Kikwete: Nimelipa deni la taifa la 1958

Kikwete: Nimelipa deni la taifa la 1958

hilo deni la mwaka 1958 litakuwa liliachwa na mkolini muingereza. Kumbe tanganyika tulianza kukopa hata kabla ya uhuru

Mkuu mwingereza hukufanya lolote lile! Miundo mbinu mingi ilijengwa na mjeruman akishirikana na wamisionari! rejea kuanzishwa kwa uchumi wa kikoloni afrika masharik ikiwemo tanganyika utapata majibu sahihi
 
Kuna hatari ikaombwa risiti ya malipo ya mkopo huo wa 1958 !!! Kisha isiwe ajabu hiyo risiti kukosekana.
 
Hizo pesa amemlipa nani na sh.ngapi lini
 
Ndiyo mwaka 1958 kulikuwa na Tanganyika chini ya ukoloni wa Muingereza (Trustship).

Ameshindwa kulipa deni la wazabuni wa hapa akalipa la wakoloni?? du du ! anyway tuliyataka wenyewe na tunayataka wenyewe na mengine Octoba siyo mbali tutayakumbatia tu tena!
 
Pia najiuliza kwann deni hilo lisilipwe toka awamu ya kwanza,pili au ya tatu? Nimepitia hotuba zote za mwl.jk! Sijaona wala kusikia n wap kalizungumzia hilo den! Huu n usanii polen watz! Kwa kupata kiongoz wa kihistoria kama huyu!
 
Kwanza huyu jamaa kwa miaka 10 kaishi angani Mwaka 1.
Ebu mtalaam wa Route za Rais wetu JK atupe idadi, kafikisha ngapi? Je kwa sasa anaongoza Rekodi ya kusafiri au yule wa Nigeria bado ni top?

Deni 2005 Trillion 7 mwaka 2015 June Deni Trillion 35!! Daah JK unasifa za ajabu ajabu!!

Tungeweza hata jua kuhusu huyu Mtu ana IQ kiasi gani! Manufacture of teachers! ha ha ha ha ha !! presidaa of Tanzania!
 
bado ni na wasiwasi na hoja hii, ikumbukwe sisi hatukuendeleza serikali ya kikoloni sisi tulianza serikali mpya kabisa, yaani ya tanganyika sina hakika sana kama tulirithi madeni ya mkoloni. na sidhani kama tulirithi deni hili wakati tunafutiwa madeni hili lazima lingekuwemo sasa mzee amelitoa wapi?

Ndio ujue haya malipo ni skendo mpya tena!!
 
Ameshindwa kulipa deni la wazabuni wa hapa akalipa la wakoloni?? du du ! anyway tuliyataka wenyewe na tunayataka wenyewe na mengine Octoba siyo mbali tutayakumbatia tu tena!
Hata hilo deni la wakoloni huenda hukulipa ila alikuwa anajipandishia chati tu huku akijua hakuna atakaye fuatilia!
 
Kichekesho, unakopa milioni moja laki nane inateketea kwenye kiti kirefu, laki mbili inatumika kuwazugia wananchi na ujenzi wa barabara zisizokidhi viwango.
 
"mimi siendi kung'ang'a Macho IKulu" Lowassa, nahisi alimaanisha wapo walionda Ikulu kufanya alichosema hatofanya yeye akipewa ridhaa kwenda ikulu
 
Mkuu msome tanga kwetu alikuwepo mkutanoni na amefafanua zaidi!

Mkuu unataka kusema ili mtu kupata habari lazima uwe kwenye mkutano husika? Nini maana ya vyombo vya habari. Acheni kupotosha umma.

Raisi tumemwona akisema mwenyewe kwenye TV Kuwa kalipa deni la mwaka 1958 lilokopwa kwa ajili ya kujenga morogoro road.

Ningemwomba Mh waziri wa Fedha atoe ufafanuzi kuhusu hilo deni la mkoloni tulilolipa kabla ya kuhitimisha vikao vya bunge kwa kuwa kipindi hicho kodi yote ilipelekwa kwa Malkia.
 
Mkuu unataka kusema ili mtu kupata habari lazima uwe kwenye mkutano husika? Nini maana ya vyombo vya habari. Acheni kupotosha umma.Raisi tumemwona akisema mwenyewe kwenye TV Kuwa kalipa deni la mwaka 1958 lilokopwa kwa ajili ya kujenga morogoro road.Ningemwomba Mh waziri wa Fedha atoe ufafanuzi kuhusu hilo deni la mkoloni tulilolipa kabla ya kuhitimisha vikao vya bunge kwa kuwa kipindi hicho kodi yote ilipelekwa kwa Malkia.
Sasa aliyepotosha umma ni nani?
 
Rais Kikwete amesema serikali imelipa deni lilikopwa mwaka 1958 ambalo lilitumika kuijenga Morogoro Road.

Amesisitiza hakuna nongwa yoyote kwa madeni anayoacha kuja kulipwa na mrithi wake.

Amemalizia kuwa duniani kote ili nchi iendelee ni lazima ikope kama ilivyo kwa wafanyabiashara ili kukua lazima utakopa.

Chanzo: ITV habari

Bora kalipa Barbara ya Morogoro ...Sasa yeye pesa alizokopa tutaonyeshwa nini ?? Tatizo kuna harufu ya kukopa kufanya Miradi hewa
 
Kikwete ni raisi bora afrika nzima.... kama ronaldooo
 
Rais Kikwete amesema serikali imelipa deni lilikopwa mwaka 1958 ambalo lilitumika kuijenga Morogoro Road.

Amesisitiza hakuna nongwa yoyote kwa madeni anayoacha kuja kulipwa na mrithi wake.

Amemalizia kuwa duniani kote ili nchi iendelee ni lazima ikope kama ilivyo kwa wafanyabiashara ili kukua lazima utakopa.

Chanzo: ITV habari

Tunapenda kudanganywa ndiyo maana akaamua kuongea huu -----...........Duh ipo Bongo tu:shock::shock::shock:
 
Inawezekana ktk issue kuna watu wamefanya ufisadi. Watu wanatafuta madeni yasiyo na wenyewe kama epa na escrow kisha wanapiga hela ndefu. Nakubaliana na Makongoro kuwa tatizo si kikwete bali vibaka wanaomzunguka!

Baada ya kugundua tatizo liko kwa watendaji wake vibaka yeye kama raisi aliwachukulia hatua gani hao vibaka..? Kuna kibaka yeyote aliefukuzwa au kufikishwa mahakamani na kushtakiwa na kupatikana na hatia..?

Kama vibaka unaowasema wewe na Makongoro wameendelea kubaki kwenye nyadhifa zao na kuendelea kupeta huoni tatizo sasa haliko kwa vibaka bali liko kwa mfuga vibaka..?

Halafu haingii akili kujisifia kulipa deni la mwaka 58 wakati deni ndani ya miaka yake 10 ya uraisi deni limepanda toka Tshs Trilioni 7 mpaka kufikia karibu Trilioni 35..! Ni punguani peke yake anaweza kusifia maajabu haya ya 10 ya dunia..!
 
Back
Top Bottom