Kikwete: Nimelipa deni la taifa la 1958

Kikwete: Nimelipa deni la taifa la 1958

Akapimwe akili naona cancer imepanda kwenye ubongo
 
Mkuu, kwani madeni yaliyokopwa na serikali ya Tanganyika hayawezi kulipwa na serikali ya Tanzania? Ukilaza mwingine huu bana!

Na wasiwasi na ilo deni. litakuwa deni hewa na wizi kama escrow. Barabara ya Morogoro kama ilijengwa ni kilomita ngapi kwa wakati huo?. Pia enzi hizo Tanganyika ilikuwa mali ya Uingereza na gharama za kuendesha nchi zilitolewa na Malkia.Kuna maswali mengi kuliko majibu.Kikwete amepwaya na kuwa mdebwedo asidanganye watu wenye akili zao.
 
Siamini kuwa kweli mwaka 1958 Mwingereza alikopa kujenga eti kutujengea Morogoro road. Iwapo reli ya kati yenyewe haikukopwa iweje Morogoro road? Sina data kwa hiyo nitanashangaa ntu.

Asije akatuambia kuwa kalipa deni la ujenzi wa reli ya kati iliyojengwa na Mjerumani mwaka 1905 tu!
 
Mama wa WAMA ndiye RAIS wa nchi hii!

AMINI USIAMINI, yule mwingine ni FUTO tuu!
 
Hapana,naomba serikali itoe maelezo ya kina!Kama ni kweli tumelipa nadhani hii itakuwa EPA nyingine,watu wametumia fursa kupiga pesa!
wataanza kumbana kuanzia hapa JF alafu akishagundua kuwa alikuwa haongei na wajukuu zake bali taifa kama kawaida utasikia ..."washauri wangu wamenipotosha"!
Sio ajabu safari hii na washauri wote wanataka kuingia ikulu wenyewe maana wamechoka kusingiziwa.


 
Kwanza huyu jamaa kwa miaka 10 kaishi angani Mwaka 1.
Ebu mtalaam wa Route za Rais wetu JK atupe idadi, kafikisha ngapi? Je kwa sasa anaongoza Rekodi ya kusafiri au yule wa Nigeria bado ni top?

Deni 2005 Trillion 7 mwaka 2015 June Deni Trillion 35!! Daah JK unasifa za ajabu ajabu!!
 
hilo deni la mwaka 1958 litakuwa liliachwa na mkolini muingereza. Kumbe tanganyika tulianza kukopa hata kabla ya uhuru
 
wataanza kumbana kuanzia hapa JF alafu akishagundua kuwa alikuwa haongei na wajukuu zake bali taifa kama kawaida utasikia ..."washauri wangu wamenipotosha"!
Sio ajabu safari hii na washauri wote wanataka kuingia ikulu wenyewe maana wamechoka kusingiziwa.




Mkuu uko sawa kabisa maana mpaka sasa nadhani waliochukua fomu wamefikia 39.Idadi hii ni tafsiri tosha ya udhaifu wa Raisi kama ulivyo tajwa -Mbunge.Na kwa bahati nzuri kweli kijana anajua kuna kitu kwenye maisha inaitwa unafiki ni mwiko.
Haiwezekana nafasi adimu na ya muhimu kama Uraisi ionekane kila mtu anaweza-kuna haja ya kuiangalia kisayansi hili jambo.
 
Inawezekana ktk issue kuna watu wamefanya ufisadi. Watu wanatafuta madeni yasiyo na wenyewe kama epa na escrow kisha wanapiga hela ndefu. Nakubaliana na Makongoro kuwa tatizo si kikwete bali vibaka wanaomzunguka!
 
Rais Kikwete amesema serikali imelipa deni lilikopwa mwaka 1958 ambalo lilitumika kuijenga Morogoro Road.

Amesisitiza hakuna nongwa yoyote kwa madeni anayoacha kuja kulipwa na mrithi wake.

Amemalizia kuwa duniani kote ili nchi iendelee ni lazima ikope kama ilivyo kwa wafanyabiashara ili kukua lazima utakopa.

Chanzo: ITV habari
Aisee
Nilikuwa nimeacha kunywa pombe.
Wapi naweza pata whisky nzuri na Country music kwa mbaali
 
Hakuna mtu anaekataa serikali kukopa, ila mkopo huo umetumika vipi.
Huyu jamaa ni failure wa kila kitu, aondoke tu akapumzike zake.
 
