Kile kipindi ambacho nilipotea

Kile kipindi ambacho nilipotea

BaaDa ya ya kufika gambosi aka gamboshi wengi muiitavyo, nilikutana na dunia nyingine kabisa! Ambayo iko ndani ya huu ulimwengu tunaoishi!, picha linaanza sehemu ya kulala, naambiwa fuatana na Huyo jogoo mwekundu! Atakapolala na wewe utalala hapohapo! Na kweli ikawa hivyo! Jogoo alikuwa na hirizi kubwa shingoni, njiani tukakutana na na mlevi mmoja akanitukana mno! Nikataka kumvagaa! Jogoo akanirukia akanikaba shingoni!.... Inaendelea!..............

Akakukaba ... ? mh huyo jogoo mtata sana mkuu
 
Mwaka 2008, December, nikiwa mfanyakazi wa kampuni Fulani kubwa kuliko zote hapa tz ya uchimbaji wa madini aina ya dhahabu, kwa sasa inaitwa acacia janja janja ya ukwepaji Kodi angalia bio yangu as a mine engineer,@(underground) mshikaji wangu mmoja mussa alinipeleka huko gambosi nilipata kesi Moja tata sana!, mwendo wa masaa 2 toka magu MZA, tulitumia Massa 12 kwa bodaboda , nafika gambosi naulizwa!" Umefiwa na ndugu yako!!?? " "uliza huo mkwaju mkubwa utakujibu kama nduguyo Yuko hapa!" Nilichoka! Huo mkwaju uko pembeni ya shule ya msingi gambosi, na ukwaju wake huwa hauliwi! Nilishinda kesi kwa mazingira tata sana! Inaendelea...............!
mkuu kama busara ungeanzisha thread yako tuisome kwa nafasi humu kama mtatuchanganya
 
Inaendelea
Kiukweli ni kwamba nilisizi, Lakini Sikuwa pekeyangu karibia wapangaji kama wane hivi walitoka vyumbani mwao
Mimi sikurudi tena kulala mule ndani nilichukua kibegi changu na kwenda kukesha Ibiza mpaka alfajiri nilipotimkia bandarini
Tukiwa kwenye boat kurejea Nyamisati story zilikuwa za ile gesti na vituko walivyokumbana navyo usiku mzima, hasa ile harufu ya udongo mbichi na mchele, kuna baadhi walijiapiza kuwa hawatakaa warudi Mafia
Tulifika Nyamisati saa tatu hivi asubuhi bila kituko chochote....nilipumzika mpaka mchana tulipokodi fiber boat kwenda kwenye visiwa vilivyo karibu na hapo Nyamisati
Sorry kwa kupotea hewani si kweli kwamba jitu refu lilinitumbua...
Tuendeleee
Pale Nyamisati kuna fiber boats nyingi za kukodi ila sisi tulipata shida kweli kupata moja, mwishowe kijana mmoja akatuambua boat inayotufaa sisi ni ya jamaa anaitwa rasta nyoka
Basi akatafutwa na ndani ya dakika kumi akawa kafika
Huyu jamaa ni mrefu mweusi mwembamba mwenye rasta zilizofungwa kitambaa kote ndefu karibia na kiuno
Tulipatana na kuondoka Nyamisati saa saba mchana, nilikuwa nimeshamweleza kuwa tunataka kufanya ziara kwenye visiwa visivyopungua kumi, akasema hakuna shida kwakuwa kote anakufahamu vema
Ni baada ya kupanda ile boat na kuondoka pale ndio mwili wangu uliota vipele kwa taharuki, na hii ni baada ya kusikia ile harufu ya udongo na mchele, nilimwangalia nahodha wetu kwa kuibia na kugundua ni yule yule bwana
Hata wale raia niliokuwa nao niliweza kuona hofu ya wazi kwenye nyuso zao! Tuliangaliana wote bila kuongeleshana chochote
zile harufu za udongo na mchele zikawa zinakuja na kutoweka hapo tayari tukiwa kwenye mapori ya mikoko ndani ya bahari kuu
Ilibidi niweke hofu pembeni na kuanza kuongea na nahodha! Hakuwa mtu wa kawaida anafahamu mengi ya bahari mengi sana na ilikuwa akipiga story ya kutisha kuna wakati alikuwa anarusha mate kama nyoka...hii niliishuhudia si chini ya mara kumi
Visiwa hivi vilivyoko karibu na Nyamisati karibia vyote vimezungukwa na mikoko na kwa baadhi ya sehemu kuna vijiji na kwingine kuna kambi za uvuvi na kilimo, ni visiwa ambavyo viko naweza kusema nje ya utaratibu wa dunia, huko dili kubwa ni uchawi na kusafirisha mikoko
Rasta nyoka nahodha wetu ni mtu maarufu huko huko visiwani lakini unaweza kufika Nyamisati ukawaulizia kuhusu yeye na hakuna mtu anaweza kukiri kumfahamu! Yeye ndio mwamuzi wa kutaka akumbukwe au adahauliwe
Tulikuja kuweka kambi kisiwa kimoja kinaitwa Kilwani karibu na meli kubwa ya wajerumani iliyoachwa hapo wakati wa vita ya pili ya dunia, kwasasa haionekani tena imezama kabisa
 
