Maandishi hayo yanapatikana kwenye thread Hii Hapa Ya JF Tshirt.mkuu invisible, ingawa ninaweza kujiprintia ya kwangu lakini nitapenda kununua mbili, yangu moja na my wife (naoa desemba 23), medium moja na large moja tena ziwe polo shirts. Ninashauri pia kuwepo na aina tatu au nne za messages ktk tshrts halafu ukizipost hapa iwe rahisi members kuchagua. ujue ktk forums yako kuna wana ccm, chadema, tlp nk, pia na sisi wengie tusioamini ktk siasa. naona nimeongea sana (tatizo nilimeza kasuku utotoni).
Mkuu
thats is what i wanted from you guys.
wengine wanadhani kusupport haruc ni kuchangia mifwedha ila naamini kuwa jamii ikikubariki basi hata ndoa hudumu. cha msingi kuunga mkono kwa namna yeyote...
nilikuwa outline muda sasa thus sijatembelea threads lakini sasa nakenda huko
(unaweza kuipost hii comment ktk thread)
Thanx sana Steve D
mbona hatukualikana wakati anatongoza?
Wana JF,
Hii ni kumwombea mema ndugu yetu Msanii kwenye siku yake ya ndoa.
Tukiwa kama jamii yenye kupenda muungano kwenye matukio yanayo tuzingira kama Wanadamu, kwenye raha na kwenye majonzi, napenda kumtakia kheri na faraja Msanii kwenye siku yake aliyo itaja hapa chini:
Maandishi hayo yanapatikana kwenye thread Hii Hapa Ya JF Tshirt.
Nimatumaini yangu hapo juu kuwa Msanii ametaja hiyo siku akimaanisha 23-12-2007, na siyo 23-12-2008.
Ni hayo tu, Kila la Kheri Msanii.
SteveD.
Msanii,
Hongera sana... Kila la kheri mkuu! Sisi wengine hatuoi wala kuolewa. Labda tuunganishwe na robots nyingine.
Kwa niaba ya JF Administration crew, nakupa pongezi na kukuomba uwe mvumilivu katika ndoa yako. Upendo utawale daima na furaha iifunike familia yenu.
Majaribu ni mtaji, tumia kila fursa ipatikanayo kuwaelimisha wanenu (mkijaaliwa) pamoja na mkeo na wewe usijisahau kujiendeleza kimasomo.
Epuka ugomvi usio na msingi baina yako na mkeo. Mke ni mkeo, mheshimu, elewa ni ubavu wako. Ndoa ni tamu wawili mkiamua kuifanya iwe hivyo. Inaweza kuwa chungu mkiamua pia.
Hakuna upendo unaokwisha, huchuja na hatimaye hujengwa na wahusika (wawili bila kuwaingiza majirani ama ndugu). Mapenzi ni hisia, hujengwa kwa wawili kufanyiana matendo ya upendo ambayo ndiyo huyajenga mapenzi ya dhati. Epuka kuwaingiza ndugu katika mahusiano yenu. Washirikishe mengine lakini si maamuzi ya nini umfanyie mkeo na nini usimfanyie. Huyo ni wewe na wewe ni yeye!
Penye nia pana njia, huyo ni malaika wako, ubavu wako, damu yako, chaguo lako (wengine si mali kitu kwa sasa). Mfanye aone faida ya kuwa na wewe.
Kila la kheri katika ndoa yako na Mwenyezi Mungu awajaalie mpate watoto wenye afya njema na busara katika jamii.
Invisible
mkuu brazameni,
nilisita kuwaalika wakati natongoza ndito yangu kwa kuwa mngekuwa mnanipigia makelele wakati naconcentrate.
ninasubiri pongezi kutoka kwa invisible, ole, worm, shy, mwanakijiji, mwafrika wa kike, bubu mtamka ovyo, zitto, mtu (alikuwepo ktk jopo la mshenga) pamoja na ninyi nyooote....
mniombee tu nisije nikakosea njia wakti wa honeymoon nikaingia mlango wa no entry....
Thanx Steve D
Mungu Akubariki kwa kuanzisha thread hii kwa ajili ya haruc yangu
Kama unapata maziwa rejareja ya nini kununua ng'ombe mzima na kupata taabu za kuasafisha banda, kutafuta majani, madawa nk.
Mambo ya kujitafutia uzee hayo....