Hii kauli huwa naishangaa sana. Unajua Mgabe ameiingiza Zimbabwe shimoni? Si kila udikteta ni mzuri. Actually madikteta wengi huziua kabisa nchi; angalia Congo ya Mobutu, Zimbabwe ya Mugabe, Africa ya kati ya Kina Bocassa, Nigeria ya kina Sani Abacha. Tuwe waangalifu sana. Tunachanganya udikteta na uzalendo. Zimbabwe leo hii kama huna business ya kukuletea American Dollar huna maisha - Mugabe akiwadanganya eti anapambana na wazungu.

Tuache kulilia udikteta, hapo tunalilia kisu kitakachotuchinja! Udikteta haufai kabisaa. Kumbuka wakati wa Mkapa; ununuzi wa rada na rushwa zake, Ununuzi wa Ndege ya rais na rushwa zake, EPA ilifanyika wakati wa Mkapa, Kuanzisha Kampuni from Ikulu. Mkapa angekuwa bado rais leo hii, yeye na genge lake wangekuwa mamilionea kwa rushwa za mtindo huu. Na genge lake ndo hao tunawaona wakijiandaa kuingia Ikulu kwa nguvu zote!!! God forbid.

sijafananisha utendaji wa mkapa na mugabe ila nimesema endapo angeendelea kudumu madarakan kama mugabe tungekuwa mbali kwani utendaji wa mkapa ni mzuri na naamin endapo angeendelea had sasa haya madudu ya jk yasingekuwepo kwa kiasi hiki halafu mbona hujamzungumzia kagame na mafanikio yake
 
sijafananisha utendaji wa mkapa na mugabe ila nimesema endapo angeendelea kudumu madarakan kama mugabe tungekuwa mbali kwani utendaji wa mkapa ni mzuri na naamin endapo angeendelea had sasa haya madudu ya jk yasingekuwepo kwa kiasi hiki halafu mbona hujamzungumzia kagame na mafanikio yake

Madudu ya Kikwete ni mwendelezo wa madudu ya mkapa. Nimekutolea mifano ya Ununuzi wa rada na rushwa zake za wazi wazi, ununuzi wa ndege ya rais, EPA; yoote haya yalikuwa wakati wa Mkapa. Tena Mkapa aliingia katika historia kwa kuanzisha kampuni akiwa Ikulu na rekodi zipo. Sasa ni madudu gani ya JK ambayo unaona yasingekuwepo kwa udikteta wa mkapa?
 
Rais Kikwete amesema serikali imelipa deni lilikopwa mwaka 1958 ambalo lilitumika kuijenga Morogoro Road.

Amesisitiza hakuna nongwa yoyote kwa madeni anayoacha kuja kulipwa na mrithi wake.

Amemalizia kuwa duniani kote ili nchi iendelee ni lazima ikope kama ilivyo kwa wafanyabiashara ili kukua lazima utakopa.

Chanzo: ITV habari
Sijui hayo madeni ya kale yamelipwa kwa hela ipi, wakati madeni ya ndani yameshindikana mwaka wa tatu sasa!
 
Naam mkuu,

Kama kumbukumbu zangu ziko sawa ni wakati wa sera Ben Mkapa ya UBINAFSISHAJI. Ilifikia kipindi wakati Mr Clean akijiandaa kustaafu kwa majigambo makuu akasema "Ndege ya uchumi wa Tanzania iko kwenye runway tayari kwa kupaa"..!!! Maweeeeeeeeee.... Laiti angejua mtu anayemfuata.....

BACK TANGANYIKA

Alikwenda mbele zaidi na kusema kuwa "Anatuachia uchumi unaopaa". na watu wengi walikubaliana naye kwa wakati ule. Good enough Kikwete alipoingia alisema "Rais anayeondoka alijenga msingi, mimi kazi yangu itakuwa ni kujenga ukuta. Huo ukuta wa Kikwete sijui kama kuna mtu ameuona .......... Labda alikuwa anatujengea ukuta wa madeni.

Wote tunakubali kukopa ni kawaida .... lakini kukopa bila mpango au kutumia pesa ya mkopa hovyo ndiyo kitu kibaya!! Cha kujiuliza hapa, je pesa zetu za mikopo tumezitumia vizuri!!??Isije kuwa ndiyo hizi hizi pia wanazozitumia kulipana mafao ....!!
 
hilo deni la mwaka 1958 litakuwa liliachwa na mkolini muingereza. Kumbe tanganyika tulianza kukopa hata kabla ya uhuru

Mkuu mwingereza hukufanya lolote! Miundo mingi ilitengenezwa na mjeruman akishirikana na mmisionari
 
Back
Top Bottom