Sumaye amuunga mkono Kikwete rushwa CCM

Tina

JF-Expert Member
Jul 9, 2007
572
579
Sumaye anazungumza na waandishi now Court Yard, anasema anamuunga mkono JK kuhusu rushwa CCM ila anataka azungumzie na rushwa serikalini.

Press Conference Nov 2013
MKUTANO WA MHE. FREDERICK SUMAYE NA WAANDISHI WA HABARI
PROTEA COURTYARD HOTEL, TAREHE 5 NOVEMBA, 2013.

Ndugu waandishi wa habari,
Wageni wengine,
Mabibi na mabwana.

Shukurani

Kwanza niwashukuru sana nyote kwa kuitikia wito wangu wa kuja ili nizungumze nanyi machache niliyonayo. Ninawaahidi mkutano wangu utakuwa tu mfupi ili muweze kuendelea na mambo mengine ya kuwapasha habari wananchi.

Pili napenda niwashukuru na kuwapongeza sana waandishi wa habari wote na watangazaji wa habari kwa kuwahabarisha wananchi juu ya matukio na habari mbali mbali katika nchi yetu. Nataka nikiri kuwa viwango vyenu vya utoaji habari vimekuwa bora kuliko huko nyuma japo vinapishana kutoka gazeti moja na nyingine au chombo kimoja na kingine. Sasa hivi wananchi wengi wanapata habari za nini kinachoendelea sehemu nyingine ya nchi na kwa sehemu kubwa wameelimika sana. Na hii ni kazi yenu wana habari. Kazi hii nzuri mnayoifanya najua ina changamoto zake zingine zikiwa za hatari hata kuhatarisha maisha lakini wengi wenu mmesonga mbele kishujaa. Napenda niwapongeze sana kwa ushujaa na ujasiri huo na wala msikate tamaa.

Ujumbe

Leo nimewaita kuzungumzia maeneo kama matatu hivi. Jambo la kwanza ni kumshukuru na kumwunga mkono Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kwa hotuba yake ya hivi karibuni aliyoitoa mjini Dodoma wakati akifunga semina ya watendaji wa Chama na wenyeviti. Eneo la pili ninalotaka kuzungumzia linahusu hujumu zinazofanywa kwa shughuli za kijamii kwa malengo ya kisiasa likiwa na vipengere viwili vya mialiko na usambazaji wa taarifa kwa umma, hasa kwa sisi wanasiasa na hasa tunaoonekana labda tutagombea Urais 2015 na eneo la tatu linahusu propaganda chafu zinazotengenezwa kuelekea uchaguzi wa 2015.

Kumwunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa

Hivi karibuni wakati akifunga semina ya wenyeviti wa wilaya na watendaji wa ngazi ya mikoa na wilaya, mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete alikemea rushwa kwa nguvu sana na kutahadharisha chama chetu (CCM) kuwa kama rushwa iliyoko haitadhibitiwa hata chama chetu kinaweza kushindwa katika uchaguzi katika muda si mrefu ujao. Mimi binafsi nataka nimpongeze mwenyekiti wa CCM Taifa kwa dhati kwa kukemea ovu hili lililokithiri katika nchi yetu katika ngazi na Nyanja zote. Mwenyekiti amelikabidhi jukumu la utekelezaji kwa makamu wake Ndugu Philip Mangula ambaye tunajua ni jemadari imara katika vita dhidi ya rushwa. Imani yetu ni kuwa ndugu yetu Mangula jambo hili hutalionea haya na hutaangalia sura ya mhusika wakati wa kuchukua hatua maana ni ukweli usiofichika wengi wa watoa rushwa ni watu wazito kwa kila namna. Aidha tunaamini secretariat na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa watampa Ndugu Mangula ushirikiano usioyumba.

Kama tunavyojua rushwa haiko ndani CCM peke yake. Rushwa ipo katika vyama vingine vya siasa, katika taasisi zinazojitegemea, serikalini na maeneo mengineyo mengi nchini. Kama mwenyekiti ndugu Kikwete alivyomwagiza makamu wake kushughulikia rushwa katika CCM, namwomba mwenyekiti asikomee hapo bali amwagize na Rais wa Jamhuri Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete naye pia ashughulikie rushwa katika serikali na vyombo vyote vilivyoko chini ya serikali yake. Vita hivi tutashinda askari wote tukishikamana na kuunganisha nguvu pamoja. Ni vita vikali, vikubwa na vya hatari lakini tukiwa pamoja tutashinda kwa uhakika. Wanachama wa CCM na wananchi wote tumepata matumaini mapya kwamba kauli ya mwenyekiti wa chama tawala haitapotelea hewani bali itatekezwa na italeta mabadiliko makubwa katika vita dhidi ya rushwa nchini. Ndugu mwenyekiti wangu mimi nakupongeza sana sana kwa kukemea rushwa na ninakuunga mkono katika vita hii na ninaamini unajua kuwa mimi ni askari wako mojawapo wa mstari wa mbele.
Hujuma zinazofanywa katika shughuli za jamii kwa maslahi ya kisiasa

Mialiko

Taasisi, vikundi vya jamii au madhehebu ya dini hualika viongozi mbali mbali kuwasaidia katika shughuli zao ambazo zinaweza kuwa na lengo la kuwahamasisha, kutoa ujumbe, kuzindua jengo au mradi ama kuchangia fedha. Mara nyingi wale wahusika ndiyo humtafuta mgeni rasmi kutegemeana na hitaji lao. Lakini pia ipo njia nyingine ambayo nayo hutumika hasa nyakati za kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo anayetaka kuwa mgeni rasmi hutumia mbinu mbali mbali kutengeneza mwaliko ambao ataalikwa yeye.

Kama nilivyosema awali mgeni rasmi hutafutwa kutegemeana na hitaji la wahusika. Kwa mfano kama wahusika wanataka fedha nyingi watamtafuta mgeni rasmi ambaye ama atatoa fedha nyingi au ana uwezo wa kuleta fedha nyingi, kama hitaji ni kuzungumzia maadili katika taifa au katika jamii atatafutwa mgeni rasmi ambayo ana kifua cha kukemea maovu yanayowasibu jamii, nakadhalika. Kila kiongozi au mgeni rasmi ana eneo ambalo analiweza kuliko mwingine kwa sababu mbali mbali, nyingine ni karama tu na nyingine kutokana na matendo au tabia yake.

Kwa mfano unaweza kuwa huna uwezo wa kuchangia fedha nyingi kwa sabau tu hukujaliwa kuwa nazo na hukujaliwa karama ya kupiga magoti kwa walio nazo, lakini mwingine akawa kinyume chake kabisa. Akawa anazo au pengine kajaliwa karama ya kuomba kwa walio nazo. Hao walio nazo watampa kwa sabau ya urafiki wao lakini mara nyingi kutakuwa na masharti yatakayoambatana nayo. Mfano mwingine ni pale labda taasisi inahitaji kukemea maovu kama rushwa au madawa ya kulevya. Hapo lazima taasisi hiyo itamtafuta mtu ambaye ana dhamira safi (moral authority) katika eneo hilo. Hawawezi kumwalika mtu ambaye yeye ni kinara wa kutoa au kupokea rushwa au kinara wa madawa ya kulevya. Hana ‘moral authority' ya kufanya hivyo. Dhamira yake itamshitaki.

Pamoja na sababu na namna mialiko inavyopatikana, mialiko hii ina umuhimu sana hasa kama mwaliko ulitokana na hitaji la wahusika. Kama ni wa kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi, ni dhahiri baada ya harambee hiyo jengo linalokusudiwa kujengwa litajengwa na likikamilika litawahudumia wahusika, iwe kanisa, msikiti, darasa, zahanati nk. Kama lengo ni kukemea maovu basi jamii itakuwa imepata faida ya kupata elimu zaidi juu ya jambo hilo na njia mbali mbali za kukabiliana nalo.

Hakuna ubishi kuwa mialiko hii ina faida kubwa kwa wahusika na hata kwa jamii nzima kwa ujumla. Kwa hiyo ni wazi kuwa mwaliko uliopangwa unapovurugika kwa sababu yoyote ile ambayo isingestahili kuwepo tunawacheleweshea wahusika maendeleo yao au tunawacheleweshea manufaa ambayo wangeyapata kutokana na shughuli hiyo inayohusiana na mwaliko wenyewe. Ziko sababu ambazo zinaweza kuzuia shughuli za mwaliko kihalali kama sababu za kiusalama, za kiafya nk. Lakini mbinu zinazotengenezwa na makundi yasiyo rasmi tena kwa kificho na kurubuni watu kwa rushwa kwa lengo la kuruga mialiko ni mbinu za woga, za haramu na zinazochelewesha maendeleo ya watu.

Kwa mfano kama agenda ya mwaliko ni kukemea rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya na maovu mengine, wala rushwa na watoa rushwa, mafisadi na wauza madawa ya kulevya watafanya mbinu zao chafu ikiwa ni pamoja na kutoa rushwa ili kuvuruga mipango mizuri yenye manufaa kwa wananchi. Wataivuruga kwa sababu wana wasiwasi kuwa mjumuiko huo utaifanya jamii ielewe kwa undani na kwa umakini mbinu zao chafu na mambo yao machafu. Hawa ni watu ambao wamejijengea himaya zao za kuwadhulumu watu, kuwalaghai watu, kuwanyonya watu, kuwarubuni watu, kuwanunua watu na hata kuwaumiza ikibidi ili mradi malengo yao machafu yatimie. Shughuli yoyote hata kama ni ya halali kiasi gani ili mradi inagusa maslahi yao itahujumiwa kwa sababu wanaona unagusa maslahi na himaya zao.

Napenda nitoe mifano miwili ya haya ninayoyazungumza ambayo yamenipata mimi. Mara ya kwanza ni tarehe 27 Oktoba wakati nilikuwa na mwaliko wa kikundi cha joggers cha Dar es Salaam ambacho kiliponialika kupokea jogging yao hapo viwanja vya Mnazi moja. Dakika za mwisho nikapewa taarifa kuwa shughuli imeshindikana kwa sababu imeingiliwa na kikundi chenye kulinda maslahi yake au ya mtu wao. Shughuli hiyo baadaye naambiwa ilifanyika na alipatikana "mgeni rasmi mwingine." Nina hakika vijana wale na umma kwa ujumla walikosa ujumbe mahsusi ambao nilikuwa niutoe kwa vijana wetu na jamii nzima. Ujumbe huo nitawagawia leo ili watakaopenda kuutoa wautoe kwa vijana na kwa jamii.

