Kikwete mnyongeni lakini haki yake mpeni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete mnyongeni lakini haki yake mpeni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwakwasu, Feb 14, 2012.

 1. M

  Mkwakwasu Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karibia watu wote niliowahoji wanadai Jk hajafanya lolote la maana kama kiongozi wa nchi.

  Mimi naona si kweli.Jk amefanikiwa sana kukuza Demokrasia kuliko watangulizi wake japo ameshindwa kukuza uchumi.Watu wana uhuru wa kuongea, Uhuru wa media umeboreka, maoni ya wapinzani yanafanyiwa kazi, unaweza hata kumkosoa rais au kiongozi yeyote hadharani nk. Hayo mambo ni ya muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.

  Ndiyo yaliyomng'oa Gadafi japo alifaulu sana katika nyanja ya uchumi. wadau mnasemaje?

  Naomba kutoa hoja.
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Umesema kweli kwa kiasi flani Mkuu, binafsi nakuunga mkono! Ila kwann umemuita "Baba Mwanaasha"?
   
 3. O

  Omr JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Subiri matusi sasa.
   
 4. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  bwana wee sawa, lakini maubadhirifu anayofanaya hata hayo machache unayoyazungumzia kama mema ameyafanya yanamezwa humo.
   
 5. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja!!Tatizo siasa za Tanzania zinahitaji uelimishaji sana kwa wananchi!Watu wakishakuwa against na wewe hata ufanye nini wataendelea kukuponda tu!Kwa democracy Jamaa amejitahidi na atabaki kuwa mfano wa kuigwa!!

  Nawasilisha!!
   
 6. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Baba Mwanaasha, interesting name. Binti amekuwa maarufu ghafla.
   
 7. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Upo Sahihi Kabisa.
   
 8. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  uchumi na demokrasia kipi bora?
   
 9. M

  Mkwakwasu Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi kwa nini watu huwa hawapendi ukisema hali halisi iliyopo?wanapenda zaidi ushabiki?
   
 10. M

  Mkwakwasu Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu nilitaka kuweka Title itakayo vutia wachangiaji.Au nimekosea mkuu?
   
 11. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Tutapata "maisha bora kwa kila mtanzania" kutokana na longo longo za jk au kutokana na uchumi imara? Watanzania wanachohitaji ni maisha bora walioahidiwa na jk na chama chake na wala siyo fursa ya kuwakosoa viongozi kwa uhuru.
   
 12. M

  Mkwakwasu Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila mtu ana uwezo wake aliojaliwa na mwenyezi Mungu.Tuombe sasa atakaefuata awe na uwezo wa kiuchumi mkuu
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ukiangalia hayo yote ambayo unaona kuwa ameyafanya, utabaini kuwa hayana uhusiano wa moja kwa moja na kuboreka kwa maisha ya mtu wa kawaida. Ndio maana watu wengi uliozungumza nao wanaona kuwa kama hajafanya lolote la maana. kama anataka aonekane kuwa amefanya kitu, basi ahakikishe hali za maisha ya watu zinakuwa bora zaidi. watu hawali demokrasia au uhuru wa vyombo vya habari
   
 14. M

  Mkwakwasu Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vyote vinakwenda pamoja mkuu
   
 15. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Haya ni mawazo ya kiendawazimu kutoka kwa mtu aliyefirisika kimawazo. Nani kakwambia kuwa uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kutoa mawazo na demokrasia vinahitaji fadhila toka kwa Baba Mwanaasha?? Hiyo ni haki yetu ya msingi ya kikatiba, tena hatuna uhuru wa kutosha katika nyanja hizo hadi vyombo vya habari vya serikali vinatumika kama propaganda ya chama tawala!!! Mawazo yako ni sawa na mzazi anayedhania kuwanunulia wototo wake chakula ni fadhila na sio wajibu. Soma vizuri katiba kijana, nakushauri usishiriki katika kuunda katiba mpya utapotosha watanzania.
   
 16. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Matatizo au changamoto anazokabiliana nazo ni kama ifuatavyo:
  1. Kwa kiasi kikubwa ameshiriki au kuhusishwa ufisadi mkubwa ambao umelikumba taifa na hivyo kukosa nguvu za kuwaadabisha wazembe na wabadhilifu waliopo katika serikali yake.
  2. Bado anaendeleza matanuzi makubwa bila huruma kwa wananchi wake.
  3. Inaelekea hajui uwezo wa mapato wa serikali yake na kama anajua basi hajui kupanga vipaumbele!
  4. Hachukui hatua za haraka pale anapohitajika sana kutoa msimamo wa serikali
  5. Hafahamiki lini amefurahi na lini amechukizwa na utendaji wa serikali yake; anacheka pale anapopaswa kuonekana amechukia.
  Nia ajabu na kweli!
   
 17. M

  Mkwakwasu Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kuwa tayari tuna demokrasia,Rais atakaefuata ashughulikie uchumi.JK Uwezo huo hana.hayo aliyo yafanya ndiyo mwenyezi Mungu alimwangazia. kumbuka kila mtu ana strength na weakness.
   
 18. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,115
  Trophy Points: 280
  Mimi nitamwoa huyo MwanaAsha
   
 19. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika kama kuna ambalo JK amefanya na amewashinda wote hata Mwalimu ambae ni muaasisi ni kukubali swala la uhauru wa kujieleza na kusema chochote kile ila tu usivunje sheria,yani kwa lugha nyepesi amekuza demokrasia.

  Mimi si mwanachama wa chama chochote kile kwangu Tanzania kama Taifa ndio chama changu,hivyo kwa Jk anastahiki heshima hiyo leo hii tuna jamii forum na majarida kibao ambayo yanatoa criticisms kibao n kwa wingi kuhusu Serikali na utawala ulioko madrakani.na bado Serikali ikawaona watoaji kama Watanzania wa kawaida bila kuwaghasi na kutishia usalama wao kwa ni ya kuwatia woga na vitisho vingine japo kwa uchache yapo baadhi yametokea katika sehemu ya maandamano ambayo yanaitaji kupata kibali cha Polisi ambao nao ndio wamekuwa mbele kukwamisha eneo hilo wananchi kujieleza kupitia kada hiyo.

  Nilichojifunza kama kijana wa Kitanzania JK ameridhi mambo mengi, ya ovyo, kifisadi,wizi, udanganyifu na mengineyo mengi kutoka kwenye limbikizo la mlolongo wa vijatabia na matabia machafu ya watendaji na watawala wa Serikali, toka enzi ya Mwalimu ba hatimae uuzaji wa Maliasili za Nchi kwa kasi kubwa enzi za Mzee BWM.

  Kwa misingi hiyo yeye JK binafsi anaweza kuwa na kusudio la dhati la kuikwamua Tanzania na watanzania lakini, kwa mfumo [system] iliyopo ambayo yeye amekuwemo yahitajika moyo mgumu sana tena wa chuma,kwa kuwa kwenye kuwageuza watu ambao kwa kiwango ama kiasi kimoja kila mmoja ndani ya mfumo anaona anamchango wake katika kumfikisha JK kwenyue kiti cha enzi basi ni kazi kuwaambia kuwa moyo wake toka alikotoka ulikuwa ni kuwa siku moja atakuwa Rais wa Watanzania na atawatatulia shida zao na kuwapa neema ya maisha bora,na ndio maana pasipo kujua mbele atakumbana na nini akajenga slogan yenye neno neema ndani yake ambayo yeye mwenyewe leo hii anasema anashindwa kujua Tanzania na Watanzania kwanini tu maskini.

  Ni kweli lazima anapata shida sana kwa kujiuliza maswali ambayo hayana majibu,ukweli ni kuwa alikuwa na dhamira safi na ndio maana spirtually watanzania asilimia 80% ya watanzania waliopiga kura nikiwemo mimi tulimchagua mwaka 2005 kwa kishindo.Hivyo kosa lake kubwa hakuchagua team ya kumsaidia kujenga Nchi spirtually, kwa maana ya kumuomba Mungu amsaidie kumpa wasaidizi wenye moyo wa kujenga Nchi.Hatimae sasa tumeanza kubaini kuwa uenda mwenye dhamira safi ni yeye lakini ndani ya Serilali na chama chake cha CCm wenye dhamira kama zake ni wachache sana na mfano tumeona wakati wa marekebisho ya vifungu vya sheria na za ujio wa katiba mpya.

  Kwa jicho la haraka tulio wengi tunaona JK anaweza kuibadilisha Nchi kwa kuwabana mafisadi na wezi wa Seriakali kirahisi rahisi,kumbe tuna sahau kuwa tuna utawala wa sheria ambao nao nio muhimili unaojitegemea binafsi,hivyo kwa kuwa kama Taifa tumefika katika ufisadi wa hali ya juu basi hata mapambano yake binafsi yanataka akili ya juu sana.Vinginevyo njia ya mkato ni kuwa dikteta kama Kagame ambae amesimamia ujenzi wa Taifa kwa kuakikisha kuwa hakuna system ya matendo machafu inayokuwa ndani ya utawala.

  Tanzania yetu inamifumo ya aina mbili kuna mfumo wa watanzania wanaoshabikia mambo ya kihalifu na wale wenye kusimamia haki ,mfano mkubwa ni jinsi wanajamii wanavyoshabikia jirani yao aliyekwapua pesa kwenye shirika au seriikalini kisha kujenga hekaru kubwa mtaani kisha kuonekana ni mjanja na mwenye maalifa ya kupewa dhamana ya kuongoza watanzania.Na kuna watanzania wengine wenye kupenda kuona watu wengi wanapata haki sawa, kwa kada hii imekosa baadhi ya watu mahili wenye mbinu maarifa ya kusimama na kupinga kundi la wezi na mashabiki wao mitaani kwetu.

  Tufike sehemu tujue dhamira ya Jk lakini je walioko upande wake tunawajua,kwa kuwa JK kukaa upande wake pekee, hata kwake yeye mwenyewe usalama wake uko mashakani, ndio maana juzi juzi tumesikia shutuma kuwa wataka atue kofi moja wakasahau kuwa walishatua enzi ya Mwalimu na Mwinyi lakini utata ukapatikana wakaamua kuludishia.Tufike sehemu tujue tunavita na kundi ovu ambalo limejijenga chini ya kivuli cha matajiri na baadhi ya wanasiasa wafanyabishara wanaoendesha biashara zao chini ya kofia ya uwanasiasa.

  Na hakika kwa wanajamii forum tutambue ni tuko kwenye vita ya mfumo.na vita ya mfumo inaitji umakini na sio pupa,vinginevyo njia nyepesi ya kuondoa mfumo uliomea yapata miaka 24 sasa ni kutumia udikteta wa kijeshi wa kukamata waalifu, na yeyeyote anaetuhumiwa bila kumpa nafasi ya kujitetea mbele ya mahakama na kuweka wote ndani,na hivyo kwa hatua hiyo tutaondoa mfumo huo je ndio njia sahihi tunayotakiwa kutumia?.Au tupitie njia ya mfumo wa demokrasia ambayo kunawakati inachukiza pande zote mbili wataka haki na wavunja haki kisha kuachia ukweli ukajisamia na jamii kusimamia haki na ukweli wa jambo husika uko wapi.

  Kwa waelevu waliompa heshima ya udaktari wa sheria walijua bidii na mchango wake kuona hekima na busara zake katika mapambano ya kuondoa mfumo ovu ndani ya Serikali na ndani ya Chama chake kwa style shirikishi ya kuwaalika wananchi kujua kinachoendelea na wao kufuatilia na kujua hatima yake mpaka kieleweke ndani ya Taifa.
   
 20. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ulu ulishamuuliza Jenerali ulimwengu dhama zake wakati wa mzee BWM hali likuwaje,yaliyomtokea usingesema haya,kama ulikuwa mfuatiliaji wa magazeti ya RAI basi usingesema haya ya kuwa hiyo ni haki yako.Unajua haki ipo siku zote lakini haki hiyo inatendeka?
  Na hakika JK anagombana sana na wasaidiz wake nikimaanisha watawala wa Serikali na chama chake kwa uhuru huu wa habari ambao wao wnaona kama umekithiri na kuleta changamoto kubwa sana kwenye utawala kwa kuwa Wananchi husika wako well informed na mambo mengi yanayoendelea ndani ya Taifa na ndani ya Serikali.
   
Loading...