Mambo matano usiyofahamu kumhusu Rais Samia Suluhu

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
1. Upinzani
“Tukianza kutafuta asiye na dhambi ili tujadili naye kuhusu kesho yetu hatutampata,hivyo tuna kila lazima ya kuacha chuki na visasi na kuwaamini viongozi wetu"

"Siwezi kuwa chawa wa Mama (Rais Samia) na wala sio wa chawa wa mama, lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, utawala wa Mama japo alikuwa ni makamu wa Hayati Rais Magufuli wana tofauti kubwa sana ni kama mbingu na mchanga, mtu yoyote mkweli ataliona hilo"

"Nina imani sana na Rais Samia na Serikali yake ya chama chake,hadi sasa naona kuna nia na dhamira njema"

Haya yalikuwa ni maneno machache ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Aikael Mbowe alipopata nafasi ya kumuelezea Rais Samia wakati akizungumza kwenye mitandao na Watanzania waishio nje ya nchi.

Kifupi tunaweza kusema ni mtu wa watu anayependwa na watu wote.

2. Muumini safi wa Uhuru wa vyombo vya Habari na Uhuru wa kujieleza na Demokrasia
Katika siku 365 za Rais Samia Suluhu, kitu cha kwanza alichokifanya , ni kuhakikisha vyombo vya habari vinafanya kazi kwa Uhuru bila bugudha na kuhakikisha vyombo vya habari vinakua, lengo la Rais Samia ni kuona watu wakijitokeza hadharani na kusema yale ambayo yamejificha.

Waandishi na wahariri wamekiri wazi "Ndani ya siku 365, vyombo ya habari vimepumua Kalamu zetu ziko huru kufanya kazi, lakini kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa"- Joyce Shebe Mwandishi wa Habari.

Askofu Bagonza amwagia sifa Rais Samia "Ni mwaka wenye mafanikio makubwa, Orodha ya mafanikio ni kubwa kuliko urefu wa mwaka wenyewe. Jambo la pekee ni uwezo wa Mama kusikiliza.. Uhuru wa watu kutoa maoni yao ni mkubwa"

Hapa Jamii Forums ni ushahidi tosha kuwa watu wapo huru kusema wale wayatakayo.

3. Ni Mtimiza Ahadi
Moja jambo kubwa lililoitatiza mikoa ya Dar es salaam kipindi cha Ukame ni upungufu mkubwa wa maji, Serikali imesaini tayari mradi wa utekelezaji wa Bwawa la Kidunda, Bwawa la Kidunda litakalo fungua fursa ya upatiakanaji wa Maji ya kutosha kwa matumizi ya nyumbani na viwandani, kukamilika kwa mradi huu kutafungua fursa za Uvuvi na kilimo vilevile mradi huu utasaidia upatikanaji wa Umeme wa uhakika nchini.

Mradi wa Bwawa la kidunda ulisanifiwa toka Mwaka 1961 serikali ya Rais Samia kupitia Wizara ya Maji chini ya Waziri wa Maji Mhe. Jumaa imetoa Pesa kwa mradi huu kuanza na kukamilika ndani ya wakati.”

Tanzania tangu imepata Uhuru, kanda nzima ya Ziwa, hakukuwa na hospitali hata moja iliyokuwa na mashine ya MRI. Kwa mara ya kwanza mashine ya MRI zimefungwa mkoani Mwanza ndani ya Mwaka mmoja wa Rais Samia.

4. kiongozi mwenye huruma na Upendo
Kwa upendo wake Rais Samia aliyoa maelekezo Serikali kugharamia matibabu ya aliyekuwa Mbunge wa Mikumi na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Bw. Joseph Haule (Prof. Jay) aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi aliporuhusiwa kurudi nyumbani.

Upendo wake umeonekana zaidi pale alipolitaka Bunge kulipa stahiki za Mbunge wa Ikungi na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Antipass Lissu pamoja na gharama zake zote matibabu baada ya kupata ajali ya shambulio la Risasi September 7.

5. Mchumi anayeivusha Tanzania ya 5G. Tunaweza kukopa na kulipa madeni yote aliyorithishwa
Kwa kifupi tumeona uwekezaji uliovunja rekodi tangu tupate Uhuru.

“Hatujawahi kuvutia uwekezaji kwa kiwango cha trilioni 24.5 thamani ya uwekezaji ndani ya miezi 18 uwekezaji wa Rais samia miezi 9 unazidi uwekezaji wa miaka 4 iliyopita hana sifa ya kujikosha na kujitweza, haya mambo ndiyo yanawanyima usingizi na Raha wahasidi wake.”

Tusichokijua kwa Rais Samia kitaaluma amesomea UCHUMI tena ni mchumi kutoka vyuo vikuu vinavyoheshimika Uingereza mambo yake yanaonekana.

Kuhusu kodi amevunja rekodi hivyo ana uwezo wa kukopa na kulipa madeni yote aliyorithishwa.

Amethibiti mfumuko wa Bei kwa asilimia 3.4, amefanikiwa kupandisha pato nchi kwa asilimia 5.8 ukuaji wa kasi ya 4G tunasubiria Mradi wa LNG ukamilike 2025 Watakuwa wanakuja Tanzania kuomba misaada ya hapa na Pale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom