Sidhani kama Tanzania tume mature vya kutosha kisiasa kutuwezesha kuwa na kofia hizi mbili chini ya watu wawili tofauti bila ya kuleta migogoro ya uongozi. Binafasi nadhani litakuwa kosa kubwa sana kufanya hivyo kwani tofauti na nchi nyingine zilizoendelea ambako wenyeviti wa vyama husika mara nyingi (kama sio zote) huwa hawajihusishi na mbio za Urais, kwa Tanzania hali ni tofauti. Kumtoa Mwenyekiti wa sasa wa CCM katika nafasi hiyo kitatuletea vurugu nyingi sana kuelekea 2015. Sioni kama ujio wa mwenyekiti mpya utamaliza migogoro ya sasa kwani tatizo lililopo sasa ni pana sana. Hata hivyo kikao chenye mamlaka ya kumtoa mwenyekiti na makamu wake ni Mkutano Mkuu wa Taifa, na haujawahi kufanya hilo, na badala yake wenyeviti waliopita aidha waliondoka kwa hiari zao au baada ya kumaliza muda wao wa uongozi. Itakuwa ni maajabu ya kihistoria kama hilo litafanikiwa. Napinga hoja.