Kikwete sasa aja na ANGUKA ZAIDI kwenye mbio za 2010! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete sasa aja na ANGUKA ZAIDI kwenye mbio za 2010!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Jun 24, 2010.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Watanzania wanalia, kina Mkapa wako wapi?

  Baada ya kushindwa kutekeleza ahadi yake ya mwaka 2005 ya kuleta "Maisha Bora kwa kila Mtanzania" kupitia kauli mbiu yake ya Ari mpya, NGUvu mpya na KAsi mpya (ANGUKA), sasa CCM inakuja na Ari zaidi, Nguvu zaidi na Kasi zaidi (ANGUKA ZAIDI) kwenye uchaguzi wa 2010.

  Laiti kama Rais Jakaya Kikwete angekuwa ni muungwana basi angeitendea haki Tanzania kwa kung'atuka madarakani baada ya kipindi chake cha kwanza kwa kushindwa kutekeleza ahadi yake kuu ya kuboresha maisha ya Watanzania. Kikwete angetoa fursa kwa kiongozi mwingine ajaribu kutekeleza ilani ya CCM baada ya yeye kushindwa. Badala yake, kachukua tena fomu za kugombea Urais kwa mbwembwe bila haya na anaelekea kuwa mgombea pekee. Viongozi wa CCM wamebaki kunong'oneka chini kwa chini kuhusu jinsi JK alivyoivuruga nchi na kukidhoofisha chama kwa kuachia genge la mafisadi wa RICHMONDULI likiteke chama. Hivi ni kweli hakuna hata mwanasiasa mmoja mwenye ujasiri ndani ya CCM wa kuchukua fomu kum-challenge Kikwete kwa kushindwa kutekeleza ilani ya chama na kukidhoofisha chama?

  Wote tumeshuhudia jinsi ukali wa maisha ulivyozidi kukithiri tangu JK aingie madarakani na idadi ya Watanzania wanaoishi kwenye umasikini imeongezeka. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za serikali yenyewe.

  Serikali hii hii ya JK imedhihirisha kuwa wala haijui umasikini halisi wa wananchi wake baada ya majuzi tu kuweka viingilio vya kati ya shilingi elfu 30 na laki mbili kwenye mechi ya Taifa Stars na Brazil na kudhani kuwa eti Watanzania wanaweza kumudu gharama hizo. Matokeo yake ni kuwa nusu ya uwanja ulikuwa mtupu huku wananchi wengi wasio na kipato wakibaki kushangaa tu.

  Sipendi kuamnini kuwa ndani ya CCM hakuna kiongozi mwenye ushupavu wa kusimama na kuchukua fomu kugombea Urais 2010 ili aiepushe Tanzania na zigo hili la Kikwete kwa miaka mitano zaidi.

  Uku wapi Waziri Mkuu mstaafu Frederick Tluway Sumaye? Simama tukuone Katibu Mkuu wa zamani wa OAU Dk. Salim Ahmed Salim. Amka usingizini Prof. Mark Mwandosya.

  Dk. Harison Mwakyembe je? Onyesha ushupavu wako Spika Samuel Sitta.

  Na mwisho kabisa, ewe BENJAMIN WILLIAM MKAPA tuokoe Watanzania wenzako tunalia. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki dunia mwaka 1999 huku nchi ikiwa mikononi mwako. Yeye ndiye aliyekuamini wewe na kukukabidhi uongozi wa nchi.

  Ni kweli MKAPA umetukabidhi Watanzania kwa Kikwete? Ni kweli unaachia nchi iendelee kuteketea kwenye dimbwi la umasikini na hopelessness kwa miaka 5 zaidi?

  Ewe Mkapa, unalalaje usiku huku ukijua kuwa nchi imerudi miaka 10 nyuma kimaendeleo chini ya uongozi legevu wa JK ambao wewe ndiyo umeurithisha kutawala nchi hii?

  Zinduka MKAPA, nchi inateketea!
   
 2. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ..... kwa kuzingatia mada....NANI MWENYE MORAL AUTHORITY YA KUKEMEA MADUDU NA KUSIMAMA KIDETE AGAINST USANII NA PAPO HAPO KWA INTEREST YA WADANGANYIKA???

  Mwalimu RIP!
  Dr Slaa tegemeo letu so far.
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  RIP mzee wetu Nyerere.
  Bora huyaoni haya!!!
   
 4. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2010
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyo Mkapa unayemtaja....mbona yeye ndiye aliyefungua milango ya wizi na kuiuza.....
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Liko mikononi mwenu, muhimu ni kuwapiga chini tu hawa jamaa. Najua itatuchukua muda kubadilika but all the same one day yes!
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,924
  Trophy Points: 280
  Duh!Ukiona Mkapa analiliwa basi tumekwisha!
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ari, NGUvu, KAsi (zaidi) watu kwa kuunganisha hamjambo.
   
 8. K

  Kashishi JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2010
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 1,101
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Watanzania wasitegemee kwamba ati Mkapa ataibukua kuungana nao kuutomeza "Ombwe la Uongozi" katika utawala wa awamu ya nne. Kumbukeni kuwa yeye mwenyewe ni " beneficiary" wa misamaa ya makosa yake mengi aliyokwisha yafanya katika utawala wake. Ni majuzi tu issues za Kiwira na nyinginezo zimemalizwa ki-utu uzima, hata pasipo hata Wabunge kupewa fursa ya kujadili. Na hata yeye mwenyewe Mkapa ameanza kutembea kifua mbele kwa sasa na kuibukia katika vikao vya CC kule Dodoma siku hizi. Hivyo naamini hatathubutu kufanya uamuzi wa ku-risk kama huo hata kama anaona mambo yanakwenda kombo. Amefungwa mdomo na "fadhila" za Wana-Mtandao. Na Wana -Mtandao wana hakika kuwa hawezi Kufurukuta wala "Kuthubutu".
   
 9. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180

  Mhhh yaani ni sawa na unataka kutoroka jela halafu unaomba msaada wa bwana jela
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Level ya ufisadi uliyofikia sasa hivi ni kwamba hakuna cha kusema ni bora kibovu hiki kuliko kibovu kile. Mkapa na JK ni dugu moja. Aidha tatizo hapa si individual leaders, but ni the ruling party itself. It has outlived its usefulness, hence its credibility. It's now a gang of Mafiosi brought in direct from Sicily!!!
   
 11. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  walau wakati wa mkapa bei ya sukari, chumvi. bia, soda na bidhaa yinginezo ilikuwa inashikika , leo kaja JK ni majungu tupu hali ya uchumi imekuwa ngumu, vyakula vimepanda bei na sasa kwa kutumia ujanja anataka kujionesha kuwa anakubarika kwa kuwaghiribu ccm wenzake wasigombee na amepeleka dhambi hiyo hadi kwenye upinzani don be shocked this year kikwete akapita bila kupingwa, siku zote mtendaji dhaifu anatumia gharama ubwa kuendelea kuwa madarakani, ole wako jk malipo ni hapa hapa duniani, ole wako kwa hila, ghiriba, ufisadi, uzandaki, choyo, masihara, wivu, umbea, uhuni nk.:mmph:
   
 12. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Tatizo kwa Tz si JK tu, ni mfumo unaotawala Tz, CCM ni mlezi wa mfumo huo yaani mfumo wa uovu, CCM na wanaCCM wanafaidika na mfumo huo. Hivyo tusihamasishe watu kujitokeza kugombea kupitia CCM. Ni wakati wakuhamasisha watu kuangusha CCM. Kinyume na hapo ni vigumu kuleta mabadiliko katika nchi hii.

  Chukua hatua kuibua mjadala wa kuangusha CCM
   
 13. MANI

  MANI Platinum Member

  #13
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Sir R uko sahihi kabisa hi ndio njia pekee.
   
 14. MANI

  MANI Platinum Member

  #14
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Sir R uko sahihi kabisa hi ndio njia pekee.
   
 15. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkapa anazinduka nini wakati yeye ndiye aliyepigilia msumari wa mwisho ili Salim na Mwandosya wasiwe na nafasi ya kuchaguliwa kugombea urais? Mkapa yupi hiyo tunayedhani alikabidhiwa nchi na Mwalimu ambaye hata kabla Mwalimu hajafariki alishamtolea nje Mwalimu kwa kumwambia "I am the President" wakati Mwalimu akimsihi asiibinafsishe NMB? Mkapa yupi huyo, ni yule aliyekufuru na kusema kwamba "Mwalimu akifufuka atashangaa kuona jinsi ubepari unavyojenga nchi?" Laiti Mkapa huyu asingelilewa madaraka na kujiona yuko juu ya mbingu nchi hii ingesalimika~
   
Loading...