Kikwete: Uvumilivu sasa basi...

Hapa mi naona kama Rais anazidi kuwatukana wana wa kusini!
Hivi watu wa kule hawana ufahamu wa kutambua kuwa rasilimali zinazopatikana huko zinapaswa kuwanufaisha wao kwanza na pia kujengwa kwa mitambo ya kuichakata hiyo gesi huko kutawanufaisha mpaka wahamasishwe na wanasiasa?
Hata kama wanasiasa wamefanya hivyo, je sio haki ya wana mtwara kufahamu faida itakayopatikana na rasilimali za nchi yao?

Kikubwa wala hapaswi kuwaadaa wananchi wenzetu wa huko kwa kauli za kipuuzi namna hiyo,na hapaswi kuwatupia lawama wanasiasa kwani wametimiza wajibu wao wa kuujulisha umma namna yeye na serikali yake wanavyozihujumu rasilimali zetu.
SULUHU NI KUJENGA MTAMBO WA KUCHAKATA GESI NA KUZALISHA UMEME HUKO HUKO MTWARA NA BAADAYE UINGIZWE KWENYE GRIDI YA TAIFA ILI UWANUFAISHE WATANZANIA WOTE KAMA WANAVYOTUHUBIRIA.
Kwa kufanya hivyo kutawapatia watu wa mtwara ajira!

HILO NDO SULUHISHO LA BUSARA BABA RIZIWANI, NA DILI MNAYOTAKA KUIPIGA KWENYE UJENZI WA BOMBA TAFUTENI MAHALA PENGINE, WATU WA KUSINI WAMEAMKA,HAWATAKI KUFANYWA MAVELU bhaaaa!
 
Anza na NAPE NNAUYE yeye na ile 4MCHAGGA... akaandika kila MAHALI chuki zake na hilo KABILA...
 
Bahati mbaya sana makusudi rais as a stateman ameamua kusambaza siasa za tumbo. kwa kupotosha madai ya wanamtwara kwa kuamua makusudi kabisa kuchukua maana finyu ya madai ya wanamtwara kwa kusema eti wanataka gesi iwanufaishe wao tu. Kama hajapata nakala ya madai yao, apewe.

ukisema dar kuna viwanda na miundombinu iliyotayari kwa kutumia hiyo gesi, hiyo siyo sababu ya kufanya usafirishe hiyo gesi, kwa sababu hiyo miundombinu inayoongelewa sio kama mlima kilimanjaro, kwamba by nature they are there, ilijengwa, kwa hiyo, as long term plans za nchi, wekeni mitambo mtwara, viwanda vitajengwa. sio lazima vijengwe in two, three, etc years, inaweza ikawa hata baada ya miaka mitano, ishirini, hata dar hivi viwanda tunavyoongelewa havikuja siku moja, vimechukua muda.

All in all, wanasiasa hasa walioko madarakani, wasilete vitisho, bali wajibu hoja. maendeleo yanatakiwa yatoke kila kona ya nchi sio dar tu.
 
Hii mikwala haina maana, badala ya kuja na mikwala Mr. Prezidaa angejiuliza kwa nini wana-mtwara na lindi wamakuja juu kuhusu suala la gesi asilia.

Ni wazi wamejifunza ktk maeneo mengine raslimali hazijawanufaisha wananchi! haya Mhe. Mkono anawaunga mkono kwa100% kwa vile naye kaona wananchi wa Buhemba hawakunufaika na dhahabu...badala yake wanafaidika na mashimo yaliyoacha na wakwapuaji.

Labda serikali ije na mpango mkakati wa kujaza mashimo hayo maji na kufuga samaki. ajabu mhe. Mkono eti ndo naye sasa anajifanya kushtuka. alikuwa wapi hadi wakwapuaji wakabeba dhahabu yote ya Buhemba!

Hawa viongozi wa CCM wanaojifanya kuwatetea wananchi ni wanafiki...wameona CDM imewapa elimu wananchi nao wameamuka..sasa viongozi hao wana hofu ya kutupwa nje ya sanduku la kura 2015 kama wasipokumbatia 'nguvu ya umma'!
 
He huyu Mzee sasa anazeeka vibaya wanasiasa gani anao wasema labda Murji aliyeungana na Wananchi kudai haki yao au anamsema Muhongo Mr Matusi anayedharau kila mtu ambaye hajasoma,au Simbachawene tunayesikia alivarishwa nguo za jeshi badala ya kuonana na wananchi ,kama ndio msimamo huo kwenye maandishi hapo juu,Raisi wetu ammue moja aiache ikulu uchaguzi uitishwa
 
Inakuwaje mwanzilishi wa udini analalamika tena mwenyewe alionywa akapuuza sasa atakula matapishi yake KIkwete bwana wa ajabu sana
 
Blistering Barnacles....:A S angry:

Hivi kumbe walikuwa wanavumiliana wakati watu wanapoteza mali zao, uhai wao na kushindwa kuenedelea na shughuli zao za kila siku ?

Sasa watawalipa nini wale waliokumbwa na haya matatizo sababu ya uzembe wao ?; Ni kweli better late than never ila inabidi wale waliovumilia hizi nyufa mpaka sasa tunajenga ukuta nao wawajibike
 
Suala ya kuamini Dar ndio kitovu cha uchumi bongo milele sio UKANDA wenyewe huu? Kwa hiyo watu wa dar ndio wanaojua kufanya kazi na kutumia vizur kufaidika na rasilimali hizo peke yao tz nzima? lini mikoa mingine itajipenyeza kuongeza ukuaji wa uchumi kieneo?

Hapa tunapigwa changa hakuna lolote.
 
Rais anawalaumu wanasiasa ! Kila sehemu ni kulaumu tu. Acha lawama fanya kazi wewe ndo umeshika mpini. Kwani Rais sio mwanasiasa mbona ni wale wale kundi moja.
 
Rais kaongea jambo zuri.rasilimali za taifa zinufaishe watu wote kama taifa na si kila mkoa udai rasilimali zake na kama ni suala la kila kwenye rasilimali zitumike palepale tu; sasa kwa nini tunafikiri katika level ya mkoa na isiwe level ya kata,kijiji au mtaa n.k bali mkoa?
 
Blistering Barnacles....:A S angry:

Hivi kumbe walikuwa wanavumiliana wakati watu wanapoteza mali zao, uhai wao na kushindwa kuenedelea na shughuli zao za kila siku ?



Sasa watawalipa nini wale waliokumbwa na haya matatizo sababu ya uzembe wao ?; Ni kweli better late than never ila inabidi wale waliovumilia hizi nyufa mpaka sasa tunajenga ukuta nao wawajibike

Oh wow... CAPTAIN HADDOCK... wa TINTIN
 
Back
Top Bottom