Wakuu,ni ukweli usiofichika kuwa Rais Kikwete anastahili kupewa credit kwa kuleta mahusiano mazuri na nchi za nje.ikiwemo Marekani. Rais Kikwete aliweza kuconvice jumuia ya Leon Sullivan Foundation kufanyia mkutano Arusha. Sullivan Summits are a bridge between America and Afica and the world serving as a forum for economic and cultural cooperation. Kikwete was able bring Mr Bush to Tanzania na kusaini mkataba wa misaada kupitia Millenium Challenge. . Haya mambo si rahisi. Kwa hiyo kwenda kukutana na Obama ni achievement ktk kuleta mahusiano mazuri na Marekani. Baadhi ya wachangiaji nadhani mnayo chuki na Rais Kikwete. Hata afanye zuri lipi hamlikubali.
kikwete anakuwa rais wa kwanza wa afrika kusini mwa jangwa la sahara kukutana na obama
So what? Just a photo-opportunity. Very simplistic. Nothing. Nothing at all.
Sidhani kama Obama amemwita JK, hakuna dalili zozote za kuashiria hilo.
Obviously kwenye hii safari, ni JK aliyejipendekeza na ni kwa manufaa yake binafsi na wala sio kwa ajili ya Watanzania. JK amebembelezea mpaka White House wakampa nafasi ya kupiga picha na Obama ili akaitumie Mwakani kwenye uchaguzi.
- Mkutano muhimu kihistoria kama huo kati ya two black presidents, the first US black president na an African head of state ungepigiwa mabango kitambo, huko US na TZ-Daily News kwa angalau wiki mbili hivi mfululizo. Lakini ni mpaka JK alipokuwa West Coast ndio tangazo likatolewa na White house hapo jana, ikionyesha kabisa hii ni kama mgeni asiyekuwa na mpango.
- Umuhimu wa TZ kwa serikali ya Obama ni mdogo sana au haupo kabisa otherwise angeshateua balozi mwenye uzito kama alivyofanya Bush.
- Obama hamhitaji JK ili aongee na ndugu zake Kenya, after all amekuwa anaongea nao kila siku directly au through dada yake ambaye alikuwa naye tokea kwenye kampeni.
- Zaidi ya hayo, Odinga na Obama ni ndugu na wanafahamiana vizuri sana kabla hata Obama hajawa raisi. Kwa hiyo hakuna dalili zozote za Obama kumhitaji JK kwa ajili ya kuongea na Wakenya.
Kweli White House kiboko, yaani baada ya Obama kumaliza shughuli zake zote za siku mpaka kuchill na Pittsburgh steelers, ndio jioni wakati rush hour ikikaribia kuanza anakutana na JK ahahahahahahah
GodBless Tanzania
Tell them Makaa! JK needs the pictures just to feel good. Members please monitor the duration of the meeting; will it be 5, 10 or 15 minutes?
Endelea.....Matunda yapo, unataka tuanze kuzitaja?
1. Safari ya Bush TZ na Millenium.....
2. Kupata Misaada (soma MIKOPO)
3.
4
5.....
DC ya wapi tena? Si yuko hapa Washington DC?Lini Rais wetu atakuwa DC?
"An al-Qaeda suspect is to become the first inmate at the Guantanamo Bay camp to stand trial in a US civilian court".
Tanzania's President Jakaya Kikwete is to hold talks with President Obama - the first African head of state to meet the new US leader in Washington".
Mkuu nakukubali naelewa fika hakuna njia bora kama kuboresha miundombinu lakini jaribu kutazama upande wao hawa kina JK wanafikiria nini!. Pengine wanafikiri kwamba kama huna mwekezaji ya nini kuboresha Miundombinu..ya nini kununua mbeleko mwana hajazaliwa!..ndivyo tunavyofikiria na kuweka haramu ktk kufanya hivyo.Mkandara,
Njia bora pekee ya kuvutia wawekezaji Tanzania ni kuboresha miundombinu na kupunguza urasimu. Hizi safari hata Mheshimiwa asafiri mara ngapi hazitasaidia kitu. Waswahili wanasema chema kinajiuza.
Wakuu kuna kitu kimoja ambacho hadi leo sijaelewa na ndio maana nashindwa sana kumlaumu Kikwete na hizi safari zake..Sielewi malengo yake lakini kama kweli anajaribu kuiuza Tanzania basi bila shaka hakuna njia nzuri kama rais wetu kuwafuata makwao hawa jamaa kwa sababu hatuwezi kujiuza kama wenzetu nchi za Asia..
Nasema hivi kwa sababu navyofahamu mimi Mataifa makubwa na all big corporates hawawezi hata siku moja kuingia ktk Tender za nchi maskini hasa tunapotaka kuuza mali au kutafuta wawekezaji. Tender zetu zote toka wakati wa Mkapa zimechukuliwa na mashirika mbuzi mashirika ya kifisadi vile vile kwa sababu mara nyingi uwekezaji inatakiwa nchi host ndio ijitangaze inacho offer badala ya haya mashirika kutuma maombi.
Tanzania bado kabisa haijafikia uwezo wa kujitangaza na masirika au mataifa makubwa kugombea nafasi za uwekezaji nchini isipokuwa tunatakiwa sisi kujitangaza kwao. Na ukweli utauona ktk mashirika yote ya Umma tuliyowahi kuuza.. tumewauzia matapeli, mashiurika yasiyokuwa na record ya kazi hizo zaidi ya tungo za resume ili kupita ktk Mchekecho wa Tender.
Hata siku moja huwezi kuwaona Amtrak wakiomba kuendesha reli yetu, Hata siku moja huwezi kuwaona Bell wakijipanga ktk tender za kusambaza nyaya za simu na mawasiliano nchi maskini. Hata siku moja huwezi kuona Intel au AMD wakifikiria kuwekeza Tanzania kutengeneza PC hardware pamoja na kwamba raw za vifaa vingi zinapatikana Afrika..
Ni muhimu sana sisi Watanzania kusoma wakati, kufahamu tamaduni ya biashara ya nchi hizi.. lazima tujitangaze na tuwe mbele kutoa offer kwao kwani hawa jamaa ni kama wahindi.. Mke ndiye hutafuta mchumba na kutoa mahalai sii sawa na utamaduni wetu ambao kila siku tunatangaza tender ktk magazeti na wanaokuja kutuchumbia ni mfano wetu.. Matapeli!
Hivyo nafanya subira, sidhani kama Kikwete ni mjinga kiasi hicho cha U Vasco tuuu kivinjari dunia..Naomba Mungu isiwe hivyo, ila uwe ni mtazamo mpya wa kutafuta wawekezaji kutokana na imani ya wana CCM - Progressive. Siupendi mfumo huu na sintapendelea nchi yetu kuuzwa kwa wageni lakini sina budi kukubali ndio mbinu bora za wana Progressive kuvuta wawekezaji wenye uwezo mkubwa na kwamba naelewa nini malengo ya misafara hii badala ya kumlaumu Kikwete. Pengine yawezekana miaka mitano ijayo tutaweza kuona matunda ya kukoloniwa, ndipo tutakapo shika adabu na kuelewa tofauti ya mirengo hii.