Kikwete na viwanda vya uongo - Mwanahalisi, gas Mtwara etc

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
obama_n_kikwete_500x307.jpg

Katika moja ya hotuba za Kikwete mwaka jana, alitamka jambo hili: "viwanda vya uongo." Nimelikumbuka neno hili katika matukio ya sasa hivi, nikakumbuka rais wangu alivyosema kuhusu viwanda vya uongo. Naam, ukiona mtoto anakuwa mwongo ujue ni kutokana na malezi ya familia yalivyo, maana yake baba na mama wana hulka ya uongo ingawa hutokea mtoto akawa na tabia ya peke yake wasiyokuwa nayo wazazi.

Gazeti la Mwanahalisi kufungiwa.
Kikwete akiwa katika kikao cha viongozi wa bara la Afrika, amejenga utetezi kuhusu kulifungia gazeti la Mwanahalisi kwamba lilichochea askari kugoma. Kumbukumbu zangu gazeti jingine ndilo liliandika habari hiyo, na Mwanahalisi limefungiwa sababu ya kufunua ukweli juu ya aliyehusika kuteka, kumtesa na kisha kumtupa msitu wa Mabwepande Mwenyekiti wa Madaktari nchini.
Mtazamo wangu
Aliyeongopa ni mwanahabari aliyemnukuru Rais au kama Rais mwenyewe alitamka basi jambo hilo linahitilafu na linaonekana kama ni wongo kwani gazeti la Mwanahalisi halijawahi kuandika kushawishi askari kugoma.

Gas ya Mtwara
Katika kampeni Kikwete aliahidi mengi kila kona ya nchi ikiwemo Mtwara kuahidi uanzishwaji wa viwanda na kuwa na kinu cha kufua umeme megawati 300. Ajabu katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka na alipowahutubia pia mabalozi wa nchi za nje nchini aligusia hilo bila kukumbuka ahadi yake ambayo aliithibitisha alipotembelea eneo la Mtwara kuwashukuru wapiga kura.
Mtazamo wangu
Suala la gas Mtwara limeenda kinyume cha ilani ya uchaguzi CCM hali kadhalika ahadi za Rais, inaongekana ukweli ulivyoibua kuanza mradi huo kumekuwa na dalili za kuongopa na kupindisha makusudia ya awali. Viongozi wa karibu dini zote, wanasiasa, wanaharakati, wananchi wote wamemnukuru Rais alivyoahidi na ilani ya uchaguzi ya CCM. Je, nani anaongopa?

Polisi kuua raia
Katika tafrija ambayo Rais Kikwete aliwakaribisha wanadiplomasia wa kigeni Ikulu kuwashirikisha kuukaribisha mwaka mpya kipindi kilichopita mara baada ya kutawazwa mara ya pili kukalia kiti cha Magogoni baada ya mauaji ya Arusha na North Mara na mengineyo, Kikwete baada ya kuulizwa na mmojawapo wa wanadiplomasia alijibu kwa kusema "Nawahakikishieni mauaji hayatatokea tena. Serikali yangu itafanya kila liwezekanalo kuzui yasitokee tena." Tafrija ya juzi mabalozi hawakumwuliza tena juu ya jambo hilo kwa kumlindia heshima na wala yeye kutogusia ila suala la gas Mtwara kwamba linahamasishwa na wanasiasa.​
Mtazamo wangu
Matukio ya kuuawa raia hutokea pale polisi wanapojiingiza kwa nguvu, na itokeapo mikusanyika ya raia peke yao bila polisi hakujatokea mauaji. Wanadipolomasia waliongopewa kwani mauaji bado yanaendelea.

Nina shaka kidogo kama hotuba za Rais zinaandaliwa na Rais mwenyewe au mtu mwingine huziandaa, maana Rais anachokiongea baadaye hufanyika mambo kinyume. Vinginevyo huwa hazipitii hutoba hizo kabla ya kuhutubia vinginevyo kasoro hizo angezigundu, kwani sasa kasoro hizo zinaonekana kumwelemea Rais mwenyewe badala ya watayarishaji wa hotuba zake.

