Najiuliza bila kupata jibu na naomba msaada wa jibu au hoja zenu wataalam. Hivi Jakaya Kikwete kuongea na wanahabari kesho ni kutokana na kuona manufaa aliyopata Dr Slaa kwa mdahalo wa wiki jana? au ilikuwa sehemu ya program ya kampeni?
Kama anreact kutokana na mambo ya Slaa, do we need reactive or proactive Leaders?
Nauliza kwa sababu toka mwanzo wa kampeni CCM walisema TV na midahalo sii sehemu yao na wanataka kuwafikia Wapiga kura kwa Jukwaa tu. Sasa vipi??
Hivi nini maana ya mdahalo? Labda tukijua maana yake tutaweza kuelewa CCM walisema nini.
Nisahihisheni kama nimekosea, mimi nafikiri alichofanya Dr. Slaa au atakachofanya JK sio mdahalo ni mahojiano. Mdahalo ni pale unapopambanisha watu zaidi ya mmoja kujadili juu ya hoja mbalimbali. Kwa kiingereza mdahalo ni debate wakati ambacho wamekubali CCM sasa ni interview au mahojiano.