Mara ya pili ni mwaliko wa kuzindua SACCOS ya Nshamba Muleba, Kagera. Nilipata mwaliko wa kuzindua SACCOS kule Nshamba Muleba tarehe 28 Oktoba mwezi huu. Mwaliko huo sikuuomba bali viongozi wa chama walinipendekeza kwa sababu zao wenyewe. Wakati najiandaa kwenda Kagera nikaambiwa shughuli zimeingiliwa na watu fulani kwa kutoa rushwa kwa baadhi ya viongozi wa SACCOS hiyo ili shughuli hiyo isifanyike na kupewa maelekezo kuwa haiwezekani Sumaye afike Kagera kabla ya mtu wao. Hata matangazo yaliyolipiwa fedha kutangaza mkutano huo ilibidi yasitishwe na fedha kurudishwa. Watu wa SACCOS ya Nshamba wamecheleweshewa shughuli zao za kiuchumi kwa sababu ya uhuni wa watu wasio na uchungu na wananchi. Poleni watu wa Muleba lakini ninawaahidi nitafika tu huko muda si mrefu.

Nataka niwataarifu hao wanaohangaika na mialiko yangu wajue kuwa miako ninayo mingi mpaka mingine nakosa muda wa kuifanya, na siitwi kwa sababu ya fedha maana wanajua sina fedha za aina hiyo maana sijaiibia nchi na watu wake. Jinsi wanavyojitahidi kunizima kwa rushwa ili ati nisizungumzie juu ya rushwa, ufisadi na madawa ya kulevya ndivyo wanavyonipa nguvu na mifano hai ya jinsi rushwa na ufisadi vilivyo mbaya katika taifa. Fisadi huliibia taifa fedha nyingi kiasi cha wananchi kutaabika sana halafu huja kutoa kijisehemu ya fedha alizofisadi kwa njia ya rushwa kukandamiza maendeleo ya watu. Fisadi akikuhonga na wewe ukafurahi ni sawa na mtu aliyekupa ugonjwa mbaya usiopona halafu wakati wa maumivu makali anakuletea panadol ya kupunguza maumivu na wewe unaimba kwamba huyo ni mwungwana anayekupenda. Unasahau kuwa kama siyo yeye kufanya hayo aliyoyafanya usingekuwa katika hali hiyo. Hawa ni watu hatari sana katika jamii tusiwakubalie watununue kuvuruga mipango yetu tuliyojipangia.

Utoaji taarifa katika vyombo vya habari

Pamoja na majukumu mengine, vyombo vya habari vina jukumu kubwa la habarisha jamii. Vyombo hivi ndivyo vinavyo wahabarisha umma nini kinatokea katika sehemu nyingine ya nchi na nani anafanya nini. Kiwe kinamilikiwa na serikali au mtu au kampuni binafsi havipishani katika umuhimu wa kuhabarisha umma. Aidha vyombo hivi vinatakiwa vitoe taarifa au habari kama ilivyotolewa na mtoa habari na siyo habari iliyochakachuliwa kwa madhumuni fulani. Ninyi mtakubaliana nami kuwa kuna wakati baadhi ya waandishi wa habari na wasimamizi wa vyombo walikuwa waandika au kutoa taarifa kwa maelekezo ya watu fulani fulani. Maelekezo hayo yanaweza kuwa na lengo la kumchafua mtu anayelengwa au basi taarifa za mtu huyo zisitoke katika vyombo hivyo. Katika hali hiyo mwandishi utakuwa unadhalilisha taaluma yako na wakati mwingine unajihatarisha kupelekwa mahakamani kama uliyoyaandika hameathiri heshima ya mtu.

Mimi nimekumbana na haya yote na wakati mwingine imebidi kupeleka mastaka mahakamani ili kutafuta haki, na ninyi ni mashahidi kesi zote nilishinda kwa sababu nilikuwa nasingiziwa kwa utaratibu huo huo wa waandishi kuelekezwa. Unalotakiwa kulijua ni kuwa wakati kesi, huyo aliyekurubuni hutamwona na wakati huo fedha alizokupa ndiyo zimeshayeyuka. Nimekumbana pia na kuzuiwa taarifa zangu kutotolewa kwa maelekezo ya watu fulani.

Hivi umejiuliza kwanini mtu akwambie usiandike au usitangaze habari za mtu fulani? Anaogopa nini habari ambazo siyo zake? Na anakwambie wewe yeye kama nani wakati hata hiyo taaluma haijui? Mtu wa namna hiyo jambo la kwanza ni mwovu hivyo anaogopa uovu wake kufichuliwa na pia hajiamini na ana mapungufu mengi ndiyo maana anaona atakalosema mwingine kitang'aa zaidi na yeye hana uwezo wa kujilinganisha naye. Jambo la pili anapokupa rushwa ili ufanye kile anachotaka yeye maana yake amekudharau sana kuwa huna akili ya kutumikia taaluma yako hadi akuelekeze yeye kwa fedha zake. Msikubali kudharaliwa kiasi hicho.

Ndugu wanahabari wote nataka niseme kwa dhati ya moyo wangu kuwa hali hii sasa imebadilika sana sana. Wengi wenu sasa mmekataa kuisaliti taaluma yenu na mnatoa taarifa za watu ikiwa ni pamoja na mimi. Kuna wakati hali ilikuwa ngumu lakini mmeiboresha na ninyi ni mashahidi kama mimi nilivyo shahidi kuwa jamii sasa hivi inavitegemea vyombo vya habari kuliko wakati mwingine wowote. Mimi nawapongeza sana na ninawaomba msipoteze mwelekeo huo kwa sababu ya vihela vya kuhongwa. Vyombo vya habari vina wajibu wa kuwaanika wala rushwa na watoa rushwa, mafisadi, wauza unga, majangiri nakadhalika. Iweje wewe upokee rushwa ili uandike uwongo? Afanyae hivyo unaidhalilisha taaluma yako na wewe mwenyewe. Najua mnafanya kazi katika mazingira magumu sana na wakati mwingine inahitaji ujasiri mkubwa kukataa hiyo rushwa lakini piga moyo konde na useme ‘taaluma yangu na utu wangu kwanza.'

Propaganda kuelekea uchaguzi wa 2015

Muda wa kuelekea wakati wa uchaguzi hasa uchaguzi mkuu huwa kuna mbinu mbali mbali zinazotumika na wahusika wanaotafuta nafasi mbali mbali kufanikisha malengo yao. Ziko mbinu nzuri za kistaarabu na ziko mbinu chafu kama za kupakazana matope (character assassinations). Mbinu ya kwanza ya kistaarabu ni pale mhusika anapowashawishi wanaomsikiliza kuwa yeye ni mtu safi atakayemudu nafasi hiyo bila kumwathiri mtu mwingine ambaye ama naye pia anadhaniwa anawania hiyo nafasi au hata kama hawanii nafasi hiyo.

Mtu wa aina ya kwanza tungeweza kusema huyo anajisafishia njia yake kwa kufyeka miiba na kuondoa magogo njiani ili wakati ukiwadia mbio zake zisikwazwe na vigingi vyovyote. Sifa ya mtu kama huyo ni kuwa miiba na magogo anayoyatoa katika njia yake huyatupa mahali salama au kuyachoma ili yasije yakamkwaza mtu mwingine au mshindani wake ambaye naye anachonga barabara yake.

Aina ya pili ya mbinu hizo ambazo ni chafu ni pale mhusika anatengeneza mbinu ama za kuwamaliza wengine wanaodhaniwa kuwa washindani wake baadaye au kuwawekea vikwazo katika mbinu zao za kujisafishia njia. Mtu wa namna hiyo ama anawachafua wenzake kwa kuwapakaza matope ya uwongo mtupu au anawajengea mazingira yeye kupendwa kwa kutumia migongo ya wengine. Tukirudi kwenye mfano wetu wa kufyeka barabara basi huyo ama anachimba mitaro kwenye barabara wanazofyeka wenzake au anatupia miiba na magogo yanayotoka kwake na kuyatupia kwa wenzake ili mradi wenzake wakwame wakati ukiwadia.
Mimi mtu akihangaika kujisafishia njia bila kuathiri wengine au kuathiri mambo fulani ya msingi huwa hainisumbui sana, lakini ikiwa inaathiri mtu mwingine itabidi tuiambie jamii ukweli na hivi ndivyo nitakavyofanya leo na hata wakati mwingine jambo kama hilo likijitokeza.

Gazeti la Mwananchi la tarehe 16 Septemba 2013, liliandika kuwa siri ya mradi wa kuvuta maji Ziwa Victoria yafichuliwa, na katika maelezo yake mtoa habari alisema ni mawaziri wawili tu waliouunga mkono mradi huo na wengine wote waliupinga. Kwa maelezo yake waliouunga mkono ni Mheshimiwa Jakaya Kikwete aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na Mheshimiwa Mohamed Seif Khatib waziri katika ofisi ya makamu wa rais. Najua mhusika ameutumia sana mradi huu kisiasa na sisi wengine tumenyamaza japo ukweli tunaujua sana. Lakini ili mradi ametukanyaga vidole wengine na kutupia miiba na magogo kwenye njia yetu wengine, amenilazimisha niseme ukweli kuhusu mradi huu kwa sababu mimi ndiye niliyekuwa waziri mkuu na mradi umetelezwa chini ya uangalizi wangu kama kiongozi na msimamizi mkuu wa utekelezaji wa shughuli zote za serikali.

Pamoja na kwamba hilo lililolielezwa ni uwongo mkavu, mhusika kama waziri mwandamizi wakati huo na sasa kama anayewinda nafasi kubwa katika nchi hakutegemewa kutoa siri za baraza la mawaziri; labda amediriki kufanya hivyo kwa sababu anajua anayoyasema siyo ya kweli vinginevyo ni kosa la jinai na akishitakiwa anafungwa jela.

Pili mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ni mradi wa serikali na siyo wa mtu. Ni kweli kwa mkataba uliokuwepo wa miaka ya 1952 au 1953 nchi za huku juu mito ya Nlie inapoanzia na inakopitia hazikutakiwa zitumie maji ya Mto Nile ili nchi za Misri na Sudan zisiathirike. Nchi hizi Tanzania ikiwamo ziliona makubaliano hayo siyo sahihi na tulianza kudai mabadiliko ya sheria hiyo.

