Utitiri wa watangaza nia CCM, ni kielelezo cha wigo mpana wa Demokrasia CCM, au Udhaifu wa Kikwete

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,641
Wanabodi,

Tukubali tukatae hadi sasa, watangaza nia ya urais kupitia CCM wameishavuka idadi ya watu 20, na inasemekana watakwenda hadi kufikia 30!, hivyo huu sasa ni utitiri wa watangaza nia ya urais kupitia CCM.

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliwahi kupaita "Ikulu ni Mahali Patakatifu, ukimuona mtu anapakimbilia ikulu, huyo ni wa kuogopwa kama ukoma!", na kuuliza hivi Ikulu kuna bishara gani?!, sasa hadi watu zaidi ya 30 watake kupakimbilia?!.

Swali linakuja, je, utitiri huu ni uthibitisho wa wigo mpana wa demokrasia ndani ya Chama cha Mapinduzi, wenye kuthibitisha kila mwanachama mwenye sifa ya uongozi, yuko huru kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama ukiwemo urais?!.

Au utitiri huu, ni kufuatia JK kusemekani ndio amekuwa rais dhaifu kuliko rais mwingine yoyote wa Tanzania, na mfano mmoja tuu wa vitendo vya kuudhihirisha udhaifu wa JK kwenye taasisi ya urais, ni kile kitendo watu kukutwa na kuthibitishwa pasi shaka kuwa wamekwiba fedha za umma kupitia EPA, badala ya kushitakiwa na kuiachia sheria ifuate mkondo wake, JK kwa kutumia mamlaka ambayo hayapo mahali popote kikatiba, aliamua kuwasamehe kwa nia njema ili nchi isitikisike!.

Maamuzi kama haya yamepelekea taasisi ya urais kuonekana ni kitu cha kawaida tuu, yaani ni very cheap, na kuelezwa kuwa kama JK ameweza kuwa rais kwa miaka yote hii kumi, then every Tom, Dick and Harry can be a president, na hii ndio imepelekea utitiri huu wa watia kupitia CCM!. Jee kuna ukweli wowote katika hili?!.

Hawa ni baadhi ya watia nia na watia nia watarajiwa kupitia CCM. Hapa nawataja kwa prominence, power na electability:


  1. Mhe. Edward Ngoyai Lowassa
  2. Mhe. Dr. Mohamed Gharib Bilal
  3. Mhe. Mizengo Kayanda Pinda
  4. Mhe. Dr Asharose Migiro
  5. Judg. Augustine Ramadhani
  6. Dr. Augustine Philip Mahiga
  7. Mhe. Bernard Kamilius Membe
  8. Mhe. Prof. Mark Mwandosya
  9. Mhe. Prof. Sospeter Muhongo
  10. Mhe. Samwel John Sitta
  11. Mhe. John Pombe Magufuli
  12. Mhe. January Yusufu Makamba
  13. Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba
  14. Mhe. Stephen Masatu Wassira
  15. Mhe. Lazaro Samuel Nyalandu
  16. Mhe. Mathias M Chikawe
  17. Mhe. Titus Mlengela Kamani
  18. Mhe. Dr. Hamisi Andrea Kigwangala
  19. Fredrick Tluway Sumaye
  20. Hassy Besen Kitine
  21. Mhe. Luhaga Joelson Mpina
  22. Mhe. Charles Makongoro Nyerere
  23. Balozi Amina Salum Ali
  24. Balozi Ali Karume
  25. Dr. Mwelecele Ntuli Malecela
  26. Dr Muzzamil Mussa Kalokola
  27. Monica Ngenzi Mbega
  28. Amos Robert Siyatemi
  29. Musa Godwin Mwapango
  30. Peter Isaiah Nyalali
  31. Boniface Thomas Ndengo
  32. Maliki Salum Marupu
  33. Leonce Nicholas Mulenda
  34. Lidephonce M Bilohe

Mimi binafsi yangu, nimewagawa watia nia hawa wa CCM kwenye makundi Saba...

Kundi la Kwanza ni ni wale nawaita ambao ni serious, hao ni wa kweli, wanautaka urais kiukweli kweli, wana mission na vision wanataka kuifanyia nini Tanzania, na wanautaka urais ili kuiondoa Tanzania hapa ilipo na kuipeleka kule ilikopaswa iwe. Kundi hili linaundwa na watu ambao ni presidential material. Kundi hili lina watu wachache na humu ndimo rais atatoka.

Kundi la Pili la watia nia, ni kundi la Wasindikizaji tuu, hawa nawaita 'pace makers' wameletwa ili kuonyesha urais una unashindani, ni wale ambao wanajijua kamwe kuchaguliwa hawawezi, lakini watagombea ili tuu kuwasindikiza baadhi ya wagombea wao makini just in case of anything can happen, mgombea wao asipopitishwa kwa sababu zozote zile, then watumike kama fall back positions.

Kundi la Tatu, ni ni la wagombea zuga au boshen, tuu ili kuzipooza hasira za watu, kundi hili mostly litahusisha wagombea kutoka Zanzibar, au wagombea wanawake. Kufuatia urais wa muungano ni suala la muungano na ulipaswa kupokezana kati ya Bara na Zanzibar, na pia kuna mpekezano wa Dini kati ya Mkristu na Muislamu.

Then, alipomaliza Mkapa ambaye ni Mkristu kutoka Bara, alipaswa afuatiwe na Muslamu kutoka Zanzibar, lakini kwa vile kitu kinachoitwa "Mtandao" kiliishabuniwa na kuwepo in place, kikaangalia aliyepaswa kumpokea Mkapa ni Muislamu kutoka Zanzibar, ili kubadili mchezo, Huyo Muislamu kutoka Zanzibar ilimbidi ashughulikiwe na kupotezewa kabla!, ili game liweze kurudi bara kwa excuse kuwa Zanzibar hakuna mtu!, kilichomkuta wengi mnakijua!,

Na "jamaa wa sehemu walihakikisha no post-mortem' ili kuthibitisha ni kazi ya Mungu!. Sasa kufuatia 1995 rais alitoka bara, 2005 rais akatoka tena bara, this time 2015 ki haki, kimuungano na kihalali ni zamu ya Zanzibar, lakini kwa vile mgombea wa CCM aliyemaliza ni Muislamu, na mgombea wa CCM wa 2015 tayari yupo, huu mchakato ni zuga tuu, then CCM wakituletea Muislamu mwingine, 'Kanisa' linaweza lisikubali.

Waliangalia uwezekano wa kumshawishi Jaji Ramadhani, ili kumtumia tuu kama zuga kuwazuga Wazanzibari, akaishtukia hii dili, akawagomea kata kata na hakuna Mkristo mwingine Presidential materia kutoka Zanzibar, hivyo CCM itahakikisha inawachagiza baadhi ya wagombea kutoka Zanzibar kugombea ili kuzugia tuu!.

Kundi la Nne ni la watia madekio na madodoki ya kusafishia watu!. Kufuatia baadhi ya wagombea kusemekena sio safi, wako wenye kashfa za rushwa, wako wenye tuhuma za ufisadi, wako wenye tuhuma za usaliti ambao walihama chama na kuingia upinzani kisha wakaingia bungeni waliposhindwa wakarejea CCM, wako wenye tuhuma za kukataliwa na Baba wa Taifa.

Hivyo kuna wagombea wamechagizwa kugombea bila ya wao kujijua, huku anafahamika wazi sio presidential material, na wanajijua, ila wameshawishiwa na 'wenyewe' wagombee kwa kuahidiwa watapewa urais kwenye silver plater, kumbe lengo ni kuwatumia tuu kama ma dekio ya kusafishia wengine njia, au madodoki ya kusafishia wengine!.

Kundi la Tano ni Watangaza Nia Chinja chinja, Vichinjio, au visu vyenye makali kuwili!. Hili ni kundi ambalo wenyewe hawautaki urais, ila ni heavy guards, hawa wameshawishiwa kutangaza nia ili CCM iwatumie kama chinjio la kuchijia wale heavy guards wasiotakiwa!.