Ahadi zawa mwiba kwa JK
AHADI za ujenzi wa barabara za lami zilizopata kutolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati akiomba kura mwaka 2010, zimezua balaa na kuibua mzozo bungeni. Hali hiyo ilitokana na swali la Mbunge wa Buhambwe, Felix Mkosamali (NCCR- Mageuzi), kuhoji utekelezaji wa ahadi ya Rais Kikwete ya kujenga barabara ya Nyakanazi-Kibondo-Kigoma katika kiwango cha lami. Pia alihoji ahadi ya Rais Kikwete ya ujenzi wa barabara ya Kibondo Mjini yenye urefu wa kilomita 1.5 na ujenzi wa barabara ya kimataifa ya kutoka Kibondo –Mabamba mpaka wa Burundi.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge alisema serikali bado iko mbioni kutekeleza ahadi hizo kutegemea na upatikanaji wa fedha. Alisema ahadi za rais zitatekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha kwani mwisho wa ahadi zake ni mwaka 2015.

Kutokana na majibu hayo, Mkosamali aliuliza swali la nyongeza na kutumia maneno yaliyotafsiriwa kama ni kashfa kwa Rais Kikwete. "Mhesmiwa Naibu Spika, sikubaliani na majibu mepesi ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Hivi unataka kusema ahadi za Rais Kikwete kujenga barabara ya Kibondo ilikuwa ya uongo? Ina maana alisema uongo ili kupata sifa ya kuchaguliwa kuwa rais?"

Swali hilo la nyongeza ambalo hata hivyo lilijibiwa vizuri na Naibu Waziri wa Ujenzi, lilimkera Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ambaye alisimama na kuomba mwongozo wa spika akipinga lugha iliyotumiwa na Mkosamali dhidi ya Rais Kikwete. "Mheshimiwa Naibu Spika, mbunge aliyeuliza swali la msingi kuhusu ahadi za rais, wakati akiuliza swali la nyongeza, alitumia maneno makali dhidi ya rais kinyume cha kanuni za Bunge. "Anasema rais alisema uongo au alisema uongo ili achaguliwe, sio maneno ya kistaarabu kutumika hasa kwa rais. "Mheshimiwa Naibu Spika, kanuni ya 61 (2) inasema mbunge hatatumia kumdhihaki rais au kulishawishi Bunge kuamua jambo fulani dhidi ya rais. "Nimesimama sio kutaka aombe radhi, bali kuwakumbusha vijana wawe makini na matumizi ya lugha, hasa lugha ya kuudhi. Mwongozo wangu ni kutaka uwakumbushe wabunge matumizi mazuri ya lugha, ni hilo tu," alisema na kuketi.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) ambaye ni mnadhimu kambi ya upinzani bungeni, kwanza alimtaka Waziri Lukuvi afute kauli yake kwamba kuna vijana kwa madai kuwa ndani ya Bunge hakuna vijana. "Pili, Waziri Lukuvi amemwelewa vibaya mbunge maana hajasema rais muongo. Alitaka kujua kama ahadi ya rais ni ya uongo. Na tatu mbunge hakutaka kushawishi Bunge kuchukua hatua dhidi ya rais," alisema Lissu.

David Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), naye alisimama na kuongeza kuwa waziri amepotosha umma na huo ni uchochezi.

Mkosamali naye alisimama na kusema kuwa hajamtukana rais bali alitaka kujua kama ahadi hiyo ni ya uongo au la.
Akitoa mwongozo wake, Naibu Spika aliwataka wabunge kutumia lugha ya kistaarabu.

Mbali ya swali la Mkosamali, wabunge wengine waliohoji ahadi ya ujenzi wa barabara katika maeneo yao ni Ester Bulaya (Viti Maalumu), Paul Rwanji (Manyoni Magharibi), wote CCM na Said Arfi wa Mpanda Kati (CHADEMA), ambao nao waliohoji ahadi za Rais Kikwete za ujenzi wa barabara katika maeneo yao.


 
Kama angekuwa kiongozi wa nchi kubwa Kama USA au nyingine zilizoendelea kwenye demokrasia angekuwa kesha temwa zamani kwa uongo huo hapo juu. Pia ungekuta anahudhuria mahakamani kujibu mashtaka
 
Uchambuzi miayo.Rais wa Tanzania aliyetokea kupendwa kuliko wote.Lami mpaka chooni mnataka nini tena.Shule za kata kila sehemu zimejaa.Hongera Kikwete unafaa uongezewe mitano(5) mingine
 
Kiwanda kimojawapo cha uongo ni cha yule jamaa ambaye alisema hajachukua pesa za ruzuku na michango ya wanachama, lakini baada ya kubanwa na binti machachari wa vijana akakiri kuwa alijikopesha na ameanza kurudisha.

