Gama na Wana JF,
Kabla ya kuchangia kwanza napenda kujua chanzo cha habari hii(source of info.) imeanzia wapi? Haya maneno JK kayatamka wapi na lini?
Hata hivo kama ni ya kweli basi JK na CCM yake wanaweza kuwa wamesha anza kuandaa mtu wao ambaye kwa hivi karibuni hata media zimemtaja Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Mhe. Januari Makamba kuhusishwa na kinyang'anyiro hicho! Inawezekana kabisa kuwa CCM wameshaona nguvu kubwa iko kwa Vijana na ndio walio wengi kwa asilimia katika Wapiga Kura wa nji hii!
Kwa mtazamo wangu kama CCM watakuwa na mpango huo watakuwa wanajidanganya sana. Kwanza kwa utamaduni tuliojiwekea Watz mpaka sasa lazima kuwe na usawa katika kuchagua Marais kulingana na IMANI zao. Kama awamu inayomaliza ni ya MKRISTO, basi awamu inayofuata lazima iwe ya MWISLAMU au kinyume chake.
Tunajua Rais JK ni Mwislamu kwa hiyo tunategemea kuwa piga Ua Rais ajaye LAZIMA AWE MKRISTO. Hii ni lazima na siyo hiari. Hata kama CCM watapendekeza mgombea wao kwa mwaka 2015 lazima awe MKRISTO. Nchi hii haina DINI lakini kwa hekima,busara na maarifa yaliyoachwa na Waasisi wa Taifa hili, kubadilishana kwa watawala toka katika hizi imani 2 ni ya msingi na lazima. Kwa mantiki hiyo basi,kama JK anamaanisha kurithiwa na Januari Makamba amabye ni Mwislamu atakuwa anataka kuchochea vurugu ambazo hatutaki kuziona hapa Tanzania. Awe ni Zitto kutokea CCM au CDM madhali ni Mwislamu Watz hatutaki na hatutaelewa.Hatutaki CCM watuchagulie Rais awe kijana au Mzee na hasa kama atakuwa MWISLAMU.
Tunataka CCM na vyama vingine waelewe hivo kuwa swala la kupokezana kwenye Urais lipo hata kama halijawekwa kwenye Katiba ya JMT. Sanduku la Kura ndiyo litatupa Rais wa nji hii awe mzee au kijana na kutoka chama chochote isipokuwa CCM na lazima awe Mkristo. Hatutaruhusu Nchi hii iongozwe na Marais Waislamu kwa Awamu mbili mfululizo kwani kufanya hivo ni kutaka kuifanya nchi hii ionekana ni nchi ya Kiislamu! Kutawaliwa na Rais wa Kiislamu au Kikristo kwa miaka 20 mfululizo inaweza kuanzisha mzozo wa Kikatiba usio wa Lazima. Tunaomba hili liepukwe mapema.
Nina hakika Watanzania kwa mamilioni,vijana kwa wazee wanataka kuona mageuzi ya kweli ndani ya nji yao. Watz wameshachoka na CCM, chama ambacho kwa zaidi ya miaka 50 kiko madarakani lakini ustawi wa Watanzania unazidi kudorora na kuporomoka siku hadi siku pamoja na nchi hii kuwa imezungukwa na Raslimali lukuki.
Wasalaamu