Kwa vile kwenye wasaka urais kwa udi na uvumba yupo mtu wa level fulani, mfano wa calibre ya Waziri Mkuu Mtaafu, huwezi kumchinja hivi hivi tuu, sasa ili kuhalalisha kumchinjia baharini, CCM imemshawishi Waziri Mkuu mwingine mstaafu nae agombee, na Waziri Mkuu incumbent pia agombee ili kwenye kikao cha maamuzi, ijengwe hoja hatuwezi kupitisha mawaziri wakuu wastaafu watatu, tutapitisha mmoja, huyu ni yupi.

Hatuwezi kumkata incumbent tukampitisha wa zamani, hivyo wa kwanza kuchinjwa atakuwa ni wazamani hadi wa sasa hivyo kitendo cha Waziri Mkuu au Makamo wa Rais kuchinjwa, kutakufanya kujikuta unatulia na kujichwa kimya kimya huku umetulia!.

Kundi la Sita, la wagombea la watangaza nia waoteaji , Akiba Uzeeni, hawa wanatumia mtindo unaoitwa the JK style. Hili ni kundi la vijana ambao umri bado sana, hivyo wanatangaza nia kwa kuotea tuu ili kujenga profile nzuri kwa 2025, kama alivyofanya JK 1995 na kuja kuchukua 2005.

Kundi la Saba,
ni kundi la watia ni kujulisha "nipo nipo", au "Remember Me", hili ni kundi la watu ambao kwanza sio presidential material. wala urais hawautaki, bali wanagombea tuu ili kujenga profile za kujulikana, kukumbukwa, ili angalau angalau wataeuliwe uwaziri au post yoyote. Kwenye kundi hili humu ndimo wanagombea watu just for show off tuu kuwa na wao wanaweza!, yaani nao japo hawavumi lakini wamo!.

Kwa kumalizia, jee utitiri huu, ni healthy kwa ujenzi wa demokrasia ndani ya CCM au ndio aibu ya udhaifu wa JK kuufanya urais kuwa too cheap?!.

Wasalaam

Jumapili Njema.

Pasco
 
Mimi sioni ubaya kwani ndo demokrasia hiyo. Pamoja na ughali wake, demokrasia pia ni vurugu na ndo maana kuna mchujo. Mwisho wa siku atapatikana mmoja atakayebeba bendera ya chama chao kuelekea kwenye uchaguzi mkuu atakapombana na wagombea wa vyama vingine.

Hata huko Marekani, watangaza nia ya kugombea kupitia chama cha Republican wanaotaka uteuzi wa chama chao kwa uchaguzi mkuu ujao wa mwakani (2016) sasa hivi wapo 10 na idadi inaongezeka karibu kila siku.

Hivyo, kwangu hata hao watangaza nia wa CCM wakifika 100 sina tatizo kabisa. Kwanza walau inaonyesha ni jinsi gani 'bench' la CCM lilivyo na kina.
 
Mimi sioni ubaya kwani ndo demokrasia hiyo. Pamoja na ughali wake, demokrasia pia ni vurugu na ndo maana kuna mchujo. Mwisho wa siku atapatikana mmoja atakayebeba bendera ya chama chao kuelekea kwenye uchaguzi mkuu atakapombana na wagombea wa vyama vingine.

Hata huko Marekani watangaza nia ya kugombea kupitia chama cha Republican wanaotaka uteuzi wa chama chao kwa uchaguzi mkuu ujao wa mwakani (2016) sasa hivi wapo 10 na idadi inaongezeka karibu kila siku.

Hivyo, kwangu hata hao watangaza nia wakifika 100 sina tatizo kabisa. Kwanza walau inaonyesha ni jinsi gani 'bench' la CCM lilivyo na kina.

Mkuu, umemaliza kabisa.
 
Vyama vya upinzani hapa nchini nafasi ya urais haipaswi kuombwa na mtu mwingine yeyote isipokuwa mfalme mmoja tu wa kila siku.

Na ikitokea mtu anaisema sema tu nafasi ya urais jina atakaloitwa sio jingine bali ni msaliti. Wenyewe wanasema, "mgombea wetu amepita bila kupingwa". Kumbe ni upuuzi wa kuwabana wanachama kuomba ridhaa ya chama ili kugombea nafasi hiyo kwa usawa kwa wanachama wote walio na sifa.
 
kutafuta mgombea safi kutoka ccm ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano
 
Kujitokeza kwa wingi kwa wagombea wa urais (soma urahisi) ni kutokana na watanzania wenyewe! ie Ni warahisi sana kudang'anywa na kusombwa na mkumbo wa ''mchugue fulani''.