Mh Nyamisati: ulipitia Bungu Mketo. Ila bandari kwa magendo ile, vipi hukuwa na nyala za serikali lakini? 😀😀😀😀😀😀😀
 
Thanks bro. Hapa panazidi kunoga. Yaani bro hukupiga selfie na yule MTU MREFU, basi hata huyu RASTA NYOKA nae huna tupicha twake?
 
Rasta nyoka Huyu nahodha wetu ndio yule jamaa mrefu , alitusimulia mengi kwa sharti la kutoyasema popote nami sitayasema hapa...nitaandika yale aliyokubali tu kusemwa, Huyu jamaa husafiri bure popote kama akiamua hula chochote popote bila kulipa, mambo anayofanya si kwa utashi wake bali kuna roho ndio zinamuongoza
Rasta zake si nywele kama nywele za kawaida, gesti tuliyolala anasema ni kituo na mapito, muda mwingi huishi huko visiwani kwenye mapori ya mikoko
Husaidia majahazi ya Zanzibar na Pemba kupeleka mbao za mikoko bila kukamatwa na maliasili, pesa anayolipwa hatumii yeye
Hana wazazi hana familia, amekulia visiwa vya nyamisati, mengine hayasemi mengine sitayasema
Tulifanya ziara ya woga kwenye visiwa vine tu hatukuwa tayari kulala kisiwa chochote na nahodha wetu
Tulimaliza na kisiwa cha Simbaulanga, kisiwa mdomo wa kuingia baharini au kuingia njia ya Nyamisati
 
Tulirejea nyamisati jioni tukalala pale, rasta nyoka hakuwepo tena hatukupeana namba sikumuona na somu hakupenda tupige picha hata moja
Kuna mengi sikuyasimulia hapa nimetii agizo , ila hapo Nyamisati Gezani , kilwani na visiwa vinginevyo Kuna siri kubwa kuhusiana na rasta nyoka...ukibahatika kwenda huko jaribu kumuulizia
 
Mh Nyamisati: ulipitia Bungu Mketo. Ila bandari kwa magendo ile, vipi hukuwa na nyala za serikali lakini? 😀😀😀😀😀😀😀
Magendo kule ndio maisha na hata ujambazi ile ndio highway ya kuodokea ndio maana mkuranga na yote hiyo rate ya ujambazi na mauaji viko juu
 
Thanks bro. Hapa panazidi kunoga. Yaani bro hukupiga selfie na yule MTU MREFU, basi hata huyu RASTA NYOKA nae huna tupicha twake?
26545474874453dd908761509607ce4a.jpg
 
Tulirejea nyamisati jioni tukalala pale, rasta nyoka hakuwepo tena hatukupeana namba sikumuona na somu hakupenda tupige picha hata moja
Kuna mengi sikuyasimulia hapa nimetii agizo , ila hapo Nyamisati Gezani , kilwani na visiwa vinginevyo Kuna siri kubwa kuhusiana na rasta nyoka...ukibahatika kwenda huko jaribu kumuulizia

Tumefurahia habari hii ambayo hatukuijua kamwe pamoja na kupunguza mengi ambayo hukuruhusiwa kutuelezea.
 
Tulirejea nyamisati jioni tukalala pale, rasta nyoka hakuwepo tena hatukupeana namba sikumuona na somu hakupenda tupige picha hata moja
Kuna mengi sikuyasimulia hapa nimetii agizo , ila hapo Nyamisati Gezani , kilwani na visiwa vinginevyo Kuna siri kubwa kuhusiana na rasta nyoka...ukibahatika kwenda huko jaribu kumuulizia
mtani yani ndiyo umemalizia hivyo?
 
Back
Top Bottom