Kampeni hii ya Sifa ya ujana, mbali ya kwamba inabeba dhana ya ubaguzi lakini pia inabeba dhana ya uoga na hofu!
Hiyo ni mbali na mkakati mwingine ulioko nyuma ya mapazia.
Wanaoipigia chapuo kama ndiyo sifa kubwa ya wao kufanikisha tamaa, uchu wa kuwa blockers wa kisiasa, (naamini akina Warioba na Salim hawamo katika hila hizo) wanasumbuliwa na mambo hayo!
Naona hiki kikampeni kimefufuliwa tena. Kilikufa kifo cha mende wakati fulani hasa baada ya Mzee Butiku kuwalipua pale Ukumbi wa Nkrumah, UDSM!
Ilikuwa baada ya wanazuoni makini na mahiri vijana kama Sabatho Nyamsenda, Bashiru Ally et all kuandika kwa details na kuonesha ubaguzi huo wa kukimbilia ujana eti sifa ya kupambana na watu wengine wenye umri mkubwa wenye sifa za uongozi lakini wanawatia kiwewe vijana.
Ilikuwa ni baada ya wananchi kuendelea kuonesha imani kubwa na watu wengine badala ya watu wanaojigamba kwa sifa ya ujana pekee huku wakiwa wameharibikiwa kweli kweli kwenye sifa za msingi za uongozi.
Nao wanajua kuwa jambo pekee wanaweza kujivunia nalo ni umri, mbali ya hapo ni questionable tu!
Waambieni wafanye Kazi, wafuate ushauri wa Butiku. Ujanja ujanja huu hautasaidia.
Hakuna mahali panasema Mwalimu Nyerere, Warioba na Salim walifanya vizuri kwa sababu walikuwa vijana unless mnataka kusema walipoongezeka umri waliboronga katika nafasi zao! Jambo ambalo si kweli kwa sababu hao hao tumewaona wakifanya mambo makubwa zaidi ya uongozi uliokomaa wakiwa umri mkubwa wa kutosha kuitwa wazee!