Kikwete, sasa umemwelewa Sumaye?

Kikwete, sasa umemwelewa Sumaye?

Alishasemaga pia haelewi kwanini Watanzania ni masikini!
 
Hata mimi kusema ukweli ile siku anatangaza kuamia upinzani sikumuelewa, lkn siku zinavyozidi kwenda nazidi kumuelewa
​wewe ni jiwe sasa jikumbushe mara kwa mara usije sahau kumpigia kura lowassa!
 
Gold, Silver na Stone. Na mimi naongezea moja hapo...Dafu! Huyu sio tu hafundishiki bali hata kusikia hasikii. Hata mkimwambia asisafiri, atasafiri tu.
 
Vipi CCM wanaojifariji kwa kujaza umati kwa malori...kuhonga....wanafunzi...wasanii inawasaidia nini?

Ingekuwa haiwasaidii ungekuwa shaba ranks hapa unafoka foka tu si utulie au wasanii ulitaka waje UKAWA hahaha . tufe bwana
 
Ndugu wana JF,

Nimelazimika kumwandikia rafiki yangu kipenzi JK waraka huu wa swali kwamba sasa amemwelewa Sumaye? Ktk makundi ya wanafunzi tunazo aina tatu yaani gold...silver...stone.

Gold huweza kuelewa bila msaada wa mwalimu na kwa haraka sana... Silver huelewa mara moja akifundishwa na
mwalimu na hahitaji nguvu ya ziada ... Stone yeye hata akifundisha ni ngumu kuelewa na huhitaji mbinu kali zaidi aelewe ikibidi kwa kurudia rudia somo lkn hawa hawafiki mbali kielimu.

Nimeanza na utangulizi huo nikiikumbuka kauli ya rafiki yangu JK pale jangwani kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM aliposema amemsikiliza Sumaye hajamwelewa!! anasema mpaka siku hiyo anapokwenda uwanjani alikuwa hajamwelewa!!!!

Lakini ktk sokomoko hilo tumeshuhudia CCM ikibadili mbinu na sera... Bajeti ya kampeni ikiongezeka maradufu na hata kuwakumbatia wale JK aliowaita wanamiliki viwanda vya uongo ili tu kupunguza mvumo wa kauli na sumu za Sumaye majukwaani ndo nauliza sasa JK amemwelewa Sumaye?

Ndani ya vikao vya siri ajenda imekuwa Sumaye... ndugu yangu BM hana raha tangu Sumaye aondoke CCM...

Vilio na kutupiana lawama vimetawala ndani ya CCM juu ya kile Sumaye anafanya huko UKAWA!!!

Mafaili machafu dhidi yake yametafutwa yamekosekana!! hata hoja ya shamba halali la mvomero iliyoletwa na Makamba haijauza sasa wanaulizana ITAKUWAJE SUMAYE ANAYETUJUA SISI BINAFSI AKIAMUA KUFUNGUKA??

Siku anajitoa CCM Sumaye alisema huko CCM mmemuona ni sisimizi tu kiasi cha kuandika barua kutojibiwa hivyo wataona umuhimu wake akiwa Upinzani na ni dhahiri sasa anawatetemesha ndipo nauliza JK sasa umemwelewa Sumaye?

Nimeuliza kote walikopita wana UKAWA nimeambiwa watu wamekua na shauku kubwa mno yakumsikiliza bwana zero kuliko yeyote na amekuwa akitoa hamasa sana ....

Sumaye amejenga ujasiri sana kwa wapinzani na wapenda mabadiliko... ameondoa hofu na woga... amejenga kujiamini sasa vinaanza vitisho kuwa nchi haiendi upinzani!!!!

Nauliza tena JK uliyesema kwa dharau humwelewi Sumaye sasa umemwelewa au abadili mbinu za ufundishaji? umuulize na mdogo wako Makongoro ule mchezo wa CHANDIMU vipi mbona amechoka mapema??

Ahsante kwa kunisoma natumai umenielewa!!!

Ndimi LUSUNGO.
Atakuwa kamwelewa ndio maana kuna Kikao kilfanyika ....Ndoto Hotel Arusha
 
Atakuwa kamwelewa ndio maana kuna Kikao kilfanyika ....Ndoto Hotel Arusha


Ndio maana nimemkumbusha kwa swali ili tujue kaelewa au bado anahitaji nondo zaidi...
 
Back
Top Bottom