Kikwete: Uvumilivu sasa basi...

Kikwete: Uvumilivu sasa basi...

Sijawahi kumwona Rais kama huyu kazi kupiga domo tu bila vitendo
 
Halafu anatumia hoja za kijinga. Eti Bukoba na ndizi zao, akisahau kuwa Bukoba wanauza ndizi na kufaidika nazo. Kilimanjaro na kahawa yao, hawa pia wanauza kahawa na kufaidika nayo. Awape uwezo watu wa Mtwara wazalishe na kuuza gesi tuone kama wataendelea kulalamika. What logic!
 
“Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwambahatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha,” alisema Rais Kikwete.
Mkulu angelianza na moto huu kwenye suala la EPA tungelimuamini zaidi leo hii lakini bado hizi kauli zinaonyesha mashaka, na hapo kwenye red wafuatiliaji wa mambo jazeni hapo kinachomaanishwa
“Ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa wanasiasa kujaribu kuigawa nchivipandevipande kwa sababu ya kujitafutia umaarufu kwa kutumia rasilimali zataifa,” alisema Rais Kikwete
kwamba ccm wanafanya yote hayo sio kwa ajili ya huo umaarufu, na je taifa maana yake ni Dar es Salaam?? Mtwara, Kigoma, Kagera sio taifa?
“Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja wakati kila mmoja anadai rasilimalikutoka kwenye eneo moja ibakie na kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwana nchi moja na yenye umoja wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kunanchi ya kahawa kule Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba,”alisema Rais Kikwete na kuongeza:
kwa hiyo mnada wa kahawa uhamie Dar es Salaam no kwa ajili ya kulinda umoja wa kitaifa? na kiwanda cha kuprocess na kupaki kahawa nacho kihamishiwe Gerezani kutoka Bukoba kama ilivyofanyika?
“Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara tu,basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu waMsimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara,kilomita 200 kutoka Newala.”
simply devide and rule, sijui ni nani sasa wa kuwa macho maana siasa ndizo zinataka kutumika kuwanyanganya rasilimali zao wananchu wa kusini.
Msisahau maneno ya Mzee Marechela
ya 'waridi kununia waridi'

 
Naona sasa ametimiza malengo yake aliyokuwa amedhamiria kuyafanya kumbe vurugu zote zilikuwa na baraka zake ndiyo maana yalipotokea hakukemea!
 
Kauli za kitoto hizi,tangu 2005 tulishaziskia na tumeshazichoka uvumilivu huo unao wewe lakini sisi wananchi hatuwezi kukuvumilia kamwe kama uamini subiri 2015.
 
Kauli ya Rais Kikwete kuhusu gesi na Wanasiasa wakati akimuaga Balozi wa Uingereza

16/01/2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia suala la raslimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujifatufia umaarufu wa kisiasa na kuwapotosha wananchi.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa wanasiasa kujaribu kuigawa nchi vipande vipande kwa sababu ya kujitafutia umaarufu kwa kutumia raslimali za taifa.

Rais Kikwete ameyasema hayo leo, Jumatano, Januari 15, 2013 wakati alipokutana na Balozi wa Uingereza nchini ambaye anamaliza muda wake, Mheshimiwa Dianne Corner ambaye alifika Ikulu, Dar Es Salaam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi katika Tanzania.

Rais Kikwete na Balozi Corner wamezungumzia masuala mbali yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Uingereza, masuala ya ukanda wa Afrika Mashariki na masuala ya kimataifa.

Kuhusu ugunduzi wa gesi asilia uliofanywa na Kampuni BG ya Uingereza katika eneo la Msimbati kwenye Bahari ya Hindi, walikubaliana kuwa hilo ni jambo jema na lenye kuleta matumaini kwa Tanzania hasa wakati itakapoanza kuvunwa katika miaka michache ijayo.

Kuhusu siasa zilizoanza kujitokeza kufuatia ugunduzi huo mkubwa wa gesi asilia, Rais Kikwete amesema kuwa ni tabia ya hatari kwa wanasiasa kutumia gesi asilia hiyo ama raslimali nyingine kujijengea umaarufu wao ambao umeporomoka.

"Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja wakati kila mmoja anadai raslimali kutoka kwenye eneo moja ibakie na kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye umoja wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa kule Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba," amesema Rais Kikwete na kuongeza:

"Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara bali ni watu wa Msimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara, kilomita 200 kutoka Newala."

Ameongeza: " Unajua nchi yetu inao baadhi ya wanasiasa wenye uchu wa umaarufu na ambao wanatumia jambo hili jema kwa manufaa yao binafsi bila kujali umoja na jadi ya taifa letu la raslimali zetu kutumika kuiendeleza nchi nzima."

Kuhusu uhusiano kati ya Tanzania na Uingereza, Rais Kikwete amemshukuru Balozi Corner kwa kazi nzuri ya kuimarisha uhusiano huo. "Umeufikisha uhusiano wetu kwenye hatua ya juu kabisa na tunakushukuru kwa jambo hili."


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

15 Januari, 2013

Source: wavuti.com - wavuti
 
nahisi ndio mwendelezo uleule wa kushauliwa vibaya na wasaidizi wake,nimeamini rahisi kweli tunae!!!!!!!!!!
 
I conquer with H.E Jakaya the govt should now flex its muscles and stem out all sorts of hooliganisms coming in the forms of religious and resources activism.
 
Well, and the leadership by misinformation is just going strong on and on inexorably!
 
Hana jipya huyu.......................Mi simwelewi hata anataka kusema nini.
 
SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana. Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.
 
Kweli tanzania wenzetu afrika mashariki wana marais sisi tunaye rahisi jk.
 
Kuhusu gesi
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.
 
"Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu wa Msimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara, kilomita 200 kutoka Newala."
MWANANCHI
 
KITAIFA

Na Waandishi Wetu

Posted Jumanne,Januari15 2013 saa 20:0 PM


KWA UFUPI


"Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha," alisema Rais Kikwete.



SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana.
Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.



Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.



"Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha," alisema Rais Kikwete.



Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Juma Mpango alisema jumuiya ya mabalozi imefurahishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa ikishughulikia vurugu za kidini ambazo zilitaka kujitokeza bila kusababisha madhara kwa wananchi.



"Tumeridhishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa inashughulikia mambo yake vizuri. Tunaomba mwendelee kushughulikia amani ya nchi hii maana ndiyo mhimili wa nchi za Maziwa Makuu," alisema Balozi Mpango.



Kuhusu gesi
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.



Wakati Rais Kikwete akitoa kauli hiyo jana, habari kutoka Mtwara zilidai kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amewekewa magogo barabarani kumzuia asiende kwenye kijiji kinachozalisha gesi hiyo, huku Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo akizomewa.



Hata hivyo, polisi walikiri wananchi kuweka magogo barabarani kwa lengo la kumzuia waziri huyo, lakini ikaeleza kuwa gari lililozuiwa siyo la Simbachawene.



Akizungumza na Balozi Corner, Rais Kikwete alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia suala la rasilimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujitafutia umaarufu wa kisiasa na kuwapotosha wananchi.



"Ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa wanasiasa kujaribu kuigawa nchi vipandevipande kwa sababu ya kujitafutia umaarufu kwa kutumia rasilimali za taifa," alisema Rais Kikwete na kuongeza:



"Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja wakati kila mmoja anadai rasilimali kutoka kwenye eneo moja ibakie na kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye umoja wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa kule Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba," alisema Rais Kikwete na kuongeza:



"Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu wa Msimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara, kilomita 200 kutoka Newala."



"Nchi yetu inao baadhi ya wanasiasa wenye uchu wa umaarufu na ambao wanatumia jambo hili jema kwa manufaa yao binafsi, bila kujali umoja na jadi ya taifa letu la rasilimali zetu kutumika kuiendeleza nchi nzima."

DC azomewa
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea na viongozi wawili wa CCM Mkoa wa Lindi; Mwenyekiti Albert Mnali na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, Fadhili Liwaka, juzi walijikuta katika wakati mgumu, baada ya umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wake kuanza kumzomea alipowataka waache kuunga mkono mgogoro wa gesi.



"Serikali haina nia mbaya na wakazi wa Lindi na Mtwara, kinachofanyika ni kuipeleka hii gesi sokoni ili iweze kutumika kwa faida ya Watanzania wote kwani soko la gesi lipo huko inakopelekwa na ni sehemu ya mgawanyo wa rasilimali zetu za Taifa," alisema DC Chonjo.



Zomeazomea ilianza baada ya kuwataka wananchi wa Nachingwea kutokujiingiza kwenye maandamano yanayoandaliwa hivi karibuni katika Miji ya Mtwara na Lindi kuishinikiza Serikali kuacha mpango wa kuhamisha gesi kwenda Dar es Salaam.



Katika mkutano huo, Chonjo alisema wakazi wa Nachingwea hawana sababu ya kushiriki migomo hiyo kwani tangu awali, wamekuwa wakitumia rasilimali zilizo nje ya wilaya na mkoa wao, akitaja baadhi kuwa ni umeme na Barabara ya Kibiti hadi Lindi ambayo ujenzi wake umetegemea rasilimali zilizotoka nchi mzima



Alizomewa baada ya kuruhusu maswali na mkazi aliyejitambulisha kuwa ni Geofrey Membe wa Kata ya Nachingwea kumweleza kuwa wanapaswa kutambua kuwa gesi hiyo ni muhimu kubaki Mtwara ili mitambo ya kuzalishia umeme wa gesi ijengwe Mtwara.



"Mikoa ya Mtwara na Lindi inachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa kupitia zao la korosho," alisema. Kauli hiyo ilipokewa kwa shangwe na wananchi waliohudhuria.
Baada ya mkuu huyo wa wilaya kumaliza mkutano huo na kuondoka, kundi la vijana lilianza kuwafuata viongozi wa CCM wakiimba ‘gesi haitoki… gesi haitoki'.



Simbachawene
Ilidaiwa kwamba msafara wa Simbachawene uliwekewa magogo barabarani juzi saa nane mchana na kumfanya waziri huyo na msafara wake kugeuzia katika Kijiji cha Ziwani na kurejea mjini Mtwara.



Habari hizo ambazo zimekanushwa na Simbachawene zilidai kuwa aliwasili Mtwara kwa ndege asubuhi na kupokewa na viongozi wa mkoa kabla ya kuanza safari ya kwenda Msimbati kimyakimya.



Mwenyekiti wa Kijiji cha Msimbati, Salum Athumani Tostao alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa polisi walikwenda kijijini hapo na kufyatua mabomu ya machozi.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mary Nzuki alithibitisha wananchi kufunga barabara lakini alikanusha madai kwamba Naibu Waziri Simbachawene alikuwapo ziarani mkoani hapa.
"Waandishi wa habari waliokwenda katika ziara za kazi zao za kawaida ndiyo waliozuiliwa na wananchi hao… Naibu Waziri (Simbachawene), hajawahi kufika Mtwara kwa siku ya jana… Wananchi walidhani hilo gari ni la waziri lakini ukweli si yeye," alisema Kamanda Nzuki.



Akizungumzia madai hayo Simbachawene alisema: "Hapana si kweli, ningekuja hapo mjini nisingejificha… Tatizo la wananchi wetu hawajapata elimu sasa nitaendaje huko kimyakimya ili iweje? Jana nilikuwa ofisini na vikao kutwa nzima… Nenda ‘airport' (uwanja wa ndege) kaulize… Hata mimi nimeona kwenye jamii forum mtu yeyote anaweza kuweka chochote."

Habari hii imeandikwa na Christopher Lilai, Nachingwea na Abdallah Bakari, Mtwara na Mkinga Mkinga Dar



 
Huyu sasa na sisi wananchi uvumilivu unatushinda! Hawezi kuongea kitu kimoja ca kueleweka!! anachanganya mambo mengi pamoja, aseme tu kwa kilamoja tujue anaakili!!
Udini aseme kwa uwazi.......ache unafiki ilhali ni yeye anaye wapeleka watu wa TISS Iran wajifunze mbinu za kuuingiza udini nchini!!

Uvumulivu unatushida kuwa na raisi mbovu hivi!!
 
Back
Top Bottom