Nina uhakika wananchi tungekuwa makini katika kuchagua viongozi kwa kuangalia vigezo vya ''historia ya mgombea'' kama uchapa kazi na uadilifu, ni wengi wasingesumbuka kugombea.

Style ya Kikwete aliyoingia nayo madarakani (kupata urais bila kuwa na historia iliyotukuka ya utendaji na kutumia fedha) ndio hasa imefanya wengi waone kuwa usanii, ghilba na fedha vinaweza kumpa mtu urais.

Na hili limewapa jeuri kubwa watu kama kina Lowassa kiasi ambacho anathubutu kuwapa viti vya mbele watu walioondolewa serikalini kwa aibu kama kina mam Tibaijuka na Karamagi.

Hata mtu asiye na rekodi nzuru ya utendaji kama January Makamba au Mwingulu nao wanaona kuwa wanaweza ''kubahatisha'' urais. Na mwisho wengi wa wagombea CCM wamekariri ile dhana kwamba ''ukipitishwa na CCM basi wewe ni 100% rais wa Tanzania
 
Hamna ubaya wowote ndiyo ukuwaji wa demokrasia hata wakifika 100 siyo tatizo.

Maalimu, kisimngi mimi ningefurahi hata wangejitokeza watu laki moja. Ila inakatisha tamaa pale wanapojitokeza watu wenye kila aina ya sifa mbaya na wasio na rekodi ya utendaji kama kina Lowassa, Mwingulu na January Makamba
 
Nimependa sana post na 1 mpaka 4 ni nzuri sana. Utamu wa Demokrasia ndiyo huu, bora Kikwete amejaribu kipimo cha kiongozi ni jinsi anavyokusanya Kodi, tujue aliyemtangulia alikusanya kiasi gani kwa mwezi kulinganisha na huyu anayeondoka
 
Pasco

Kama ingekuwa ni suala la Democrasia, walikuwa wapi 2010? Mbona tuliona mmoja tu?

The other argument is valid

Kwa utendaji uliotukuka wa JK wote ndani ya chama tuliona ni vyema kumuacha aendelee na nafasi yake ya urais. Vipi kwa UKAWA, una lipi la kusema huko?
 
Mkuu Pasco;

Kwanza neno utitiri lina maana pana sana na linategemea mazingira.

Demokrasia kwa sasa inakuwa/inapanuka ndani ya CCM!. Cha muhimu ni kupata mgombea anayetokana na kanuni au taratibu walizojiwekea.

Kujitokeza kwa wagombea ''wengi'' kuna maana kuwa waliojitokeza wanadhani hakuna mgombea ambaye CCM imemtayarisha au mwenye uwezekano mkubwa wa kupewa nafasi hiyo.

Pamoja na kwamba demokrasia ya vyama vingi ndiyo ilikuwa inaingia, mwaka 1995 kulijitokeza wagombea 17 ndani ya CCM. Wengi walikuwa wanasukumwa na dhana ya kutokuwepo na mgombea mwenye uwezekano mkubwa wa kupewa nafasi.

Mwaka 2005 walipungua na kuwa 11 pamoja na demokrasia kukua kwa kiasi fulani, hii ilisababishwa na kuwepo kwa mgombea mwenye uwezekano mkubwa wa kupewa nafasi hiyo.

Mwaka huu wamekuwa wengi zaidi kwa sababu demokrasia imepanuka na hakuna mwenye uwezekano mkubwa wa kushinda ukilinganisha na wengine.

CCM kwa sasa haina mgombea ambaye unaweza kusema katika mantiki kama huyu ndiyo atateuliwa kulingana na vigezo vya maoni ya wananchi wengi.
 
Mkuu Pasco

Heshima kwako

Asante kwa bandiko hili fikirishi.

Kwamba utitiri huu wagombea ni kielelezo cha demokrasia pana ndani ya CCM? Sidhani. Maana kwa mujibu wa uchambuzi wako, ni dhahiri makundi ndani ya CCM yana malengo tofauti na yanasigana. Hii si salama kwa chama.

Kwamba utitiri huu unakisi udhaifu wa Raisi anayeondoka? Pia sidhani, isipokuwa hii inafanywa kimkakati kwa baraka za CCM yenyewe maana "commentator na pundits" wa siasa humu JF wamekuwa wakidai ati CCM hawana wanasiasa wenye mvuto wa kujaza wasikilizaji kama ilivyo UKAWA. Pengine CCM inajibu hoja hii kwa vitendo, kisiasa zaidi na kimkakati zaidi. Sio ajabu mwisho wa siku hizi timu zote zikafa. Ikabaki timu moja. Ambayo itakuwa na mwenyeji mzito karibu kila kona ya nchi (pengine).

Hata hivyo hofu yako ya utitiri huu sioni kama imezama kwenye hojaji zako mbili. Nachelea kusema hofu yako imo ndani ya sintofahamu ya itakuwaje mgombea mwenye washabiki wengi akitoswa na vikao vya awali vya chama? (Zingatia kundi la vichinjio). Je, haya makundi yataweza kuvumiliana ukizingatia investments za mtia nia mwenye wafuasi wengi? Je, demokrasia itatamalaki? Nadhani hapa ndio hojaji yako ilipojificha.

Wasalaam
 
Kwa utendaji uliotukuka wa JK wote ndani ya chama tuliona ni vyema kumuacha aendelee na nafasi yake ya urais.

Vipi kwa UKAWA una lipi la kusema huko?

Tuambie kilichomtoa Shibuda ccm 2010. Twende kwa Zitto ambapo ccm wengi mnapigia propaganda za kizee, alisema anautaka urais akiwa cdm, kwa mujibu wa propaganda zenu akanyimwa na kuitwa msaliti.

Leo mbona ni kiongozi mkuu huko aliko na uchaguzi huu hapa, kwanini haendelei kutangaza nia? Iweje aliweza akiwa cdm na uchaguzi ulikuwa bado, leo uchaguzi uko mdomoni yuko kimya!!? Tafakari chukua hatua
 
Tuambie kilichomtoa Shibuda ccm 2010. Twende kwa Zitto ambapo ccm wengi mnapigia propaganda za kizee, alisema anautaka urais akiwa cdm, kwa mujibu wa propaganda zenu akanyimwa na kuitwa msaliti.

Leo mbona ni kiongozi mkuu huko aliko na uchaguzi huu hapa, kwanini haendelei kutangaza nia? Iweje aliweza akiwa cdm na uchaguzi ulikuwa bado, leo uchaguzi uko mdomoni yuko kimya!!? Tafakari chukua hatua

Katiba inasemaje kuhusu suala la umri vile? Hemu nikumbushe kidogo....Zitto alilisema hilo la urais akiwa CHADEMA kwa sababu alijua katiba mpya ingeshusha umri wa urais

Ila kwa sasa hana njia mbadala zaidi ya kusubiri wakati wake ufike...maana hana sifa ya kuwania urais. Hilo nalo umeshindwa kujua? Kweli CHADEMA, Kila kitu mnataka kutafuniwa tu? Eti ndio mnataka serikali!!! Dah!
 
Tuambie kilichomtoa Shibuda ccm 2010. Twende kwa Zitto ambapo ccm wengi mnapigia propaganda za kizee, alisema anautaka urais akiwa cdm, kwa mujibu wa propaganda zenu akanyimwa na kuitwa msaliti.

Leo mbona ni kiongozi mkuu huko aliko na uchaguzi huu hapa, kwanini haendelei kutangaza nia? Iweje aliweza akiwa cdm na uchaguzi ulikuwa bado, leo uchaguzi uko mdomoni yuko kimya!!? Tafakari chukua hatua

Mkuu, naona wanajaribu kabisa kutupeleka kwenye mkumbo lakini hawatapata wote. Ukiangalia hao wote waliojitokeza na sifa zao za utendaji utagundua pasi shaka kuwa watu wameshaona kuwa ''kila mtu'' hata kichaa anaweza kuwa rais.

Mimi ningefurahi kama wanaojitokeza ni watu wenye rekodi nzuri za utendaji. Jamani hata Mwingulu nae awe rais? Hata Januari Makamba nae awe rais? Du ni kama matusi kabisa!
 
Back
Top Bottom