Sijasikia au kushuhudia tamko la kwamba hajachukua pesa, ila imetokea karibuni kutoa ufafanuzi wa kilichotokea na kwamba pesa zilizochukliwa zilisharudishwa. uwongo hapa haujathibitishwa.
 
Hivi kuna kiwanda kikubwa cha uongo duniani kama kile cha Jakaya Kikwete Lies' Factory (JKFL)? Ziko wapi ahadi za maisha bora kwa wote? Wako wapi wauza unga, majambazi, wadokozi bandarini, Babu Seya na wengine wengi? Tanzania inaweza kusema kuwa ina viwanda vikubwa viwili vya nuklia vya uongo yaani JMK na CCM. Hapa bado hujagusa viwanda vidogo vidogo kama Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, Al Shabaab Kinana, Philip Mangula, Yusuf Makamba na vingine vingi tu.
 
Vipi Kigoma itakuwa lini Dubai ya Africa? Ahadi ya sultani kikwete 2010

Umetukumbusha hilo tena, maana CCM wako Kigoma sasa, Zitto awaagize wanakigoma hiyo Dubai imeshajengwa au lini ujenzi utaaanza maana miaka mitano si mbali ndo miwili na zaidi imeshakatika hivi. Ndio maana wa Mtwara wameshashtukia deal.
 
Hivi kuna kiwanda kikubwa cha uongo duniani kama kile cha Jakaya Kikwete Lies' Factory (JKFL)? Ziko wapi ahadi za maisha bora kwa wote? Wako wapi wauza unga, majambazi, wadokozi bandarini, Babu Seya na wengine wengi? Tanzania inaweza kusema kuwa ina viwanda vikubwa viwili vya nuklia vya uongo yaani JMK na CCM. Hapa bado hujagusa viwanda vidogo vidogo kama Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, Al Shabaab Kinana, Philip Mangula, Yusuf Makamba na vingine vingi tu.

Hapo sasa, imeandikwa katika maandiko matakatifu: "kimtokacho mtu ndicho kimchafuacho!" Jana tulikuwa tunaongea habari hizi wa watu mbalimbali, mmoja wetu aliongea kwa lugha ya kwao kutoka kusini nyanda za juu kabila nimelisahau alisema kama ifuatavyo: "Uvudesi vuhonga mpelela!" Niliulizia maana ya usemi huo, na nilijibiwa kimaelezo kwamba uwongo husababisha mauaji, kama mwanaukoo au mwanafamilia akiongopa anaweza kusababisha maafa katika familia au ukoo. Nikayakumbuka ya Mtwara na mengineyo, nikabaki nimeduwaa.
 
Kiwanda kingine cha uongo ni kile cha yule jamaa aliyechukua pesa za michango ya chama na kusema ameedna kununua helikopta Uingereza, lakini mpaka sasa wanachama wameambulia picha ya helikopta tu...

obama_n_kikwete_500x307.jpg


Ukiisoma picha hii unaweza kuona taswira ya Obama inavyoeleza na kutoa tafsiri nyingi. Anaelekea kushangaa au kutoamini kwa kinachoongelewa na mgeni wake.

Hawa jamaa mgeni mkubwa kama huyo anapomtembelea huwa wapelelezi, balozi wao na wengineo wameshampa stori nyingi tu, sasa unapokazana kujieleza na kumsadikisha mwenzako anapooanisha na aliyo nayo kuhusu wewe anabaki kushika shavu kukutazama na kukushangaa.
 
by the way, kipo kiwanda kingine cha uongo cha yule jamaa aliyetelekeza mke wake wa ndoa na watoto aliowazaa halafu akaenda kumuahidi mjane wa Mwangosi kuwa atamsaidia kusomesha watoto mbele ya kadamnasi, lakini sasa hivi kila akipigwa simu noti richabo...
Mkuu anzisha thread ya hili la mwangosi lakini kwa hapa jikite kwenye hoja husika
 
Yeah huyo jamaa alikuwa mkweli maana huwezi kutegemea kuvuna machungwa toka kwenye mpilipili. Ni bahati mbaya kuwa wadanganyika walimchagua Kikwete kutokana na "ujana' wake na "uchangamfu wake" Ni ajabu kuwa sifa hizo ziliyeyuka siku alipokanyaga ikulu. Kimsingi ni kwamba licha ya kuwa msanii Kikwete ni mnafiki wa wajabu na pretender aliyewaingia mkenge wadanganyika.
Hapo sasa, imeandikwa katika maandiko matakatifu: "kimtokacho mtu ndicho kimchafuacho!" Jana tulikuwa tunaongea habari hizi wa watu mbalimbali, mmoja wetu aliongea kwa lugha ya kwao kutoka kusini nyanda za juu kabila nimelisahau alisema kama ifuatavyo: "Uvudesi vuhonga mpelela!" Niliulizia maana ya usemi huo, na nilijibiwa kimaelezo kwamba uwongo husababisha mauaji, kama mwanaukoo au mwanafamilia akiongopa anaweza kusababisha maafa katika familia au ukoo. Nikayakumbuka ya Mtwara na mengineyo, nikabaki nimeduwaa.
 
Yeah huyo jamaa alikuwa mkweli maana huwezi kutegemea kuvuna machungwa toka kwenye mpilipili. Ni bahati mbaya kuwa wadanganyika walimchagua Kikwete kutokana na "ujana' wake na "uchangamfu wake" Ni ajabu kuwa sifa hizo ziliyeyuka siku alipokanyaga ikulu. Kimsingi ni kwamba licha ya kuwa msanii Kikwete ni mnafiki wa wajabu na pretender aliyewaingia mkenge wadanganyika.
Tena wengi Waliodanganyika ni wanawake kwa kumsifia ni handsome lakini hata wanaume wengine Kama Ritz na chama waliuvaa huu mkenge
 
jk ni mtambo wa uongo! Iko wapi meli mpya ziwa tanganyika? Meli mpya ziw vixtoria? Barabara za juu dsm? Reli za umeme dar - mwz? Reli ubungo - tegeta? Machinga complex kila manispaa? Wadau ongezeeni hapa. Muongo mkubwa.
 
ahahaha,mmenikumbusha ahadi za jamaa.ilifika wakati,akipita sehemu akakutana na dimbwi anaahidi vifaa vya uvuvi,akidhani alichokiona niziwa.
 
Kiwanda kimojawapo cha uongo ni cha yule jamaa ambaye alisema hajachukua pesa za ruzuku na michango ya wanachama, lakini baada ya kubanwa na binti machachari wa vijana akakiri kuwa alijikopesha na ameanza kurudisha.

una akili sana kama mwanaasha jk
 
Kiwanda kingine cha uongo ni kile cha yule jamaa aliyechukua pesa za michango ya chama na kusema ameedna kununua helikopta Uingereza, lakini mpaka sasa wanachama wameambulia picha ya helikopta tu...

ari zaidi,nguvu zaidi,kasi zaidi. Muulize jk kama amesema hii slogan baada ya uchaguzi
 

Nina shaka kidogo kama hotuba za Rais zinaandaliwa na Rais mwenyewe au mtu mwingine huziandaa, maana Rais anachokiongea baadaye hufanyika mambo kinyume. Vinginevyo huwa hazipitii hutoba hizo kabla ya kuhutubia vinginevyo kasoro hizo angezigundu, kwani sasa kasoro hizo zinaonekana kumwelemea Rais mwenyewe badala ya watayarishaji wa hotuba zake.

Nadhani zinaandaliwa na watu tofauti tofauti, na hawawasiliani kujua kuwa iliyopita mwenzake aliandika nini...
 
jk ni mtambo wa uongo! Iko wapi meli mpya ziwa tanganyika? Meli mpya ziw vixtoria? Barabara za juu dsm? Reli za umeme dar - mwz? Reli ubungo - tegeta? Machinga complex kila manispaa? Wadau ongezeeni hapa. Muongo mkubwa.
1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora 2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36.Kulinda haki za walemavu - Makete
37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43.Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
Back
Top Bottom