Kikwete: Nataka kurithiwa na rais kijana!

Kikwete: Nataka kurithiwa na rais kijana!

Ikumbukwe kuwa Zitto ni representative ya vijana WASILITI,WAOGA na WABINAFSI!Aidha kijana mwingine anayepigiwa chapua J.Makamba alikuwa akitoza dola 500 mpaka 1500 kama kiingilio cha kuonana na rais IKULU.Vilevile ana kashfa ya kuiba paper pale Galanos Sec(Galax).Nawaonjesha tu wale fata upepo.sioni kijana mwenye credibility.Chama changu nakitakia malezi mema kwa J.Mnyika na Tundu Lisu hawa ni wazalendo

John Mnyika hawezi hata kuwa Waziri. Umesahau kuwa alifeli Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam? Huyo hana tofauti na mwenyekiti wake Mr. Zero
 
1. Awe kijana
2. Awe ni rais atakayeliunganisha taifa
3. Awe anaijua historia ya nchi yake vizuri kwa maana ya ilikotoka, iliko na inakokwenda
4. Awe na uwezo wa kufanya uamuzi mgumu kwa ajili nchi yake.
5.Awe tayari kuondoa matabaka yaliyoko nchini(ukabila, udini n.k

Akifafanua sifa ya ujana ZITTO alitolea mfano viongozi wa Tanzania waliopewa nafasi za uongozi wakiwa vijana na kufanya vizuri kuwa ni pamoja na JULIUS NYERERE, Jaji Mstaafu Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim.

ZITTO KABWE anaungana na Jaji Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim Katika mtazamo wa Rais ajae kuwa Kijana.

source: jambo leo

ha ha ha

source: jambo leo

hivi katiba ya nchi inasemaje? ... qualifications za kuwa rais ni miaka 21 - 45 au? waache kutuzingua! kila mtu ana uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa ili mradi atimize vigezo vilivyowekwa na katiba ya nchi!
 
Ikumbukwe kuwa Zitto ni representative ya vijana WASILITI,WAOGA na WABINAFSI!Aidha kijana mwingine anayepigiwa chapua J.Makamba alikuwa akitoza dola 500 mpaka 1500 kama kiingilio cha kuonana na rais IKULU.Vilevile ana kashfa ya kuiba paper pale Galanos Sec(Galax).Nawaonjesha tu wale fata upepo.sioni kijana mwenye credibility.Chama changu nakitakia malezi mema kwa J.Mnyika na Tundu Lisu hawa ni wazalendo

Akili yako imetunzwa kwenye makabati ya ufipa... hatutaraji uchangie cha maana zaidi ya upuuzi...
 
Kampeni hii ya Sifa ya ujana, mbali ya kwamba inabeba dhana ya ubaguzi lakini pia inabeba dhana ya uoga na hofu!

Hiyo ni mbali na mkakati mwingine ulioko nyuma ya mapazia.

Wanaoipigia chapuo kama ndiyo sifa kubwa ya wao kufanikisha tamaa, uchu wa kuwa blockers wa kisiasa, (naamini akina Warioba na Salim hawamo katika hila hizo) wanasumbuliwa na mambo hayo!

Naona hiki kikampeni kimefufuliwa tena. Kilikufa kifo cha mende wakati fulani hasa baada ya Mzee Butiku kuwalipua pale Ukumbi wa Nkrumah, UDSM!

Ilikuwa baada ya wanazuoni makini na mahiri vijana kama Sabatho Nyamsenda, Bashiru Ally et all kuandika kwa details na kuonesha ubaguzi huo wa kukimbilia ujana eti sifa ya kupambana na watu wengine wenye umri mkubwa wenye sifa za uongozi lakini wanawatia kiwewe vijana.

Ilikuwa ni baada ya wananchi kuendelea kuonesha imani kubwa na watu wengine badala ya watu wanaojigamba kwa sifa ya ujana pekee huku wakiwa wameharibikiwa kweli kweli kwenye sifa za msingi za uongozi.

Nao wanajua kuwa jambo pekee wanaweza kujivunia nalo ni umri, mbali ya hapo ni questionable tu!

Waambieni wafanye Kazi, wafuate ushauri wa Butiku. Ujanja ujanja huu hautasaidia.

Hakuna mahali panasema Mwalimu Nyerere, Warioba na Salim walifanya vizuri kwa sababu walikuwa vijana unless mnataka kusema walipoongezeka umri waliboronga katika nafasi zao! Jambo ambalo si kweli kwa sababu hao hao tumewaona wakifanya mambo makubwa zaidi ya uongozi uliokomaa wakiwa umri mkubwa wa kutosha kuitwa wazee!

bro Makene asante sana kwa kutoa clarification nzuri tena yenye vision sahihi.
 
mimi napendekeza 40 hadi 45, hao wazee basi jamani.

