Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Tido rudi BBC ukaendeleze kipindi chako cha "Wiki hii" kila siku ya Jumamosi asubuhi
Mimi na baba yangu tulikuwa mashabiki wakubwa wa kipindi hicho na redio yetu ya mbao a.k.a mkulima

Sijui nini kilikupata mkubwa wangu wewe mpaka ukaamua karudi huku gizani wakati ulikuwa nuruni

Hili ndio bara la giza
 
Tido hajakutwa na hatia bado. Mahakama iachwe ififanye kazi yake!
 
Nadhani kitendo cha kumtuma mwamdishi Nairobi kumhoji bwana yule was a doctrine of last straw
 
Usikute the issue sio Tido bali ni Azam!, haiwezekani Tido alipokuwa TBC, TBC ilingara, sasa yuko Azam, Azam inangara!, hivyo ikatafutwa namna yya kumcontain ili aondolewe Azam!, hata akiondolewa, jee ...itangara?.

Pole Tido, tuko nyuma yako!.

Paskali

Kwa hiyo PAC chini ya uenyekiti wa Zitto nao walimhoji kwa sababu hiyo hiyo ya kung'ara kwa Azam?

Wabongo wana reasoning ya ajabu kweli!!
 
KIUJUAMLA HAKUTAKIWA KUFANYA KAZI TANZANIA..NISHIDA .JAMAA ANANYOOSHAGA AANGALII SURA YA MTU MAMBOHYA SIO KUYAFANYA UKIWA AFRICQ
 
Kwa hiyo PAC chini ya uenyekiti wa Zitto nao walimhoji kwa sababu hiyo hiyo ya kung'ara kwa Azam?

Wabongo wana reasoning ya ajabu kweli!!
Ni kweli wabongo tuna reasoning ya ajabu. Deal ilifanyika miaka 10 iliyopita, kesi ndio inapandishwa leo, hivyo wanaojiuliza why now ndio wanaonekana waajabu!.

Ni kazi PAC kuhoji any queries according to CAG report. Hata hao PAC sio perfect, ni human beings tuu na niliwahi kuwa blast hapa
Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !
P
 
Akiwa BBC Nairobi miaka hiyo aliingia matatizoni na serikali ya Rais Moi kwa kufichua mauaji ya Robarth Auko. Wakenya wengi na serikali walikuwa wakidhani Tido ni Mkenya lkn kumbe alikuwa ni Mtanzania.

Alikuwa akiwindwa sana na kwa sababu hizo BBC ikamuondoa Kenya na kumpeleka London. Akiwa London alifanya kazi ya utangazaji kwa mafanikio makubwa sana na inaelezwa historia yake haijavunjwa na mtangazaji yeyote kwa kuwahoji viongozi wengi hususan marais tena kwa ujasiri mkubwa. Ikumbukwe aliwahi kumhoji Marehemu Laurent Kabila juu ya uongozi wake usalama wake na usalama wa nchi kwa ujumla na baada ya mahojiano yale haikupita wiki kabila akauwawa.

Kwa wakati huo miaka takriban 50 ya BBC haijawahi kuongozwa na mtu mweusi katika nafasi ya ukurugenzi.

Lkn Tido mhando alifanikiwa kuwa mkurugenzi wa BBC wa kwanza mweusi tena tena mtanzania baada ya yule mama wa kizungu aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kuhamishwa kwenda kuwa mkurugenzi wa BBC katika bara Asia.

Nikutokana na uchapakazi wake uliomletea sifa na heshima dunia nzima katika fani ya utangazaji ndipo Rais kikwete alipomuomba arudi Tanzania kuja kuboresha kama siyo kukifufua chombo cha habari cha Taifa.

Wakati huo kulikuwa na Radio Tanzania na television ya Taifa TVT zilizounda kitu kilichoitwa taasisi ya utangazaji Tanzania TUT. Ilikuwa ni vigumu sana kumshawishi Tido akubali kazi yake aliyokuwa akilipwa ma pound ya Uingereza lkn hatimae kwa uzalendo wake alikubali kuacha kazi yake na kuja Tanzania.

Alipofika kitu cha kwanza aliomba apewe mamlaka kamili ya kukisuka upya chombo cha Taifa huku akifafanua kwamba ni aibu kwa nchi kama Tanzania kutokuwa na shirika la utangazaji akitolea mfano kama BBC, KBC, UBC, CNN nk.

Ndipo alipopewa mamlaka ya kuisuka na ndio akaanzisha shirika la utangazaji la Taifa TBC. Akafanikiwa kulifanya kuwa shirika pendwa na lenye wapenzi wengi kuliko chombo chochote Tanzania.

Kilichokuja kumponza ni kipindi cha uchaguzi kilipofika alipoanzisha kipindi cha mchakato majimboni.

Kipindi kilikuwa kikiongozwa na yeye mwenyewe na alikuwa akikutanisha wagombea wa CCM na wa upinzani kujinadi pamoja na kuelezea sera zao. Na kisha kuruhusu maswali kwa watazamaji.

Ngoma ilielekea kuwa ngumu sana kwa CCM kutokana na kushambuliwa kila kona na wananchi kwenye maswali ndipo CCM walipogoma kuendelea na kipindi cha mchakato majimboni na wakamwambia Tido akiondoe kipindi kisiendelee.

Tido alikataa akasema ameshasaini mkataba na hakielimu kama wadhamini wakuu wa kipindi hivyo kuuvunja mkataba ni gharama akashauri kama CCM wameamua kujitoa basi yeye ataendelea na ambao wako tayari

Kweli kipindi kiliendelea na kilisaidia wapinzani kupata wabunge wengi na kushuhudia anguko la wabunge wengi maarufu wa CCM kwenye uchaguzi ule. Hivyo kitendo kile hakikuwafurahisha mabwana wakubwa wakamuondoa Tido TBC

Walipomuondoa alichukuliwa na Mwananchi Comunication kama mkurugenzi mkuu ambapo pia alifanya kwa mafanikio makubwa kabla ya kumaliza mkataba wake na kuchukuliwa na Azam Tv. Ambapo kama kawaida yake amefanikiwa kukufanya king'amuzi cha Azam kuwa kinga'amuzi kinachoongoza kwa mauzo mengi kuliko king'amuzi chochote Tanzania.

Sasa pichani hapo chini ni Tido Mhando akiwa amefikishwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi akiwa TBC. Binafsi nimeumia roho sana maana nimjuavyo Tido ni jembe na CV zake zinamruhusu Kufanya kazi kwenye chombo chochote cha habari duniani kwa nafasi ya ukurugenzi.

Ila kwakuwa mahakama ni chombo cha haki ngoja tuiachie itende haki ila kwakweli inasikitisha sana. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Wewe ni Lichadema tu, huna unachoumia, Mishetani ndivyo mlivyo
 
Ni kweli wabongo tuna reasoning ya ajabu. Deal ilifanyika miaka 10 iliyopita, kesi ndio inapandishwa leo, hivyo wanaojiuliza why now ndio wanaonekana waajabu!.

Ni kazi PAC kuhoji any queries according to CAG report. Hata hao PAC sio perfect, ni human beings tuu na niliwahi kuwa blast hapa
Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma !
P

Kwa hiyo wewe unaamini PAC walimhoji kwa sababu ya Azam kung'ara kwa kuwa hawako perfect?

Yaani CAG naye aliionea wivu Azam Tv ndiyo akaja na majungu kwa Tido?

Kwani sheria zetu zinasema case ipandishwe baada ya muda gani pekee?

Issue siyo watu kuhoji muda bali kuihusisha hii case na mambo yasiyo make hata sense.

Toka lini tuhuma ikawa na expire date?
 
Yani ukirejeshwa nchini kwaajili ya utaalam wako malipo yake majanga, namkumbuka yule mama wa kituo cha uwekezaji, mtoto wa malechela
 
Back
Top Bottom