Kikwete: Nataka kurithiwa na rais kijana!

Kikwete: Nataka kurithiwa na rais kijana!

Kwa performance hii ya JK hana sifa ya kuwachagulia Watanzania Rais ajaye.
 
Nadhani tutakosea sana tena sana kwa kuchagua mtu awe Rais awe mwenyekiti wa serikali za mtaa kwa kuangalia umri, tabasamu na hata hiki kinachoitwa 'mtu wa watu'. Kwangu mimi nategemea kamaa jamii na kama taifa, tuorodheshe matatizo ya msingi yanayotugusa na sababu zake then ndio tutafute ni mtu gani anaweza kutatua matatizo hayo. Nimetaja 'sababu za matatizo' maana tunaweza kumpata kiongozi kijana au mzee kumbe akawa ni source kama sio part of the problems tunazotaka zitatuliwe. Na sijui watu wanapata wapi ujasiri kwa kuongelea urais kwa kigezo cha ujana! Mwaka 2005 tulisikia sana habari za 'ujana' na 'mtu wa watu', sasa hivi tuko wapi?
 
Kumbe kuna watu bado wanasikiliza kauli za huyu jamaa! Funny stuff...
Kinachoniudhi ni jinsi Zitto anavyojipendekeza kwa huyu bwana kama vile hakucheza rafu 2010!
Najua tofauti ya siasi haitakiwi kuwa chuki, lakini mtu anapoiba kura alafu ukakenue kenue naye...huo ni UPUMBAVU!
 



Mimi Mwanakijiji*Nadhani, mjadala huu una sehemu kama tatu tu; kwanza ni suala la rika (siyo umri) ambalo JK amelizungumzia lakini la pili nafikiri ni kauli yenyewe ilivyokuwa ni very definitive - "msikubali" inapotolewa na mtu mwenye cheo na hadhi ya Rais*ni muhimu kuipa uzito unaostahili kwa hiyo si sawa na mtu mwingine kusema "msikubali". Tatu ni hiyo element ya "msikubali" ndio nadhani kimegomba kidogo. Ndio maana niliporeact mwanzoni nilisema ni "kauli ya kupuuzia" kwa sababu kwa mbali inaonekana nzito lakini ukiianaglia kwa karibu utaona kuwa haina msingi wala mantiki na kwa kweli ni nyepesi sana kiasi cha kuweza kutolewa na Rais. Hata hivyo, kubwa la kuangalia ni uwezo, tukipata kiongozi kijana mwenye uwezo na ameweza kutushawishi ana uwezo ni jukumu letu kusimama nyuma yake na kumuunga mkono. Lakini vile vile tukipata mtu wa makamu mwenye uwezo na akatushawishi ana uwezo ni jukumu letu vile vile kusimama nyuma yake. Swali litakuwa je akisimama kijana anayeonekana ana uwezo na mzee anayeonekana mwenye uwezo nani tusimame nyuma yake? Well - mwenye uwezo zaidi! Ujana si dawa, na uzee si kosa!

Duh.......haya ndiyo mamabo ambayo tumetajadili kwenye post za nyuma lakini watu wengine hawataki kufikiria huko.Kazi ipo hasa pale ambapo hata the enlightened ones wanapo-argue katika line ya kawaida kabisa.Taifa letu kumbe liko taabani kiasi hiki?
 
Watu wanajua sana kuutumia uwezo wao vibaya.Watagombea huko NCCR na taaraifa nilizo nazo wabunge vijana NCCR wameweka mkakati wa kuteka vijana na vyuo vikuu.Sasa Ben ni kwa nini asishirikiane na Bavicha hii kukabiliana na hawa watu.Ben kaka'angu una kipaji cha pekee kushawishi.Upo mioyoni mwa vijana wa BAVICHA waliokuwa upande wako na asilimia kubwa hawakuridhishwa na mwenendo wenu na hasa uamuzi wako dakika za mwisho na pia hawakuridhika na maamuzi yaliyochukuliwa na kamati ya wazee ya kuwaengua.Lakini ninakusihi tuangalie yajayo.Hao akina Zitto ni msala upitao.wanajua kwa vyovyote vile wewe ni majeruhi wa maamuzi yale kwa hiyo ni lazima wakuvutie kwao na mimi nanvyoona hali itakuwa tete huko baadae



Acha kizebuzebu wewe umekurupuka,afadhali mwenzako anaandika kijanja na anajenga hoja zenye ushawishi.acha ushabiki shibuda anakuharibu.shirikana na wenzako kujenga chama.nendeni Nccr bwana kule ukosoaji unaruhusiwa.wewe ni pandikizi la ccm nani asiyekujua?



