Kile kipindi ambacho nilipotea

Kwanini msichukulie kama burudani tu kama mnahisi anawaambia uongo

Inabidi aseme hii ni "fictitious". Ubunifu tu na hakuna ukweli.

Hapo watu wanajuwa kuwa ni burudani tu. Lakini mwenzetu anatetea uongo utafikiri ukweli.

Anawahadaa wengi sana na nimejaribu kujiuliza kwanini? Nikapata jibu, aaah anawatayarisha wateja.

Hii ni kama alivyoanza MziziMkavu sasa anauza dawa kiulaini. Tena at least MziziMkavu anauza dawa za tiba mbadala lakini huyu mwenzetu sijuwi mpaka sasa kama hakuna watu wapenda ushirikina aliokwisha watia chanjo za makalio, sijuwi.
 
Kuna vitu huwa anajiongelea vimejaa nadharia zaidi
 
Ulishawahi kuwa mteja wake ukachanjwa hizo sehemu?
 
Punguza fiksi kaka wewe ni mtu mzima!usitake kujifanya unajuuuua mambo ya uchawi&ushirikina nk......acha fiksi
Kwa taarifa yako mimi sijifanyi na sijawahi kujifanya, naujua uchawi naufahamu vizuri sana ushirikina
Kama unadhani hizi ni fix naomba uthibitishe hapa. ..weka ushahidi kama mimi nilivyotaja maeneo muda na wahusika
Jitengenezee uwezo wa kuaminika usiishie kusema hizi ni fix...ukishindwa hili utakuwa mpuuzi kama yule mpuuzi mwingine
 
Saa 23:50 now nalala mkuu mshana JR ila nawazo nenda pale UDSM maana ni Chuo Mama omba Ufungue short course km wale wachina na conficious Yao anzisha hata vi Basic technician na Technician certificate in witchcraft and kupaaology in the midnight!!!
Kupaaology hii Kali aisee.
 
Matangazo biashara.....kwa mwendo huu utawapata wengi tu humu!fiksi tupu!
 
Dear haters fanyeni haya kuthibitisha uongo wangu kwenye hii post
-nendeni Nyamisati, simbaulanga kilwani na gezani
-nendeni kilindoni mafia niliandika jina langu hili ninalotumia hapa pale IBIZA
-Kauluzeni habari nilizoandika hapa huko kote nilikotaja
-nimezungumzia uchawi wa hivyo visiwa
-nimezungumzia magendo ya huko, kwanini msiende kuuliza?
-kuna Boat kubwa tatu moja ya fiber zinazofanya safari kati ya mafia na Nyamisati si mkaulize hizi habari
Mnashupaa hapa kulazimisha sukari iwe chumvi mtaweza kweli?
Naweka dau la nauli ya laki moja mmoja wenu aende
 

Hayo mahadithi tulikuwa tukipigiana utotoni.

Kwani kutaja sehemu ndiyo hupatungii uongo?

Umesahau nikivyokuumbuwa? Si ulitaja mitaa ambayo ipo na ukaweka picha ukajidai hii jana usiku, kama vile umepiga wewe hiyo picha. Ngoja kesho niipekuwe library ya JF kama hawajazifuta zile post ntaibandika.

Wajinga Ndiyo Waliwao.
 
Napata kigugumiza kidogo, alikukaba kwa style gani huyo jogoo..!?
 
Mapovu yooote hayo!hasira za nini?hizi fiksi tu!humu wote si watoto......kwa kifupi sisi watu wa pwani....tuliozoea bahari....hizo stori za kawaida saaana!ni kama stori za vibwengo....majini chunusi.....nk uwe mpole tu!

Mkuu wengine hatuijui Bahari mana huku mkoani hakuna bahari, ebu acha mshana atuhabarishe basi ili siku tukifika pwani tuchukue tahadhari
 
Mshana jr nipe mimi hizo hela za kumlipia huyu nguchiro hela ya nauli na chakula na kulala guest inayonukia udongo mbichi nifanye mimi utafiti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…