Kikwete kuondolewa uenyekiti CCM

Status
Not open for further replies.
Ndoto za mchana...

nini uwenyekiti huyu hafai kuwa hata katibu kata...CCM kawa hawajui huyu bwana amekididimiza sana chama na if they are not keen chama kitamfia mikononi...maana kama sio NEC na lile lizee Makame 2010 walishabwagwa urais....
 
Tuambie hadithi mpya hiyo ya zamani sana na tumeishaichoka
 
Kwa ubavu upi wa wana CCM? labda cku jua likiibwa ndo hayo yatatokea

  • A%20S%20465.gif

nini uwenyekiti huyu hafai kuwa hata katibu kata...CCM kawa hawajui huyu bwana amekididimiza sana chama na if they are not keen chama kitamfia mikononi...maana kama sio NEC na lile lizee Makame 2010 walishabwagwa urais....

ndio mwenyekigoda sasa
 
Mangula hajawahi kuwa mwenyekiti labla umepitiwa kidogo. Ninachokifahamu huyu bwana aliwahi kuwa katibu mkuu wa magamba nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na gamba lingine kwa jina la Mukama.
soma sawasawa kabla ya kujibu sio kukurupuka alichosema mwenzako ni kwamba jk alichemka kuwakubalia kina lowassa wamng'oe mangula kwenye ukatibu mkuu na kumpa makamba kwani makamba na manguli ni sawa sawa na kifo na usingizi,hawafanani hata kwa sura!
 
Wengine tunapunguza kutupa vya moto Jamvini. Si Vuguvugu ila ni kweli kwamba Mheshimiwa sana ameshapelekewa Press ya wabunge waliotia saini kwamba sharti wamfanyizie kutokana na sababu kubwa kadhaa.

Sababu ya kwanza ni kwamba kwa kuwa Mshahara wa Mbunge ni Tsh 7.3 Millioni kwa mwezi yaani ukijumlisha Monthly package yake ambayo ikiwa ni jumuisho la mshahara na malipo mengine ikiwamo posho za vikao. Jumlisho hilo ni pamoja na posho mbalimbali kila mwezi kama vile za mafuta ya magari, ubunge, kukaa jimboni, kuendesha ofisi na simu. Posho ya mafuta ni Sh2 milioni kwa mwezi ikikadiriwa kuwa atatumia lita 1,000 ambazo makisio ni Sh2,000 kwa lita moja. Nyingine ni posho ya kukaa jimboni Sh800,000, posho ya ubunge Sh1 milioni,
kuendesha ofisi Sh700,000, simu Sh500,000 na mshahara ni Sh2.3 milioni.

Posho hizi ni mbali ya Posho za Kila siku ambapo mbunge hulipwa Posho za aina Tatu, za Kujikimu, Usafiri wa ndani na Posho ya kikao cha BUNGE.

Katika Kifurushi kile cha mwezi kilimwezesha Mbunge kuchukua Mkopo wa kiwango alichohitaji, kuanzia milioni 200 hadi 800, na kwa mantiki hiyo wabunge wengi walikurupukia mikopo hiyo bila kufikiria makato yake yatakuwaje kama vile wajanja walivyosemaga kukopa harusi lakini ngoma kwenye malipo yake. Uchunguzi wangu binafsi, wabunge wengi walikurupuka kukopa kutokana na ukata uliowakabili baada ya kutapika vyote walivyokuwa navyo ili kuukwaa Ubunge, hii ikiwa ni pamoja na kulipa madeni, kununua Nyumba za kuishi (maana wengine walikuwa mabachelor) kulipia Bili na kadhalika. wengine walitumia mikopo hiyo kununua vitegauchumi ambavyo asilimia kubwa vimeshaporomoka. wengine walitumia mikopo hiyo kuanzisha NGO lakini kwa sababu ya kukosa "NETWORK" wamebaki na makabrasha yao na njaa inaanza kuwasumbua sana.
uchunguzi wangu pia unaonyesha kwamba wabunge walioathirika zaidi ni wale wa Chama tawala hasa ukichukulia kwamba kampeni zao zilibebwa kwa matumizi makubwa ya fedha ukianzia kura za maoni ndani ya chama na hatimae mpambano live.
kwa maana hiyo Tokea makato ya mikopo hiyo yaanze, hali imekuwa mbaya kwa wabunge. wengine wamejikuta wakiambulia mshahara wa mwalimu wa shule ya msingi kwa mwezi Tsh 230,000, na wengine kidogo zaidi hasa wale waliokopo kwenye zaidi ya chanzo kimoja cha mkopaji.
kwa maana hiyo hali imekuwa mbaya hasahasa Vijana waliokurupukia Bunge na mikopo hiyo , na wengi wamekuwa wakimsumbua sana spika wa Bunge wakijua sehemu iliyobaki ni kuongeza posho za Vikao, wengi sasa wanaishi kwa kukopana. hali hiyo imewafanya kwa Muda mrefu wabunge hao kumsumbua waziri mkuu na speaker wake. hali hiyo ilipelekea wabunge hao kuwakemea wakubwa hao kwamba hawajali maslahi yao ilihali wapo hapo kwa nguvu ya kura zao. hali hiyo iliwatishia Spika na Waziri mkuu kiasi cha kuandaa Dokezo la kurusha posho za wabunge hadi Tshs330,000 kwa siku (Posho ya kikao 200,000, Kujikimu 80,000 na usafiri wa ndani 50,000). jambo hili linafanya mbunge kupokea 9,900,000 kwa mwezi na ukijumlisha na mshahara wa 7,300,000 mbunge wa Danganyika... sorry Tanzania anajizolea Tshs 17,200,000/=kwa mwezi. Aisee. Ubunge wa Tanzania FAGILIA...