Haya Ben,nimekanusha kauli yangu.Mnaudhi sana ndiyo maana wengine hata tunakaribia kutukana hadaharani.Maelezo yako ni mazuri na yanavutia ili kujenga uhalali wa kile mnachokifanya
ole wenu kwenye uchaguzi ujao wa mwenyekiti wa chama mkivuruge chama,ya chacha wangwe historia itajirudia.wenzako walihusika hatua zote na ni lazima iwarudie.sasa wewe kaka'angu ni kijana mdogo tuliza boli.ujasiri ukipita kiasi unakufanya hata ujiingize kwenye mdomo wa simba kwa kujiamini kupita kiasi

watu kama wewe sina muda wa kupoteza kuwaelimisha, maana jina kivuli, ona unavyoropoka.
Siwezi kuongea na mtu asiye na uwezo wa kujenga hoja, badala yake unakurupuka na kutaja midodono iliyojaa hilani mwako.
uliteuliwa na nani kufanya kazi hii? tafadhali tuheshimiane siko kama unavyotaka niwe.
wanijua kwa jina hata sura, ila mimi sikjui hata kwa ghundeya ujitambulishayo kwayo.
Stay away from my mouth...please.
Mimi pandikizi sio, endelea bt i promis.. i wl knw you, na hapo ndipo nitajibu kwa vitendo...i promis..
Wewe manachama halali endelea kufanya kazi yako, kila la kheri.
 
kwa hiyo wapige kura watu walio 40+?
au tuwe na rais mwenye miaka 18?

Duh.. lugha yetu ngumu. Ninasema, tukiweka mfumo kwamba mtu mzima ni yule wa kuanzia miaka 18 na ya kwamba mtu huyo (akiwa na miaka 18) anaweza kugombea uongozi wowote (Ubunge kwa mfano) sioni sababu kwanini mtu huyo huyo mzima asiwe na haki ya kugombea nafasi ya juu kabisa? Hatuchagui mfalme sisi bali Rais na kama wananchi katika haki yao wameamua kumchagua mtu wa miaka 25 kuwa Rais kwa sababu wanaamaini ana uwezo na atawaongoza vizuri kuliko walio wakubwa wake kiumri, why not?
 


Duh.......haya ndiyo mamabo ambayo tumetajadili kwenye post za nyuma lakini watu wengine hawataki kufikiria huko.Kazi ipo hasa pale ambapo hata the enlightened ones wanapo-argue katika line ya kawaida kabisa.Taifa letu kumbe liko taabani kiasi hiki?

Embu jifafanue.. sijakupata. Labda kuna mahali nafanya makosa kwenye hoja yangu.
 
watu kama wewe sina muda wa kupoteza kuwaelimisha, maana jina kivuli, ona unavyoropoka.
Siwezi kuongea na mtu asiye na uwezo wa kujenga hoja, badala yake unakurupuka na kutaja midodono iliyojaa hilani mwako.
uliteuliwa na nani kufanya kazi hii? tafadhali tuheshimiane siko kama unavyotaka niwe.
wanijua kwa jina hata sura, ila mimi sikjui hata kwa ghundeya ujitambulishayo kwayo.
Stay away from my mouth...please.
Mimi pandikizi sio, endelea bt i promis.. i wl knw you, na hapo ndipo nitajibu kwa vitendo...i promis..
Wewe manachama halali endelea kufanya kazi yako, kila la kheri.

Mbona vitisho tena mkuu, Miss P. yeye ametoa maoni yake na wewe toa maoni yako bt si kumwambia i promic u. Cjui nikikujua nitafanya kwa vitendo! Vitendo gani hivyo?funguka mkuu ucjitake kuleta mambo ya Al Qaeda hapa.

Acha kutisha watu bwana hapa kila mtu yupo huru kutumia Jina apendalo so huwez kulazimisha member yoyote humu aweke jina lake, kauli uliyotoa hapa ww hufai hata kuwa baloz wa mtaa mana unaendekeza visasi.
Ni mtazamo tu.
 
Embu jifafanue.. sijakupata. Labda kuna mahali nafanya makosa kwenye hoja yangu.
Mwanakijiji,

Hujafanya makosa.Hayo uliyoyaelerza ukipitia kwenye rekodi ya post zangu huko nyuma hayatofautiani na hilo nililo-quote hapo juu(yanashabihiana).

Sasa nashangaa ni kwanini wengine hawawezi ku-reason katika context hiyo....
 
Embu jifafanue.. sijakupata. Labda kuna mahali nafanya makosa kwenye hoja yangu.
Hata mimi bado sijampata mkuu,ila wakuu kwanini mods mmebadilisha title ya hii thread? Nitawaheshimu kama hamjawa influenced na mtu.title ya mwanzo ilikuwa na mantiki yake otherwise lengo liwe ku divert mjadala! But if so kwa faida ya nani?
 
Embu jifafanue.. sijakupata. Labda kuna mahali nafanya makosa kwenye hoja yangu.
Mwanakijiji....jiulize kwanini chama cha "demokrasia" na maendeleo huwa hakina primary election kwenye urais?....kwanini kinabana viongozi vijana wasigombee uongozi wa ngazi za juu za chama? Hii ni weakness ambayo kiaina inakuwa challenged here!!,kuna viongozi wanaamini unrealistc issues kama koo saba etc...this is weird!
Kwanini,kwa mfano jiulize....John Edwards alitoa delegates wake kwa Obama during presidential primaries za '08?Kwanini ali step out na kumpa Obama na siyo Hilary?.....Je hiyo ni demokrasia pevu au hacked one?
Mbona watu mnakuwa na wasiwasi sana when the "Authority" is being challenged?...Kwani rais akichallenge vijana kuna kosa?...The whole system needs to be challenged......hebu angalia jinsi wazee wanavyopiga mbonji bungeni aaargh!!!!
 
Nimepoteza sifa eeh! Uko sahihi.......niko nje ya mada.Haya rudi kwenye mada.Hebu onyesha umakini wako kwa kuonyesha nimetoka vipi nje ya mada,hoja yako utakuwa umeipa heshima zaidi.

Duh,ati wengi wetu hatujakomaa? Ni kweli strategically hatujakomaa kama wengine unaowafahamu!



Asante kwa ushauri wako......Thank you so so so much!! If there is anything I may do for you in return, please let me know!

BTW: Do credibility a favour,waambie wanaJF ni kwa jinsi gani sitafika mbali kisiasa na kwa sababu zipi.Thank you

Ben Sababu mbona zimeshazidadavua kwa kina tu hapa! Tafuta post yangu page ya 10 hapo nime mquote Nyakarungu, usome na uyatafakari.
Wasalaam
 
Zitto Kabwe, ambaye ameweka wazi kuwa anataka kuwa Rais wa Tanzania anasema kuwa Jakaya Kikwete amemwambia yeye na Mbunge wa NCCR Mageuzi, David Kafulila, kuwa anapendelea Rais wa 2015 awe kijana. Kikwete amewataka Zitto, Kafulila na vijana wengine wajiandae kumrithi.

Source: Post ya Zitto kwenye account ya JF ya kwenye facebook yenyewe hii hapa:

Historia ya nchi hii huifahamu vizuri........................Jk kamwe hawezi kuwa na imani na walio nje ya chama chake cha mafisadi.........................na pili JK will not be our president come 2015.....................................watch my ominous words...........................
 
Mwanakijiji....jiulize kwanini chama cha "demokrasia" na maendeleo huwa hakina primary election kwenye urais?....kwanini kinabana viongozi vijana wasigombee uongozi wa ngazi za juu za chama? Hii ni weakness ambayo kaina inakuwa challenged here!!,kuna viongozi wanaamini unrealistc issues kama koo saba etc...this is weird! Kwanini,kwa mfano jiulize....John Edwards alitoa delegates wake kwa Obama during presidential primaries za '08?Kwanini ali step out na kumpa Obama na siyo Hilary?.....Je hiyo ni demokrasia pevu au hacked one? Mbona watu mnakuwa na wasiwasi sana when the "Authority" is being challenged?
Kubana viongozi vijana? From which fact bro?lazima hapo umtaje zitto! Wathungu wanasema getting the story straight is not the same as getting the fact right! Acha stori za kusikia sikia toa mifano hai! Alafu jiulize hao vijana cdm mnaozusha wanapingwa wamejileta?
 
ni heri umueleze maana anapenda siasa za kudandia sana magari ila ukweli utamuhukumu siku moja na kurudi kwetu. anawengi kweli kweli atulizeboli aacha kukimbilia asipo pajua, maana hawa niwale wakifika wasipo pajua ama kwenye giza hachelewi kugive up. si itakuwa hatari ya chama makini kama CDM?

That is why I insist that you are insincere in your discussions and whether you admit it or not you see things through a fanatic prism.

Kudandia pia ni juhudi kwani unaona ni rahisi. . . si heri ambao hawana uoga kuliko wale wanaolishwa! Kurudi kwenu?wewe na nani na ni wapi? Ndege wanaofanana pengine ndiyo huruka pamoja,kuliko nirudi huko unakosema ni bora nipiganie haki kwa kuanzisha guerrilla movement pengine huko ndiko kunakotustahili wengine tusiosujudia..........! Wewe na chama chako cha magamba unataka kuhadaa watu.Kama wewe ni kamanda kiasi hicho si ungekuja na jina lako halisi?

Stop this petty talk. No one is aware of what goes on; why not stick to the discussions on this thread? Your unnecessary name-calling and attempts at discrediting me are pathetic. You don't see me insulting you; why not just stick to the point we are addressing. There is no prize for any winner here.
 
hivi wakati mbowe anagombea uongozi wa juu hakuwa kijana enhee? Nafikiri alikuwa mzee maana hata sasa ni kikongwe! Duniani kuna mambo!
 
nimemtaja kamanda mbowe sababu kuna watu wanajiona vijana sana now na wengine vikongwe wasiofikiri!
 
Mwanakijiji....jiulize kwanini chama cha "demokrasia" na maendeleo huwa hakina primary election kwenye urais?....kwanini kinabana viongozi vijana wasigombee uongozi wa ngazi za juu za chama? Hii ni weakness ambayo kiaina inakuwa challenged here!!,kuna viongozi wanaamini unrealistc issues kama koo saba etc...this is weird!
Kwanini,kwa mfano jiulize....John Edwards alitoa delegates wake kwa Obama during presidential primaries za '08?Kwanini ali step out na kumpa Obama na siyo Hilary?.....Je hiyo ni demokrasia pevu au hacked one?
Mbona watu mnakuwa na wasiwasi sana when the "Authority" is being challenged?...Kwani rais akichallenge vijana kuna kosa?...The whole system needs to be challenged......hebu angalia jinsi wazee wanavyopiga mbonji bungeni aaargh!!!!

Kobello, mfumo wa uchaguzi unachukuliwa na chama husika; siyo vyama vyote vina mfumo wa primaries. Binafsi nilishakosoa hili siyo kwa Chadema tu bali kwa vyama vyote vya upinzani nchini na hata CCM yenyewe kwa sababu vimecopy na kupaste mfumo wa CCM. As a matter of fact, I have already argued that unless Chadema change how it gets its presidential candidate uchaguzi wa 2015 utakuwa ni vuguru match. Hata kuwa na primaries zinaweza kuwa na kugawa sana watu kuliko unavyofikiria hivyo ni lazima kubuni mtindo mzuri zaidi. Fikiria tu vimakundi vidogo vya 2005 ndani ya CCM vilivyodumu hadi leo; fikiria migogoro kidogo tu ya Chadema ilivyotengeneza makundi hadi leo - itakuwaje kwenye kugombea Urais? Tukifuata hata mtindo huo utaona kuwa bado kutakuwa na matatizo mbeleni kwa yule ambaye kundi lake litashindwa usidhani ata "step out" kirahisi hivyo, itakuwa ni mwendelezo wa vinyongo n.k

Kwani unafikiri uchaguzi wa mwaka jana haukuwa na makundi? Kama Chadema wangekuwa wote wanataka kweli kushinda na kufanya vizuri zaidi I'm telling you hakuukwa na wakati muafaka kama mwaka jana 2010. Ilikuwa ni golden chance. Sidhani kama 2015 itakuwa na nafasi kama hiyo - japo wapo wanaoamini kuwa Chadema yaweza kufanya vizuri zaidi. Idoubt it. CCM wameanza reform yao mapema zaidi kuliko nilivyotarajia wakati ndani ya Chadema reform yenyewe hata haizungumziki - at least siyo sasa hivi wanasubiri labda mwakani au 2013! Wazee kupiga mbonji na vijana kupiga zogo hakutatui tatizo. Jamani, tumekuwa na vijana wengi tu Bungeni, wengine mnaowaona ni wazee waliingia Bungeni wakiwa vijana wakituahidi mabadiliko mengi tu!

Rais hajachallenge uongozi - kauli iliyotolewa ni kauli ya kipuuzi - I really mean it kwa sababu jinsi ilivyo inaonesha kutokuwa na uwezo wa kupima vitu vya kusema. Swali kubwa ni jinsi gani ya kutengeneza mfumo mzuri wa kidemokrasia ambao utakuwa na utaratibu wa kupunguza malalamiko. Sasa hivi, we have enough ingredients vya kuleta mgongano baadaye, tumeona kwenye suala la BAVICHA na Wanawake, na tumeona kwenye UVCCM na hata kwenye UWT.

Siamini katika siasa za "Ujana Vs. Uzee".. naamini katika uwezo na vs. kutokuwa na uwezo. That is the only kitu ambacho yatupasa kuangalia. Haya ya kushabikia vijana kama ni panacea ya uongozi wetu tutauziana madudu bure. Kama wapo vijana wanaamini wanafaa kuja kushika uongozi wa taifa letu, waache wajipambanue kwa kuonesha uwezo wao kuongoza. Hili ni jambo gumu sana kutaka? I really don't care kama mtu ana miaka 23 au 30 au 50! I don't kwa sababu kama inavyosema "age is noghing but a number!". Tunataka viongozi wenye uwezo - awe 18, 40 au 90.
 
Back
Top Bottom