Mkuu wewe ndio umepatia, nashukuru kwamba Rais Kikwete amekuwa jasiri kwa kuzungumzia tatizo sugu la nchi ya Rwanda, nashangaa hapa watu wanavyo ji-pretend kumlahumu kinafki tu huku wakijua fika kwamba ukabila na watu wengine kujiona ndio bora walio umbwa na Mungu kuwatawala raia wenzao, ni raia gani mwenye akili timamu anaweza kukubali blindly kuongozwa na a few minority 4ever, South Africa should serve as a wake up call; Wazungu walijifanya ngangali lakini baadae wakakubali hali alisi wakabwaga manyanga her military mighty notwithstanding, wakakubali mazungumzo wakaridhihana/samehana nchi ikatulia mpaka leo - hakuna cha kulipizana visasi wala nini, nyinyi mnashindwa nini kumeza your pride na kumaliza matatizo yenu SUGU kiungwana bila ya kutumia ubabe na kutisha WATU!
Ndugu zangu tujaribu kuwa wakweli tukitaka Rwanda iwe na amani ya kudumu mambo kushabekia binadamu wenzetu hita prolong matatizo sugu ya jamaa hawa - tusijidanganye FDLR na Jeshi la Serikali ya Rwanda wote wame commit genocide nchini Rwanda na Congo, hakuna ambaye ni msafi katika hilo, kinacho fanyika hapa ni kubadilisha badilisha maneno kutegemea unamu-address nani hasa hasa lengo kuu ni kutaka kubabaisha International Community! Mauuaji nchi Rwanda watasema ni genocide lakini mauuaji ya harahiki ya Wahutu kwenye makambi ya wakimbizi nchini Congo hayo wanasema ilikuwa ni njia sahihi ya Rwanda kujihami dhidi ya Wahutu sio genocide, je kuna ukweli gani katika upotoshaji huo mkubwa - UN ikiteua an independet team ya kuchunguza idadi kamili ya wahutu walio fyekwa kwenye makambi ya wakimbizi nchini Congo ndio mtashangaa. Wahutu na Watutsi wote are equally to blame katika mambo ya mauuaji, tofauti yao ni njia wanayo tumia kufanikisha malengo yao, I am sorry kulisema hilo na hakuna ninaye mtetea katika hilo.
Naona kuna baadhi ya watu wamemkalia kooni Mh.Kikwete, ukweli wa mabo ni kwamba wanao jitia kumlahumu Mh.Kikwete wanajua fika chanzo cha Wahutu kukasirika kupindukia kilitokana na kitu gani, je mtu aliye washa kiberiti karibu na gunpowder keg alitegemea muhujiza gani baada ya Rais alichaguliwa kidemokrasia kuuwawa kinyama!! Dunia nzima inakuwa held at ransom na makabila mawili ambayo yamekuwa wired kuchukiana tangu utotoni kwa sababu ambazo hazina mantiki kabisa.
Binafsi nampongeza Mh.Jakaya kwa kuona mbali na kuwaeleza ukweli Wanyarwanda wanaweza kumbeza watakavyo lakini kuna siku watamkumbuka, msijidanganye bila mazungumzo na vikundi mahasimu, Rwanda isitegemee kwamba wataweza kuishi kwa amani ya kudumu, wakae wakijua kwamba remnat ya Jeshi la Habyarimani na wao wana uwezo wa kujipanga upya kama alivyo jipanga Mh.Kagame nchini Uganda na wao wakaingia Rwanda kwa stahili hile hile ya Jeshi la Kagame, je wakifanikisha hilo si tutarudi tena back to square ONE, nchi nzima itaendelea kuzunguka in vicious circles miaka nenda rudi mpaka lini.
Nimalizie kwa kusema nimeyasema haya kwa nia nzuri tu, najua kuna watu watanisema sana au kujaribu kumlahumu Mh.Kikwete kwa ujasiri wake - tusubiri historia ndio itatuhukumu.