Kikwete: Lowassa ndiye mhusika wa Richmond

Kikwete: Lowassa ndiye mhusika wa Richmond

Status
Not open for further replies.
Itazame kauli hiyo kwa jicho jingine: hapo ni JK anamshtaki Lowassa kwa Magufuli. Manake leo hii CCM wanatuambia Magufuli atakapoingia madarakani basi atarekebisha yote waliyoharibu na kufanya yote yaliyowashinda kwa miaka 54!
alipomnadi 2010 pale Monduli na kusema ni ajari ya kisiasa ulikuwa uko wpi?

nini maoni yako kuhusu watuhumiwa wengine?
Chenge,Tibaijuka,Ngeleja,?..hawa ni wabunge watarajiwa wa CCM(pengine ni mawaziri wake,you never know)....
CC hainania ya dhati?Pumzi imekata....wake benchi wajitafakari..
 
Kwanini asingesema muda wote huo???..kwann asingemkamata kama raisi????
Kesho tukaichinje ccm bila huruma
 
Kikwete aweka wazi kuwa waziri mkuu kipindi hicho ndio muhusika mkuu kwenye Richmond, baraza la mawaziri pamoja na yeye walihusika nawalikubaliana kuwa kuna upungufu wa umeme na mitambo ikanunuliwe lakini hakuhusika kampuni gani ya kwenda kuleta hiyo mitambo .

Alisisitiza sheria za manunuzi zifuatwe lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufata na aliunda tume ya manunuzi ya kwake mwenyewe .

Amechelewa kura yangu ni kwa Lowassa
 
Kikwete Big up big Dad!!!

VIVA CCM

MAGUFULI HOYEEEEEEEEEEE

HAPA KAZI TUUUUUU

LOWASSA KWA MAGUFULI HUWEZI.

Lowassa jiandae kwenda kuchunga ng'ombe maake TINGA TINGA LINATINGA IKULU.

Lowassa OUT DK.90 Zuhura Yunus na Mangekimambi msisahau kusiriba mpaka asahau Mshenga na Shehe wake Wa Jangwani
Endelea tu, jina litabadilika ghafla, ndg marehemu.. .
 
Ni kweli Mh. J.K alisubiri nini kabla ya leo kumsema au kumchukulia hatua.Najiuliza sisi pia tulianzaje kumchafua malaika Lowasa kuwa fisadi kwa miaka 8 mfululizo huku tukijua tusipomchukua kuwa mgombea wetu hatutashinda? Watatuaminiaje wanaopenda ukweli kuyaamini tena maneno yetu?
 
Anatapa tapa huyo! Nadhani Anafaa Aingizwe Kwenye Record Ya Maajabu Ya Dunia Kwa Kuwa Rais Wa Kwanza Anaefikiri Kwa Kutumia Tumbo..

Tanzania ilikua inajitawala bila rais kwa miaka 10
 
Rais umeeleweka, nimeridhika na maelezo yako, upo sahihi mkuu wa nchi.
 
mhusika wa twiga kupandiswa ndege ya jeshi la Qatar ni nani?
 
Mimi nauliza; kama Richmond ilikuwa ya Lowassa na kama walivyosema hawakuwa na hata hawakuwa na ofisi kwani mujibu wa kamati ya Mwakyembe, kwanini waliendelea kuilipa?
Kwanini waliibadilisha jina wakaiita Symbion na ikazinduliwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa marekani miaka kadhaa baada ya kujiuzulu kwani Lowassa?

Kama kweli Richmond inamuhusu Mhe. Lowassa kwanini wasimchukulie hatua muda wote wa miaka 8 tangu aondoke serikani??

Mimi Arushaone nimejiuliza nikapata jibu kuwa ni kweli kuwa Rais Kikwete anahusika 100% na Richmond ndio sababu alinyamaza Kimya siku zote mpaka leo siku ya mwisho ya kampeni kuwa kuwa anajua hakuna muda wa kumjibia kwani muda wa kampeni umeisha.

La muhimu ni kuwa 99% ya wapigakura wameshaamua wa kumpigia kura kabla ya siku ya leo 24/10/2015.

Rais atulie atupishe tuamue rais wetu wenyewe.
CC: Mungi Crashwise Yericko Nyerere Mzee wa Rula PakaJimmy Ben Saanane et al.
 
Last edited by a moderator:
Nchi ya walalamikaji. Hadi mzee wa Msoga analalamika. Hivi Edo asingehama CCM je? Mzee wa Msoga angeyasema hayo yote leo?
 
Leo ndo kajibu ili apate kuraa...!??atuambiem kule monduli kauli yake ya ajali ya kisiasa alimanisha nn..dah watanzania tunaonekana kama hatuna akili walah
Hapo JK alitumia lugha ya kidiplomasia, we sema mwenzake ni mzito sana kuelewa somo sijui by default,dhalau au makusudi.

Lowassa amushukuru Mungu kutokana na JK kumstahi sana,ingekuwa nchi nyingine saa hizi Lowassa angekuwa kizuizini kabisa,Nchi kama CHINA tusingekuwa nae.

Lowassa ni binadamu mwenye guts za kushangaza sana ndio maana ana ubavu wa kuwania Urais huku akijua wazi wazi hasara kubwa aliyo sababishia Taifa letu kutokana na mahamuzi yake ya kulazimisha mambo na kumu-undermine Rais aliye muweka madarakani;anafanya mambo ya ufisadi uliyo kubuhu behind JK'S back!!

Ufafanuzi wa kina wa Dk.Mwakyembe na leo JK kuhusu sakata zima la Richmond ni kielezo tosha kwamba EDO hatufai hata kidogo,kumpigia kura ya ndio EDO ni sawa sawa na kuhalalisha ufisadi wa watu wachache na ku condemn raia walio wengi kwenye lindi la umaskini.
 
Kikwete aweka wazi kuwa waziri mkuu kipindi hicho ndio muhusika mkuu kwenye Richmond, baraza la mawaziri pamoja na yeye walihusika nawalikubaliana kuwa kuna upungufu wa umeme na mitambo ikanunuliwe lakini hakuhusika kampuni gani ya kwenda kuleta hiyo mitambo .

Alisisitiza sheria za manunuzi zifuatwe lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufata na aliunda tume ya manunuzi ya kwake mwenyewe .
Na kama sheria za manunuzi hazikufuatwa yeye kama boss wake alichukua hatua gani?
Mbona yeye kama "mamlaka ya juu" alipopigiwa simu na Gray Mgonja kua Lowassa anataka kuvunja mkataba akajibu ubaki kama ulivyo??
Anayotuambia yeye tukichanganya na yetu tunapata jibu jingine
 
Kikwete aweka wazi kuwa waziri mkuu kipindi hicho ndio muhusika mkuu kwenye Richmond, baraza la mawaziri pamoja na yeye walihusika nawalikubaliana kuwa kuna upungufu wa umeme na mitambo ikanunuliwe lakini hakuhusika kampuni gani ya kwenda kuleta hiyo mitambo .

Alisisitiza sheria za manunuzi zifuatwe lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufata na aliunda tume ya manunuzi ya kwake mwenyewe .

Je yeye kama Raisi alichukua hatua gani baada ya kuona Huyo waziri mkuu alihusika? na kwa nini sikuzote alikuwa kimya lakni leo ndiyo anajifanya kuliongelea suala la Richmond. Wewe JK ndiyo muhusika mkuu wa Richmond hat TISS wanalijua hilo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom