashtaka kila uchwao. Ni uhuni juu ya uhuni!
Inatia hasira sana pale unapoona mafisadi wakuu wa ESCROW, EPA, RADA, NDEGE YA RAIS n.k. wakiwa mitaani wanakula raha, halafu watuhumiwa wa makosa ya kutengenezwa wanafikishwa mahakamani.
Tanzania yetu inaendeshwa kwa Double Standard za hali ya juu. Wapo wala rushwa na watoa rushwa wakubwa, wengine hadi wamerekodiwa wakishiriki vitendo vya rushwa, matokeo yake wanapandishwa vyeo.
Safari ya Taifa letu na wanataifa wake ni ndefu.
[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J
Kwani mafisadi wengine waliowahi kushtakiwa hakuna mema waliyowahi kufanya hapa duniani?Akiwa BBC Nairobi miaka hiyo aliingia matatizoni na serikali ya Rais Moi kwa kufichua mauaji ya Robarth Auko. Wakenya wengi na serikali walikuwa wakidhani Tido ni Mkenya lkn kumbe alikuwa ni Mtanzania.
Alikuwa akiwindwa sana na kwa sababu hizo BBC ikamuondoa Kenya na kumpeleka London. Akiwa London alifanya kazi ya utangazaji kwa mafanikio makubwa sana na inaelezwa historia yake haijavunjwa na mtangazaji yeyote kwa kuwahoji viongozi wengi hususan marais tena kwa ujasiri mkubwa. Ikumbukwe aliwahi kumhoji Marehemu Laurent Kabila juu ya uongozi wake usalama wake na usalama wa nchi kwa ujumla na baada ya mahojiano yale haikupita wiki kabila akauwawa.
Kwa wakati huo miaka takriban 50 ya BBC haijawahi kuongozwa na mtu mweusi katika nafasi ya ukurugenzi.
Lkn Tido mhando alifanikiwa kuwa mkurugenzi wa BBC wa kwanza mweusi tena tena mtanzania baada ya yule mama wa kizungu aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kuhamishwa kwenda kuwa mkurugenzi wa BBC katika bara Asia.
Nikutokana na uchapakazi wake uliomletea sifa na heshima dunia nzima katika fani ya utangazaji ndipo Rais kikwete alipomuomba arudi Tanzania kuja kuboresha kama siyo kukifufua chombo cha habari cha Taifa.
Wakati huo kulikuwa na Radio Tanzania na television ya Taifa TVT zilizounda kitu kilichoitwa taasisi ya utangazaji Tanzania TUT. Ilikuwa ni vigumu sana kumshawishi Tido akubali kazi yake aliyokuwa akilipwa ma pound ya Uingereza lkn hatimae kwa uzalendo wake alikubali kuacha kazi yake na kuja Tanzania.
Alipofika kitu cha kwanza aliomba apewe mamlaka kamili ya kukisuka upya chombo cha Taifa huku akifafanua kwamba ni aibu kwa nchi kama Tanzania kutokuwa na shirika la utangazaji akitolea mfano kama BBC, KBC, UBC, CNN nk.
Ndipo alipopewa mamlaka ya kuisuka na ndio akaanzisha shirika la utangazaji la Taifa TBC. Akafanikiwa kulifanya kuwa shirika pendwa na lenye wapenzi wengi kuliko chombo chochote Tanzania.
Kilichokuja kumponza ni kipindi cha uchaguzi kilipofika alipoanzisha kipindi cha mchakato majimboni.
Kipindi kilikuwa kikiongozwa na yeye mwenyewe na alikuwa akikutanisha wagombea wa CCM na wa upinzani kujinadi pamoja na kuelezea sera zao. Na kisha kuruhusu maswali kwa watazamaji.
Ngoma ilielekea kuwa ngumu sana kwa CCM kutokana na kushambuliwa kila kona na wananchi kwenye maswali ndipo CCM walipogoma kuendelea na kipindi cha mchakato majimboni na wakamwambia Tido akiondoe kipindi kisiendelee.
Tido alikataa akasema ameshasaini mkataba na hakielimu kama wadhamini wakuu wa kipindi hivyo kuuvunja mkataba ni gharama akashauri kama CCM wameamua kujitoa basi yeye ataendelea na ambao wako tayari
Kweli kipindi kiliendelea na kilisaidia wapinzani kupata wabunge wengi na kushuhudia anguko la wabunge wengi maarufu wa CCM kwenye uchaguzi ule. Hivyo kitendo kile hakikuwafurahisha mabwana wakubwa wakamuondoa Tido TBC
Walipomuondoa alichukuliwa na Mwananchi Comunication kama mkurugenzi mkuu ambapo pia alifanya kwa mafanikio makubwa kabla ya kumaliza mkataba wake na kuchukuliwa na Azam Tv. Ambapo kama kawaida yake amefanikiwa kukufanya king'amuzi cha Azam kuwa kinga'amuzi kinachoongoza kwa mauzo mengi kuliko king'amuzi chochote Tanzania.
Sasa pichani hapo chini ni Tido Mhando akiwa amefikishwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi akiwa TBC. Binafsi nimeumia roho sana maana nimjuavyo Tido ni jembe na CV zake zinamruhusu Kufanya kazi kwenye chombo chochote cha habari duniani kwa nafasi ya ukurugenzi.
Ila kwakuwa mahakama ni chombo cha haki ngoja tuiachie itende haki ila kwakweli inasikitisha sana. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Ndiyo nyingine tukagawana.Hivi nyumba za serikali ziliuzwa kwa tenda?
Ndio hajawahi kua mkurugenzi wa British Broadcasting corporation BBC hata siku moja. BBC hawajawahi kua na Mkurugenzi mweusi ila Tido Mhando aliwahi kua mkurugenzi wa BBC Swahili Services kitengo cha BBC kwa lugha ya kiswahili. Hivyo vitengo viko vingi vya lugha kubwa mbalimbali duniani.Kwahiyo hajawa Mkurugenzi BBC?
Kwani Mkurugenzi wa BBC Swahili sio kati ya Wakurugenzi wa BBC?Ndio hajawahi kua mkurugenzi wa British Broadcasting corporation BBC hata siku moja. BBC hawajawahi kua na Mkurugenzi mweusi ila Tido Mhando aliwahi kua mkurugenzi wa BBC Swahili Services kitengo cha BBC kwa lugha ya kiswahili. Hivyo vitengo viko vingi vya lugha kubwa mbalimbali duniani.
Hizi nchi za kiswahili ni za kuja kuzikwa tu ukishafika level za kimataifa utaharibu tu CV yako kinachoangaliwa ni siasa binafsi, ufanye watakayo hawa wakoloni weusi, ukisema usimamie kati utaalamu wako haufiki mbali utaharibu tu CV yako.Km yalomkuta mhongo msomi mzuri anaheshimika nje ya nchi,hizi nchi za kiafrica ukiwa mtaalamu na mahiri huwezi fika mbali vikwazo nyingi siasa imewekwa mbele kuliko utaalamu.
TBC inajumuisha na Radio Tanzania tofauti na TVT inahusu television pekee.Televisheni ya Taifa, jina zuri kabisa siyo kama huu ushenzi alioleta Tido Mhando wa tbc!
Nimefarijika kaka pascal kuona comment yako hapa nimeamini kweli umekomaa ki media firmsUsikute the issue sio Tido bali ni Azam!, haiwezekani Tido alipokuwa TBC, TBC ilingara, sasa yuko Azam, Azam inangara!, hivyo ikatafutwa namna yya kumcontain ili aondolewe Azam!, hata akiondolewa, jee ...itangara?.
Pole Tido, tuko nyuma yako!.
Paskali
Visasi ubabe kiburi Visirani ndizo sera za awamu ya tano!! Anashtakiwa kwa makosa ya 2008 (miaka kumi). Nchi yetu inaendelea kuendeshwa kwa kuchuma laana! Ukifuatilia utatambua kisa ni AZAM Tv kumpa airtime Tundu Lissu!! juzi tu!!kilichomponza ni ufisadi wake ameiba kodi za watanzania wanyonge CHADEMA acheni kutetea wahalifu