Bila kujali athari za Posho hizi Spika wa Bunge kwa shinikizo la wabunge hao akalisogeza faili kwa mkubwa sana wa nchi. Mkubwa akijua fukuto hilo, akatoa maelekezo kwa waziri mkuu, azisaini na waanze kulipwa kinyemela. jambo hilo likaanza kutendeka na wabunge wakaanza kupokea mshiko pandikizi toka kikao kilichopita. kwa sababu Bunge la sasa si la Chama kimoja, siri ikavuja kwa speed sana na kufanya sekta binafsi na wananchi wengine kuanza kuhoji kwanini wabunge hawa wanajilipa majisenti mengi kiasi hicho. Baada ya uvamizi wa waandishi wa habari kwa spika na waziri mkuu wote kwa Pamoja wakatupia mpira kuwa Mzee. Moto ukageukia kwa mkubwa kabisa wa TZ. nae kama kawa yake ya kujiosha akamwaga press kwamba hajabariki posho hizo, kwa maneno yenye ushwahili na mizunguko.
Kwa mantiki hiyo wabunge wameweka shilingi na rais, iwapo Rais ataendelea na shinikizo hilo kwamba wasilipwe mishiko hiyo basi ajue amekalia kiti kikavu, wataside na upinzani na kupiga kura ya kutokuwa na Imani naye. na pili watamkita down kuwa mwenyekiti wa Chama na Itakuwa rahisi kumtisha muda wowote kwamba watanyan'ganya kadi yao na kupoteza sifa za Urais.
jambo hilo wako nalo serious kulikoni tunavyodhani. Dhamira yao hiyo inachochewa na fukuto la ubaguzi ndani ya chama ambapo Mkubwa huyo inadaiwa amewaondoa wazee wa mashauri na kuamini zaidi watu wa ukoo wake.
TZ kuna kazi.. na kazi ina TZ
 
Hakika kama ni kwa stye hii,basi ni kweli huyu mwenyekiti wao yuko mashakani,ukiunganisha na wale tunaowasikia kuwa ni mahasimu wake basi kuna kimbembe cha kufa mtu na si mchezo.Vinginevyo walipane hivyo hivyo kinyemela uku akiwa na mtihani wa kujibu umma pindi ukicharuka au adinde kiume na kufanya maamuzi kama ya ben kuwaibukia Bungeni na kuwapa bonge ya karipio la kitisho.
 
Kwa sasa hakuna kiongozi wa CCM mwenye mvuto wa kikirejeshea chama hiki hadhi ya chama makini cha siasa. Karibu wote waliopo ni wachumia matumbo wanaoganga njaa zao tu.

CCM ni mufilisi kisiasa na kwa sasa wanabebwa na nguvu za dola!
 
Kweli? Haijawahi kutokea katika miaka 50 ya uhuru. Kwa sababu mwenyekiti wa Chama ni Rais wa nchi, mawazo ya kumvua uenyekiti ni sawa na kumvua Urais, jambo ambalo ni uhaini.
 
Mpango kabambe wa kumvua kikwete kofia ya chama umeiva, mpango huu unaongozwa na vijana. Wana CCM tegemeeni mabadiliko makubwa
Tatizo sio Mheshimiwa Kikwete, hata kama wataondoana woote ni kazi bure CCM na sysytem yake yoote imeoza!!!! Ili kuwa na nchi nzuri inahitajika the whole system ya CCM IPIGWE CHINI ili ijifunze uadilifu, wajifunze nje ya box wakiwa ndani hukuna wa kumfundisha mwingine!!!!! Samaki akioza mmoja kwenye kapu wote wameoza na wananuka hiyo ni CCM!!!!

naona ff,ms,rejao wamekususa leo,au nape kakupendelea wewe leo mambo ya airtime
Mkuu Nyabhingi hao kina FF, Rejao, MS si kwamba wamemsusa bali wanakuja na ID zingine kama mama Porojo and so on!!!!! Bali njanja fijo mweee!!!

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom