Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Kumharasi Tido ni kuchezea m asikio ya wakubwa huko nje Huyu jamaa anajifanya haogopi ila ni upimbi tu
 
Akiwa BBC Nairobi miaka hiyo aliingia matatizoni na serikali ya Rais Moi kwa kufichua mauaji ya Robarth Auko. Wakenya wengi na serikali walikuwa wakidhani Tido ni Mkenya lkn kumbe alikuwa ni Mtanzania.

Alikuwa akiwindwa sana na kwa sababu hizo BBC ikamuondoa Kenya na kumpeleka London. Akiwa London alifanya kazi ya utangazaji kwa mafanikio makubwa sana na inaelezwa historia yake haijavunjwa na mtangazaji yeyote kwa kuwahoji viongozi wengi hususan marais tena kwa ujasiri mkubwa. Ikumbukwe aliwahi kumhoji Marehemu Laurent Kabila juu ya uongozi wake usalama wake na usalama wa nchi kwa ujumla na baada ya mahojiano yale haikupita wiki kabila akauwawa.

Kwa wakati huo miaka takriban 50 ya BBC haijawahi kuongozwa na mtu mweusi katika nafasi ya ukurugenzi.

Lkn Tido mhando alifanikiwa kuwa mkurugenzi wa BBC wa kwanza mweusi tena tena mtanzania baada ya yule mama wa kizungu aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kuhamishwa kwenda kuwa mkurugenzi wa BBC katika bara Asia.

Nikutokana na uchapakazi wake uliomletea sifa na heshima dunia nzima katika fani ya utangazaji ndipo Rais kikwete alipomuomba arudi Tanzania kuja kuboresha kama siyo kukifufua chombo cha habari cha Taifa.

Wakati huo kulikuwa na Radio Tanzania na television ya Taifa TVT zilizounda kitu kilichoitwa taasisi ya utangazaji Tanzania TUT. Ilikuwa ni vigumu sana kumshawishi Tido akubali kazi yake aliyokuwa akilipwa ma pound ya Uingereza lkn hatimae kwa uzalendo wake alikubali kuacha kazi yake na kuja Tanzania.

Alipofika kitu cha kwanza aliomba apewe mamlaka kamili ya kukisuka upya chombo cha Taifa huku akifafanua kwamba ni aibu kwa nchi kama Tanzania kutokuwa na shirika la utangazaji akitolea mfano kama BBC, KBC, UBC, CNN nk.

Ndipo alipopewa mamlaka ya kuisuka na ndio akaanzisha shirika la utangazaji la Taifa TBC. Akafanikiwa kulifanya kuwa shirika pendwa na lenye wapenzi wengi kuliko chombo chochote Tanzania.

Kilichokuja kumponza ni kipindi cha uchaguzi kilipofika alipoanzisha kipindi cha mchakato majimboni.

Kipindi kilikuwa kikiongozwa na yeye mwenyewe na alikuwa akikutanisha wagombea wa CCM na wa upinzani kujinadi pamoja na kuelezea sera zao. Na kisha kuruhusu maswali kwa watazamaji.

Ngoma ilielekea kuwa ngumu sana kwa CCM kutokana na kushambuliwa kila kona na wananchi kwenye maswali ndipo CCM walipogoma kuendelea na kipindi cha mchakato majimboni na wakamwambia Tido akiondoe kipindi kisiendelee.

Tido alikataa akasema ameshasaini mkataba na hakielimu kama wadhamini wakuu wa kipindi hivyo kuuvunja mkataba ni gharama akashauri kama CCM wameamua kujitoa basi yeye ataendelea na ambao wako tayari

Kweli kipindi kiliendelea na kilisaidia wapinzani kupata wabunge wengi na kushuhudia anguko la wabunge wengi maarufu wa CCM kwenye uchaguzi ule. Hivyo kitendo kile hakikuwafurahisha mabwana wakubwa wakamuondoa Tido TBC

Walipomuondoa alichukuliwa na Mwananchi Comunication kama mkurugenzi mkuu ambapo pia alifanya kwa mafanikio makubwa kabla ya kumaliza mkataba wake na kuchukuliwa na Azam Tv. Ambapo kama kawaida yake amefanikiwa kukufanya king'amuzi cha Azam kuwa kinga'amuzi kinachoongoza kwa mauzo mengi kuliko king'amuzi chochote Tanzania.

Sasa pichani hapo chini ni Tido Mhando akiwa amefikishwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi akiwa TBC. Binafsi nimeumia roho sana maana nimjuavyo Tido ni jembe na CV zake zinamruhusu Kufanya kazi kwenye chombo chochote cha habari duniani kwa nafasi ya ukurugenzi.

Ila kwakuwa mahakama ni chombo cha haki ngoja tuiachie itende haki ila kwakweli inasikitisha sana. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

 
Huu sio wakat wa kukosoa,kushauri....,ni wakat wa kusifia tuu hata kama ni mabaya we sifia tuuu
 
Kitendo cha upinzani kusapoti na kutetea kila anayetuhumiwa na serikali ni kitu cha ajabu san.
Nyie na mkiti wenu mnaotetea wabakaji kina Babu Seya siyo tu ni kitendo cha ajabu bali ni kitendo cha aibu kwa jamii iliyostaarabika.
 
Kumhoji lissu kule nairobi ndio kumeleta hii issue,Mungu anawaona!
 
tvt si n TBC kwa kiingereza? ama kweli ccm inapendwa na mazwazwa nimeamin


Sasa kwa nini Tido Muhando akaondoa TVT yetu na kuweka ujinga wake wa tbc? Mwanzoni TV zetu zilikuwa zina nembo ya TVT alivyokuja yeye ktk kwa Muzungu akafuta na kuweka tbc, kwa nini?
 
B
kilichomponza ni ufisadi wake ameiba kodi za watanzania wanyonge CHADEMA acheni kutetea wahalifu
Bwana laki si pesa japo huna utamaduni wa kujisomea lakini nakushauri na kuwashauri wanaowatuma japo kidogo mjisomee taratibu za utawala na kutawala. Hivi huyu tido huo ufisadi alifanya mwenyewe? Wapo wapi wengine?
 
Huu utetezi wa Tido unatokea wapi? Mbona mama wa mboga pamoja na kuwa boss wa un alitumbuliwa! Mbona mchechu pamoja na kuwa Rais wa Baclays Bank ulaya na asia hajapata utetezi hivi?

Tusianzishe utetezi wa kitoto tuache mahakama usikilize shauri la jinai yake.
 
Tunaleta "afirmative action" kama za wanawake, kademu kaki supp kanasingizia kalimnyima uroda prof ndo maana kame supua,

kama alitupiga hela ndefu awajibike kwa wizi wake, akaungane na akina kitilya ruge singasinga zakaria kirumile na bado wengine wanakuja akina kimei mchechu
 
huyu jamaa ata kama ana makosa, asamehewe tu kwasababu amefanya mema mengi kuliko mabaya. TBC toka aondoke imekuwa takataka, hakuna cha Ayoub rioba mwenye phd wala nini, kokote anakoenda kunafanikiwa, azam sasaivi ni bora kuliko tv zote tz kwasababu yake. hata wakimprosecute lakini ni mtu mwenye weledi sana. kipindi icho kulikuwa na TVT nakumbuka, yeye ndo akaja kulichambua ikawa TBC1, TBC2 na zingine zote, na ubora halisi wa tv kibiashara ukaongezeka.
 
Back
Top Bottom