Kikwete: Nimelipa deni la taifa la 1958

Kikwete: Nimelipa deni la taifa la 1958

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,600
Rais Kikwete amesema serikali imelipa deni lilikopwa mwaka 1958 ambalo lilitumika kuijenga Morogoro Road.

Amesisitiza hakuna nongwa yoyote kwa madeni anayoacha kuja kulipwa na mrithi wake.

Amemalizia kuwa duniani kote ili nchi iendelee ni lazima ikope kama ilivyo kwa wafanyabiashara ili kukua lazima utakopa.

Chanzo: ITV habari
 
Kopa hlf tuone maendeleo yanayoendana na mkono. Deni la taifa limekuwa maradufu maendeleo hakuna hlf anakuja na kusema nchi zote zinakopa. Hoja mbovu. Utawala wake umeshindwa kabsa watz walikuwa na matumaini makubwa. Aende zake tuu. Hana jpya
 
Tatizo sio kukopa tatizo ni kukopa Mamilioni ya Dola kwenda kuaga nchi wahisani kwa kukubali kutukopesha
Sidhani kama hoja yako ina mashiko. Mikopo ya serikali ipo wazi kama ile ya ujenzi wa bomba la gesi. Tatizo Watanzania tunajitia vipofu
 
Sidhani kama hoja yako ina mashiko. Mikopo ya serikali ipo wazi kama ile ya ujenzi wa bomba la gesi. Tatizo Watanzania tunajitia vipofu

Unamaanisha Mikopo ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo na Makusanyo ya ndani ndio ya kwenda kuwaaga wanaotukopesha?
 
Sidhani kama hoja yako ina mashiko. Mikopo ya serikali ipo wazi kama ile ya ujenzi wa bomba la gesi. Tatizo Watanzania tunajitia vipofu

Sisi sii vipofu, tunapima kiwango cha mkopo na matimizi halisi. Sio kutuambia umetumia mil 300 kukarabati vymba viwili. Gharama halisi haiendani na matumizi.
 
Mkuu, kwani madeni yaliyokopwa na serikali ya Tanganyika hayawezi kulipwa na serikali ya Tanzania? Ukilaza mwingine huu bana!
Ni ajabu kudai umelipa deni lisilokuwepo, huu ni mwendelezo tu wa wizi. Kabla waropokaji hawajaanza kutoa kauli za ajabu ajabu, naomba mjue kuwa upo wakati madeni yote yalisamehewa tukaanza upya on a clean slate!
 
Hapo "Nyerere doctrine of state succesesion" haikutumika kwenye hilo deni? Tangu mwaka 1958 hadi mwaka 2005 wakati Kikwete anaingia madarakani ni miaka 47 imepita. kwa miaka yote hiyo hilo deni ni kwa nini lilikuwa halijalipwa?
 
Sisi tunaangalia net deni limeongezeka maradufu. Huwez kujisifu umelipa sh elfu 1 wakti umekopa na kuongeza deni la bilion 100.
 
‘Nyerere doctrine of State succession'. Julius Nyerere, the first President of Tanzania, considered that international agreements dating from colonial times should be renegotiated when a State becomes independent, as the nation should not be bound by something that the nation was not in a sovereign position to agree to at that time. According to this doctrine, a newly independent State can – upon independence – review the international treaties that it stands to inherit and decide which of the agreements it will accept and which it will repudiate. Although such an "optional" approach to events of State succession was not new and was already recognized by customary international law, Nyerere is recognized for the modern formulation of the optional doctrine of the law of State succession. It is worth mentioning that this doctrine came to existence after Nyerere (the Prime Minister of newly independent Tanganyika) made a unilateral declaration to the Acting general Secretary of the UN in 1961.

Further, with regards to multilateral treaties, the new government would review them and indicate to the depositary concerned what steps would be taken in relation to each such instrument, whether by way of confirmation of termination, confirmation of succession or accession. Nyerere doctrine is advantageous in several ways;

a) It allows states to fill the void created by the lapse of predecessor's treaties while maintaining the right to examine each treaty individually before deciding whether to maintain such legal obligations.

b) With the above advantage, Nyerere doctrine is also important as it rectifies the aforementioned shortcomings with regards to negative succession or clean-slate doctrine.

c) Unlike the clean-slate doctrine under which a new State starts without any of the obligations of the predecessor State, Nyerere doctrine of succession however, does not rule out or prejudice the possibility or desirability of renewal (after a legal interruption during the succession) of commitments or agreements of mutual interest to the parties concerned.

Imefafanuliwa na Alpha Bisimba!!
 
Ni ajabu kudai umelipa deni lisilokuwepo, huu ni mwendelezo tu wa wizi. Kabla waropokaji hawajaanza kutoa kauli za ajabu ajabu, naomba mjue kuwa upo wakati madeni yote yalisamehewa tukaanza upya on a clean slate!
Mkuu una uhakika na unachokisema?
 
Sidhani kama hoja yako ina mashiko. Mikopo ya serikali ipo wazi kama ile ya ujenzi wa bomba la gesi. Tatizo Watanzania tunajitia vipofu
unajua cha juu ni kiasi gani kwa huo mkopo wa bomba la gesi? Kama hujui kitu kaa kimya
 
Mag3 nimeiweka "Nyerere Doctrine of state succession" kama ilivyofafanuliwa na Alpha Bisimba! Ikihitajika tafsiri yake kwa kiswahili tutafanya kwa manufaa ya umma.
 
Last edited by a moderator:
Ni ajabu kudai umelipa deni lisilokuwepo, huu ni mwendelezo tu wa wizi. Kabla waropokaji hawajaanza kutoa kauli za ajabu ajabu, naomba mjue kuwa upo wakati madeni yote yalisamehewa tukaanza upya on a clean slate!

Naam mkuu,

Kama kumbukumbu zangu ziko sawa ni wakati wa sera Ben Mkapa ya UBINAFSISHAJI. Ilifikia kipindi wakati Mr Clean akijiandaa kustaafu kwa majigambo makuu akasema "Ndege ya uchumi wa Tanzania iko kwenye runway tayari kwa kupaa"..!!! Maweeeeeeeeee.... Laiti angejua mtu anayemfuata.....

BACK TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom