Kikwete: Nimelipa deni la taifa la 1958

Kikwete: Nimelipa deni la taifa la 1958

labda tulikuwa tubilioni tutanotu ndo maana aliweza kulipa
 
Sorry deni la 1958??? Nani alikopa kwa niaba ya watanganyika?? Je tulipaswa kulipa maana tulikua chini ya mkolon..
 
Mkapa alivyokuwa anasema analipa madeni alikuwa analipa ya mwaka gani sasa?
 
Mi ntakuwa wa mwisho kuamini kuwa DR.KIKWETE alimaanisha hivyo! 'za kuambiwa changanya na zako'-by PROF. KIKWETE
 
Nashangaa mpaka sasa faizafoxy hajafika hapa povu likimtoka
 
Rais Kikwete amesema serikali imelipa deni lilikopwa mwaka 1958 ambalo lilitumika kuijenga Morogoro Road.

Amesisitiza hakuna nongwa yoyote kwa madeni anayoacha kuja kulipwa na mrithi wake.

Amemalizia kuwa duniani kote ili nchi iendelee ni lazima ikope kama ilivyo kwa wafanyabiashara ili kukua lazima utakopa.

Chanzo: ITV habari

brother kachokaa anatamani hata kesho aludi msoga maana mnaona
mnamchanganya saana
 
Hivi Tukimsimamisha Kizimbani Atadai Sie Tuna Siasa Za Visasi Kweli?
 
Kama kukopa ni maendeleo basi Tz tulitakiwa tuwe mbali angalau....mikopo yetu ni kama wachache wananufaika!! Napinga kauli ya JK, kukopa YES but mikopo yenye malengo yanayo onekana, pia deni lisilo ongezeka kadri miaka inavyo kwenda!
 
Huyu mkulu mchokozi sasa! Anatulazimisha tusiyoyazoea.
Nisaidieni wanajamvi, hizi hasira zilizonipanda sasa hivi baada ya kuusoma uzi huu nizifanyeje kwani kifua kimejaa upepo na nataka kupasuka? Deni la mwaka 58! Najuta kujua kusoma.
 
Hivi Mwizi akija kuiba nyumbani kwako akakukata mapanga wewe na familia yako, akiwa anakimbia akaacha baadhi ya vifaa alivyotumia kuvunjia mlango kama mashoka, mapanga n.k,

Je, aliyeibiwa ana wajibu wa kulipia hivi vitu kwa mwizi kama mwizi alivikopa hardware store?
Je, mwizi anatakiwa kulipiwa nauli aliyokopa ya kuja kukuibia nyumbani kwako?

Waingereza na wajerumani ni wezi, wametok aulaya na vifaa vya kuja kutuibia rasilimali zetu, ili kufanikisha wizi huo walikopa huko walikotoka kwa wayahudi n.k (wajerumani madeni ya wayahudi yaliwashinda wakaanzisha world war II), sasa mikopo ya hawa wezi wa rasilimali zetu kwa nini tulipe sie tulioibiwa?inaingia akilini kweli?

Hatukuwatuma wakakope ili kuja kufanikisha wizi wao. Kumbukeni, hizi barabara na reli walizojenga wakoloni, zilikuwa na dhumuni moja tu, kukusanya kila kinachoibika Africa na Tanzania na kukihamishia Ulaya.

Sasa Kuna mantiki gani sisi kulipa madeni ya hawa wezi wetu?
 
tayari kuna harufu ya ufisadi mkubwa sana sehemu au kuna siri za ufisadi zipo karibuni kuwekwa hadharani. Watu wanaanza kutafuta vichaka vya kujifichia. Nawashauri ccm waache sera yao ya kuomba mdahalo please please hali si shwari maeneo fulani fulani
 
swali hili hawezi jibu amezoea kukopa kwa ajili ya matanuzi

President Kikwete niko tayari kukulipa studio tukarekodi ngoma moja kali studio. Huyu jamaa ni zaidi ya msanii wa maigizo. Alafu chini ya mkapa madeni yote ya Tanzania yalifutwa kwahiyo asitudanganye hata kidogo.
 
Ni ajabu kudai umelipa deni lisilokuwepo, huu ni mwendelezo tu wa wizi. Kabla waropokaji hawajaanza kutoa kauli za ajabu ajabu, naomba mjue kuwa upo wakati madeni yote yalisamehewa tukaanza upya on a clean slate!

Yaani Kabla ya uhuru mkoloni alikopa Demi akatuachia Sisi tulipe? Au ulimi umeteleza kama aliyesema Saddam alikuwa Rais wa Kuwait?
 
Mwaka 1958 barabara ya Morogoro ilikuwa vumbi tupu. Lami ilikuwa Tanga mpaka Korogwe ya DUMIZ. Labda1985
 
Back
Top Bottom