Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Kitendo cha upinzani kusapoti na kutetea kila anayetuhumiwa na serikali ni kitu cha ajabu san.
Kwa hiyo mkuu wewe unaona Mzee Mhando anatendewa haki?toka aondoke tbc hadi leo kweli ndo huo ubadhirifu umeonekana? muwe mnaona aibu na pia kuwe japo na hofu ya Mungu kidogo kwa mfano mm binafsi sio mdau kabisa wa siasa za huko nyumbani lakini huyu bwana ni wazi anaonewa na Mungu yupo atamlinda usiku mwema mkuu
 
Nimegundua ni ngumu sana kuwa mzalendo kwenye hii nchi iliyolaaniwa!

Viongoz wanaacha kufanya mambo ya maana wapo busy na kina dr shika, Nabii tito pamoja na wengine wasio na hatia.

Inafika mahala naona aibu kujitambulisha mimi ni mtanzania
Hama nchi
 
Quinine Kwa nini alifuta TVT yetu na kuleta jina baya na la kishenzi TBC?
Jina lina mahusiano gani na performance ya shirika? Tido alikuta TVT ikiwa ya hovyo, akairudisha kwenye chati. Hata wewe mwenyewe ni shahidi. Baada ya kuondoka TBC imerud hatua mia nyuma.
Hata kama hamkubali kisasa , kubalini basi kazi aliyoifanya.
 
Very painful yaani walafi wachache ccm qakiongozwa na mwenyekiti wao hawataki kujenga nchi bali kuiharibu kila kukicha?.mbwa kabisa ccm
 
Jina lina mahusiano gani na performance ya shirika? Tido alikuta TVT ikiwa ya hovyo, akairudisha kwenye chati. Hata wewe mwenyewe ni shahidi. Baada ya kuondoka TBC imerud hatua mia nyuma.
Hata kama hamkubali kisasa , kubalini basi kazi aliyoifanya.


Lkn kimbele mbele gani kilichomfanya aite TV yetu ya Taifa, tbc?
 
Namkumbuka tido,ndio aliyekuja kulifanya gazeti la mwananchi liwe bora kuliko magaxeti yote,kwa sababu ya misingi aliyoiweka kwenye gazeti la mwananch,mwanaspot na the citizen, mpaka Leo ni magazeti bora.amefanya mageuz makubwa sana kwenye tasnia ya habari Tanzania.
Kufanya kazi kwake vizuri hakumfanyi asishtakiwe kama ana tuhuma atajibu!
 
Inaumiza! Anashtakiwa miaka saba tangu astaafu! Hivi wengine tunaowafahamu kuisababishia hasara serikali miaka iliyopita watashtakiwa pia?
 
Kinyongo cha CCM dhidi ya Tido ni pale aliporusha midahalo ya wagombea ubunge majimboni la ajabu CCM waligoma kushiriki wakidai siyo sera yao kuwajuza wananchi juu ya wasifu na malengo ya kugombea ya wateule wao.

Baada ya hapo, JK kwa ghadhabu kubwa alitengua uteuzi wa mwathirika huyu wa umangimeza wa CCM!

Leo azushiwa jinai za manunuzi huku haohao leo wananunua from single source mifano mfukoni lakini.

Hata kandarasi kubwa kubwa waheshimiwa hawa hudai..."waachiwe wao" kwani mkandarasi tayari wanaye mfukoni.

Sijui wako juu ya sheria au kuna nini hapo.

Sheria ya manunuzi inaruhusu single sourcing sasa uhujumu uchumi unachipukia wapi?

Viwanda vya kusulubiana kwa sababu za chuki na vinyongo vya kisiasa ni tishio kwa usalama wa taifa!

Acheni uhasama tujenge nchi, pliiiiiiiiiiz

SAHIHISHO CHA KICHWA CHA HABARI

Siyo uwaziri bali uwazi
 
Back
Top Bottom