Kila Mtaa/ Kijiji kiwe na Database ya wananchi wake hasa Vijana na Mikopo itolewe kwa njia hizo

Kila Mtaa/ Kijiji kiwe na Database ya wananchi wake hasa Vijana na Mikopo itolewe kwa njia hizo

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,339
Reaction score
1,493
Habari Tanzania !

Nawaomba wenye Mamlaka kwa kuwa mmewaza kuanzisha Wizara rasmi inayohusu Vijana. Napendekeza mfumo mzuri wa kusaidia vijana hasa kuanzia ngazi ya chini wanakoishi.

1. Kila Kijiji/ Mtaa pawepo na Ofisi ya Vijana (Vijana Village/ Street Department).
(Kata = Vijana Ward Department; Wilaya = Vijana District Department; Taifa = Vijana National Department).

2. Kila Kijiji/ Mtaa pawepo na Database - kuhusu vijana kuanzia Idadi yao; Jinsia, Umri, Elimu nk).

3. Hizi Departments ziongozwe na vijana pekee toka maeneo husika na sio mambo ya upendeleo na milango ya kisiasa, udini na ukanda.

4. Mwisho; kwenye hizo Departments wekeni Fedha Vijana wajiajiri na wajipambanie maisha yao, pasiwepo na mambo ya masharti yoyote kupata hizo pesa yaani wapeni pesa.

Mfano;
Kila Kijiji/ Mtaa wapewe pesa isiyopungua 200milioni, wapewe msukumo wa mawazo wajiajiri wenyewe na hizo Tenda zote ambazo ni Local kuanzia Mtaani/ Vijijini wapewe yaani iwe ni haki yao.

Wasiingiliwe maamuzi yao kivyovyote vile; Serikali itakachokifanya ni kufanya Ukaguzi wa Fedha kupitia Ofisi ya CAG kila mwaka.

Karibu
 
Hayo yote yatafanyika serikali ya huyu mama muuaji ikitoka madarakani.

Yani utuulie ndugu zetu kisha utoe rushwa ya pesa tukae kimya,haiwezekani.

Lazima damu ya waliouliwa kikatili kuanzia Oct 29 ilipwe kwa namna yoyote kisha ndo turudi kwenye hiyo mipango uliyoisema hapo.

Sheikh Hasina wa Bangladesh kahukumiwa kunyongwa kwa kuua watu 1,400 tu.

Huku Samia ambaye ni rais haramu kaua watu 10,000 unataka mambo yapite tu kirahisi rahisi as if waliouliwa ni paka sio binadamu!

Lazima watu wawajibike kwenye hili.
 
Back
Top Bottom