Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Samia ni Jembe - Mbowe

Mtu wa Asali

Senior Member
May 9, 2022
152
291
"Tukianza kutafuta asiye na dhambi ili tujadiri naye kuhusu kesho yetu hatutampata,hivyo tuna kila lazima ya kuacha chuki na visasi na kuwaamini viongozi wetu"

"Siwezi kuwa chawa wa Mama (Rais Samia) na wala sio wa chawa wa mama, lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, utawala wa Mama japo alikuwa ni makamu wa Hayati Rais Magufuli wana tofauti kubwa sana ni kama mbingu na mchanga, mtu yoyote mkweli ataliona hilo"

"Nina imani sana na Rais Samia na Serikali yake ya chama chake,hadi sasa naona kuna nia na dhamira njema"

Freeman Mbowe - Mwenyekiti CHADEMA #ClubHouse
 
Ukishalamba asali huna namna nyingine
IMG-20220603-WA0006.jpg
 
Tuwekee ka-clip mkuu. Vinginevyo tutaona kama ni majungu kama majungu mengine

Lkn ukweli ni kwamba mama ni binadamu wakati mtangulizi wake alikuwa shetani. Hili lilithibitishwa hata na mtumishi wa Mungu Askofu Mwingira
 
"Tukianza kutafuta asiye na dhambi ili tujadiri naye kuhusu kesho yetu hatutampata,hivyo tuna kila lazima ya kuacha chuki na visasi na kuwaamini viongozi wetu"

"Siwezi kuwa chawa wa Mama (Rais Samia) na wala sio wa chawa wa mama, lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, utawala wa Mama japo alikuwa ni makamu wa Hayati Rais Magufuli wana tofauti kubwa sana ni kama mbingu na mchanga, mtu yoyote mkweli ataliona hilo"

"Nina imani sana na Rais Samia na Serikali yake ya chama chake,hadi sasa naona kuna nia na dhamira njema"

Freeman Mbowe - Mwenyekiti CHADEMA #ClubHouse
Ndugu Mbowe weka akiba ya maneno, Ikitokea wamekugeuka utakosa ujasiri wa kuwasema.

Wamesharuhusu wanyama hai wanasafirishwa hv sasa, unakaa na Mr tembo mchana, usiku vijana wake wanaanza operation.

Tunahitaji chama kipya Ili wakati taratibu hizo za NDOA zikiendelea, tuwe na whistle blower mwingine kutusemea usiyoyaona sasa Kwa ubusy wa HARAKATI za NDOA.
 
Mbowe kayasema haya wapi mkuu. Ni muhimu kukamilisha nukuu yako ili tuwe na uhakika nayo bila ya mashaka yoyote.

Hata kama yamesemwa na Mbowe, bado hajaeleza ni katika mambo gani hasa kuna tofauti kati ya yule 'kichaa' na huyu 'Maza Mizinguo'.
Kama mlinganisho ni katika maeneo ya "UKICHAA", hakika hapo hakuna ushindani kati ya huyu na yule. Hili liko wazi kabisa.

Lakini uongozi wa nchi hauishii kwenye 'ukichaa' pekee. Kuna mambo mengi mengine ambayo yanahitajika kutazamwa na kuyapima katika utendaji wa watu wanaolinganishwa.

Nitaungana na Mbowe katika kusifu juhudi za Maza Mizinguo katika eneo la kujali utu wa wengine; lakini kwa sasa sifa zangu zitaishia hapo.
Sikubaliani na Maza kwenye mambo yake ya "ufunguzi wa nchi" kiholela bila kuwa na mikakati ya kudhibiti uchafu unaoendana na wahusika wanaopewa uhuru usio kikomo kuendesha na kuvuna mali za waTanzania.

Mbowe hajazungumzia chochote kuhusu "sera" za Maza. Hakuna kinachotofautisha sera za CHADEMA na CCM ya Maza Mizinguo?

Hili halihusu "Kutafuta asiye na dhambi", na wala kutofautiana katika sera hakuhusu "chuki wala visasi". Sasa Mbowe aseme, akipinga sera za CCM itaonekana ana chuki na kutafuta visasi?
Akidai Katiba Mpya, ataonekana hana shukrani na aliyotendewa na Maza Mizinguo, hata kama ilikuwa ni haki yake kutendewa hivyo?

Mwisho, kama Mbowe anaona kuwa Maza anafaa, basi amuhimize asifanye kampeni za kujiuza hata kabla ya kuanza kampeni za uchaguzi 2025. Mtu anayeonekana kwa wananchi anafanya vizuri hahitaji kujiuza namna anayofanya sasa hivi. Hii ni kasoro kubwa kwake.
 
"Tukianza kutafuta asiye na dhambi ili tujadiri naye kuhusu kesho yetu hatutampata,hivyo tuna kila lazima ya kuacha chuki na visasi na kuwaamini viongozi wetu"

"Siwezi kuwa chawa wa Mama (Rais Samia) na wala sio wa chawa wa mama, lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, utawala wa Mama japo alikuwa ni makamu wa Hayati Rais Magufuli wana tofauti kubwa sana ni kama mbingu na mchanga, mtu yoyote mkweli ataliona hilo"

"Nina imani sana na Rais Samia na Serikali yake ya chama chake,hadi sasa naona kuna nia na dhamira njema"

Freeman Mbowe - Mwenyekiti CHADEMA #ClubHouse
Mada inahusu nini?
 
Hahaa
Mimi naona Mbowe kaanza kuwa mtu pragmatic, na kufanya siasa za possibility. Sio ule wehu wa 'Tutaandamana hadi uchaguzi urudiwe'

Ni kweli Samia na Magufuli wapo tofauti sana, na Samia ni improvement kubwa, ameaomua kuzungumza nao na pengine kuna compromise kadhaa atafanya kuhusu madai ya wapinzani, ndivyo siasa zinatakiwa kuwa
Ukitaka radical changes kwa Tanzania hii rafiki yangu ni kupigama na ukuta
 
Mama yuko kazini

Tuna imani na mama

Ni mtu aliyechanganyikiwa pekee ambaye haoni kazi njema ya Rais Samia.
 
..Raisi ameonyesha nia njema.

..Nia njema inatakiwa ifuatiwe na kukomesha unyanyasaji na dhuluma dhidi ya wapinzani.

..Tunataka kuona mikutano ya hadhara ikifunguliwa kwa vyama vyote.

..Tunataka tume huru ya uchaguzi, na katiba mpya na bora.

..Tunataka kuundwa kwa Tume ya maridhiano na ukweli.
 
Ndugu Mbowe weka akiba ya maneno, Ikitokea wamekugeuka utakosa ujasiri wa kuwasema.

Wamesharuhusu wanyama hai wanasafirishwa hv sasa, unakaa na Mr tembo mchana, usiku vijana wake wanaanza operation.

Tunahitaji chama kipya Ili wakati taratibu hizo za NDOA zikiendelea, tuwe na whistle blower mwingine kutusemea usiyoyaona sasa Kwa ubusy wa HARAKATI za NDOA.
Mkuu

Malkia anaekupuliza na kukupapasa

Ni hatari Sana kuliko kikosi kile cha kung'oa kucha cha awamu ya jiwe!!

Kumbuka hata utawala wa Rumi uliporuhusu ukristo Kuwa Dini na kuketi na watumishi wa kristo kwenye meza zao ndefu zenye vitam!

Ndipo ukristo ulipoanguka chini na Kuwa giza Totoro kuliko hata kipindi cha yale mateso ya alina stefano!!!

Naona UPINZANI ukiyumba kwa kupapaswa na kupulizwa na kulambishwa vitamu na kutazamwa kwa jicho la huba la yezebeli!!!

State pekee Ndio ituokoe na mchakato wa KATIBA kufa!!

Maana state inategemea vyama ku push ajenda hii!Sasa kama vimetekwa Ndio Basi Tena!

NIMEUMIA Sana!
 
"Tukianza kutafuta asiye na dhambi ili tujadiri naye kuhusu kesho yetu hatutampata,hivyo tuna kila lazima ya kuacha chuki na visasi na kuwaamini viongozi wetu"

"Siwezi kuwa chawa wa Mama (Rais Samia) na wala sio wa chawa wa mama, lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, utawala wa Mama japo alikuwa ni makamu wa Hayati Rais Magufuli wana tofauti kubwa sana ni kama mbingu na mchanga, mtu yoyote mkweli ataliona hilo"

"Nina imani sana na Rais Samia na Serikali yake ya chama chake,hadi sasa naona kuna nia na dhamira njema"

Freeman Mbowe - Mwenyekiti CHADEMA #ClubHouse
Mbowe ana imani na CCM pia! Angewapa benefit of doubt, CCM ni ileile na viongozi wake ni walewale.

Vv
 
Back
Top Bottom