Jambo hili lilishughulikiwa mwanzo na Waziri Dr. Pius Ng'wandu na baadaye likakamilishwa na ‘Agreed Minutes' zilizoweka msingi wa makubaliano baina ya nchi hizo kusainiwa na nchi kumi na kwa Tanzania aliyesaini ambaye kwa bahati nzuri alikuwa ndiye mwenyekiti wa baraza hilo la nchi kumi alikuwa Mheshimiwa Musa Nkhangaa aliyekuwa Waziri wa maji wakati huo. Katika kusukuma jambo hili mbele hata mimi niliwahi kukutana Addis Ababa na marehemu Meles Zenawi, aliyekuwa waziri mkuu wa Ethiopia. Baada ya hapo Waholanzi walitusaidia kuandika mradi huo baada ya waziri Nkhangaa kutembelea chanzo cha kuchukulia maji cha Smith Sound na kuona mradi unawezekana. Hapo ndipo Rais Mkapa aliposhauriwa kuwa mradi huo unawezekana na ndipo Rais Mkapa alipotoa ahadi Shinyanga kuwa Shinyanga itapata maji kutoka Ziwa Victoria kwa gharama yoyote na ndivyo ilivyokuwa.

Matatizo ya maji Shinyanga yalivyotutesa isingewezekana baraza la mawaziri kuupinga mradi huo na mimi nisingeupinga kabisa maana wakati mji wa Shinyanga ukikosa maji nilikuwa silali usingizi.

Jambo ambalo ni kweli ni kuwa mradi huo uliiva wakati Mhe. Lowassa akiwa waziri wa maji na ameusimamia hadi ukakamilika kama ambavyo angeusimamia waziri mwingine wa maji. Nataka ieleweke wazi kuwa hakuna waziri mwenye uwezo wa kutekeleza mradi kama baraza la mawaziri likiukataa. Fedha atapata wapi za kuendesha mradi huo? Pili mradi wowote ni wa serikali na unatengenezwa na wizara husika. Katika wizara wanaofanya kazi sana ni wataalam chini ya katibu mkuu. Pamoja na kuwa sisi wanasiasa tunapenda kubeba sifa zote mambo yakienda vizuri na kuwatupia lawama wataalam yakienda vibaya, ni vema tujue tunafanya kama timu moja na mwenye serikali ni moja tu yaani Rais.

mwisho

Huwa sipendi kuingilia mambo ya watu wengine lakini yanaponigusa sitanyamaza. Lakini pia ni wajibu wangu kueleza ukweli pana ambapo ukweli unapotoshwa kwa makusudi. Nataka niwaase hasa wanasiasa wenzangu kuwa tuwatendee watanzania haki kwa kuwapa ukweli mtupu na tusiwape uwongo uliopakwa utamu wa ukweli juu kumbe ndani ni machungu ya uwongo.

Aidha sote tuseme rushwa ni adui wa haki. Unapompa mtu rushwa ujue kuna anayedhulumika na kuumia na hiyo rushwa yako. Unapofanya ufisadi kwa mradi wa serikali unaliumiza taifa katika siku zijazo kwa kuipiga kiharusi cha uchumi na huduma kwa jamii. Na unapouza dawa za kulevya wewe ni mwuuaji wa taifa kwa sababu unaangamiza vijana wa taifa hili ambao ndiyo nguvu kazi yetu tunayoitegemea.

Basi tujiulize kama unafanya haya au baadhi ya haya wewe unafaa kutuongoza?

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hivi alipokuwa waziri mkuu alifanya nini cha maana kuhusu rushwa?

Hivi ni fashion mtu ukistaafu unakuwa "outspoken" wakati ukiwa madarakani unajifanya huyaoni??!!
 
Press Conference Nov 2013
MKUTANO WA MHE. FREDERICK SUMAYE NA WAANDISHI WA HABARI
PROTEA COURTYARD HOTEL, TAREHE 5 NOVEMBA, 2013.

Ndugu waandishi wa habari,
Wageni wengine,
Mabibi na mabwana.

Shukurani
Kwanza niwashukuru sana nyote kwa kuitikia wito wangu wa kuja ili nizungumze nanyi machache niliyonayo. Ninawaahidi mkutano wangu utakuwa tu mfupi ili muweze kuendelea na mambo mengine ya kuwapasha habari wananchi.

Pili napenda niwashukuru na kuwapongeza sana waandishi wa habari wote na watangazaji wa habari kwa kuwahabarisha wananchi juu ya matukio na habari mbali mbali katika nchi yetu. Nataka nikiri kuwa viwango vyenu vya utoaji habari vimekuwa bora kuliko huko nyuma japo vinapishana kutoka gazeti moja na nyingine au chombo kimoja na kingine. Sasa hivi wananchi wengi wanapata habari za nini kinachoendelea sehemu nyingine ya nchi na kwa sehemu kubwa wameelimika sana. Na hii ni kazi yenu wana habari. Kazi hii nzuri mnayoifanya najua ina changamoto zake zingine zikiwa za hatari hata kuhatarisha maisha lakini wengi wenu mmesonga mbele kishujaa. Napenda niwapongeze sana kwa ushujaa na ujasiri huo na wala msikate tamaa.

Ujumbe
Leo nimewaita kuzungumzia maeneo kama matatu hivi. Jambo la kwanza ni kumshukuru na kumwunga mkono Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kwa hotuba yake ya hivi karibuni aliyoitoa mjini Dodoma wakati akifunga semina ya watendaji wa Chama na wenyeviti. Eneo la pili ninalotaka kuzungumzia linahusu hujumu zinazofanywa kwa shughuli za kijamii kwa malengo ya kisiasa likiwa na vipengere viwili vya mialiko na usambazaji wa taarifa kwa umma, hasa kwa sisi wanasiasa na hasa tunaoonekana labda tutagombea Urais 2015 na eneo la tatu linahusu propaganda chafu zinazotengenezwa kuelekea uchaguzi wa 2015.

Kumwunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa
Hivi karibuni wakati akifunga semina ya wenyeviti wa wilaya na watendaji wa ngazi ya mikoa na wilaya, mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete alikemea rushwa kwa nguvu sana na kutahadharisha chama chetu (CCM) kuwa kama rushwa iliyoko haitadhibitiwa hata chama chetu kinaweza kushindwa katika uchaguzi katika muda si mrefu ujao. Mimi binafsi nataka nimpongeze mwenyekiti wa CCM Taifa kwa dhati kwa kukemea ovu hili lililokithiri katika nchi yetu katika ngazi na Nyanja zote. Mwenyekiti amelikabidhi jukumu la utekelezaji kwa makamu wake Ndugu Philip Mangula ambaye tunajua ni jemadari imara katika vita dhidi ya rushwa. Imani yetu ni kuwa ndugu yetu Mangula jambo hili hutalionea haya na hutaangalia sura ya mhusika wakati wa kuchukua hatua maana ni ukweli usiofichika wengi wa watoa rushwa ni watu wazito kwa kila namna. Aidha tunaamini secretariat na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa watampa Ndugu Mangula ushirikiano usioyumba.

Kama tunavyojua rushwa haiko ndani CCM peke yake. Rushwa ipo katika vyama vingine vya siasa, katika taasisi zinazojitegemea, serikalini na maeneo mengineyo mengi nchini. Kama mwenyekiti ndugu Kikwete alivyomwagiza makamu wake kushughulikia rushwa katika CCM, namwomba mwenyekiti asikomee hapo bali amwagize na Rais wa Jamhuri Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete naye pia ashughulikie rushwa katika serikali na vyombo vyote vilivyoko chini ya serikali yake. Vita hivi tutashinda askari wote tukishikamana na kuunganisha nguvu pamoja. Ni vita vikali, vikubwa na vya hatari lakini tukiwa pamoja tutashinda kwa uhakika. Wanachama wa CCM na wananchi wote tumepata matumaini mapya kwamba kauli ya mwenyekiti wa chama tawala haitapotelea hewani bali itatekezwa na italeta mabadiliko makubwa katika vita dhidi ya rushwa nchini. Ndugu mwenyekiti wangu mimi nakupongeza sana sana kwa kukemea rushwa na ninakuunga mkono katika vita hii na ninaamini unajua kuwa mimi ni askari wako mojawapo wa mstari wa mbele.
Hujuma zinazofanywa katika shughuli za jamii kwa maslahi ya kisiasa

Mialiko
Taasisi, vikundi vya jamii au madhehebu ya dini hualika viongozi mbali mbali kuwasaidia katika shughuli zao ambazo zinaweza kuwa na lengo la kuwahamasisha, kutoa ujumbe, kuzindua jengo au mradi ama kuchangia fedha. Mara nyingi wale wahusika ndiyo humtafuta mgeni rasmi kutegemeana na hitaji lao. Lakini pia ipo njia nyingine ambayo nayo hutumika hasa nyakati za kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo anayetaka kuwa mgeni rasmi hutumia mbinu mbali mbali kutengeneza mwaliko ambao ataalikwa yeye.
Kama nilivyosema awali mgeni rasmi hutafutwa kutegemeana na hitaji la wahusika. Kwa mfano kama wahusika wanataka fedha nyingi watamtafuta mgeni rasmi ambaye ama atatoa fedha nyingi au ana uwezo wa kuleta fedha nyingi, kama hitaji ni kuzungumzia maadili katika taifa au katika jamii atatafutwa mgeni rasmi ambayo ana kifua cha kukemea maovu yanayowasibu jamii, nakadhalika. Kila kiongozi au mgeni rasmi ana eneo ambalo analiweza kuliko mwingine kwa sababu mbali mbali, nyingine ni karama tu na nyingine kutokana na matendo au tabia yake.
Kwa mfano unaweza kuwa huna uwezo wa kuchangia fedha nyingi kwa sabau tu hukujaliwa kuwa nazo na hukujaliwa karama ya kupiga magoti kwa walio nazo, lakini mwingine akawa kinyume chake kabisa. Akawa anazo au pengine kajaliwa karama ya kuomba kwa walio nazo. Hao walio nazo watampa kwa sabau ya urafiki wao lakini mara nyingi kutakuwa na masharti yatakayoambatana nayo. Mfano mwingine ni pale labda taasisi inahitaji kukemea maovu kama rushwa au madawa ya kulevya. Hapo lazima taasisi hiyo itamtafuta mtu ambaye ana dhamira safi (moral authority) katika eneo hilo. Hawawezi kumwalika mtu ambaye yeye ni kinara wa kutoa au kupokea rushwa au kinara wa madawa ya kulevya. Hana ‘moral authority' ya kufanya hivyo. Dhamira yake itamshitaki.
Pamoja na sababu na namna mialiko inavyopatikana, mialiko hii ina umuhimu sana hasa kama mwaliko ulitokana na hitaji la wahusika. Kama ni wa kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi, ni dhahiri baada ya harambee hiyo jengo linalokusudiwa kujengwa litajengwa na likikamilika litawahudumia wahusika, iwe kanisa, msikiti, darasa, zahanati nk. Kama lengo ni kukemea maovu basi jamii itakuwa imepata faida ya kupata elimu zaidi juu ya jambo hilo na njia mbali mbali za kukabiliana nalo. Hakuna ubishi kuwa mialiko hii ina faida kubwa kwa wahusika na hata kwa jamii nzima kwa ujumla. Kwa hiyo ni wazi kuwa mwaliko uliopangwa unapovurugika kwa sababu yoyote ile ambayo isingestahili kuwepo tunawacheleweshea wahusika maendeleo yao au tunawacheleweshea manufaa ambayo wangeyapata kutokana na shughuli hiyo inayohusiana na mwaliko wenyewe. Ziko sababu ambazo zinaweza kuzuia shughuli za mwaliko kihalali kama sababu za kiusalama, za kiafya nk. Lakini mbinu zinazotengenezwa na makundi yasiyo rasmi tena kwa kificho na kurubuni watu kwa rushwa kwa lengo la kuruga mialiko ni mbinu za woga, za haramu na zinazochelewesha maendeleo ya watu.
Kwa mfano kama agenda ya mwaliko ni kukemea rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya na maovu mengine, wala rushwa na watoa rushwa, mafisadi na wauza madawa ya kulevya watafanya mbinu zao chafu ikiwa ni pamoja na kutoa rushwa ili kuvuruga mipango mizuri yenye manufaa kwa wananchi. Wataivuruga kwa sababu wana wasiwasi kuwa mjumuiko huo utaifanya jamii ielewe kwa undani na kwa umakini mbinu zao chafu na mambo yao machafu. Hawa ni watu ambao wamejijengea himaya zao za kuwadhulumu watu, kuwalaghai watu, kuwanyonya watu, kuwarubuni watu, kuwanunua watu na hata kuwaumiza ikibidi ili mradi malengo yao machafu yatimie. Shughuli yoyote hata kama ni ya halali kiasi gani ili mradi inagusa maslahi yao itahujumiwa kwa sababu wanaona unagusa maslahi na himaya zao.
Napenda nitoe mifano miwili ya haya ninayoyazungumza ambayo yamenipata mimi. Mara ya kwanza ni tarehe 27 Oktoba wakati nilikuwa na mwaliko wa kikundi cha joggers cha Dar es Salaam ambacho kiliponialika kupokea jogging yao hapo viwanja vya Mnazi moja. Dakika za mwisho nikapewa taarifa kuwa shughuli imeshindikana kwa sababu imeingiliwa na kikundi chenye kulinda maslahi yake au ya mtu wao. Shughuli hiyo baadaye naambiwa ilifanyika na alipatikana "mgeni rasmi mwingine." Nina hakika vijana wale na umma kwa ujumla walikosa ujumbe mahsusi ambao nilikuwa niutoe kwa vijana wetu na jamii nzima. Ujumbe huo nitawagawia leo ili watakaopenda kuutoa wautoe kwa vijana na kwa jamii.
Mara ya pili ni mwaliko wa kuzindua SACCOS ya Nshamba Muleba, Kagera. Nilipata mwaliko wa kuzindua SACCOS kule Nshamba Muleba tarehe 28 Oktoba mwezi huu. Mwaliko huo sikuuomba bali viongozi wa chama walinipendekeza kwa sababu zao wenyewe. Wakati najiandaa kwenda Kagera nikaambiwa shughuli zimeingiliwa na watu fulani kwa kutoa rushwa kwa baadhi ya viongozi wa SACCOS hiyo ili shughuli hiyo isifanyike na kupewa maelekezo kuwa haiwezekani Sumaye afike Kagera kabla ya mtu wao. Hata matangazo yaliyolipiwa fedha kutangaza mkutano huo ilibidi yasitishwe na fedha kurudishwa. Watu wa SACCOS ya Nshamba wamecheleweshewa shughuli zao za kiuchumi kwa sababu ya uhuni wa watu wasio na uchungu na wananchi. Poleni watu wa Muleba lakini ninawaahidi nitafika tu huko muda si mrefu.
Nataka niwataarifu hao wanaohangaika na mialiko yangu wajue kuwa miako ninayo mingi mpaka mingine nakosa muda wa kuifanya, na siitwi kwa sababu ya fedha maana wanajua sina fedha za aina hiyo maana sijaiibia nchi na watu wake. Jinsi wanavyojitahidi kunizima kwa rushwa ili ati nisizungumzie juu ya rushwa, ufisadi na madawa ya kulevya ndivyo wanavyonipa nguvu na mifano hai ya jinsi rushwa na ufisadi vilivyo mbaya katika taifa. Fisadi huliibia taifa fedha nyingi kiasi cha wananchi kutaabika sana halafu huja kutoa kijisehemu ya fedha alizofisadi kwa njia ya rushwa kukandamiza maendeleo ya watu. Fisadi akikuhonga na wewe ukafurahi ni sawa na mtu aliyekupa ugonjwa mbaya usiopona halafu wakati wa maumivu makali anakuletea panadol ya kupunguza maumivu na wewe unaimba kwamba huyo ni mwungwana anayekupenda. Unasahau kuwa kama siyo yeye kufanya hayo aliyoyafanya usingekuwa katika hali hiyo. Hawa ni watu hatari sana katika jamii tusiwakubalie watununue kuvuruga mipango yetu tuliyojipangia.
Utoaji taarifa katika vyombo vya habari
Pamoja na majukumu mengine, vyombo vya habari vina jukumu kubwa la habarisha jamii. Vyombo hivi ndivyo vinavyo wahabarisha umma nini kinatokea katika sehemu nyingine ya nchi na nani anafanya nini. Kiwe kinamilikiwa na serikali au mtu au kampuni binafsi havipishani katika umuhimu wa kuhabarisha umma. Aidha vyombo hivi vinatakiwa vitoe taarifa au habari kama ilivyotolewa na mtoa habari na siyo habari iliyochakachuliwa kwa madhumuni fulani. Ninyi mtakubaliana nami kuwa kuna wakati baadhi ya waandishi wa habari na wasimamizi wa vyombo walikuwa waandika au kutoa taarifa kwa maelekezo ya watu fulani fulani. Maelekezo hayo yanaweza kuwa na lengo la kumchafua mtu anayelengwa au basi taarifa za mtu huyo zisitoke katika vyombo hivyo. Katika hali hiyo mwandishi utakuwa unadhalilisha taaluma yako na wakati mwingine unajihatarisha kupelekwa mahakamani kama uliyoyaandika hameathiri heshima ya mtu.
Mimi nimekumbana na haya yote na wakati mwingine imebidi kupeleka mastaka mahakamani ili kutafuta haki, na ninyi ni mashahidi kesi zote nilishinda kwa sababu nilikuwa nasingiziwa kwa utaratibu huo huo wa waandishi kuelekezwa. Unalotakiwa kulijua ni kuwa wakati kesi, huyo aliyekurubuni hutamwona na wakati huo fedha alizokupa ndiyo zimeshayeyuka. Nimekumbana pia na kuzuiwa taarifa zangu kutotolewa kwa maelekezo ya watu fulani.
Hivi umejiuliza kwanini mtu akwambie usiandike au usitangaze habari za mtu fulani? Anaogopa nini habari ambazo siyo zake? Na anakwambie wewe yeye kama nani wakati hata hiyo taaluma haijui? Mtu wa namna hiyo jambo la kwanza ni mwovu hivyo anaogopa uovu wake kufichuliwa na pia hajiamini na ana mapungufu mengi ndiyo maana anaona atakalosema mwingine kitang'aa zaidi na yeye hana uwezo wa kujilinganisha naye. Jambo la pili anapokupa rushwa ili ufanye kile anachotaka yeye maana yake amekudharau sana kuwa huna akili ya kutumikia taaluma yako hadi akuelekeze yeye kwa fedha zake. Msikubali kudharaliwa kiasi hicho.
Ndugu wanahabari wote nataka niseme kwa dhati ya moyo wangu kuwa hali hii sasa imebadilika sana sana. Wengi wenu sasa mmekataa kuisaliti taaluma yenu na mnatoa taarifa za watu ikiwa ni pamoja na mimi. Kuna wakati hali ilikuwa ngumu lakini mmeiboresha na ninyi ni mashahidi kama mimi nilivyo shahidi kuwa jamii sasa hivi inavitegemea vyombo vya habari kuliko wakati mwingine wowote. Mimi nawapongeza sana na ninawaomba msipoteze mwelekeo huo kwa sababu ya vihela vya kuhongwa. Vyombo vya habari vina wajibu wa kuwaanika wala rushwa na watoa rushwa, mafisadi, wauza unga, majangiri nakadhalika. Iweje wewe upokee rushwa ili uandike uwongo? Afanyae hivyo unaidhalilisha taaluma yako na wewe mwenyewe. Najua mnafanya kazi katika mazingira magumu sana na wakati mwingine inahitaji ujasiri mkubwa kukataa hiyo rushwa lakini piga moyo konde na useme ‘taaluma yangu na utu wangu kwanza.'
Propaganda kuelekea uchaguzi wa 2015
Muda wa kuelekea wakati wa uchaguzi hasa uchaguzi mkuu huwa kuna mbinu mbali mbali zinazotumika na wahusika wanaotafuta nafasi mbali mbali kufanikisha malengo yao. Ziko mbinu nzuri za kistaarabu na ziko mbinu chafu kama za kupakazana matope (character assassinations). Mbinu ya kwanza ya kistaarabu ni pale mhusika anapowashawishi wanaomsikiliza kuwa yeye ni mtu safi atakayemudu nafasi hiyo bila kumwathiri mtu mwingine ambaye ama naye pia anadhaniwa anawania hiyo nafasi au hata kama hawanii nafasi hiyo.
Mtu wa aina ya kwanza tungeweza kusema huyo anajisafishia njia yake kwa kufyeka miiba na kuondoa magogo njiani ili wakati ukiwadia mbio zake zisikwazwe na vigingi vyovyote. Sifa ya mtu kama huyo ni kuwa miiba na magogo anayoyatoa katika njia yake huyatupa mahali salama au kuyachoma ili yasije yakamkwaza mtu mwingine au mshindani wake ambaye naye anachonga barabara yake.
Aina ya pili ya mbinu hizo ambazo ni chafu ni pale mhusika anatengeneza mbinu ama za kuwamaliza wengine wanaodhaniwa kuwa washindani wake baadaye au kuwawekea vikwazo katika mbinu zao za kujisafishia njia. Mtu wa namna hiyo ama anawachafua wenzake kwa kuwapakaza matope ya uwongo mtupu au anawajengea mazingira yeye kupendwa kwa kutumia migongo ya wengine. Tukirudi kwenye mfano wetu wa kufyeka barabara basi huyo ama anachimba mitaro kwenye barabara wanazofyeka wenzake au anatupia miiba na magogo yanayotoka kwake na kuyatupia kwa wenzake ili mradi wenzake wakwame wakati ukiwadia.
Mimi mtu akihangaika kujisafishia njia bila kuathiri wengine au kuathiri mambo fulani ya msingi huwa hainisumbui sana, lakini ikiwa inaathiri mtu mwingine itabidi tuiambie jamii ukweli na hivi ndivyo nitakavyofanya leo na hata wakati mwingine jambo kama hilo likijitokeza.
Gazeti la Mwananchi la tarehe 16 Septemba 2013, liliandika kuwa siri ya mradi wa kuvuta maji Ziwa Victoria yafichuliwa, na katika maelezo yake mtoa habari alisema ni mawaziri wawili tu waliouunga mkono mradi huo na wengine wote waliupinga. Kwa maelezo yake waliouunga mkono ni Mheshimiwa Jakaya Kikwete aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na Mheshimiwa Mohamed Seif Khatib waziri katika ofisi ya makamu wa rais. Najua mhusika ameutumia sana mradi huu kisiasa na sisi wengine tumenyamaza japo ukweli tunaujua sana. Lakini ili mradi ametukanyaga vidole wengine na kutupia miiba na magogo kwenye njia yetu wengine, amenilazimisha niseme ukweli kuhusu mradi huu kwa sababu mimi ndiye niliyekuwa waziri mkuu na mradi umetelezwa chini ya uangalizi wangu kama kiongozi na msimamizi mkuu wa utekelezaji wa shughuli zote za serikali.
Pamoja na kwamba hilo lililolielezwa ni uwongo mkavu, mhusika kama waziri mwandamizi wakati huo na sasa kama anayewinda nafasi kubwa katika nchi hakutegemewa kutoa siri za baraza la mawaziri; labda amediriki kufanya hivyo kwa sababu anajua anayoyasema siyo ya kweli vinginevyo ni kosa la jinai na akishitakiwa anafungwa jela.
Pili mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ni mradi wa serikali na siyo wa mtu. Ni kweli kwa mkataba uliokuwepo wa miaka ya 1952 au 1953 nchi za huku juu mito ya Nlie inapoanzia na inakopitia hazikutakiwa zitumie maji ya Mto Nile ili nchi za Misri na Sudan zisiathirike. Nchi hizi Tanzania ikiwamo ziliona makubaliano hayo siyo sahihi na tulianza kudai mabadiliko ya sheria hiyo. Jambo hili lilishughulikiwa mwanzo na Waziri Dr. Pius Ng'wandu na baadaye likakamilishwa na ‘Agreed Minutes' zilizoweka msingi wa makubaliano baina ya nchi hizo kusainiwa na nchi kumi na kwa Tanzania aliyesaini ambaye kwa bahati nzuri alikuwa ndiye mwenyekiti wa baraza hilo la nchi kumi alikuwa Mheshimiwa Musa Nkhangaa aliyekuwa Waziri wa maji wakati huo. Katika kusukuma jambo hili mbele hata mimi niliwahi kukutana Addis Ababa na marehemu Meles Zenawi, aliyekuwa waziri mkuu wa Ethiopia. Baada ya hapo Waholanzi walitusaidia kuandika mradi huo baada ya waziri Nkhangaa kutembelea chanzo cha kuchukulia maji cha Smith Sound na kuona mradi unawezekana. Hapo ndipo Rais Mkapa aliposhauriwa kuwa mradi huo unawezekana na ndipo Rais Mkapa alipotoa ahadi Shinyanga kuwa Shinyanga itapata maji kutoka Ziwa Victoria kwa gharama yoyote na ndivyo ilivyokuwa.
Matatizo ya maji Shinyanga yalivyotutesa isingewezekana baraza la mawaziri kuupinga mradi huo na mimi nisingeupinga kabisa maana wakati mji wa Shinyanga ukikosa maji nilikuwa silali usingizi.
Jambo ambalo ni kweli ni kuwa mradi huo uliiva wakati Mhe. Lowassa akiwa waziri wa maji na ameusimamia hadi ukakamilika kama ambavyo angeusimamia waziri mwingine wa maji. Nataka ieleweke wazi kuwa hakuna waziri mwenye uwezo wa kutekeleza mradi kama baraza la mawaziri likiukataa. Fedha atapata wapi za kuendesha mradi huo? Pili mradi wowote ni wa serikali na unatengenezwa na wizara husika. Katika wizara wanaofanya kazi sana ni wataalam chini ya katibu mkuu. Pamoja na kuwa sisi wanasiasa tunapenda kubeba sifa zote mambo yakienda vizuri na kuwatupia lawama wataalam yakienda vibaya, ni vema tujue tunafanya kama timu moja na mwenye serikali ni moja tu yaani Rais.
mwisho
Huwa sipendi kuingilia mambo ya watu wengine lakini yanaponigusa sitanyamaza. Lakini pia ni wajibu wangu kueleza ukweli pana ambapo ukweli unapotoshwa kwa makusudi. Nataka niwaase hasa wanasiasa wenzangu kuwa tuwatendee watanzania haki kwa kuwapa ukweli mtupu na tusiwape uwongo uliopakwa utamu wa ukweli juu kumbe ndani ni machungu ya uwongo.
Aidha sote tuseme rushwa ni adui wa haki. Unapompa mtu rushwa ujue kuna anayedhulumika na kuumia na hiyo rushwa yako. Unapofanya ufisadi kwa mradi wa serikali unaliumiza taifa katika siku zijazo kwa kuipiga kiharusi cha uchumi na huduma kwa jamii. Na unapouza dawa za kulevya wewe ni mwuuaji wa taifa kwa sababu unaangamiza vijana wa taifa hili ambao ndiyo nguvu kazi yetu tunayoitegemea.
Basi tujiulize kama unafanya haya au baadhi ya haya wewe unafaa kutuongoza?
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Jambo ambalo ni kweli ni kuwa mradi huo uliiva wakati Mhe. Lowassa akiwa waziri wa maji na ameusimamia hadi ukakamilika kama ambavyo angeusimamia waziri mwingine wa maji. Nataka ieleweke wazi kuwa hakuna waziri mwenye uwezo wa kutekeleza mradi kama baraza la mawaziri likiukataa. Fedha atapata wapi za kuendesha mradi huo? Pili mradi wowote ni wa serikali na unatengenezwa na wizara husika. Katika wizara wanaofanya kazi sana ni wataalam chini ya katibu mkuu. Pamoja na kuwa sisi wanasiasa tunapenda kubeba sifa zote mambo yakienda vizuri na kuwatupia lawama wataalam yakienda vibaya, ni vema tujue tunafanya kama timu moja na mwenye serikali ni moja tu yaani Rais.
 
Press Conference Nov 2013
MKUTANO WA MHE. FREDERICK SUMAYE NA WAANDISHI WA HABARI
PROTEA COURTYARD HOTEL, TAREHE 5 NOVEMBA, 2013.

Ndugu waandishi wa habari,
Wageni wengine,
Mabibi na mabwana.

Shukurani
Kwanza niwashukuru sana nyote kwa kuitikia wito wangu wa kuja ili nizungumze nanyi machache niliyonayo. Ninawaahidi mkutano wangu utakuwa tu mfupi ili muweze kuendelea na mambo mengine ya kuwapasha habari wananchi.
Pili napenda niwashukuru na kuwapongeza sana waandishi wa habari wote na watangazaji wa habari kwa kuwahabarisha wananchi juu ya matukio na habari mbali mbali katika nchi yetu. Nataka nikiri kuwa viwango vyenu vya utoaji habari vimekuwa bora kuliko huko nyuma japo vinapishana kutoka gazeti moja na nyingine au chombo kimoja na kingine. Sasa hivi wananchi wengi wanapata habari za nini kinachoendelea sehemu nyingine ya nchi na kwa sehemu kubwa wameelimika sana. Na hii ni kazi yenu wana habari. Kazi hii nzuri mnayoifanya najua ina changamoto zake zingine zikiwa za hatari hata kuhatarisha maisha lakini wengi wenu mmesonga mbele kishujaa. Napenda niwapongeze sana kwa ushujaa na ujasiri huo na wala msikate tamaa.
Ujumbe
Leo nimewaita kuzungumzia maeneo kama matatu hivi. Jambo la kwanza ni kumshukuru na kumwunga mkono Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kwa hotuba yake ya hivi karibuni aliyoitoa mjini Dodoma wakati akifunga semina ya watendaji wa Chama na wenyeviti. Eneo la pili ninalotaka kuzungumzia linahusu hujumu zinazofanywa kwa shughuli za kijamii kwa malengo ya kisiasa likiwa na vipengere viwili vya mialiko na usambazaji wa taarifa kwa umma, hasa kwa sisi wanasiasa na hasa tunaoonekana labda tutagombea Urais 2015 na eneo la tatu linahusu propaganda chafu zinazotengenezwa kuelekea uchaguzi wa 2015.
Kumwunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa
Hivi karibuni wakati akifunga semina ya wenyeviti wa wilaya na watendaji wa ngazi ya mikoa na wilaya, mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete alikemea rushwa kwa nguvu sana na kutahadharisha chama chetu (CCM) kuwa kama rushwa iliyoko haitadhibitiwa hata chama chetu kinaweza kushindwa katika uchaguzi katika muda si mrefu ujao. Mimi binafsi nataka nimpongeze mwenyekiti wa CCM Taifa kwa dhati kwa kukemea ovu hili lililokithiri katika nchi yetu katika ngazi na Nyanja zote. Mwenyekiti amelikabidhi jukumu la utekelezaji kwa makamu wake Ndugu Philip Mangula ambaye tunajua ni jemadari imara katika vita dhidi ya rushwa. Imani yetu ni kuwa ndugu yetu Mangula jambo hili hutalionea haya na hutaangalia sura ya mhusika wakati wa kuchukua hatua maana ni ukweli usiofichika wengi wa watoa rushwa ni watu wazito kwa kila namna. Aidha tunaamini secretariat na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa watampa Ndugu Mangula ushirikiano usioyumba.
Kama tunavyojua rushwa haiko ndani CCM peke yake. Rushwa ipo katika vyama vingine vya siasa, katika taasisi zinazojitegemea, serikalini na maeneo mengineyo mengi nchini. Kama mwenyekiti ndugu Kikwete alivyomwagiza makamu wake kushughulikia rushwa katika CCM, namwomba mwenyekiti asikomee hapo bali amwagize na Rais wa Jamhuri Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete naye pia ashughulikie rushwa katika serikali na vyombo vyote vilivyoko chini ya serikali yake. Vita hivi tutashinda askari wote tukishikamana na kuunganisha nguvu pamoja. Ni vita vikali, vikubwa na vya hatari lakini tukiwa pamoja tutashinda kwa uhakika. Wanachama wa CCM na wananchi wote tumepata matumaini mapya kwamba kauli ya mwenyekiti wa chama tawala haitapotelea hewani bali itatekezwa na italeta mabadiliko makubwa katika vita dhidi ya rushwa nchini. Ndugu mwenyekiti wangu mimi nakupongeza sana sana kwa kukemea rushwa na ninakuunga mkono katika vita hii na ninaamini unajua kuwa mimi ni askari wako mojawapo wa mstari wa mbele.
Hujuma zinazofanywa katika shughuli za jamii kwa maslahi ya kisiasa
Mialiko
Taasisi, vikundi vya jamii au madhehebu ya dini hualika viongozi mbali mbali kuwasaidia katika shughuli zao ambazo zinaweza kuwa na lengo la kuwahamasisha, kutoa ujumbe, kuzindua jengo au mradi ama kuchangia fedha. Mara nyingi wale wahusika ndiyo humtafuta mgeni rasmi kutegemeana na hitaji lao. Lakini pia ipo njia nyingine ambayo nayo hutumika hasa nyakati za kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo anayetaka kuwa mgeni rasmi hutumia mbinu mbali mbali kutengeneza mwaliko ambao ataalikwa yeye.
Kama nilivyosema awali mgeni rasmi hutafutwa kutegemeana na hitaji la wahusika. Kwa mfano kama wahusika wanataka fedha nyingi watamtafuta mgeni rasmi ambaye ama atatoa fedha nyingi au ana uwezo wa kuleta fedha nyingi, kama hitaji ni kuzungumzia maadili katika taifa au katika jamii atatafutwa mgeni rasmi ambayo ana kifua cha kukemea maovu yanayowasibu jamii, nakadhalika. Kila kiongozi au mgeni rasmi ana eneo ambalo analiweza kuliko mwingine kwa sababu mbali mbali, nyingine ni karama tu na nyingine kutokana na matendo au tabia yake.
Kwa mfano unaweza kuwa huna uwezo wa kuchangia fedha nyingi kwa sabau tu hukujaliwa kuwa nazo na hukujaliwa karama ya kupiga magoti kwa walio nazo, lakini mwingine akawa kinyume chake kabisa. Akawa anazo au pengine kajaliwa karama ya kuomba kwa walio nazo. Hao walio nazo watampa kwa sabau ya urafiki wao lakini mara nyingi kutakuwa na masharti yatakayoambatana nayo. Mfano mwingine ni pale labda taasisi inahitaji kukemea maovu kama rushwa au madawa ya kulevya. Hapo lazima taasisi hiyo itamtafuta mtu ambaye ana dhamira safi (moral authority) katika eneo hilo. Hawawezi kumwalika mtu ambaye yeye ni kinara wa kutoa au kupokea rushwa au kinara wa madawa ya kulevya. Hana ‘moral authority’ ya kufanya hivyo. Dhamira yake itamshitaki.
Pamoja na sababu na namna mialiko inavyopatikana, mialiko hii ina umuhimu sana hasa kama mwaliko ulitokana na hitaji la wahusika. Kama ni wa kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi, ni dhahiri baada ya harambee hiyo jengo linalokusudiwa kujengwa litajengwa na likikamilika litawahudumia wahusika, iwe kanisa, msikiti, darasa, zahanati nk. Kama lengo ni kukemea maovu basi jamii itakuwa imepata faida ya kupata elimu zaidi juu ya jambo hilo na njia mbali mbali za kukabiliana nalo. Hakuna ubishi kuwa mialiko hii ina faida kubwa kwa wahusika na hata kwa jamii nzima kwa ujumla. Kwa hiyo ni wazi kuwa mwaliko uliopangwa unapovurugika kwa sababu yoyote ile ambayo isingestahili kuwepo tunawacheleweshea wahusika maendeleo yao au tunawacheleweshea manufaa ambayo wangeyapata kutokana na shughuli hiyo inayohusiana na mwaliko wenyewe. Ziko sababu ambazo zinaweza kuzuia shughuli za mwaliko kihalali kama sababu za kiusalama, za kiafya nk. Lakini mbinu zinazotengenezwa na makundi yasiyo rasmi tena kwa kificho na kurubuni watu kwa rushwa kwa lengo la kuruga mialiko ni mbinu za woga, za haramu na zinazochelewesha maendeleo ya watu.
Kwa mfano kama agenda ya mwaliko ni kukemea rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya na maovu mengine, wala rushwa na watoa rushwa, mafisadi na wauza madawa ya kulevya watafanya mbinu zao chafu ikiwa ni pamoja na kutoa rushwa ili kuvuruga mipango mizuri yenye manufaa kwa wananchi. Wataivuruga kwa sababu wana wasiwasi kuwa mjumuiko huo utaifanya jamii ielewe kwa undani na kwa umakini mbinu zao chafu na mambo yao machafu. Hawa ni watu ambao wamejijengea himaya zao za kuwadhulumu watu, kuwalaghai watu, kuwanyonya watu, kuwarubuni watu, kuwanunua watu na hata kuwaumiza ikibidi ili mradi malengo yao machafu yatimie. Shughuli yoyote hata kama ni ya halali kiasi gani ili mradi inagusa maslahi yao itahujumiwa kwa sababu wanaona unagusa maslahi na himaya zao.
Napenda nitoe mifano miwili ya haya ninayoyazungumza ambayo yamenipata mimi. Mara ya kwanza ni tarehe 27 Oktoba wakati nilikuwa na mwaliko wa kikundi cha joggers cha Dar es Salaam ambacho kiliponialika kupokea jogging yao hapo viwanja vya Mnazi moja. Dakika za mwisho nikapewa taarifa kuwa shughuli imeshindikana kwa sababu imeingiliwa na kikundi chenye kulinda maslahi yake au ya mtu wao. Shughuli hiyo baadaye naambiwa ilifanyika na alipatikana “mgeni rasmi mwingine.” Nina hakika vijana wale na umma kwa ujumla walikosa ujumbe mahsusi ambao nilikuwa niutoe kwa vijana wetu na jamii nzima. Ujumbe huo nitawagawia leo ili watakaopenda kuutoa wautoe kwa vijana na kwa jamii.
Mara ya pili ni mwaliko wa kuzindua SACCOS ya Nshamba Muleba, Kagera. Nilipata mwaliko wa kuzindua SACCOS kule Nshamba Muleba tarehe 28 Oktoba mwezi huu. Mwaliko huo sikuuomba bali viongozi wa chama walinipendekeza kwa sababu zao wenyewe. Wakati najiandaa kwenda Kagera nikaambiwa shughuli zimeingiliwa na watu fulani kwa kutoa rushwa kwa baadhi ya viongozi wa SACCOS hiyo ili shughuli hiyo isifanyike na kupewa maelekezo kuwa haiwezekani Sumaye afike Kagera kabla ya mtu wao. Hata matangazo yaliyolipiwa fedha kutangaza mkutano huo ilibidi yasitishwe na fedha kurudishwa. Watu wa SACCOS ya Nshamba wamecheleweshewa shughuli zao za kiuchumi kwa sababu ya uhuni wa watu wasio na uchungu na wananchi. Poleni watu wa Muleba lakini ninawaahidi nitafika tu huko muda si mrefu.
Nataka niwataarifu hao wanaohangaika na mialiko yangu wajue kuwa miako ninayo mingi mpaka mingine nakosa muda wa kuifanya, na siitwi kwa sababu ya fedha maana wanajua sina fedha za aina hiyo maana sijaiibia nchi na watu wake. Jinsi wanavyojitahidi kunizima kwa rushwa ili ati nisizungumzie juu ya rushwa, ufisadi na madawa ya kulevya ndivyo wanavyonipa nguvu na mifano hai ya jinsi rushwa na ufisadi vilivyo mbaya katika taifa. Fisadi huliibia taifa fedha nyingi kiasi cha wananchi kutaabika sana halafu huja kutoa kijisehemu ya fedha alizofisadi kwa njia ya rushwa kukandamiza maendeleo ya watu. Fisadi akikuhonga na wewe ukafurahi ni sawa na mtu aliyekupa ugonjwa mbaya usiopona halafu wakati wa maumivu makali anakuletea panadol ya kupunguza maumivu na wewe unaimba kwamba huyo ni mwungwana anayekupenda. Unasahau kuwa kama siyo yeye kufanya hayo aliyoyafanya usingekuwa katika hali hiyo. Hawa ni watu hatari sana katika jamii tusiwakubalie watununue kuvuruga mipango yetu tuliyojipangia.
Utoaji taarifa katika vyombo vya habari
Pamoja na majukumu mengine, vyombo vya habari vina jukumu kubwa la habarisha jamii. Vyombo hivi ndivyo vinavyo wahabarisha umma nini kinatokea katika sehemu nyingine ya nchi na nani anafanya nini. Kiwe kinamilikiwa na serikali au mtu au kampuni binafsi havipishani katika umuhimu wa kuhabarisha umma. Aidha vyombo hivi vinatakiwa vitoe taarifa au habari kama ilivyotolewa na mtoa habari na siyo habari iliyochakachuliwa kwa madhumuni fulani. Ninyi mtakubaliana nami kuwa kuna wakati baadhi ya waandishi wa habari na wasimamizi wa vyombo walikuwa waandika au kutoa taarifa kwa maelekezo ya watu fulani fulani. Maelekezo hayo yanaweza kuwa na lengo la kumchafua mtu anayelengwa au basi taarifa za mtu huyo zisitoke katika vyombo hivyo. Katika hali hiyo mwandishi utakuwa unadhalilisha taaluma yako na wakati mwingine unajihatarisha kupelekwa mahakamani kama uliyoyaandika hameathiri heshima ya mtu.
Mimi nimekumbana na haya yote na wakati mwingine imebidi kupeleka mastaka mahakamani ili kutafuta haki, na ninyi ni mashahidi kesi zote nilishinda kwa sababu nilikuwa nasingiziwa kwa utaratibu huo huo wa waandishi kuelekezwa. Unalotakiwa kulijua ni kuwa wakati kesi, huyo aliyekurubuni hutamwona na wakati huo fedha alizokupa ndiyo zimeshayeyuka. Nimekumbana pia na kuzuiwa taarifa zangu kutotolewa kwa maelekezo ya watu fulani.
Hivi umejiuliza kwanini mtu akwambie usiandike au usitangaze habari za mtu fulani? Anaogopa nini habari ambazo siyo zake? Na anakwambie wewe yeye kama nani wakati hata hiyo taaluma haijui? Mtu wa namna hiyo jambo la kwanza ni mwovu hivyo anaogopa uovu wake kufichuliwa na pia hajiamini na ana mapungufu mengi ndiyo maana anaona atakalosema mwingine kitang’aa zaidi na yeye hana uwezo wa kujilinganisha naye. Jambo la pili anapokupa rushwa ili ufanye kile anachotaka yeye maana yake amekudharau sana kuwa huna akili ya kutumikia taaluma yako hadi akuelekeze yeye kwa fedha zake. Msikubali kudharaliwa kiasi hicho.
Ndugu wanahabari wote nataka niseme kwa dhati ya moyo wangu kuwa hali hii sasa imebadilika sana sana. Wengi wenu sasa mmekataa kuisaliti taaluma yenu na mnatoa taarifa za watu ikiwa ni pamoja na mimi. Kuna wakati hali ilikuwa ngumu lakini mmeiboresha na ninyi ni mashahidi kama mimi nilivyo shahidi kuwa jamii sasa hivi inavitegemea vyombo vya habari kuliko wakati mwingine wowote. Mimi nawapongeza sana na ninawaomba msipoteze mwelekeo huo kwa sababu ya vihela vya kuhongwa. Vyombo vya habari vina wajibu wa kuwaanika wala rushwa na watoa rushwa, mafisadi, wauza unga, majangiri nakadhalika. Iweje wewe upokee rushwa ili uandike uwongo? Afanyae hivyo unaidhalilisha taaluma yako na wewe mwenyewe. Najua mnafanya kazi katika mazingira magumu sana na wakati mwingine inahitaji ujasiri mkubwa kukataa hiyo rushwa lakini piga moyo konde na useme ‘taaluma yangu na utu wangu kwanza.’
Propaganda kuelekea uchaguzi wa 2015
Muda wa kuelekea wakati wa uchaguzi hasa uchaguzi mkuu huwa kuna mbinu mbali mbali zinazotumika na wahusika wanaotafuta nafasi mbali mbali kufanikisha malengo yao. Ziko mbinu nzuri za kistaarabu na ziko mbinu chafu kama za kupakazana matope (character assassinations). Mbinu ya kwanza ya kistaarabu ni pale mhusika anapowashawishi wanaomsikiliza kuwa yeye ni mtu safi atakayemudu nafasi hiyo bila kumwathiri mtu mwingine ambaye ama naye pia anadhaniwa anawania hiyo nafasi au hata kama hawanii nafasi hiyo.
Mtu wa aina ya kwanza tungeweza kusema huyo anajisafishia njia yake kwa kufyeka miiba na kuondoa magogo njiani ili wakati ukiwadia mbio zake zisikwazwe na vigingi vyovyote. Sifa ya mtu kama huyo ni kuwa miiba na magogo anayoyatoa katika njia yake huyatupa mahali salama au kuyachoma ili yasije yakamkwaza mtu mwingine au mshindani wake ambaye naye anachonga barabara yake.
Aina ya pili ya mbinu hizo ambazo ni chafu ni pale mhusika anatengeneza mbinu ama za kuwamaliza wengine wanaodhaniwa kuwa washindani wake baadaye au kuwawekea vikwazo katika mbinu zao za kujisafishia njia. Mtu wa namna hiyo ama anawachafua wenzake kwa kuwapakaza matope ya uwongo mtupu au anawajengea mazingira yeye kupendwa kwa kutumia migongo ya wengine. Tukirudi kwenye mfano wetu wa kufyeka barabara basi huyo ama anachimba mitaro kwenye barabara wanazofyeka wenzake au anatupia miiba na magogo yanayotoka kwake na kuyatupia kwa wenzake ili mradi wenzake wakwame wakati ukiwadia.
Mimi mtu akihangaika kujisafishia njia bila kuathiri wengine au kuathiri mambo fulani ya msingi huwa hainisumbui sana, lakini ikiwa inaathiri mtu mwingine itabidi tuiambie jamii ukweli na hivi ndivyo nitakavyofanya leo na hata wakati mwingine jambo kama hilo likijitokeza.
Gazeti la Mwananchi la tarehe 16 Septemba 2013, liliandika kuwa siri ya mradi wa kuvuta maji Ziwa Victoria yafichuliwa, na katika maelezo yake mtoa habari alisema ni mawaziri wawili tu waliouunga mkono mradi huo na wengine wote waliupinga. Kwa maelezo yake waliouunga mkono ni Mheshimiwa Jakaya Kikwete aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na Mheshimiwa Mohamed Seif Khatib waziri katika ofisi ya makamu wa rais. Najua mhusika ameutumia sana mradi huu kisiasa na sisi wengine tumenyamaza japo ukweli tunaujua sana. Lakini ili mradi ametukanyaga vidole wengine na kutupia miiba na magogo kwenye njia yetu wengine, amenilazimisha niseme ukweli kuhusu mradi huu kwa sababu mimi ndiye niliyekuwa waziri mkuu na mradi umetelezwa chini ya uangalizi wangu kama kiongozi na msimamizi mkuu wa utekelezaji wa shughuli zote za serikali.
Pamoja na kwamba hilo lililolielezwa ni uwongo mkavu, mhusika kama waziri mwandamizi wakati huo na sasa kama anayewinda nafasi kubwa katika nchi hakutegemewa kutoa siri za baraza la mawaziri; labda amediriki kufanya hivyo kwa sababu anajua anayoyasema siyo ya kweli vinginevyo ni kosa la jinai na akishitakiwa anafungwa jela.
Pili mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ni mradi wa serikali na siyo wa mtu. Ni kweli kwa mkataba uliokuwepo wa miaka ya 1952 au 1953 nchi za huku juu mito ya Nlie inapoanzia na inakopitia hazikutakiwa zitumie maji ya Mto Nile ili nchi za Misri na Sudan zisiathirike. Nchi hizi Tanzania ikiwamo ziliona makubaliano hayo siyo sahihi na tulianza kudai mabadiliko ya sheria hiyo. Jambo hili lilishughulikiwa mwanzo na Waziri Dr. Pius Ng’wandu na baadaye likakamilishwa na ‘Agreed Minutes’ zilizoweka msingi wa makubaliano baina ya nchi hizo kusainiwa na nchi kumi na kwa Tanzania aliyesaini ambaye kwa bahati nzuri alikuwa ndiye mwenyekiti wa baraza hilo la nchi kumi alikuwa Mheshimiwa Musa Nkhangaa aliyekuwa Waziri wa maji wakati huo. Katika kusukuma jambo hili mbele hata mimi niliwahi kukutana Addis Ababa na marehemu Meles Zenawi, aliyekuwa waziri mkuu wa Ethiopia. Baada ya hapo Waholanzi walitusaidia kuandika mradi huo baada ya waziri Nkhangaa kutembelea chanzo cha kuchukulia maji cha Smith Sound na kuona mradi unawezekana. Hapo ndipo Rais Mkapa aliposhauriwa kuwa mradi huo unawezekana na ndipo Rais Mkapa alipotoa ahadi Shinyanga kuwa Shinyanga itapata maji kutoka Ziwa Victoria kwa gharama yoyote na ndivyo ilivyokuwa.
Matatizo ya maji Shinyanga yalivyotutesa isingewezekana baraza la mawaziri kuupinga mradi huo na mimi nisingeupinga kabisa maana wakati mji wa Shinyanga ukikosa maji nilikuwa silali usingizi.
Jambo ambalo ni kweli ni kuwa mradi huo uliiva wakati Mhe. Lowassa akiwa waziri wa maji na ameusimamia hadi ukakamilika kama ambavyo angeusimamia waziri mwingine wa maji. Nataka ieleweke wazi kuwa hakuna waziri mwenye uwezo wa kutekeleza mradi kama baraza la mawaziri likiukataa. Fedha atapata wapi za kuendesha mradi huo? Pili mradi wowote ni wa serikali na unatengenezwa na wizara husika. Katika wizara wanaofanya kazi sana ni wataalam chini ya katibu mkuu. Pamoja na kuwa sisi wanasiasa tunapenda kubeba sifa zote mambo yakienda vizuri na kuwatupia lawama wataalam yakienda vibaya, ni vema tujue tunafanya kama timu moja na mwenye serikali ni moja tu yaani Rais.
mwisho
Huwa sipendi kuingilia mambo ya watu wengine lakini yanaponigusa sitanyamaza. Lakini pia ni wajibu wangu kueleza ukweli pana ambapo ukweli unapotoshwa kwa makusudi. Nataka niwaase hasa wanasiasa wenzangu kuwa tuwatendee watanzania haki kwa kuwapa ukweli mtupu na tusiwape uwongo uliopakwa utamu wa ukweli juu kumbe ndani ni machungu ya uwongo.
Aidha sote tuseme rushwa ni adui wa haki. Unapompa mtu rushwa ujue kuna anayedhulumika na kuumia na hiyo rushwa yako. Unapofanya ufisadi kwa mradi wa serikali unaliumiza taifa katika siku zijazo kwa kuipiga kiharusi cha uchumi na huduma kwa jamii. Na unapouza dawa za kulevya wewe ni mwuuaji wa taifa kwa sababu unaangamiza vijana wa taifa hili ambao ndiyo nguvu kazi yetu tunayoitegemea.
Basi tujiulize kama unafanya haya au baadhi ya haya wewe unafaa kutuongoza?
MUNGU IBARIKI TANZANIA
chama cha ccm na serikali yake haiwezi kuwashughulikia watoa rushwa. dawa ni kuiondoa serikali ya ya ccm kuongoza Nchi, na kuiweka chadema kiunde serikali hapo tutakuwa na imani ya kupiga rushwa vita, kama ccm wanashindwa kuwachukulia viongozi wake walioshinda kwa rushwa kama tulivyoambiwa na Mangula watawezaje kwa serikali? hivi watanzania hili hatulioni?
 
=> .atulie kabisa huyu...enzi yake rushwa ilikuwa wazi wazi.....

=> Lowassa kamnyoosha...na bado...
 
Duh! kwa hiyo sasa asiseme? Nadhani tujadili hoja si mtoa hoja.

Lakini kuna hili tulijadili pia! kwa mara ya kwanza anamtaja Lowassa moja kwa moja.

Gazeti la Mwananchi la tarehe 16 Septemba 2013, liliandika kuwa siri ya mradi wa kuvuta maji Ziwa Victoria yafichuliwa, na katika maelezo yake mtoa habari alisema ni mawaziri wawili tu waliouunga mkono mradi huo na wengine wote waliupinga. Kwa maelezo yake waliouunga mkono ni Mheshimiwa Jakaya Kikwete aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na Mheshimiwa Mohamed Seif Khatib waziri katika ofisi ya makamu wa rais. Najua mhusika ameutumia sana mradi huu kisiasa na sisi wengine tumenyamaza japo ukweli tunaujua sana. Lakini ili mradi ametukanyaga vidole wengine na kutupia miiba na magogo kwenye njia yetu wengine, amenilazimisha niseme ukweli kuhusu mradi huu kwa sababu mimi ndiye niliyekuwa waziri mkuu na mradi umetelezwa chini ya uangalizi wangu kama kiongozi na msimamizi mkuu wa utekelezaji wa shughuli zote za serikali.
Pamoja na kwamba hilo lililolielezwa ni uwongo mkavu, mhusika kama waziri mwandamizi wakati huo na sasa kama anayewinda nafasi kubwa katika nchi hakutegemewa kutoa siri za baraza la mawaziri; labda amediriki kufanya hivyo kwa sababu anajua anayoyasema siyo ya kweli vinginevyo ni kosa la jinai na akishitakiwa anafungwa jela.
Pili mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ni mradi wa serikali na siyo wa mtu
. Ni kweli kwa mkataba uliokuwepo wa miaka ya 1952 au 1953 nchi za huku juu mito ya Nlie inapoanzia na inakopitia hazikutakiwa zitumie maji ya Mto Nile ili nchi za Misri na Sudan zisiathirike. Nchi hizi Tanzania ikiwamo ziliona makubaliano hayo siyo sahihi na tulianza kudai mabadiliko ya sheria hiyo. Jambo hili lilishughulikiwa mwanzo na Waziri Dr. Pius Ng'wandu na baadaye likakamilishwa na ‘Agreed Minutes' zilizoweka msingi wa makubaliano baina ya nchi hizo kusainiwa na nchi kumi na kwa Tanzania aliyesaini ambaye kwa bahati nzuri alikuwa ndiye mwenyekiti wa baraza hilo la nchi kumi alikuwa Mheshimiwa Musa Nkhangaa aliyekuwa Waziri wa maji wakati huo. Katika kusukuma jambo hili mbele hata mimi niliwahi kukutana Addis Ababa na marehemu Meles Zenawi, aliyekuwa waziri mkuu wa Ethiopia. Baada ya hapo Waholanzi walitusaidia kuandika mradi huo baada ya waziri Nkhangaa kutembelea chanzo cha kuchukulia maji cha Smith Sound na kuona mradi unawezekana. Hapo ndipo Rais Mkapa aliposhauriwa kuwa mradi huo unawezekana na ndipo Rais Mkapa alipotoa ahadi Shinyanga kuwa Shinyanga itapata maji kutoka Ziwa Victoria kwa gharama yoyote na ndivyo ilivyokuwa.
Matatizo ya maji Shinyanga yalivyotutesa isingewezekana baraza la mawaziri kuupinga mradi huo na mimi nisingeupinga kabisa maana wakati mji wa Shinyanga ukikosa maji nilikuwa silali usingizi.
Jambo ambalo ni kweli ni kuwa mradi huo uliiva wakati Mhe. Lowassa akiwa waziri wa maji na ameusimamia hadi ukakamilika kama ambavyo angeusimamia waziri mwingine wa maji. Nataka ieleweke wazi kuwa hakuna waziri mwenye uwezo wa kutekeleza mradi kama baraza la mawaziri likiukataa. Fedha atapata wapi za kuendesha mradi huo? Pili mradi wowote ni wa serikali na unatengenezwa na wizara husika. Katika wizara wanaofanya kazi sana ni wataalam chini ya katibu mkuu. Pamoja na kuwa sisi wanasiasa tunapenda kubeba sifa zote mambo yakienda vizuri na kuwatupia lawama wataalam yakienda vibaya, ni vema tujue tunafanya kama timu moja na mwenye serikali ni moja tu yaani Rais.
 
Maelezo yote haya na kulalamika kote huku, Chorus ni LOWASA? Mh umechoka pumzika yako mengi uliharibu. ENL amesema kiongozi analalamika, wanachi wanalalamika tutaishia wapi. Sioni ulichowakusanyia waandishi wa habari ili uwape watuletee. Kumbe ni maji ya Ziwa Victoria, Mungu wangu, eti kama baraza la mawaziri halikubali kitu hakiwezi fanyika, sasa ndio naona kuwa ni kweli wewe ulikataa ila JK na Mh. Khatibu. Halafu eti anatoa siri za baraza la mwaziri, wewe umefanyeje sasa. Napata shida sana na kama ni hivi URAHISI samahani urais utakutoa roho. Ninachokushauri usiwe unamwota ENL HATA KWA NDOTO ZA MCHANA, AMEKUACHA MBALI KIASI. Sijawahi kusikia ENL anazungumzia mtu huwa anazungumza hoja 'issues'' na kwako hilo silioni. Naomba kama huna hoja TULIA. Halafu unajipendekeza kwa press ehee. You're tired, you need to retire politics completely. Ni ushauri wa bure
 
Sumaye ametaja neno madawa ya kulevya mara nyingi sana, tena hata siku za nyuma amewahi kusema kuna hatari nchi inaweza kuongozwa na wauza madawa ya kulevya.

Kuna kitu kimejificha kwenye kauli yake hiyo. Sumaye hawezi kuwa anataja kila siku bure bure tu.
 
Kwa mwanaCCM kuhutubia mwanzo mwisho bila kuitaja chadema huo ndio ukomavu wa kisiasa. Ni kweli wakati yeye akiwa Waziri mkuu kulikuwa na maovu vilevile lakini ameyajadili kama ni makosa ya serikali ya CCM bila kuonyesha kutaka kutupia lawama wengine nje ya CCM. Maana kwa sasa ili u win confidance ya wanachama wenzako basi ukisema neno ili lipate utamu unaweka chumvi (Chadema) kidogo ili wale wenye akili za samaki waburudike na mipasho. Hongera Sumaye
 
Sumaye anaweza kuwa na makosa yake huko nyumba BUT points zake ni muhimu

1. Rushwa - Kutenda haki
2. Dawa za kulevya
 
Dah hii sasa basi hizi mbio zakupokezana vijiti zitawatoa kucha wengi Hivi huyu mzee siamelipwa kiinua mgongo na mafao anapata? na kodizangu zinaendelea kumlisha? au ndo mda wakumikia mastazi yake? mbona gari la ccm limejaa viti atakaa wapi? amtafute wakumshusha ila mimi simuoni wakumshusha!
 
Summay huyu huyu akiwa waziri mkuu na Mbunge alitetea na hatimaye kupitisha TAKRIMA huku akijua takrima ni rushwa, leo anajipambanuaje kuwa mpinga rushwa??
 
sumaye huna lolote,wewe ndiye muasisi wa rushwa uliingia madarakani tuu ukajenga jumba ,kuulizwa ukasema eti umekopeshwa PPF wakati wachangiaji wa miaka nenda rudi hawajawahi kukopeshwa na PPF.Ukaenda kujigawia maekari huko /kibaigwa,mvomero turiani ikabidi Mkapa akutetee.Kila mkoa Sumaye unahodhi maeneo makubwa bila hata ya kuyaendeleza mengine umeayaandika majina ya familia yako.HAKUNA MTU MLA RUSHWA NA MLAFI KAMA WEWE!!!
Umekaa Uwaziri mikuu hakuna hata kitu ulichofanya katika huo muda wa miaka 10 zaidi ya kuuigawa arusha na kuanzisha mkoa wako MANYARA.NYOTE MNATOKA ZAMANI ARUSHA kwa nini hupatani na LOWASA na MAGUFULI?enzi za magufuli waziri wa ujenzi nawe PM hukuwahi hata siku moja kuweka jiwe la msingi au kuzindua ujenzi wa barabara
 
Hizi ngonjera tu, kuusema uovu wa mtu tu, haikupi fursa ya wewe kufaa, unataka urais sema. kuna uovu, kemea na ikibidi wataje kwa majina kama Chadema wanavyofanya. Eti wanahujumu harambee zangu, KUMBE mnazipenda?? Mbona Dr. Slaa, Mbowe, Zitto, hawajahujumiwa kwenye Harambee zao? Na kwa nn mwalikwe nyie tu. NYote wezi tu. Mashamba yetu ww umerudisha? Sumaye na Mkapa ndio waliuza nchi, na hao LOWASA, KIkwete, walikuwa vijana wao kwenye Serikali, wakawa wanapiga deal kama Boss wao. saizi ya Sumaye kwa sasa ni Nagu. Atabaki kuunga tu mkono na kulalamika kukosa harambee!!!
 
Sumaye anazungumza na waandishi now Court Yard, anasema anamuunga mkono JK kuhusu rushwa CCM ila anataka azungumzie na rushwa serikalini.

Hana lolote huyo. Ametoka serikalini ndo akaiona rushwa?? Hebu mtu mmoja atupe maana ya rushwa ndo tujionee jinsi kila mtanzania anavyotoa na kupokea rushwa. Hakuna mtanzania asiyetoa wala kupokea rushwa, kama yupo ajitokeze tumchambue. Kila siku mnatwambia wanaokamatwa tu, twambieni na wasiopokea wala kutoa rushwa ili tuige mfumo wa maisha yao mazuri. HAKUNAAAAAAAAAA!!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom