Kikwete mnyongeni lakini haki yake mpeni!

mie nakuunga mkono kabisa mdau, imefika wakati watanzania tujaribu kuchanganua mambo kwa mapana na marefu, tunahitaji kuwa na serikali inayojali utawala wa kisheria na demokrasia matatizo ya kiuchumi yaliyopo TZ kama utakuwa umetembea nchi nyingi za afrika bado watanzania tuna nafasi kubwa ya kusema tuna uchumi mzuri ukilinganisha na nchi zingine kama kenya, uganda, burundi hata rwanda, sudan nk. Ukubwa wa TZ huwezi linganisha na rwanda, mfumo wa barabara na miundo mbinu bado tz tuko vizuri tuuunge mkono serikali ili tuzidi kujiimarisha kiuchumi, tusubiri 2015 kama mnataka kubadilisha chama basi tumieni haki yenu ya kikatiba lakini mkianza kampeni leo kwa kweli mnatuyumbisha wananchi wengine, tafakari, chukua hatua
Hakika kama kuna ambalo JK amefanya na amewashinda wote hata Mwalimu ambae ni muaasisi ni kukubali swala la uhauru wa kujieleza na kusema chochote kile ila tu usivunje sheria,yani kwa lugha nyepesi amekuza demokrasia.

Mimi si mwanachama wa chama chochote kile kwangu Tanzania kama Taifa ndio chama changu,hivyo kwa Jk anastahiki heshima hiyo leo hii tuna jamii forum na majarida kibao ambayo yanatoa criticisms kibao n kwa wingi kuhusu Serikali na utawala ulioko madrakani.na bado Serikali ikawaona watoaji kama Watanzania wa kawaida bila kuwaghasi na kutishia usalama wao kwa ni ya kuwatia woga na vitisho vingine japo kwa uchache yapo baadhi yametokea katika sehemu ya maandamano ambayo yanaitaji kupata kibali cha Polisi ambao nao ndio wamekuwa mbele kukwamisha eneo hilo wananchi kujieleza kupitia kada hiyo.

Nilichojifunza kama kijana wa Kitanzania JK ameridhi mambo mengi, ya ovyo, kifisadi,wizi, udanganyifu na mengineyo mengi kutoka kwenye limbikizo la mlolongo wa vijatabia na matabia machafu ya watendaji na watawala wa Serikali, toka enzi ya Mwalimu ba hatimae uuzaji wa Maliasili za Nchi kwa kasi kubwa enzi za Mzee BWM.

Kwa misingi hiyo yeye JK binafsi anaweza kuwa na kusudio la dhati la kuikwamua Tanzania na watanzania lakini, kwa mfumo [system] iliyopo ambayo yeye amekuwemo yahitajika moyo mgumu sana tena wa chuma,kwa kuwa kwenye kuwageuza watu ambao kwa kiwango ama kiasi kimoja kila mmoja ndani ya mfumo anaona anamchango wake katika kumfikisha JK kwenyue kiti cha enzi basi ni kazi kuwaambia kuwa moyo wake toka alikotoka ulikuwa ni kuwa siku moja atakuwa Rais wa Watanzania na atawatatulia shida zao na kuwapa neema ya maisha bora,na ndio maana pasipo kujua mbele atakumbana na nini akajenga slogan yenye neno neema ndani yake ambayo yeye mwenyewe leo hii anasema anashindwa kujua Tanzania na Watanzania kwanini tu maskini.

Ni kweli lazima anapata shida sana kwa kujiuliza maswali ambayo hayana majibu,ukweli ni kuwa alikuwa na dhamira safi na ndio maana spirtually watanzania asilimia 80% ya watanzania waliopiga kura nikiwemo mimi tulimchagua mwaka 2005 kwa kishindo.Hivyo kosa lake kubwa hakuchagua team ya kumsaidia kujenga Nchi spirtually, kwa maana ya kumuomba Mungu amsaidie kumpa wasaidizi wenye moyo wa kujenga Nchi.Hatimae sasa tumeanza kubaini kuwa uenda mwenye dhamira safi ni yeye lakini ndani ya Serilali na chama chake cha CCm wenye dhamira kama zake ni wachache sana na mfano tumeona wakati wa marekebisho ya vifungu vya sheria na za ujio wa katiba mpya.

Kwa jicho la haraka tulio wengi tunaona JK anaweza kuibadilisha Nchi kwa kuwabana mafisadi na wezi wa Seriakali kirahisi rahisi,kumbe tuna sahau kuwa tuna utawala wa sheria ambao nao nio muhimili unaojitegemea binafsi,hivyo kwa kuwa kama Taifa tumefika katika ufisadi wa hali ya juu basi hata mapambano yake binafsi yanataka akili ya juu sana.Vinginevyo njia ya mkato ni kuwa dikteta kama Kagame ambae amesimamia ujenzi wa Taifa kwa kuakikisha kuwa hakuna system ya matendo machafu inayokuwa ndani ya utawala.

Tanzania yetu inamifumo ya aina mbili kuna mfumo wa watanzania wanaoshabikia mambo ya kihalifu na wale wenye kusimamia haki ,mfano mkubwa ni jinsi wanajamii wanavyoshabikia jirani yao aliyekwapua pesa kwenye shirika au seriikalini kisha kujenga hekaru kubwa mtaani kisha kuonekana ni mjanja na mwenye maalifa ya kupewa dhamana ya kuongoza watanzania.Na kuna watanzania wengine wenye kupenda kuona watu wengi wanapata haki sawa, kwa kada hii imekosa baadhi ya watu mahili wenye mbinu maarifa ya kusimama na kupinga kundi la wezi na mashabiki wao mitaani kwetu.

Tufike sehemu tujue dhamira ya Jk lakini je walioko upande wake tunawajua,kwa kuwa JK kukaa upande wake pekee, hata kwake yeye mwenyewe usalama wake uko mashakani, ndio maana juzi juzi tumesikia shutuma kuwa wataka atue kofi moja wakasahau kuwa walishatua enzi ya Mwalimu na Mwinyi lakini utata ukapatikana wakaamua kuludishia.Tufike sehemu tujue tunavita na kundi ovu ambalo limejijenga chini ya kivuli cha matajiri na baadhi ya wanasiasa wafanyabishara wanaoendesha biashara zao chini ya kofia ya uwanasiasa.

Na hakika kwa wanajamii forum tutambue ni tuko kwenye vita ya mfumo.na vita ya mfumo inaitji umakini na sio pupa,vinginevyo njia nyepesi ya kuondoa mfumo uliomea yapata miaka 24 sasa ni kutumia udikteta wa kijeshi wa kukamata waalifu, na yeyeyote anaetuhumiwa bila kumpa nafasi ya kujitetea mbele ya mahakama na kuweka wote ndani,na hivyo kwa hatua hiyo tutaondoa mfumo huo je ndio njia sahihi tunayotakiwa kutumia?.Au tupitie njia ya mfumo wa demokrasia ambayo kunawakati inachukiza pande zote mbili wataka haki na wavunja haki kisha kuachia ukweli ukajisamia na jamii kusimamia haki na ukweli wa jambo husika uko wapi.

Kwa waelevu waliompa heshima ya udaktari wa sheria walijua bidii na mchango wake kuona hekima na busara zake katika mapambano ya kuondoa mfumo ovu ndani ya Serikali na ndani ya Chama chake kwa style shirikishi ya kuwaalika wananchi kujua kinachoendelea na wao kufuatilia na kujua hatima yake mpaka kieleweke ndani ya Taifa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom