Kikwete kuondolewa uenyekiti CCM

Kikwete kuondolewa uenyekiti CCM

Status
Not open for further replies.
hata wakivuana wooote nyadhifa hadi selikalini ccm hakuna mwenye akili hata 1 angalia walivo feli kutatua mgogoro wa mgomo wa madaktari hii wiki ya 3 sasa hawajui hata wafanye nini, hivi kama ungekuwa ni uvamizi wa mipaka taifa lingekuwa mateka? Kikwete mwenyewe karudi badala ya kutatua tatiza yuko bize na kufungua benki. Ovyo kabisa

Leo mpond alikuw anatetemeka mikono sijui ni kawaida akiwa mbele ya bunge au ni cz anajua anasema uongo.
 
ni vizuri kufanya mabadilliko ya kwamba mtu akitaka kuwa Raisi na akachaguliwa basi kama alikuwa mwenyekiti wa chama aachie ngazi hii itakuza demokrasia katika kuendesha nchi na chama vile vile, ANC wapo hivyo, sasa hivi Kenya wanaelekea huko. hii ya Mwenyekiti na kuwa Raisi na kuishia kupanga watu wake ina ua demokrasia na kukandamiza fikra mbadala
 
KUNDI LAIBUKA KUTAKA AACHIE CHAMA, ABAKI NA URAIS

na Mwandishi wetu

WAKATI uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya taifa ukikaribia, kundi linalopigania mabadiliko kutaka kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti limeibuka upya kutaka mabadiliko hayo.

Hoja hiyo imeibuka sasa wakati zimebaki siku saba kabla ya CCM kuanza kutoa fomu za kuwania uongozi ngazi ya taifa.

Mtandao wa kundi hili pana unaunganisha baadhi ya vigogo wa CCM, wakiwamo wenyeviti na makatibu wa mikoa na wilaya na makada maarufu ambao hujulikana kama majeruhi wa kisiasa waliotokana na makundi yenye uhasama ndani ya chama hicho tawala.


Kundi la mlengo huo wa mabadiliko hayo linataka Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, aachie nafasi ya uenyekiti ili abaki kuwa rais, kumalizia muda wake.


Hata hivyo, kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya sasa, nafasi ya mwenyekiti na makamu wake hazigombewi, bali hutokana na uteuzi wa Kamati Kuu (CC) ambayo chini ya utaratibu wa sasa, rais ndiye anayekuwa mwenyekiti wa chama taifa.


Muundo huo wa uongozi uliasisiwa na Mwalimu Nyerere wakati ule, kwa hofu kwamba kama rais na mwenyekiti wanakuwa watu tofauti, ikitokea kwamba hawaelewani, nchi haitatawalika.


Sababu kubwa inayotajwa na kundi linalotaka mabadiliko hayo, ni kutaka kumpunguzia majukumu rais ili abaki kuiongoza serikali na shughuli za chama zisimamiwe na mtu mwingine, ambaye atakuwa na nafasi ya kutosha kukisimamia na kukiendesha.


"Baadhi ya wana CCM wanatuelewa vibaya kwamba tunataka kufanya uasi ndani ya chama, hapana.

Huu ni muundo mzuri unaotumika katika nchi nyingi duniani, na mfano ni Afrika Kusini. Lengo letu tunataka kumpunguzia rais majukumu na chama kibaki na mtu mwingine," alisema mmoja wa vigogo wa mkakati huo.


Uchukuaji wa fomu kuwania nafasi za uongozi wa CCM taifa, unatarajiwa kuanza Agosti 22 hadi 28.


Akizungumzia tishio la kutaka kumng'oa Rais Kikwete, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema kundi hilo linajidanganya kwani mkakati huo hauwezekani kwa sasa.


"Ni kweli tunajua kuna presha hiyo. Lakini ni mambo ya kushangaza, kwa sababu nafasi ya mwenyekiti na makamu hazigombewi, hao wanaotaka mtu mwingine agombee nafasi hiyo hizo fomu anazipata wapi na nani atakayempa?" alihoji Nape.


Alisema fomu za ngazi ya taifa zitakazotolewa kuanzia Agosti 22, zinahusu wajumbe wa halmashauri kuu pekee na si nafasi ya mwenyekiti wala makamu wake.


"Kwa kawaida nafasi ya mwenyekiti na makamu wake inapendekezwa na Kamati Kuu na kisha majina yao yanathibitishwa na NEC. Na hata kwenye kuomba kura, anaombewa na wajumbe wa Kamati Kuu," alisema Nape.


Kwa mujibu wa Nape, kundi linalotaka mabadiliko hayo kwanza lijitokeze na kisha lilete hoja hiyo katika utaratibu unaopaswa, na si kujificha na kutaka kufanya uhaini, jambo ambalo halikubaliki ndani ya chama.

 
Kachangia sana kuingiza Ufisadi ndani ya CCM,hadi Diwani ana nafasi nzuri ya kufisadi?
 
Mbona walianza siku nyingi, hawa magamba maneno tu actions zero, wamng'oe kama wana ubavu!!!
 
Hapa ndio mahali Nape angejipatia umaarufu kwa kupendekeza mabadiliko katika huo utaratibu wa kuchanganya hizo kofia mbili.

Mwalimu aliziunganisha katika mfumo wa chama kimoja, kwamba tuwe na kiongozi mmoja.

Katika mfumo wa vyama vingi kuendelea kuukumbatia ni upuuzi kwa sababu chama na serikali ni vitu viwili tofauti. Sasa Nape, kama kijana (mzee?) asiwe vuvuzela tu wa kuimba nyimbo za wazee, apendekeze mabadiliko ya mfumo yatakayosaidia kuleta ufanisi kwenye chama.
 
CCM ingekuwa na uongozi dhabiti (mwenyekiti , katibu etc) wanaojua wanafanya nini; chama kingekuwa mbali sana. CCM tatizo lao kubwa sana ni uongozi. Ukiwa na kiongozi asiyetaka kupingwa/kuwa-challenged,asiye na vision, na asiyejua kama hajui; ni ngumu sana ku-implement anything ukafanikisha. Anyways nawatakia kila la kheri wenye nia njema na chama; lakini hii yakusema wajitokeze kwanza ndio wapeleke maombi yao mmh!!!!.
 
Ni kweli Mkuu ana majukumu mengi. Mimi naona apunguziwe majukumu ya kuteua wakuu wa wilaya, mikoa, wakurugenzi na kadha wa kadha, ili abaki na majukumu yake ya kichama.
 
Ni kutokana na uongozi uliyoko chin yake na baadhi ya wizara kwahiyo unakuta lawama zote anazibeba yeye!! Dah ila kuongoza nchi kunahitaji moyo coz lawama zote lazma ztakuhusu!!
 
Wamvue na Urais pia ili tufanye uchaguzi mpya maana siyo siri kazi imemshinda.
 
Kachangia sana kuingiza Ufisadi ndani ya CCM,hadi Diwani ana nafasi nzuri ya kufisadi?

wewe si chadema so ufisadi wa hao jamaa unakusumbua kivije?si uwaache na ufisadi wao ili nyie chama cha watakatifu mje mchukue madaraka...
 
Hao jamaa watakuwa wanapiga domo tu, inabidi uwe na moyo wa mwenda wazimu! The man is still the president, wajiangilie.
 
wewe si chadema so ufisadi wa hao jamaa unakusumbua kivije?si uwaache na ufisadi wao ili nyie chama cha watakatifu mje mchukue madaraka...

Umeona Tatizo lako? Unaniona Nachangia humu Unanipa Chama cha CHADEMA, Mimi ni

​Mzalendo napenda nchi yangu nitakosoa nionapo ni kosa... sina hizo tittle za vyama...
 
Mpango kabambe wa kumvua kikwete kofia ya chama umeiva, mpango huu unaongozwa na vijana. Wana CCM tegemeeni mabadiliko makubwa

Kimsingi thread hii , ni ya kufikirika, kwa mantiki, kuwa mtu akiwa amiri jeshi mkuu, ni vyema masuala ya kichama yakaangaliwa kwa undani zaidi, kwamba raisi ndo mkuu wa intelenjesia, kabla ya mchakato huo kufanyika wote watakao fanya hivyo ;watakuwa kwenye msukosuko mkubwa inawezekana hata usiwezekane..nakumbuka jinsi iddi simba alivyofanyiwa kwenye jumuiya ya wazazi, ni serikali na usalama wa taifa walitumika.Changuzi zetu zimekuwa si huru na za haki , sababu usalama wa taifa wamekuwa wakitumika kuchakachua matokeo.ulimboka yaliyomkuta , ndo matokeo ya usalama wa taifa.Kwa hiyo haya ni mawazo ya kufikirika.yanatokea arusha kwa godbless lem, ni matokeo ya usalama wa taifa.Ya ole miliya yote hayo ni ya riz one kwa kutumia usala taifa kumfanya aone uvccm . si mahala salama.bashe nzega ni ritz one na usalama wa taifa walimtoa kisa msomali mbona rage ni msomali na ni mbunge wa tabora?abdurahaman kinana mbona mbona ni msomali na habaguliwi?hivyo ccm kwa ujumla wanamgwaya JK huyo anyefikiria hayo watamlimboka inawezekana akafa kabisa.
Kimsingi JK anavuruga ccm na taifa kwa ujumla , ccm imekuwa haina msemaji wala vikao;vikao vipi kwa mjibu wa katiba ya ccm , na havina nguvu, bali kula posho tu.wala si kweli kwenye taasisi kubwa kama ccm kuwakawa na wajinga kama nape, nchemba, wasira, lusinde ndo wajenge chama.j hakuna wayu weledi kama prof.muhongo, na wengine.?lakini JK kawa kiziwi , hataki kuambiwa kitu chochote..Anayethubutu kusema adui wa ccm.mafisadi, wafanyabiashra wakubwa ndo rafiki wa ccm.wanyonge na walalahoi si rafiki tena wa ccm kama itikadi ya ccm.hata wadhamini wa ccm wamebakia kubwata kama mbwa koko, pembeni bila kusema vikaoni, na kumwacha jk atanue kama hakutokea ccm.Itachukua muda mrefu ccm kukubalika kwenye umma kama jk ataendelea kuwa na fikra hii na falsafa hii.na nachela kusema bila rushwa na katiba mbovu , tegemea anguko baya la mwaka 2015.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom