Nini suluhisho la kudhibiti Deni la Taifa?

Nini suluhisho la kudhibiti Deni la Taifa?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,217
Reaction score
15,567
Wakati deni la Taifa lizidi kupaa, baadhi ya wataalamu wa uchumi wameonya kuhusu matumizi ya fedha za mikopo, wakitaka Serikali iwekeze nguvu kudhibiti upotevu wa mapato kabla ya kufikiria kuongeza wigo wa mapato.

Soma> Serikali: Deni la taifa lafikia Tsh. Trilioni 107 ikiwa ni ongezeko la 14.9%

Deni la Taifa lilifikia Sh107.7 trilioni kutoka Sh91.7 trilioni katika kipindi kama hicho Mwaka 2024, sawa na ongezeko la Asilimia 14.9. Kati ya hizo, deni la ndani ni Sh Trilioni 34.25 na lile la nje likiwa Dola za Marekani 26.67 bilioni.

Deni la Taifa ni nini?
Ofisa Program wa Mtandao wa Madini na Maendeleo Tanzania (TCDD), Boniface Komba anafafanua maana ya Deni la Taifa:

"Deni la Taifa ni jumla ya fedha ambazo serikali inakopa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya fedha ili kuziba mianya ya kifedha. Serikali inaweza kukopa kutoka ndani au nje ya nchi kwa ajili ya kufadhili miradi ya maendeleo."

"Deni la Taifa limegawanyika katika sehemu kuu mbili: deni la ndani na deni la nje. Deni la ndani ni fedha ambazo serikali inakopa kutoka vyanzo vya ndani inawezekana zikawa ni benki za kibiashara au taasisi nyingine za kifedha, wakati deni la nje ni fedha zinazokopwa kutoka taasisi za kimataifa au benki za nje au taasisi za fedha."

"Katika deni la Taifa kuna deni la umma ambalo Serikali ilikopa iwe ni kwenye vyanzo vya ndani au vya nje, na ina wajibika kulipa. Pia kuna madeni binafsi yakihusiha mikopo iliyochukuliwa na kampuni na taasisi binafsi. Serikali inawajibika kuisimamia na kuidhibiti kwani ndiyo inaumba Deni la Taifa."

Akifafanua zaidi, Mhadhiri wa Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Abel Kinyondo anasema deni ni chanzo halali cha mapato cha Serikali, kwa kuwa mapato ya kodi huwa hayatoshi.​


"Bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi ya nchi kwa wakati huo, sasa ili uwe na makadirio ya wakati huo inabidi uanishe vyanzo vya mapato hayo. Chanzo kikuu cha mapato cha Serikali yoyote ile ni kodi, lakini sasa inatokea mara nyingi kwa nchi nyingi uniani, kwamba mapato yanayotokana na kodi huwa hayana uwiano mzuri wa matumizi, kwa hiyo nchi karibu zote duniani, zikaona zitumie chnzo kingine cha mapato yake ili kufidia ambacho ni madeni."

"Pili, mikopo huwa imegawanyika katika hali mbili ambazo ni concessional (mikopo nafuu) ambayo riba yake ni ndogo na ya muda mrefu na pili kuna commercial ambayo ni ya kibiashara na riba yake huwa ni kubwa. Sasa huwa inashauriwa Serikali ichukue zaidi mikopo ambayo ni concessional kwa kuwa riba yake ni ndogo na italipa kwa muda mrefu kuliko commercial ambayo inanenepesha deni kwa haraka."

"Tatu, deni liwe linatokana na concessional au commercial linaweza kuvumilika kama linachukuliwa kwa asili ya miradi ya maendeleo. Kwa mfano unachukua kwa ajili ya SGR maana yake wafanyabiashara watasafirisha mizigo fedha zitarudi, lakini kama unachukua halafu unanunua magari hasa V8, maana yake fedha hazitarudi."

Hali ya deni la Tanzania ikoje?
Akifafanua zaidi, Profesa Kinyondo anaeleza vipimo vinavyotumika kuangalia hali ya Deni la Taifa na njia nyingine za uhalisia, akisema kipimo kinachotumika ni uwiano wa deni la pato la Taifa (Debt with GDP Ratio).

"Sasa wachumi wakasema huu uwiano unapokuwa hauzidi asilimia 77, hilo deni ni himilivu, kwa kigezo hicho, ni kweli Serikali inaposema deni ni himilivu kwa sababu uwiano huo kwetu sisi ni 40.3."

Pamoja na uhimilivu wa deni la Tanzania, Profesa Kinyondo anasema vipimo haviishii tu kwenye nadharia.

"Kwa kuchukua tu huo uwiano, huwa hakuna uhalisia kwa sababu kwanza: ni aina ya mkopo unachukua, kwamba ni mkopo nafuu au wa kibiashara? Je, unauchukua kwa sababu ya maendeleo au matumizi tu ya kawaida yasiyo ya lazima?"

"Pili, hiki kipimo sio msaafu auhalisia wa nchi kuwa na unafuu. Kwa mfano Marekani deni lake lake uwiano wake ni asilimia 126, maana yake wamezidisha zaidi ya asilimia 50. Japan wao uwiano wao wa deni kwa GDP ni asilimia 263, maana yake wamezidisha kwa karibu mara tatu."

"Kwa hiyo kwa sababu Marekani na Japan wamezidisha hicho kiwango, unafikiri wana hali mbaya kuliko sisi? Hapo ndipo utapata jibu kwamba kipino hicho sio uhalisia, kwamba ukubwa wa uchumi na uwezo wa kuhimili hilo deni."

"Kama ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo, madeni hayakwepeki, lakini kama ni matumizi ya kawaida, madeni ni ya kukimbia. Tusifanye ubabe, kusema kwamba tunapewa mikopo kwa sababu uchumi wetu ni mzuri, hapana. Madeni ni biashara. IMF (Shirika la Fedha la Kimataifa) na WB (Benki ya Dunia) wako pale kuuza madeni, ni kwa sababu wanajua watapata riba."

Kwa nini grafu ya deni imekuwa ikipanda bila kushuka?
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT), Dk. Norah Kavishe anasema ni kutokana na Serikali kutozingatia matumizi ya mikopo hiyo.

"Ongezeko la deni na kama ambavyo limekuwa ikielezwa kuwa linatokana na kukopa kwa ajili ya kufadhili miradi ya maendeleo hasa miradi ya kimkakati. Kama ni hivyo maana yake ni kwamba tunashindwa kukusanya fedha za ndani vizuri na ndio maana Serikali inalazimika kwenda kukopa ili kufadhili hiyo miradi."

"Kwa nini tunashindwa kukusanya na kusababisha deni kupanda ni mambo mengi. Huwezi kusema ni kukusanya kodi peke yake ndio kutasaidia. Ni sawa tunaweza kukusanya kodi nyingi, lakini kodi sio tu kukusanya, je tunatumiaje tunachokikusanya? Kama tunashidw akudhibiti tunachokusanya, bado kodi haitakuwa suluhisho la kupunguza kasi ya ukopaji."

"Kwa hiyo kwanza tutengeneze mifumo mizuri ya kodi ituwezeshe kukusanya kodi na kampuni zinazofanya biashara zao hapa wahakikishe wanalipa mapato sahihi kwa Serikali, lakini tuhakikishe kwamba mapato hayo yanakwenda kwenye miradi itakayoleta tija na maendeleo kwa wananchi na hiyo itafanyika kwa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kuhakikisha wale watakaobainika kushindwa kusimamia hizo fedha basi wachukuliwe hatua ili kuwafanya wananchi waiamini Serikali na hapo ndipo watapata morali ya kulipa kodi."

Tunawezaje kuondoka hapa tulipo?
Profesa Kinyondo anasisitiza ku pia kuzingatia matumizi ya mapato kabloa ya kufikia vyanzo vipya.

"Kwa mfano tunasema mwakani tunataka kupata Sh51 trilioni, sawa, lakini tunapaswa kujiuliza, hivi matumizi yako sahihi kweli? hakuna ambayo tunaweza kupunguza, hakuna ambayo tunaweza kuondoa kabisa? Kwa sababu kama yapo ambayo tunaweza kuondoa au kupunguza matumizi na kuyaondoa, maana yake tutapunguza mahitaji ya kifedha na uhitaji wa mapato na kile tutakachoondoa ni deni."

"Nadhani umeona mawaziri wa fedha kwenye nchi nyingine wakienda kutoa hiotuba za bajeti wakiwa na baiskeli na wengine wanaenda na Bolt, sisi tunakwenda na V8 kama 10 hivi. Huo ni mfano kwetu matumizi yetu hayako sawa."

"Jambo la pili ni rushwa, kwamba kila mwaka CAG anatukumbusha kwamba kuna matumizi ambayo ni ya kijinai yanatokea. Kama tutakuwa na ufunguo wa kufunga pale palipotoboka, maana yake tutakuwa na uwezo mkubwa wa kubaki na fedha kwenye maeneo yaliyopo kiasi kwamba hatuhitaji tena madeni."

"Wewe una uwezo kabisa wa kununua Toyota Hiace, lakini unakwenda kununua V8 tena kwa bei ya kiwanda yaani kilometa 0 Sh550 milioni. Ungeweza kunua gari la Sh200 milioni na lingedanya kazi nzuri tu na hii Sh300 milioni ingefanya kazi nyingine. Hayo ni matumizi halali lakini ni mabaya."

Soma, Pia
 
Ni kukamata majitu ya ccm yote na kuyafilisi kila kitu na ccm warudishe mali za umma zote walizojimilikisha bs
 
Ni kuongeza uzalishaji tuu, kukopa au kuongezeka taxes ni temporary solutions, ingawaje madeni kama infrastructure sio mabaya 💯, tuweke mkakati wa kujenga barabara zetu wenyewe, contractors wa nje ni pesa nyingi sana tena za kigeni, tujitahidi kuzalisha chakula cha kutosha tunaweza, promote magari ya umeme ili tupunguze kuagiza mafuta yanagharimu pesa nyingi sana
 
Niliwahi kuuliza ni nini hasara ya kuwa na serikali isiyodaiwa kabisana faida za kuwa na serikali inayodaiwa madeni lukuki. Mpaka Sasa sijapata majibu
 
Hivi na kampuni binafsi zikikopa huwa inajumlishwa kwenye deni la taifa ?
 
Hivi na kampuni binafsi zikikopa huwa inajumlishwa kwenye deni la taifa ?
The national debt is the total amount of money owed by the government to its creditors
. It includes borrowing from the public, like individuals and foreign governments, and intragovernmental debt, which is money the government owes to its own departments
 
Lazima tujitahidi kupunguza kuagiza bidhaa tunazoweza kuzalisha. Bahati mbaya wanasiasa ndiyo waagizaji wa bidhaa hizo au wanapiga dealkwenye uagizaji wake na wanatengeneza pesa nyingi.
 
Hili ndio jibu sahihi
1000213510.png
 
Back
Top Bottom