upendodaima
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 4,089
- 4,535
Hii nchi imefika pabaya sana mpaka najiuliza hv wazee walioipigania na kuipa sifa hawayaoni yote haya?
kumbe mshenzi tu huna mbele wala nyuma basi funga domo lako.wenye uwezo hao mabwana zako unaowalamba makalio wanaona linafaa ndo maana wameacha liendelee kutumika. kidampa jinyamazie tu
Watasemaje kitu ambacho hakipoHalafu hiyo hasara mbona haisemwi kaisababishaje !?
Hii ndo sababu haswaa! Hatuwezi kufika popote kwa mambo haya ya kishamba, kwa vile mtu kafanya hivi basi unatafuta sababu, kwani nyie kina nani??? Kumbuka nanyi MTAKUFA TU..labda kwasababu Azam TV wamefanya mahojiano na TL.
Akiwa BBC Nairobi miaka hiyo aliingia matatizoni na serikali ya Rais Moi kwa kufichua mauaji ya Robarth Auko. Wakenya wengi na serikali walikuwa wakidhani Tido ni Mkenya lkn kumbe alikuwa ni Mtanzania.
Alikuwa akiwindwa sana na kwa sababu hizo BBC ikamuondoa Kenya na kumpeleka London. Akiwa London alifanya kazi ya utangazaji kwa mafanikio makubwa sana na inaelezwa historia yake haijavunjwa na mtangazaji yeyote kwa kuwahoji viongozi wengi hususan marais tena kwa ujasiri mkubwa. Ikumbukwe aliwahi kumhoji Marehemu Laurent Kabila juu ya uongozi wake usalama wake na usalama wa nchi kwa ujumla na baada ya mahojiano yale haikupita wiki kabila akauwawa.
Kwa wakati huo miaka takriban 50 ya BBC haijawahi kuongozwa na mtu mweusi katika nafasi ya ukurugenzi.
Lkn Tido mhando alifanikiwa kuwa mkurugenzi wa BBC wa kwanza mweusi tena tena mtanzania baada ya yule mama wa kizungu aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kuhamishwa kwenda kuwa mkurugenzi wa BBC katika bara Asia.
Nikutokana na uchapakazi wake uliomletea sifa na heshima dunia nzima katika fani ya utangazaji ndipo Rais kikwete alipomuomba arudi Tanzania kuja kuboresha kama siyo kukifufua chombo cha habari cha Taifa.
Wakati huo kulikuwa na Radio Tanzania na television ya Taifa TVT zilizounda kitu kilichoitwa taasisi ya utangazaji Tanzania TUT. Ilikuwa ni vigumu sana kumshawishi Tido akubali kazi yake aliyokuwa akilipwa ma pound ya Uingereza lkn hatimae kwa uzalendo wake alikubali kuacha kazi yake na kuja Tanzania.
Alipofika kitu cha kwanza aliomba apewe mamlaka kamili ya kukisuka upya chombo cha Taifa huku akifafanua kwamba ni aibu kwa nchi kama Tanzania kutokuwa na shirika la utangazaji akitolea mfano kama BBC, KBC, UBC, CNN nk.
Ndipo alipopewa mamlaka ya kuisuka na ndio akaanzisha shirika la utangazaji la Taifa TBC. Akafanikiwa kulifanya kuwa shirika pendwa na lenye wapenzi wengi kuliko chombo chochote Tanzania.
Kilichokuja kumponza ni kipindi cha uchaguzi kilipofika alipoanzisha kipindi cha mchakato majimboni.
Kipindi kilikuwa kikiongozwa na yeye mwenyewe na alikuwa akikutanisha wagombea wa CCM na wa upinzani kujinadi pamoja na kuelezea sera zao. Na kisha kuruhusu maswali kwa watazamaji.
Ngoma ilielekea kuwa ngumu sana kwa CCM kutokana na kushambuliwa kila kona na wananchi kwenye maswali ndipo CCM walipogoma kuendelea na kipindi cha mchakato majimboni na wakamwambia Tido akiondoe kipindi kisiendelee.
Tido alikataa akasema ameshasaini mkataba na hakielimu kama wadhamini wakuu wa kipindi hivyo kuuvunja mkataba ni gharama akashauri kama CCM wameamua kujitoa basi yeye ataendelea na ambao wako tayari
Kweli kipindi kiliendelea na kilisaidia wapinzani kupata wabunge wengi na kushuhudia anguko la wabunge wengi maarufu wa CCM kwenye uchaguzi ule. Hivyo kitendo kile hakikuwafurahisha mabwana wakubwa wakamuondoa Tido TBC
Walipomuondoa alichukuliwa na Mwananchi Comunication kama mkurugenzi mkuu ambapo pia alifanya kwa mafanikio makubwa kabla ya kumaliza mkataba wake na kuchukuliwa na Azam Tv. Ambapo kama kawaida yake amefanikiwa kukufanya king'amuzi cha Azam kuwa kinga'amuzi kinachoongoza kwa mauzo mengi kuliko king'amuzi chochote Tanzania.
Sasa pichani hapo chini ni Tido Mhando akiwa amefikishwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi akiwa TBC. Binafsi nimeumia roho sana maana nimjuavyo Tido ni jembe na CV zake zinamruhusu Kufanya kazi kwenye chombo chochote cha habari duniani kwa nafasi ya ukurugenzi.
Ila kwakuwa mahakama ni chombo cha haki ngoja tuiachie itende haki ila kwakweli inasikitisha sana. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Cha ajabu ni miaka 10 iliyopita, vichekesho kweli yaaniHuo ufusadi ndo wanauona Leo auditors walikua likizo? Ukurupukaji. com. Watashindwa except Kama no maagizo kutoka juu.
Labda anataka kutuambia Bomabrdier, Tupolev na ATR walituma quotation zao beforeKwamba ile Airport ya Chato ni single source mixer kununua bombadia ni single source yani usiombee mtu akiwa na chuki na visasi ni hatari tupu yani..
Akimaliza muda wake ajiandae kuja kutueleza Chato Airport na hizo ndege zake vilipitia mchakato upi.Kwamba ile Airport ya Chato ni single source mixer kununua bombadia ni single source yani usiombee mtu akiwa na chuki na visasi ni hatari tupu yani..
Acha kabisa kuingilia uhuru wa mahakama.Ikiwa una uchungu sana huyo mh kufikishwa mahakamani mkodishie advocateKinyongo cha CCM dhidi ya Tido ni pale aliporusha midahalo ya wagombea ubunge majimboni la ajabu CCM waligoma kushiriki wakidai siyo sera yao kuwajuza wananchi juu ya wasifu na malengo ya kugombea ya wateule wao.
Baada ya hapo, JK kwa ghadhabu kubwa alitengua uteuzi wa mwathirika huyu wa umangimeza wa CCM!
Leo azushiwa jinai za manunuzi huku haohao leo wananunua from single source mifano mfukoni lakini.
Hata kandarasi kubwa kubwa waheshimiwa hawa hudai..."waachiwe wao" kwani mkandarasi tayari wanaye mfukoni.
Sijui wako juu ya sheria au kuna nini hapo.
Sheria ya manunuzi inaruhusu single sourcing sasa uhujumu uchumi unachipukia wapi?
Viwanda vya kusulubiana kwa sababu za chuki na vinyongo vya kisiasa ni tishio kwa usalama wa taifa!
Acheni uhasama tujenge nchi, pliiiiiiiiiiz
SAHIHISHO CHA KICHWA CHA HABARI
Siyo uwaziri bali uwazi
Kwahiyo hapa wewe umeandika nini cha ukweli.Mhhhh wewe ndugu unaonekana hatari sana kwa story za vijiweni ..maana maelezo yako mengi ukweli mdogo.Dunia sasa hivi kama ndimu tu kwa ukubwa wa habari au kutaka kufahamu jambo. Ukitupia habari watu wana Google tuu kuhakikisha ukweli, matokeo yake unaumbuka ,siku nyingine kabla ujaandika kitu jaribu kwanza kupitia pitia ukweli wa jambo au kitu.