Malawi wana Rais ana miaka 74 kachaguliwa mwezi May, anayarajiwa kuogoza miaka 10.
Zambia ana miaka 72.
Zimbabwe ana miaka 85+
Afrika kusini ana miaka 68+
Msumbiji anazaidi 70+

Nchi nyingi za Afrika na Ulaya zina maraisi wana 60+.
Sio Tatizo kwa hapa kwetu kuwa na Rais kama Samwel Sitta(73).
Stephen Wassira (68)
Lowassa(68)
Slaa (69)
Vijana acheni kupagawa. Wazee wana nafasi kubwa ya kuongoza kuliko vijana.
 
Makene ni kweli kwamba kila alisemalo ZITTO kwenu ni usaliti, Ubaguzi na kuwa na kitu nyuma ya pazia, lakini haya WARYOBA , SALIM AHAMED SALIM nao ni wasaliti? Lakini swali la msingi sifa ya kijana ikiwa na mashiko mnachohofu nini? CHADEMA hamna vijana wa kushndana na vijana wa vyama vingine?

Unataka kutuambia akichaguliwa kijana 100% anafaaa?

Kigezo hakiwezi kuwa umri maana probability ya ufanisi kuwa kiongozi bora haizingatii ujana kukupa reliability ya 100%

-Anaweza kuwa kijana akafanya vizuri na pia upo uwezekano akawa kijana akabolonga

-Anaweza kuwa mzee akafanya vizuri na pia upo uwezekano akawa mzee akabolonga

Hivyo uzee au ujana hauwezi kuwa sifa yakumpitisha mtu eti anafaa lazima awenasifa nyingi zingine ambazo kijana

anaweza asiwenazo mzee akawanazo.
 
Nakuunga mkono,hoja ya ujana,katika nafasi kubwa ya kuongoza nchi ni upumbafu mtupu,tunahotaji Rais makini,tena kwa upande wetu ccm,huyu atakua Mwenyekiti wa chama anahitajika mtu makini anayekijua chama chetu vema na kujua mahitaji halisi ya watanzania

Of course kwa hapa tulipofikia CCM ni sehemu ya matatizo na pia ni tatizo kubwa ndani ya nchi hii which means hatutegemei mtu atayechukua nafasi hiyo atoke CCM!

Hapa tulipokwama hatuwezi kunasuka kwa kuendelea na CCM! Tutakuwa tumeongeza kiwango cha ujinga na kutojitambua!

Wenye kampeni hii wanataka kuuzia watu mbuzi kwenye gunia kwa namna ile ile walivyofanya mtandao walipomvika Kikwete sifa za UJANA.

Nani asiyejua kuwa Kikwete aliingia kwa gia na sifa ya ujana!!!??? Leo hii hali ikoje?
 
Hii hoja ya ujana haina mashiko,namshauri Zitto aachane nayo.

Si hoja yenye nguvu hasa mbele za watu makini kama aataka uongozi na aanze kupambana kuupata lakini si kwa hiyo hoja dhaifu...Mkuu Makene Umeongea Vizuri pia...

Si unaona mtu kama Mnyika kijana mdogo kanunuliwa na Mbowe na Dr Slaa kuwaangamiza kisiasa vijana wenzake,sasa mtu kama huyo Ujana umemsaidia nini zaidi ya kuwa Mchawi tu

Huyo January mwenyewe kafanya lipi mpaka kufika hapo zaidi ya kujificha kwenye meza za ofisi za Ikulu na kumuandikia Rais hotuba za Ovyo kabisa...
 
Malawi wana Rais ana miaka 74 kachaguliwa mwezi May, anayarajiwa kuogoza miaka 10.
Zambia ana miaka 72.
Zimbabwe ana miaka 85+
Afrika kusini ana miaka 68+
Msumbiji anazaidi 70+

Nchi nyingi za Afrika na Ulaya zina maraisi wana 60+.
Sio Tatizo kwa hapa kwetu kuwa na Rais kama Samwel Sitta(73).
Stephen Wassira (68)
Lowassa(68)
Slaa (69)
Vijana acheni kupagawa. Wazee wana nafasi kubwa ya kuongoza kuliko vijana.

Mambo ya kuwa na Rais anayesinzia akiwa mkutanoni kama Wasira, ambaye mwili umeishachoka kama Lowassa, na anayevalishwa pampus ya kujikojolea kama Sata wa Zambia hatutaki.
 
Makene ni kweli kwamba kila alisemalo ZITTO kwenu ni usaliti, Ubaguzi na kuwa na kitu nyuma ya pazia, lakini haya WARYOBA , SALIM AHAMED SALIM nao ni wasaliti? Lakini swali la msingi sifa ya kijana ikiwa na mashiko mnachohofu nini? CHADEMA hamna vijana wa kushndana na vijana wa vyama vingine?
TataMadiba

Jina la tata ninakotokea maana yake ni baba! Nilitarajia uwe umenisoma vizuri kabla ya kuninukuu na kujenga hoja yako mkuu!
 
Last edited by a moderator:
1. Awe kijana
2. Awe ni rais atakayeliunganisha taifa
3. Awe anaijua historia ya nchi yake vizuri kwa maana ya ilikotoka, iliko na inakokwenda
4. Awe na uwezo wa kufanya uamuzi mgumu kwa ajili nchi yake.
5.Awe tayari kuondoa matabaka yaliyoko nchini(ukabila, udini n.k

Akifafanua sifa ya ujana ZITTO alitolea mfano viongozi wa Tanzania waliopewa nafasi za uongozi wakiwa vijana na kufanya vizuri kuwa ni pamoja na JULIUS NYERERE, Jaji Mstaafu Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim.

ZITTO KABWE anaungana na Jaji Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim Katika mtazamo wa Rais ajae kuwa Kijana.

source: jambo leo
Amesahau sifa ya usaliti
 
Ujana sio hoja hata kidogo katika utendaji uliotukuka katika kuongoza nchi. Mzee kama Warioba (ni mfano tu) waweza kumlinganisha na mtu kama January Makamba? Kuendesha nchi ni kitu kikubwa mno ambacho kinaendana na maono ya ndani sana ambayo yanahusisha maisha ya mamilioni ya watu. Kipindi hiki cha miaka 9 iliyopita tumejifunza mengi sana kuhusu nafasi hiyo na umuhimu wake katika maisha ya waTZ na maamuzi yetu ya 2005 tumejitambua kuwa yalikuwa sahihi au tulikosea.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Tuache huu "UPUMBAVU" wa kujificha nyuma ya ujana kama nafasi ya kupata uongozi. tukienda hivi hatutolifikisha hili taifa popote. watu 2005 walichagua sura, kilichotokea tunakijua.
 
1. Awe kijana
2. Awe ni rais atakayeliunganisha taifa
3. Awe anaijua historia ya nchi yake vizuri kwa maana ya ilikotoka, iliko na inakokwenda
4. Awe na uwezo wa kufanya uamuzi mgumu kwa ajili nchi yake.
5.Awe tayari kuondoa matabaka yaliyoko nchini(ukabila, udini n.k

Akifafanua sifa ya ujana ZITTO alitolea mfano viongozi wa Tanzania waliopewa nafasi za uongozi wakiwa vijana na kufanya vizuri kuwa ni pamoja na JULIUS NYERERE, Jaji Mstaafu Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim.

ZITTO KABWE anaungana na Jaji Joseph Waryoba na Salim Ahamed Salim Katika mtazamo wa Rais ajae kuwa Kijana.

source: jambo leo
Nafikiri watu wanamnukuu Mzee Warioba 'out of context'. Sidhani kama alimaanisha ujana wa umri ndiyo sifa kuu ya kubeba Rais ajaye. By the way hata China wanapomchagua wa miaka 55 humwita 'kijana'
 
Mkuu hatutamchaguwa mtu kwa

Dini yake

Kabila lake

Rangi yake

kanda atokayo

Tutamchaguwa mtu yeyote kuwa kiongozi wetu kwa kuzingatia uwezo wake kukabilina na changamoto zinazotukabili

-Uchumi mbovu

-Elimu duni

-Afya duni

-Ukosefu wa ajira hususani vijana

-Miundombinu duni, Reli, ndege za abiria na mizigo, barabara

-kuutokomeza ufisadi kabisa na vibaraka wake

-Kuutokeza udini na ukabila ambao umepaliliwa na kuchipuwa kwa kasi kubwa

-Kurejesha umoja na mshikamano kwa watanzania wote.

nk.

Hivyo suala la dini ya mtu halina nafasi maana hatuhitaji, paster, shekhe au mchungaji kutuswalisha au kutusalisha.

CCM hawawezi kufanya hayo yote hapo juu, maana wamekuwa madarakani zaidi ya miaka 50, badala ya kuboresha hali inazidi kuwa mbaya zaidi. Kwamaana hiyo iwe ni kijana au mzee kama atatokea ccm hakuna lamaana kutendeka maana mfumo utabaki kuwa uleule kulinda maslah ya wajanja wachache wakitumia mongo wa kiasiasa na ujana kuwaburuza wajinga.
 
Kwangu mimi sifa kuu ni moja tu...asiwe CCM!

Nadhani wewe umetoa jibu sahihi la utata huu. Hata tukiazimwa Malaika aje aongoze kwa muda lakini akasimama kwa tiketi ya hicho chama matatizo yataendelea kuwa yale yale.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Nitakuwa wa mwisho kuungamkono Rais kijana,hawa wakina King Mswati na kale kajamaa ka Korea kaskazini aka mzee wa kiduku,vijana bado sana,anyway napita tu bhana.
 
Back
Top Bottom