Kikwete: Lowassa ndiye mhusika wa Richmond

Kikwete: Lowassa ndiye mhusika wa Richmond

Status
Not open for further replies.
Upuuz gani huo raiswanchi unashindwakuweka wazinakuchukua hatua et swala nyet km hilo unalisemea kwenye majukwaa yasiasza? Kiongoz gani wanmna hii.unaushahd mfunge huna just keep quit and shut up
 
Tumekusikia Mh. Dr. J. K., amiri jeshi mkuu na rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Ila nins shaka na moyo wangu waumia juu ya wewe kutochukua hatua yeyote juu ya mtuhumiwa. Nakuheshimu kwa wadhifa wako, umri wako na kama kiongozi wangu lakini ninakuwa na mashaka na maneno yako, kwa mamlaka uliyopewa na wananchi wa taifa hili kwa nini hayakutumika? Je, Mahakama zilikuwa likizo?

Napata shida kuamini, hivyo ninasukumwa ndani yangu kumchagua mtuhumiwa kuwa kiongozi wangu labda iko siku atafunua shilingi tuone upande wa pili. Nilitamani na nilisisimka sana alipobainishwa kuwa ni mtuhumiwa na fisadi, hakika wewe na tume iliyoundwa kuchunguza suala la Richmond mlikuwa mashujaa kwangu, nilisubiri kwa hamu kuona haki inatendeka bila mafanikio. Nilihitimisha kichwani kwangu this is just a political game, and some of the players have to be victim on behalf of collective responsibility!!!

Tuungane kwa pamoja kulinda umoja na amani ya taifa letu, maendeleo hayajii pasipo kuchukua maamuzi magumu yanahusisha uwajibikaji na uzalendo wa kweli.

Nakupenda Tanzania, napenda rasimali zako Tanzania ziwe kwa manufaa ya watanzania na sio wageni na wachache wasiojali.
 
Being honest may not get you a lot of friends, but it'll always get you the right ones.
 
Kikwete aweka wazi kuwa waziri mkuu kipindi hicho ndio muhusika mkuu kwenye Richmond, baraza la mawaziri pamoja na yeye walihusika nawalikubaliana kuwa kuna upungufu wa umeme na mitambo ikanunuliwe lakini hakuhusika kampuni gani ya kwenda kuleta hiyo mitambo .

Alisisitiza sheria za manunuzi zifuatwe lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufata na aliunda tume ya manunuzi ya kwake mwenyewe .

Vipi kuhusu "SIMBION" ...Ninavyofahamu mimi ni kuwa RICHMOND=DOWANS= SIMBION. Mnaojua zaidi tieni nguvu hapa.
 
...sijapata kuona Rais chiriku kama huyu duniani?!
 
duh! jamani unaweza ukaona watu wanapita barabarani na ving'ora na misafara watu wanasimama shuhuli zao na safari zao kuwapisha na watu wanalala hoi kuandaa ujio wao, wanapigiwa saluti kila dakika LAKINI MH!! Nashindwa hata nitumie tusi gani la kiswahili ambalo kwenye kamusi hata nikikamatwa kamusi hiyo itanitetea!!...AIBU KWA RAIS, Kama ningekuwa mimi Mr J the pres Nisingenyamaza jumla kuliko kuja kujidhalilisha kiasi hiki. UKAWA TUSONGE MBELE :crazy:
 
Mwakyembe akiwa Star TV;

Richmond inalipwa mpaka leo 243 Milioni.

Kikwete akiwa Kirumba;

Richmond haikulipwa na wala haikuleta mitambo.duniani kuna mbo
 
Akiongea leo Mwanza kwenye kufunga kampeni za ccm Mh.Jk amesema ni kweli alishiriki kwenye makubaliano ya kutafuta kampuni ya kufua umeme baada ya Mabwawa kukauka nchi, lakini hakushiriki kutafuta kampuni gani ilete umeme, hivyo hahusiki kwa namna yoyote kwa ujio wa Richmond.

Hivyo waziri Mkuu ndio mhusika mkuu wa Richmond!

Mbona hajafunguliwa mashtaka hadi Leo??
 
Lowassa ni mwizi na atabaki kuwa mwizi daima, mnahangaika bure kumsafisha hasafishiki yule,NAONA UKAWA tangu jana JK ahutubie jangwani mmepaniki mbaya, n ahuku mtaani vijana wenu wa viroba wamenywea sana
 
Kikwete aweka wazi kuwa waziri mkuu kipindi hicho ndio muhusika mkuu kwenye Richmond, baraza la mawaziri pamoja na yeye walihusika nawalikubaliana kuwa kuna upungufu wa umeme na mitambo ikanunuliwe lakini hakuhusika kampuni gani ya kwenda kuleta hiyo mitambo .

Alisisitiza sheria za manunuzi zifuatwe lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufata na aliunda tume ya manunuzi ya kwake mwenyewe .

Huyu jamaa anafurahisha sana! Miaka 8, kwanini maingemfungulia mashtaka ya uhujumu uchumi? Tafadhali mheshimiwa Rais usiwe mwanasiasa saana weka maslahi ya Taifa mbele acha porojo najua huna zaidi ya wiki magogoni, utoke tupumue. Mimi nimefurahi sana B. Membe na J. Makamba sio warithi wako. Natumaini Rais anayekubadili atakufurumua tu.
 
Tanzania tukiendelea kuchagua marais wa type ya huyu kamwe tusijetegemea tutatoka kwenye dimbwi la umaskini.
 
Yaani hii nchi ni ya kusadikika? Au inaongozwa na majuha? Muhalifu kama huyu alinadiwa monduli 2010. Akawa kwenye kamati ya ulinzi na usalama. Leo hii mkuu wa kaya ndio anayasema haya! Si ni sawa na kujivua nguo hadharani? Waliosema ni Dhaifu hawakukosea.
 
Maajabu mengine ya wakati tulionao. Vizazi vijavyo vitatuzungumza kuwa ni wa hovyo sana.
 
Too late sana,mabadiliko ndiyo mpango!

Yes change should be. Lowasa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi the friendship now is over and the exhibition completed.kwa mujibu wa Dk. Mwakembe jana star tv.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom